Kujivunia tu katika msalaba

Mungu apishie mbali nisije nikajivunia kitu chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa Yeye ulimwengu umesulibiwa kwangu, nami nimesulibiwa kwa ulimwengu

Hauhitaji kujua mambo mengi kuhusu maisha yako ili kuwa na utofauti wa milele ulimwenguni lakini ni sharti uyajue machache makuu yenye maana, kisha uwe tayari kuyaishia na kuyafilia. Watu wanaosababisha utofauti wenye kudumu ulimwenguni sio wale walionakili mengi akilini, bali wale walionakiliwa na machache akilinii yenye ukuu. Ukitaka maisha yako iwe ya kuhesabika, ukitaka athari za kipekee ya mambo uyafanyayo yawe kama mawimbi kutoka mwisho hadi mwisho wa ulimwengu kwa miaka au jadi na jadi hadi milele yote, hauhitaji kuwa na uerevu wa hali ya juu; hauhitaji kuwa na umbo nzuri au mali; hauhitaji kuwa wa familia bora au shule bora. Unastahili kujua machacahe makuu, yenye ustawi, yasiyo badilika yenye uwazi, rahisi na yenye utukufu, kisha hayo yakutie moto.

Lakini nafahamu kwamba sio kila mtu katika umati huu anataka maisha yako yawe yenye kusababisha utofauti. Kunao mamia kati yenu—hamjali kama mtasababisha utofauti wa kudumu kwa ajili ya kitu kikuu, mnataka tu watu wawapende. Kama watu wangewapenda tu, mungetosheka. Au kama tu mwaweza kuwa na kazi nzuri, mke mzuri na watoto kadhaa na gari nzuri na wikendi ndefu pamoja na marafiki wachache wema, ustaafu wa furaha kisha kifo cha haraka na isiyo na ugumu na pasipokuwepo jehanamu—ikiwa mungekuwa na hayo (lakini bila Mungu)—Mungalitosheleka. HIYO ni janga mpangoni.

Majuma matatu yaliyopita tulipata ujumbe kuwa Rubi Eliason na Laura Edwards waliuwawa Kameruni. Rubi alikuwa na umri uliozidi miaka 80. Akiwa pweke maisha yake yote, aliyatoa kikamilifu kwa ajili ya kitu kimoja kikuu: Kumjulisha miongoni mwa wasiofikiwa, walio masikini, na wagonjwa. Laura naye mjane, daktari wa matibabu aliyekaribia miaka 80 akihudumu pamoja na Ruby huko Kameruni. Breki zilikataa kushika, na hatimaye gari lao kuruka bonde na kuanguka, nao wakafa wawili palepale. Nami nikauliza watu wangu: Je, lile lilikuwa janga? Maisha mawili yenye msukumo mmoja kimaono, yakitumika bila kutambuliwa au kusifiwa kwa masikini wanaoangamia kwa utukufu wa Yesu Kristo—miaka ishirini baada ya karibu wenzao wote kiumri wa Marekani kustaafau na kutupa maisha yao kwa anasa kule Florida au New Mexico. La. Hio sio janga. Bali ni utukufu.

Nikueleze janga ni nini. Nitakusomea kutoka kwa Readers Digest (Feb 2000, ukurasa. 98) janga. “Bob na Penny . . . Walistaafu mapema kutoka ma kazini kwao kule kaskazini mashariki miaka mitano imepita mwanaume akiwa na miaka 59 na mwanamke 51. Sasa waliishi Punta Gorda, Florida ambako walisafiri katika chombo chao cha futi 30, kucheza softi boli na kukusanya magovu kwenye maji.” Ndoto ya amerika: Fikia mwisho wa maisha yako—maisha yako ile tu ya pekee—halafu kazi kuu yako ya mwisho kabla ya kutoa hesabu kwa muumba wako, ikawe “Nilikusanya magovu. Ona magovu yangu.” Hilo ni janga. Na watu leo wanatuma mabillioni ya madola kukushawishi ili ukumbatie ndoto hilo lenye janga. Nami Napata dakika arobaini ili kukusihi: Usishawishiwe Usitupe maisha yako. Ni mafupi zaidi na ya thamani. Nililelewa kwa nyumba ambayo babangu alijitolea kama mwinjilisti ili awaletee injili ya Yesu waliopotea. Alikuwa na maono moja ya kuteketeza: Kuhubiri injili. Kulikuwa na bango kwenye jikoni yetu kwa maisha yangu yote nikiendelea kua. Sasa liko katika sebule yetu. Nimekuwa nikiliangalia karibu kila siku kwa miaka 48. Inasema “Ni maisha moja tu, na karibuni itapita. Alichofanyiwa Kristo tu ndicho cha kudumu.” Niko hapa siku moja katika hali kama baba. Nina miaka 54. Ninao wana wa kiume wanne na binti mmoja, Karsten ni mwenye umri 27, Benjamin 24 Abraham 20, Barnabas 17 naye Tabitha ana miaka minne. Machache, kama yapo, yananijaza na tamaa zaidi hizi miezi na miaka kushinda tamaa kuwa wanangu ambao wamekuwa wakubwa wasiharibu maisha yao kwa ufanisi wenye janga.

