Kuitwa kuteseka na kufurahi: kwa uzito wa utukufu wa milele

Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala sio kutoka kwetu. Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; twaudhiwa, bali hatuachwi, twatupwa chini, bali hatuangamizwi; siku zote twachukua katika mwili kuuwawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu. Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti. Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu. Lakini kwa kuwa tuna roho ile ile ya imani; kama ilivyoandikwa. Niliamini, na kwa sababu hiyo nalinena; sisi nasi twaamini; tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu, na kutudhihirisha pamoja nanyi. Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe. Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi—iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele

Mstari wa 16 unafafanua kitu ambacho kila mtu asubuhi hii anataka kushuhudia. Paulo anasema, “Hatulegei, bali utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.” Kuna kitu hapa ambacho hakuna anayekitaka na kitu ambacho kila mtu anataka.

Kitu ambacho hakuna atakaye na ambacho kila mtu anataka

Asubuhi ya leo hakuna anayetaka kukata tamaa. Hakuna aliyekuja hapa akisema, “Kweli natumai tuimbe nyimbo na tuskize ujumbe ambayo yatanisaidia kukata tamaa. Nataka kabisa asubuhi ya leo kushushwa na kile John anasemacho. “Siyo mmoja wenu. Hakuna anayetaka moyo wa kuishi utolewe ndani yako. Hata Paulo naye hakutaka.

Kinyume na hayo, kila mtu anataka kufanywa upya ndani yake siku baada ya siku. Sote twajua kwamba, hisia za nguvu na upya na tumaini na ubora wa uhodari na ari ya maisha hudumu kwa muda kidogo tu, na kisha zina potelea mbali. Kama tutakuwa na nguvu upande wa ndani na tuwe na tumaini na furaha na akiba ya upendo, tunaenda kufanywa upya siku baada ya siku. Twafahamu hilo. Maisha sio imara au haibadiliki kwa kimo. Maisha yana panda—shuka. Ni kujaza na kupunguza na kujaza tena. Ni upya, zeeka, upya, na zeeka na upya. Na kila mmoja wetu anahitaji nguvu za kufanya upya. Hakuna anyetaka kuachwa katika bonde la kupotea na utupu na kushushwa. Kama kuna siri ya kufanywa kuwa na nguvu na mwenye tumaini na mwenye furaha ana kupenda tena na tena siku baada ya siku, sisi twa tamani.

Maneno mawili yenye uzito: “kwa hiyo” na “maana”

Ina maanisha kuwa kuna maneno mawili kwenye fungu hili ambayo yanastahili kutumakinisha. Neno “kwa hiyo” katika mwanzo wa mstari wa 16 na neno “maana” katika mwanzo wa mstari wa 17. Kwa nini yaana uzito hivyo?

Mstari wa 16 kama kilele cha pembe tatu

Wazia mstari wa 16 juu ya pempe tatu ikiegemea pande mbili. Kwa hiyo tamaa yetu ikishikiliwa na mistari hizi mbili: “Hatulegei . . . lakini utu wetu wa ndani wafanywa upya siku baada ya siku.” Hilo ndilo sote twataka asubuhi hii—kuweza kusema hilo na kumaanisha kabisa.

Mstari wa 16: Hatulegei . . . lakini twafanywa upya siku baada ya siku.

Mstari wa 7-15 kama upande mmoja ukishikilia upande wa juu

Neno “kwa hiyo” mbele ya mstari huu ina maanisha kuwa Paulo amekuwa akisema vitu vingine ambavyo vilimwongoza kwa ufahamu huu na kuunga mkono: “hii ni kweli, ni kweli, ni kweli” katika mstari wa 7-15, “KWA HIYO hatulegei . . . KWA HIYO tunafanywa upya siku baada ya siku.” Kwa hivyo mstari wa kwanza wa pembe tatu ni ukweli wa mstari wa 7-15 ambao watuelekeza kwa tajriba hii ni kuunga mkono. Hiyo inayotumakinisha na kutufanya tutafute kwenye mistari hiyo ni nini. Labda ya maanisha kwetu pia!

Mstari wa 17-18 kama upande mmoja ukishikilia upande wa juu

Halafu neno “maana” mwanzoni wa mstari unaofuata (v. 17) inamaanisha kuwa Paulo yuko karibu kusema vitu ambavyo ni sababu ya mstari wa 16. “Hatulegei . . . na twafanywa upya siku hadi siku . . . MAANA (SABABU) hii ni kweli, ni kweli, ni kweli. Kwa hivyo mstari wa pili wa pembe tatu unaoteremkia upande ule mwingine ni ukweli wa mstari wa 17-18 ambao unaunga mkono tajriba ambayo ameieleza.

