Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Bwana wa majeshi

Mnamo Tarehe 1, Juni, 1973, Charles Colson alitembelea rafiki yake Tom Phillips, Wakati sakata ya watergate ilipolipuka kwenye vyombo vya habari. Alishangazwa na kushtuliwa na maneno ya Phillips  kuwa alikuwa “ amekubali Yesu kristo.” Lakini aliona kuwa Tom alikuwa katika hali ya utulivu na yeye hakuwa. Wakati Colson alitoka kwa nyumba yake, hangeweza kupata ufunguo wa gari lake na akalia kwa uchungu. Anasema,

Usiku huo nilikumbana na dhambi zangu—sio tu sakata ya Watergate, lakini dhambi ndani mwangu, uovu uliojificha na ambao huishi moyoni mwa kila binadamu. Zilikuwa chungu na sikuwa nikiweza kuziepuka. Nilimlilia Mungu na kujipata kama nimevutwa mikononi mwake. Huo ndio usiku nilimkabidhi Yesu Kristo maisha yangu na kuanza safari kuu ya kusisimua katika maisha yangu. (Loving God, p. 247).

Ufahamu mpya wa Mungu wa Charles Colson

Hadithi hii imesimuliwa zaidi ya mara mia moja kwa muda ya miaka kumi iliyopita. Tunapenda kuisikiza. Lakini wengi wanaichukulia hadithi hii kulingana na maisha yetu na ya Kanisa. Lakini si ya Charles Colson. Sio tu kuwa yule alileta sakata katika White House Mwaka wa 1973 yuko tayari kulia; pia alikuwa tayari kutubu miaka kadhaa baadaye juu ya mitazamo mibaya ya Mungu. Ilikuwa wakati wa kiangazi usio wa kawaida wa kiroho. (kama uko katika hali hiyo, jipe moyo! Watakatifu wengi wanafahamu kukumbana na matukio yanayobadilisha maisha na pia Mungu wakiwa katikati mwa jangwa). Rafiki akamshawishi Colson kutazama mkanda wa video ya mafundisho ya R.C Sproul unaohusu utakatifu wa Mungu. Hapa ni yale Colson anaandika kwenye kitabu chake kipya, Loving God (pp 14-15).

Yale nilijua kuhusu Sproul ni kwamba alikuwa mwanatheolojia, kwa hivyo sikuwa na hamu. Nilijisemesha, theologia ni ya watu ambao wako na muda wa kusoma, wakiwa wamejifungia katika vyumba vya kifahari mbali na uwanja wa vita vya mahitaji muhimu ya kibinadamu. Lakini kwa himizo la rafiki yangu nilikubali kutazama kanda za Sproul.

Kufikia mwisho wa mafundisho ya sita, nilikuwa magotini mwangu, ndani ya maombi, nikishangazwa na utakatifu mkuu wa Mungu. Ilikuwa kisa cha kubadilisha maisha kwa kuwa nilipokea ufahamu mpya na wa kipekee juu ya Mungu ninayemwamini na kumwabudu.

Ukavu wangu wa kiroho ukakomea, ingawaje huo ladha wa ukuu wa Mungu ulinifanyasha niwe na kiu zaidi ya kumtaka.

Ufikapo mwaka wa 1973 Colson alikuwa ameona ya kutosha kutoka kwa Mungu na kwake, kujua alihitaji Mungu kwa dharura na kuvutwa bila “kukataa” (ananvyosema) hadi mikononi mwa Mungu. Lakini miaka mingi baadaye, jambo lingine la kushangaza likatendeka. Mwanatheologia fulani aliongea kuhusu utakatifu wa Mungu na Charles Colson anasema, alijiangusha tena magotini mwake na “akapokea ufahamu mpya wa kipekee wa Mungu mtakatifu.” Kutokea hapo alikuwa na kile anachokiita, “ladha ya ukuu wa Mungu”. Je umeona utukufu wa Mungu kiasi cha kuwa na hamu isiyo ya kawaida ya ukuu Wake?