Kwa hivyo nawatazameni ninyi kama wana na mabinti na kuwaomba kama baba—huenda baba ambaye haukuwahi kuwa naye. Au baba ambaye hakuwahi kuwa na maono kwako kama jinsi nilivyo nayo kwako na Mungu vilevile. Au baba aliye na maono kwako, lakini yake yote ni kuhusu pesa na hadhi. Ninawatazamieni kama wana na mabinti na kuwaomba. Takeni maisha yenu yatoe hesabu kwa jambo kuu na la milele. Taka hili. Msinende maishani bila ya shauku.

Sababu mojawapo ambayo imenisababisha kupenda maono ya Shauku 99 na Siku moja ni kwamba tangazo 268 ni kuhusu yote ambayo ni kusudi ya maisha yangu kwa wazi. Tangazo hili lina msingi wa Isaya 26:8— “Naam, katika njia ya hukumu zako sisi tumekungoja, Ee BWANA: Shauku ya nafsi zetu inaelekea; Jina lako na ukumbusho wako.” Hapa sio nafasi pekee, bali nafsi yenye shauku na tamaaa. Hapa sio tu tamaa ya kupendwa au softboli na makovu, hapa ni tamaa ya kitu kikuu cha kukosa kifani na cha kutosheleza zaidi ya kukosa kifani—Jina na utukufu wa Mungu— “Jina lako na sifa yako ndio tamaa ya nafsi zetu.”

Hili ndilo jambo ninaloishi kufahamu na pia ninakumbana nayo. Habari ya huduma maishani mwangu na Kanisa ninayohudumia: “Tupo—Nipo—ili kusambaza shauku kwa ajili ya utawala mkuu wa Mungu kwa vyote kwa ajili ya furaha ya watu wote.”
Sio lazima uliseme jinsi ninavyolisema. Sio lazima uliseme jinsi Louie Giglio anavyolisema (au jinsi Beth Moore anavyolisema au kama Voddie Baucham.)

Lakini chochote ufanyacho tafuta Shauku lako kisha na njia yako yakulisema na uiishie na ulifilie. Na utafanya utofauti unaodumu. Utakuwa kama mtume Paulo. Hakuna aliyekuwa na maono ya wazo moja kwa maisha yake zaidi ya Paulo au jinsi ya Paulo. Alilisema kwa njia tofauti tofauti.

Matendo ya Mitume 20:24: “Lakini sijahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyoipokea kwa Bwana Yesu, Kuishihudia Habari njema ya neema ya Mungu."

Jambo mmoja ilijalisha: Maliza kozi langu, kimbia mbio langu.

Wafilipi 3:7-8: "Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu naliyahesabu hasara kwa sababu ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kasi wa kumjua Kristo Yesu. Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo."

Nitawasaidiaje? Nitatumiwaje na Mungu wakati huu katika Siku moja ili kuamsha ndani yenu shauku moja kwa ajili ya kweli moja kuu ambayo itakuachilia na kukuweka huru kutoka kwa ndoto ndogo na kukutumia mpaka mwisho wa dahari?

Jawabu nikifikiri ambalo Bwana alinipa ilikuwa: Wapeleke kwa kifungu kimoja cha maandiko ambacho ni karibu iwezekanavyo na kati jinsi uwezavyo kufikia na waonyeshe kwanini Paulo anasema pale kile asemacho.