Je, waweza kuiona sasa? Tajriba ambayo twahitaji iko pale kwenye pembe tatu ikiegemea pande mbili za pembe hiyo tatu. Mstari 7-15 ni kweli, “KWA HIYO hatulegei lakini twafanywa upya siku hadi siku. “Hiyo ni pande moja. “Hatukati tamaa, lakini twafanywa upya siku hadi siku” MAANA mstari 17-18 ni kweli. Kwa hivyo lengo letu ni kuangalia pande mbili za hii pembe tatu kisha tupate ukweli ambao ulimsimamisha Paulo na ukweli ambao unatusimamisha sisi.

Mstari wa 16 hufanyika katikati ya kuteseka

Lakini kwanza chunguza kidogo: Msari wa 16 watambua kuwa sio kukata tamaa na kufanywa upya vya fanyika katikati ya kuteseka. “Hatulegei, lakini ingawa mwili wa nje wa dhoofika, mtu wa ndani anafanywa upya siku hadi siku. Paulo alijua kwamba atakufa na kwamba kila mtu atakufa. Aliyapitia mateso mengi, na kwa hayo akaona kuoza na kuishi kwa maisha ulimwenguni. Kulikuwa na unyonge na magonjwa na majeraha na ugumu na presha na kuvunjwa moyo na kushushwa moyo. Na kila moja ya hayo ilimgharimu maisha yake. Njia moja ya kuisema ilikuwa “mauti inafanya kazi ndani yake” (ona. ms. 12).

Hiyo ilikuwa fungu la kusema, “Hatulegei . . . tunafanyika upya daima.” Kwa hivyo kile tunauliza saa hii sio tu, “Jinsi gani naweza kusimama maishani?” na “Jinsi gani naweza kufanywa upya siku hadi siku?” lakini” Jinsi gani naweza kujiandaa kuteseka bila kukataa tamaa?” “Jinsi gani naweza kukubali kudhofika mwilini mwangu na maisha yangu ya ulimwengu kunyauka bila kukata tamaa, lakini nipate kufanywa upya nguvu za ndani kwendelea kwa furaha hadi mwisho na matendo ya upendo?

Sasa tuko tayari kuyaona majibu ya Paulo kwa maswali haya. Kwanza katika mstari wa 7-15 na pia msari wa 17-18.

Mstari wa 7-15: Sababu nne za kutolegea

Katika mstari wa 7-15 kuna karibu sababu nne ambazo zilimsababisha Paulo kusema “ KWA HIYO hatulegei.” Na kila moja inatoa hesabu ya kutoweka kwa maisha yake ya ulimwengu. Hakosi kuona kuwa yeye ni mtu anayekufa na kuwa maisha yake yanazidi kunyauka. Kwa hivyo kile anachofanya kwenye mstari huu ni kuonyesha kilicho kweli hata ingawa, na pia kwa sababu utu wake wa nje unadhoofika na kupotelea mbali.

1. Kutukuka kwa nguvu za mungu na mwana wa Mungu

Kwanza, ingawa utu wake wa nje unachakaa kupitia kwa mateso haya nguvu za Mungu na maisha ya Mwana wa Mungu yana dhihirika na kutukuzwa.

Mstari wa 7: “LAKINI tuna hazina katika vyombo vya udongo [hiyo ni utu wa nje unaochakaa na kuwa dhaifu], kuwa nguvu kuu upitao zote uwe wa Mungu lakini sio kutoka kwetu sisi. KWA HIYO hatulegei . . . sababu nguvu za Mungu zimeinuliwa kwa unyonge wetu.

Mstari wa 10: “Siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu [hii ni sababu nyingine ya kuchakaa kwa mtu wa nje] ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu. “KWA HIYO hatulegei . . . sababu maisha ya Mwana wa Mungu yameinuliwa kwa kufa kwetu kila siku.

Mstari wa 11: “Kwa maana sisi tulio hai, siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika miili yetu ipatikanayo na mauti.” KWA HIYO hatulegei . . . ’sababu maisha ya mwana wa Mungu yanadhihirika na kutukuka ndani ya miili yetu inayo chakaa

Hivyo sababu ya kwanza Paulo hakati tamaa, kwa kuwa mtu wake wa nje unachakaa, hiyo ni kwa udhaifu wake na kufa kwake kila siku kwa ajili ya wengine nguvu za Mungu na maisha ya mwana wa Mungu yanatukuka na hilo ndilo Paulo anapenda kuliko chochote.