Ayubu aona Mungu kwa upya

“Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye jiana lake aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuiwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu, alimcha Mungu na kuepuka Ubaya” (Ayubu 1:1). Ayubu alikuwa mwenye imani, msalimina na mtu wa maombi. Kweli alijua Mungu kwa uwezo wake. Kweli, “alikuwa ameonja ukuu wa Mungu”. Lakini kukaja dhiki na taabu katika maisha yake ya kiroho na akawa kwa jangwa ya kimwili. Na katikati mwa giza ya Ayubu, Mungu akaongea kwa ukuu wake kwa Ayubu:

Je, hutasadiki hukumu yangu? Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe? Je una mkono kama wa Mungu? Nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama Yake? Basi jivike mwenyewe utukufu wa fahari … Tazama watu wote walio na kiburi na uwanyenyekeze, waponde waovu mahali wasimamapo … Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa … Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu Mimi? Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa? Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu. (40:8-14; 41:10-11)

Mwishowe Ayubu anajibu, kama Colson, kwa “ufahamu upya, kamilifu, wa Mungu mtakatifu.”

Anasema, hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi, mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua … masikio yangu yamesikia habari zako, lakini sasa macho yangu yamekuona; kwa hiyo najidharau mwenyewe na kutubu katika mavumbi na majivu (42:3-6).

Uvumilivu na tumaini katika kutafuta Mungu mtakatifu

Je, hao yanaweza kufanyika Bethlehemu? Inaweza na inatendeka. Nisineliona dalili yeyote, ninefiwa na hamu ya kuendelea inawaje ninajua uvumilivu ndio chanz cha ufufuo. A.J. Gordon aliandika katika kitabu chake, The Holy Spirit in Missions. pp 139, 140:

Ilikuwa miaka saba kabla ya Carey kubatiza muhumini wake wa kwanza nchini India; ilikuwa miaka saba kabla Judson kupata mwanafunzi wa kwanza nchini Burma; Morrison alifanya kazi kwa bidii miaka saba kabla Mchina wa kwanza kuja kwa Yesu; Moffat alikiri kwamba alinena miaka saba kuona nguvu za roho mtakatifu ukitawala juu ya watu wa Bechuana barani Afrika. Henry Richards alihudumu kwa miaka saba nchini Congo kabla ya mtu wa kwanza kuokoka kujitokeza Banza Manteka.

Uvumilivu, maombi na bidii, ndiye ufunguo wa ufufuo. Lakini pia tarajio na tumaini. Mungu amenipa dhihirisho la tumaini kuwa matukio ya Isaya, Ayubu na Charles Colson yanaweza tukia hapa tukiendelea kutafuta kwa bidii Mungu Mtukufu. Kwa mfano, mmoja wetu aliniandikia barua wiki moja uliopita akisema kuwa huduma hapa

imechukua nyakati za kale za shida, yale niliyachukua kama vilele vya milele, kuwa makuu sana, na ya ajabu, picha yenye utukufu mkuu ya Mungu akiwa juu kuliko vile nilivyofikiria … Mtazamo wangu kwa mungu unaendelea kupanuka zaidi kupitia utukufu wake upatikanapo kila pahalikila kitu kinaendelea , antosha katika yote. Kwa miezi kumi nimekuwa Bethlehemu kumekuwa na ufunuo wa ajabu moyoni mwangu na mwoto unaungua na kuangaza na kwa hakika kuliko vile ilivyo kuwa.

Ufufuo unafanyika wakati tunaona Mungu mkuu katika utukufu, na wakati tunajiona kama mavumbi ya kutotii. Kuvunjika, kutubu, furaha wa msamaha usiosemekana, “Kionjo cha utukufu wa Mungu,” njaa ya utakatifu wake – kuiona zaidi na kuiishi zaidi: hiyo ndiyo ufufuo. Na huja kupitia kuona Mungu.

Mitazamo Saba ya Mungu Katika Maono ya Isaya

Isaya anatualika kushiriki naye katika maono yake juu ya Mungu katika Isaya 6:1-4.