Kifungu hicho ni Wagalatia 6:14: “Lakini mimi hasha nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulubishwwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.

Au kuiweka kwa ubora: Onea fahari tu kwa msalaba wa Yesu Kristo. Ni wazo moja. Lengo moja. Shauku moja. Onea fahari msalaba tu. Neno linaweza kutafsiriwa kuwa, “Tukuka kwa” au “furahia kwa.” Tukuza tu kwa msalaba wa Kristo. Furahia  tu kwa msalaba wa Kristo. Paulo anasemana ikawe Shauku lako la kipekee, ona fahari tu na furaha na kutukuza. Kwa wakati huuu mkuu uitwao SIKU MOJA acha hicho KITU KIMOJA ukipendacho kitu kimoja unacho dhamini, kitu kimoja unachokisherehekea na kutukuka kwa sababu yake uwe ni msalaba wa Yesu Kristo.

Hii ni ya kushtua kwa sababu mbili.

1) Moja ni kwamba ni kama kusema: Onea fahari tu kiti kile cha umeme: Onea fahari chumba kile cha gesi ya kunyongea. Onea fahari kuchagua sindano ya sumu ya kjufisha. Kwamba na fahari yako na utukufu iwe ni kitanzi unachotiliwa. “Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo.” Hakuna aina ya kunyonywa ambao umebuniwa ambao ulikuwa wa uchungu kushinda kupigwa misumari msalabani. Ilikuwa ni jambo la kushtua. Hamungeweza kutazama—bila wewe kupiga kamsa na kuvuta nyele zako na kurarua mavazi yako. Hebu hii ikawe mojawapo ya shauku ya maisha yako.

2) Hiyo ni kitu kimoja ambacho ni cha kushtua kuhusu maisha ya Paulo. Lingine ni kwamaba anasema ua hili ndilo liwe fahari pekee la maisha yako. Furaha ya pekee. Sifa ya pekee. “Mimi hasha nisione fahari juu ya kitu chochote, ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo.” Anamaanishaje? Kweli? Hapana fahari lingine? Hapana kusifika kwingine? Hapana furaha nyingine isipokuwa msalaba wa Yesu—kifo cvha Yesu?

Je nini kuhusu sehemu zingine ambapo Paulo mwenyewe anatumia neno lile lile kwa “Kuona fahari” au “Kusifu (ka)” katika mambo mengine? Mfano:

Warumi 5:2: “NA kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.

Warumi 5:3: “Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki kazi yake ni kuleta saburi na kazi ya saburi ni kuleta uthabiti wa moyo na tumaini.”

2 Wakorintho 12:9: “Basi nitasifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi.”

1 Wathesolanike 2:19: “Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji ya kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi?”

Kwa hivyo, kama Paulo anaweza kufurahia na kuona fahari katika mambo haya yote, Paulo basi anamaanisha nini—Kwamba asione “fahari, ila katika msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo?

Lakini maanake ni nini? Je, hiyo sio kukosa msimamo? Unafurahia kitu kimoja na kusema kuwa unafurahia kingine? La. Kuna sababu kubwa sana ya kusema hivi—kwamba, furaha yote, na kuona fahari kwote katika chochote kunastahili kuwa furaha kwa sababu ya msalaba wa Yesu Kristo.

Anamanisha kwamba kwa Wakristo, kila fahari yoyote, inastahili kuwa fahari katika msalaba. Kujisifu kwote katika chochote kunastahili kujisifu katika msalaba w a Kristo. Ukifurahia matumaini ya utukufu unastahili kuwa unafurahia msalaba wa Kristo. Ukifurahia dhiki kwa sababu dhiki kazi yake ni kuleta tumaini, unastahili kujisifia msalaba wa Kristo. Ukifurahi kwa sababu ya udhaifu wako au kwa watu wa Mungu, unastahili kuwa unafurahia Msalaba wa Kristo.