2. Kutiwa nguvu kwa kanisa

Pili, ingawa utu wake wa nje unachakaa, bali kwa na kupitia mateso haya maisha yanatiririka kutoka kwake hadi kwa Kanisa. Wakristo wanatiwa nguvu na kufanywa dhaifu kwa Paulo.

Mstari wa 12: “Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu. “KWA HIYO hatulegei . . . sababu sio Mungu pekee anayetukuka, bali ninyi, wapendwa wangu, mnapokea maisha na nguvu na matumaini.

Mstari wa 15: “Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi [kupitia mateso ya Paulo kwa ajili yao] yaweza kusababisha shukrani kwa utukufu wa Mungu uliojaa. “KWA HIYO hatulegei . . . sababu (na tia maanani jinsi mstari wa 15 unavyoeleza sababu mbili za kwanza pamoja) katika huduma yangu ya mateso neema inafika kwenu na utukufu unamwendea Mungu. Hizi ndizo pendo kuu katika maisha ya Paulo: kuleta neema kwa wengine na kuleta utukufu kwa Mungu—na mstari huu unaeleza kuwa yanafanyika kwa mapito sawa. KWA HIYO Paulo halegei.

3. Uwepo wa Mungu unaohuisha

Tatu ingawa mwili wake wa nje wachakaa, kupitia kwa mateso haya Mungu anamsimamisha wala hajamuacha kushindwa.

Mstari wa 8-9 (Kumbuka kwa haya mawili anachomaanisha hasa ni: Ndio utu wa nje wachakaa lakini, La, hatukati tamaa): “Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi.” KWA HIYO hatulegei . . . Maana Mungu anatusimamisha na hatuachi kushindwa.

4. Ufufuo wetu kutoka kwa wafu

Nne, ingawa utu wa nje wa chakaa, ilhali atafufuliwa kutoka kwa wafu pamoja na kanisa na kuwa pamoja na Yesu.

Mstari wa 14: “[Tukijua] kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua nasi pamoja na Yesu na kutuhudhurisha pamoja nanyi.” KWA HIYO hatulegei . . . sababu yote yatakua sawa. Hata mauti hayawezi kutengeneza hadithi inayo mwisho mbaya. Nitaishi tena; na nitaishi nayi, watu ninao wapenda; na nitaenda kuishi na Yesu na kushiriki utukufu wake milele na milele.

KWA HIYO . . . Huo ni mstari wa kwanza wa Pembe tatu (mstari wa 7-15) ambayo inaunga mkono mapito makuu ya kutokata tamaa lakini kufanywa upya kila siku.

  1. Ninafanywa upya sababu nguvu za Mungu na maisha ya mwana wa Mungu yanadhihirika na kutukuka kwa kuchakaa na udhaifu wangu.

  2. Ninafanywa upya maana maisha yanasonga kutoka kwa mateso yangu hadi kwa kanisa ambalo napenda sana.

  3. Ninafanywa upya maana Mungu ananisimamisha katika mateso na haniachi kushindwa

  4. Ninafanywa upya maana najua nitafufuliwa kutoka kwa wafu pamoja nawe na pamoja na Yesu kuishi pamoja milele na milele.

KWA HIYO silegei!

Mstari wa 17-18: Sababu Nne za Kutolegea

Sasa tazama upande mwingine wa mstari wa pembe tatu unaounga mkono tajriba ya Paulo katika mstari wa 16, kwa jina, mistari ya 17-18. Yeye halegei, bali anafanywa upya siku hadi siku MAANA mstari wa 17-18 ni kweli. Tena kuna sababu nne za Paulo kutolegea hata ingawa utu wake wa nje unachakaa—udhaifu wake wa magonjwa yake na majeraha na ugumu maishani.

1. Dhiki ya Muda

Yeye halegei MAANA dhiki yake ni ya muda wa kitambo kidogo tu.

Mstari wa 17 “Maana dhiki yetu nyepesi iiyo ya muda kitambo kidogo tu . . . Hii haimanishi ni jambo la sekunde 60. Inamaanisha kuwa ni ya maisha haya tu (ambayo ni kitambo kidogo tu ukilinganisha na miaka milioni na mamilioni) na ni hiyo tu. Neno lamaanisha “Saa hii”—“Dhiki wa wakati huu”—dhiki ambayo haitaishi kuzidisha maisha ya sasa hivi. Sifi moyo . . . MAANAKE dhiki yangu itakwisha. Haitakuwa na usemi wa mwisho katika maisha yangu.