Katika mwaka ule mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza hekalu. Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa menngine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka. Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu, Dunia yote imejaa utukufu wake.” Kwa kutoa kwao sauti miimo ya milango na vizingiti vilitikisika, nalo hekalu likajaa moshi.

Mitazamo ya Mungu ninayaona katika mistari nne nao ni kama saba.

1. Mungu yu Hai

Kwanza yu hai. Uzia tayari amekufa, lakini Mungu anaendelea kuishi. “Wewe ni Mungu tangu milele hata milele” (Zaburi 90:2). Mungu alikuwa Mungu hai kabla dunia kuumbwa. Alikuwa Mungu aishiye wakati Socrates alikunywa sumu. Alikuwa Mungu aishiye wakati William Bradford alipotawala Ukoloni wa Plymouth. Alikuwa Mungu aishiye mwaka wa 1966 wakati Thomas Altizer alitangaza kuwa Amekufa na Gazeti La Time likamweka kwenye ukurasa wa kutangulia. Atakuwa akiishi hata miaka trilioni kumi ijayo kutoka sasa wakati wale wanaompinga watakuwa wameangamia kama BB kilindini mwa Bahari la Pacific. “Katika mwaka ule mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana.” Hakuna kiongozi wa nchi hata mmoja ambaye atakuwa hai katika muda wa miaka 50 ijayo.mabadiliko katika uongozi ulimwenguni ni aslimia mia mmoja. Kwa ufupi, miaka 110 dunia hii itajaa na idadi ya watu bilioni kumi ambao ni wapya na bilioni nne ambao wanaishi leo watakuwa wametoweka duniani kama Uzia. Lakini sio Mungu. Hakuwa na mwanzo na hivyo basi hatategemea kitu chochote kwa kuishi kwake. Amekuwa na atazidi kuwa hai.

2. Mungu ni mwenye mamlaka

Ya pili, ni mwenye mamlaka. “Nikamwona Bwana akiwa ameketi katika kiti cha enzi.” Hakuna maono ya mbingu ambayo yameona Bwana akilima uwanjani, ama akifyeka nyasi ama akipiga viatu rangi ama akijaza ripoti ama kupanga mizigo kwenye gari. Mbingu haiporomoki pahali imeshonewa kwayo. Mbingu hauraruki. Mungu hayuko katika ubishi na mambo yake ya kiroho ya mbinguni. Ameketi. Na anaketi kwenye kiti cha enzi. Yote yako katika hali ya amani na anatawala.

Kiti cha enzi ni haki yake ya kutawala dunia. Hatumpatii Mungu mamlaka juu ya maisha yetu. Anayo, tupende, tusipende. Ni upumbavu kujifanya kana kwamba tulikuwa na haki yoyote kuita Mungu kujibu maswali. Inatupasa tusikie maneno matupu sasa na hata baadaye kama ya Virginia Stem Owens ambaye alisema mwezi uliopita katika nakala ya Reformed Journal.

Wacha tukalipokee jambo mmoja kwa hakika. Mungu anaweza kufanya jambo lolote alilolipenda, na tena kwa njia nzuri. Ikimfurahisha kuharibu, basi ni hivyo, linakuwa hivyo. Matendo ya Mungu ni vile yalivyo. Hakuna kitu chochote. Bila Yeye hakungelikuwa kiumbe chochote, wakiwemo pia wanadamu ambao wanafanya kumhukumu Muumba wa vitu vyote vilivyo.

Mambo machache ni ya kunyenyekeza, mambo machache yanatupa wazo la ukuu, kuwa kweli Mungu ni mwenye mamlaka yote, Ni mahakama kuu la kisheria, na afisa mkuu mtendaji. Badala Yake hakuna kukata rufaa.