Kwa nini hii ndio hali? Kwa ajili hii: Kwa wenye dhambi waliokombolewa, kila chema—naam kila kiovu ambacho Mungu angeuza kuwa chema—Kilikombolewa kwetu sisi kupitia msalaba wa Kristo. Kando na kifo cha Kristo, wenye dhambi hawapati chochote bali hukumu. Kando na msalaba wake Kristo kuna hukumu tu. Basi kila kitu ambacho unafurahia katika Kristo—kama Mkristo kama mtu anayemwamini Kristo—una deni kwa kifo cha Kristo. Na kufurahi kwenu katika yote kunafaa basi kuwe kufurahia msalaba ambapo baraka zenu zote zilinunuliwa kwa gharama ya kifo cha Mwana wa Mungu, Yesu Kristo.

Sababu mojawapo kwanini sisi hatujajiekelea na kujihusisha kwa mambo ya Kristo zaidi na kujizamisha ndani ya Kristo jinsi tunavyostahili ni kwa sababu hatujagundua kuwa kila kitu—kila kitu chema na kila kitu kiovu ambacho Mungu anageuza kuwa chema kwa ajili ya wanawe waliokombolewa kulinunuliwa kwa kifo cha Kristo kwetu. Sisi kwa urahisi tu tunachukua maisha na pumzi na afya na marafiki na kila kitu kwa mzaha. Tunafikiria ni vyetu kwa haki lakini kweli ni kuwa sio haki yako.

Sisi hatuistahili mara dufu.

1) Sisi ni viumbe na muumbaji wetu hakushurutishwa au kuwajibika kututupa chochote—Sio uzima au afya na chochote. Anapeana, anachukua wala hatutendei kisicho haki.

2) Kando na sisi kuwa viumbe bila madai yoyote juu ya Muumba wetu, tu watenda dhambi. Tumepungukiwa na utukufu wake. Tumempuuza wala hatukumtii na tukapungukiwa wala hatukumpenda na hatukumtii wala kumwamini. Ghadhabu ya haki yake iliwaka dhidi yetu. Yote Tuliyostahili kutoka kwake ni hukumu. Basi bila pumzi tunayo pumua, kila wakati moyo unapodunda, kila siku jua linapochomoza, kila wakati tunapoona kwa macho yetu na kusikia kwa masikio yetu, kusema kwa midomo yetu au kutembea kwa miguu yetu na thawabu ambayo hatukustahili, wenye dhambi waliostahili tu hukumu.

Na ni nani aliyetununulia thawabu hizi? Yesu Kristo. Na alizununuaje? Kwa damu yake.

Kila baraka maishani imeundwa ili kuinuwa msalaba wa Kristo, au kusema kwa njia nyingine, kila kitu chema maishani kinastahili kuinua Kristo na akiwa amesulubishwa. Kwa hivyo, kwa mafano tulimaliza Dodge Spirit yetu ya miaka 1991 juma lililopita, lakini hakuna aliyeumia. Na katika salama hio ninafurahi. Ninatukuka kwa hio. Lakini kwa nini hakuna aliyeumia? Hio ilikuwa ni dhawabu kwangu na familia yangu. Kwamba hakuna aliye stahili. Sisi tu watenda dhambi na kwa asili wana wa ghadhabu bila Kristo. Hivi tulifikiaje kuwa na thawabu kama hii kwa ajili ya wema wetu? Jawabu: Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu msalabani na akatuondolea ghadhabu ya Mungu, na kutuhifadhi, hata ingawa hatukustahili, neema ya Mungu iliyo na uwezo wote ambayo inafanya yote kwa wema wetu. Kwa hivyo tunapofurahi kwa usalama wetu, tunafurahia msalaba wa Kristo.

Na bima ilitulipa dola 2800 ya gari naye Noel alichukua pesa hizo na kuenda Iowa akanunua gari aina ya Chevy Lumina akaliendesha kwenda nyumbani kwenye theluji. Na sasa tuna gari tena. Nafurahia neema ya Mungu ya kushangaza kwa wingi vile. Hivyo tu unaharibu gari lako. Uondoke bila kuumia. Bima ilipie. Upate gari lingine. Na uendelee kana kwamba hapana lililotendeka. Kwa shukrani nainamisha kichwa changu na kufurahia rehema zilizofichika hata za vitu hivi vidogo vya asili. Rehema hizi zote zinatoka wapi? Kama wewe ni mtenda dhambi aliyeokolewa, anayeaamini Yesu, zinakuja kupitia msalabani. Mbali na msalaba, kunayo tu hukumu—uvumilivu na rehema kwa msimu, lakini kisha, ikitibuliwa, hayo yote rehema inaleta ongezeko la uzito wa hukumu. Basi kila dhawabu ni ile ya kununuliwa kwa damu. Na kila kuwa na fahari—kila furaha—ni kuwa na fahari kwa Msalaba.