2. Dhiki nyepesi

Yeye halegei MAANA dhiki yake ni nyepesi

Mstari wa 17: “Maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya muda kitambo tu kidogo” . . . Hii sio hukumu ya starehe ya Amerika ya sasa. Hii ni hukumu ya Paulo mwenyewe. Ama Paulo amesahau alichosema kwa 2 Wakorintho 11:23-27.

Je, wao ni watumishi wa Kristo ? Nanena kiwazimu, mimi ni zaidi yao: Nimefanya kazi kwa bidii kuliko wao, nimefungwa gerezani mara kwa mara, nimechapwa mijeledi sana, nimekabiliwa na mauti mara nyingi. Mara tano nimechapwa viboko arobaini kasoro kimoja na Wayahudi. Mara tatu nalichapwa kwa fimbo, mara moja nalipigwa kwa mawe, mara tatu nimevunjikiwa na meli, nimekaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa. Katika safari za mara kwa mara, hatari za kwenye mito, hatari za wanyang'anyi, hatari kutoka kwa watu wangu wenyewe, hatari kutoka kwa watu Mataifa, hatari mijini, hatari nyikani, hatari baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi, ninajua kukaa njaa na kuona kiu, nimekaa mara nyingi bila chakula, Nimesikia baridi na kuwa uchi. Zaidi ya hayo yote, nakabiliwa na mzigo wa wajibu wangu kwa makanisa yote.

Paulo anaposema dhiki yake ni nyepesi, haimaanishi rahisi ama isiyo na uchungu. Anamaanisha kuwa ukilinganisha na yanayokuja hiyo sio kitu. Kulinganisha na uzito wa utukufu unaokuja, ni kama manyoya kati ya kipimo” (Warumi 8:18) “Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.” Sitalegea . . . MAANA dhiki yangu si nyepesi.

3. Uzito wa Utukufu wa Milele

Hakati tamaa MAANA dhiki yake hakika inamzalia Paulo uzito wa utukufu wa milele wala hakuna kifani.

Mstari wa 17: “Maana kitambo tu, dhiki nyepesi yatuzalia uzito wa utukufu wa milele bila kifani.” Kile kinachomjia Paulo sio cha kitambo tu, lakini cha milele. Sio nyepesi, bali ni kizito. Sio dhiki, bali utukufu. Na kimeshinda mazito yote. Wala jicho halikuyaona, sikio halikuyasikia yale Mungu ameandalia wanao mpenda (1 Wakorintho 2:9)

Na lengo sio tu kwamba dhiki huleta utukufu; zinasaidiana kuzaa utukufu. Kuna muungano wa kweli kati ya jinsi tunavyostahimili ungumu saa hii na vile tutaweza kufurahia utukufu wa Mungu katika miaka zijazo. Hakuna hata dakika moja ya uchungu tuliovumilia imepotezwa. Silegei . . . MAANA shida zangu zote zinanitengenezea uzito wa utukufu wa milele usioweza kulinganishwa.

4. Utukufu wa milele unaokuja usioonekana

Paulo halegei MAANA ameweka mawazo yake kwa utukufu wa milele usio na kipimo.

Mstari wa 18: “Tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana.” Mungu anaweza kukupa utukufu wote wa ulimwengu kukuzuia kulegea na kufanya upya nafsi yako siku hadi siku, lakini kama hukuiangalia, hakuna fida itakachotoka.

Mwaliko wa Mungu wa kifahari

Na hivyo ndivyo Mungu anavyofanya sasa hivi katika somo hili. Hili fungu ni mwaliko wa kifahari kutoka kwa Mungu kwako kuona sababu zote za kutolegea—sababu zote kwa nini ufanywe upya siku hadi siku.

  • Tazama! Nguvu za Mungu na maisha ya mwana wake zinadhihirika kwa unyonge wetu.

  • Tazama! Maisha ya Yesu yanatiririka kupitia kwa kuteseka kwetu mpaka katika maisha ya wengine.

  • Tazama! Mungu anakusimamisha kwa dhiki yako na hakuachi uangamizwe.

  • Tazama! Dhiki yako haitakuwa na neno la mwisho; Utafufuka kutoka kwa wafu na Yesu Pamoja na Kanisa la Mungu na kuishi kwa furaha milele na milele.

  • Tazama! Dhiki yako ni ya kitambo kidogo tu. Ni ya sasa tu, sio ya miaka zinazokuja.

  • Tazama! Dhiki hii inatuletea utkufu wa milele uzidio vitu vyote.

Hivyo TAZAMA! Angalizia! Tafakari! Fikiri juu ya mambo haya. Amini Mungu asemacho. Nawe hautalegea bali utu wako wa ndani utafanywa upya siku hadi siku.