3. Mungu ni mwenye enzi

Ya tatu, Mungu ni mwenye enzi. Kiti chake cha enzi si mmoja kati ya nyingine nyingi. Ni juu na kimetukuzwa sana. “Nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kimetukuzwa sana.” Kwa kuwa kiti cha enzi ni kuu kuliko vyote inadhihirisha nguvu za ajabu za Mungu ya kutumia mamlaka yake. Hakuna mamlaka inayoweza kupinga amri za Mungu. Kile amekusudia, anakitimiza. “Kusudi langu ndilo litakalosimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote” (Isaya 46:10). “Hufanya kama atakavyo kwa majeshi ya mbingu na kwa mataifa ya dunia. Hakuna anayeweza kuzuia mkono wake” (Danieli 4:35). Kushikwawa uenzi (ama ukuu) wa Mungu ni ya ajabu mno kwa sababu yu upande wetu na inashtua sababu ya kupinga kwetu. Ukuu wa mamlaka wa Mungu aishiye ni kimbilio lenye furaha na nguvu kwa wale wanaohifadhi ahadi zake.

4. Mungu anang’aa

Ya nne, Mungu anangaa. “Nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likijaza hekalu.” Umeona picha za mabibi wa harusi, mapindo ya joho lao likiwazingira na linafunika hatua yao na jukwaa. Maana inaweza kuwaje kama pindo la joho lingejaza jukwaa, viti na eneo lililotengewa waimbaji, lote likiwa pindo lililoshonwa kwa pamoja? Kuwa pindo la joho la Mungu linajaza hekalu la mbingu linamaanisha kuwa Mungu ni wa mngaro usiolinganishwa. Ukamilifu wa kungaa kwa Mungu unajionyesha kwa njia elfu moja. Mfano mojawapo, Januari Ranger Rick ana makala kuhusu aina tofauti wa samaki wanaoishi kilindini mwa bahari yenye giza na wana mataa yao ya kujijengea wenyewe-wengine wana mataa yanayoninginia mashavuni mwao, wengine wanao mapua yanayotoa mwangaza, wengine wanao mataa ya kumulikia chini ya macho yao. Kunao aina elfu ya samaki ambao wana mataa yao ambao wanaishi kilindini mwa bahari pahali hakuna mtu ambaye anaweza kuwaona na kupendezwa nao. Ni ya ajabu na ya kupendeza. Kwa nini wako hapo? Kwa nini sio tu thuluthi mbili ama aina chache tu waliochaguliwa? Sababu Mungu ni mwenye mngaro wa ajabu. Utimilifu katika uumbaji wake unadhihirika kwa urembo nyingi. Na kama dunia ni hivyo, basi Mungu ambaye alifikiria na akaumba anaweza kuwa anangaa kwa kiasi kikubwa cha aina gani!

5. Mungu anasujudiwa

Tano, Mungu anasujudiwa. “Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita. Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa mengine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka.” Hakuna anayewajua viumbe hawa wa ajabu wenye mabawa sita, miguu, macho na maarifa. Hakuna pahali wanaonekana tena katika Biblia – sio kwa jina maserafi. Kwa sababu ya tukio hilo kubwa na nguvu za malaika walioko zamu, haifai tuone picha ya watoto wachanga wanao mabawa makubwa wanaopiga kelele masikioni mwa Mungu. Kulingana na mstari 4, kwa kutoa sauti miimo ya milango na vizingiti vinatikisika. Tunaweza kufanya vizuri tukifikiria juu ya Malaika Samawati waliojirusha mbele ya mlolongo wa magari ya rais na kupiga kelele usoni mwake. Hakuna viumbe wapumbavu mbinguni. Ni wale tu wenye ukuu.

Jambo ni hili: hata wao hawawezi kuinua macho yao kwa Bwana ama wajisikie kuwa wanastahili na kuacha miguu yao bila kufunikwa mbele ya uwepo wake. Vile walivyo wakuu na wema, wasiochafuliwa na dhambi za kibinadamu, wanasujudia muumba wao kwa unyenyekevu mkuu. Malaika wanashtua binadamu kwa utukufu wake na nguvu. Na malaika wenyewe wanajificha katika uwoga wa kitakatifu na kusujudia katika mngaro wa Mungu. Nasi basi tutashtuka na kutetemeshwa kwa kiwango gano mbele ya uwepo wake Yule ambaye hawezi kustahimili kungaa kwa malaika wake!