Ole wangu mimi nikufurahia baraka zozote isipokuwa tu furaha yangu ni furaha kwa Msalaba wa Yesu Kristo.

Njia nyingine ya kusema hili ni kuwa muundo wa msalaba ni utukufu wa Kristo. Lengo la Mungu ya msalaba ni kuwa Kristo aheshimiwe Paulo anaposema katika Wagalatia 6:14, “Lakini mimi, hasha, nisione fahari kwa kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo,” Anasema kuwa mapenzi ya Mungu ni kwa amsalaba uinuliwe—kwamba Kristo aliyesulubiwa daima awe ndio fahari yetu na furaha na shangwe na sifa zetu—kwamba Kristo apate utukufu na shukran na heshima kwa kila chema maishani mwetu—na kila kiovu Mungu anachogeuza na kuwa chema.

Lakini sasa hapa kwa swali: Kama ni lengo la Mungu kuwa kifo cha Kristo—jina, kule “Kusulubiwa Kriisto” kuheshimiwe na kutukuzwe kwa mambo yote basi je, itakuwaje Kristo akapate utukufu anayostahili? Jawabu ni kwamba watoto wa ujana na watu wazima lazima wafundishwe kwamba mambo haya ni vile. Au tuseme tofauti: Chanzo cha furaha kwa msalaba wa Kristo ni elimu kuhusu msalaba wa Kristo.

Hiyo ndio kazi yangu: kutafutia Yesu utukufu kwa kuwafundisha  mambo haya. Kisha ndipo kazi yenu ni kutafuta uutukufu zaidi kwa Yesu kwa kuyatenda na kufundisha watu zaidi kuyahusu. Elimu kumhusu Yesu ni kwa kufurahia Yesu. Na tukitaka furaha isipatikane isipokuwa kwa msalaba, basi lazima tufuate elimu kuhusu msalaba—na chini ya msalaba.

Au huenda twafaa kusema, “kwenye msalaba.” Elimu kuhusu msalaba kwa furaha ya msalaba. Namaanisha nini?

Hebu angalia mlango wa 14 uliosalia: “Lakini mimi, hasha nisione fahari cho chote ila msalaba wa Bwana Yesu ambao kwa huo ulimwengu umesababishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.” Fahari kwa msalaba hutendeka wakati upo msalabani. Je, si hivyo inavyosema mlango wa 14? Ulimwengu umesulubishwa kwangu, nami nimesulubishwa kwa ulimwengu. Ulimwengu kwangu umekufa nami kwa ulimwengu nimekufa. Kwa nini? Kwa sababu nimesulubiwa. Tunajifunza kuona fahari kwa msalaba wa kufurahia msalaba wakati tukiwa msalabani.

Sasa nini maana ya hayo? Yalitendeka lini? Je ulisulubiwa lini? Jibu li katika Wagalatia 2:20, “Nimesulubiwa na Kristo; Lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” Kristo alipokufa, tulikufa maana utukufu wa kifo cha Kristo ni kuwa alipokufa, wote wake wakafa pia ndani yake. Kifo hicho, alichotufilia sote, inakuwa kifo chetu tukiunganika na Kristo kwa imani.

Lakini unasema, “Si nihai? Najihisi kwa hai.” Sawa hapa kuna haja ya elimu. Lazima tujifunze kilichotutendekea. Lazima tufundishwe mambo haya. Ndiposa Wagalatia 2:20 na 6:14 ziko kwenye Bibilia. Mungu anatufundisha kilichotutendekea, ili tuweze kufahamu wenyewe na tufahamu  njia yake ya kutenda kazi nasi na kufurahi ndani yake na mwanaye na katika msalaba tunavyopaswa.

Kwa hivyo tunasoma Wagalatia 2:20 tena ili tuone hayo, Naam tu wafu na ndio tu hai. “Nimesulubiwa pamoja na Kristo [Hivyo mimi ni mfu, naye anaendelea]; Wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu [kwa nini? Kwa sababu nilikufa, kwamba, utu wangu wa kale wenye uasi, usio amini ulikufa, na kisha anaendelea]; na maisha ninayoishi sasa katika mwili

Kwa hivyo, ndio, ni hai, bali sio “mimi” wa kale yaani “mimi” aliyekufa] Naishi kwa imani ndani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kutoa uhai wake kwa ajili yangu. Ama tuseme “mimi” aishiye ni “mimi” mpya wa imani. Kiumbe kipya anaishi. Anayeamini anaishi. Utu wangu wa kale ulikufa msalabani na Yesu.

Na ukiniuliza, “Wapi funguo za kuunganisha na kweli huu? Haya yatakuwaje yangu? Jibu limeonyeshwa katika maneno ya imani katika Wagalatia 2:20, “Na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu. Hiyo ndio unganisho. Mungu anakuunganisha na Mwanaye kwa imani. Na afanyapo vile kuna umoja na mwana wa Mungu kwamba sasa kifo chake kinafanyika kuwa kifo chako na uhai wake kuwa wako. Sasa beba hayo yote mpaka kwa Wagalatia 6:14, “Lakini mimi hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulubiwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu. Usionee chochote fahari ila tu msalaba.

Na sasa nawezaje kufikia kuwa kwamba ni wa kuvutiwa kabisa na msalaba—ili kwamba furaha yangu yote inaweza kufuatiwa na kurejea msalabani? Jibu: tambua kuwa Krsito alipokufa msalabani hata nawe ulikufa; Na ulipomwamini, kifo hicho kikaiathiri maisha yako. Paulo anasema, ni maisha yako kwa ulimwengu na cha ulimwengu kwako.

Maanake: unapoweka imani yako yako kwa Kristo, ufungwa wako kwa ulimwengu nao unavunjika. Wewe ni kiwiliwili kwa ulimwengu na ulimwengu kwako vile vile kiwiliwili. Au kwa njia bora, kulingana na mlango wa 15, wewe ni “kiumbe kipya.” Wewe wa kale ni mfu. Wewe mpya uhai. Na wewe mpya ni wewe wa imani. Na imani inafurahia kisicho cha ulimwengu, bali Kristo, na sana sana Kristo aliyesulubiwa.

Ni hivi ndivo unafanyika kuwa unavutiwa zaidi na msalaba. Kiwango cha kusema pamoja na Paulo, “Hasha sitaonea fahari chochote, isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo.” Ulimwengu sio tena hazina yangu. Sio tena chanzo cha maisha yangu na kutosheleka kwangu na furaha yangu. Ni Kristo.

Lakini nini kuhusu usalama katika ajali ya gari? Nini kuhusu malipo ya bima? Si ulisema ulifurahia hayo? Si hayo ni ya ulimwengu? Kwa hivyo je, umefia ulimwengu?

Yawezekana. Ninatumaini hivyo. Kwa sababu kufia ulimwengu haimaanishi kuondolea ulimwenguni. Na haimaanishi kutohisi mambo ya Ulimwengu. Mengine maovu mengine bora (Waraka wa kwanza na Yohana 2:15; 1 Timotheo 4:3). Maanake ni kwamba kila raha halali ulimwenguni inakuwa ushahidi wa pendo la Kristo ulionunuliwa kwa damu, na fursa ya kuonea, fahari msalaba. Tumekufia malipo ya bima kama pesa hizo hazitutoshelezi, lakini Kristo aliyesulubiwa, mpaji, anatosheleza mioyo yetu inapokimbia katika mwale wa baraka mpaka kwa chanzo chake msalabani, kisha ule uulimwengu wa baraka hizo umekufa, naye Krsito aliyesulubiwa ni vyote.

Ndilo hilo lengo la elimu kwa furaha. Kwa msalaba. O naye Mungu akapate kututimizia kuota ndoto na kupanga na kufanya kazi na kupeana na kufundisha na kuishi kwa ajili ya utukufu wa Kristo naye amesulubiwa!