6. Mungu ni mtakatifu

Sita, Mungu ni mtakatifu, “Wakiitana kila mmoja kwa mwenzake; Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Bwana Mwenye Nguvu!” Kumbuka vile Reepicheep, panya wa ajabu, mwishoni mwa kitabu cha “The Voyage of the Dawn Treader” alisafiri kwa maji mpaka mwisho wa dunia kwa kutumia dau lake dogo? Ndivyo, neno “Takatifu” ndilo dau hilo dogo ambalo linatufikisha mwishoni mwa dunia katika bahari ya lugha. Uwezekano wa lugha kubeba maana ya Mungu aste aste hadi pembeni mwa dunia na hadi hatua isiyojulikana. “Utukufu” unatubeba hadi ukingoni, na kutokea hapo uzoefu wa Mungu ni zaidi ya maneno.

Sababu yangu ya kusema hivi ni kwamba kila jitihada za kufafanua utakatifu wa Mungu hatimaye hutamatisha kwa kusema: Mungu ni takatifu ina maana kuwa Mungu ni Mungu. Wacha nieleze. Maana kuu ya takatifu pengine ni kukata au kutenga. Kitu takatifu inakatwa kutoka na kutengwa na matumizi ya kawaida (twaweza kusema kidunia). Vitu vya dunia pamoja na watu huwa takatifu wakiwa tofauti na dunia na kutolewa kwa Mungu. Hivyo Biblia inazungumzia patakatifu (Kutoka 3:5), mikusanyiko takatifu (Kutoka 12:16), sabato takatifu (Kutoka 16:23), taifa takatifu (Kutoka 19:6), mavazi matakatifu (Kutoka 28:2), mji mtakatifu (Nehemia 11:1), ahadi takatifu (Zaburi 105:42), watu takatifu (2 Petro 1:21), na wake ((1 Petro 3:5), maandiko takatifu (2 Timotheo 3:15), mikono takatifu (1 Timotheo 2:8), busu takatifu (Warumi 16:16), na imani takatifu (Yuda 20). Karibu kila kitu kinaweza kuwa takatifu ikiwa imetengwa kutoka kwa matumizi ya kawaida na kutolewa kwa Mungu.

Lakini tazama kile kinatendeka maana hii ikiwekewa Mungu Mwenyewe. Utatenganisha Mungu na nini ili umfanye awe takatifu? Uungu wa Mungu pekee unamaanisha ametengana na chochote kisichokuwa Mungu. Kuna tofauti kubwa yasiyopimika kati ya muumba na viumbe. Mungu ni wa kipekee. Sui Generis. Ni wa utakatifu mkuu. Hujasema kuwa zaidi ya yote kuwa yeye ni Mungu.

Ama ikiwa utakatifu wa binadamu unaotokana na kujitenga na ulimwengu na kujikabidhi kwa Mungu, ni kwa nani Mungu amejikabidhi ili akapokee utakatifu Wake? Hakuna, ila tu Yeye Mwenyewe. Ni kufuru kusema kuwa kuna ukweli zaidi ya Mungu ambaye inampasa afanane naye ili awe mtakatifu. Mungu ndiye ukweli kamili na zaidi yake bado ni Yeye tu. Alipoulizwa jina lake katika Kutoka 3:14, Alisema, “MIMI NIKO AMBAYE NIKO.” Maumbile na tabia yake haiiamuliwi na kitu chochote kisipokuwa Yeye mwenyewe. Yeye si mtakatifu kwa sababu anatii sheria. Aliandika sheria! Mungu si mtakatifu kwa sababu anaweka torati. Torati ni takatifu kwa sababu inadhihirisha Mungu. Mungu Anatosha. Vyote vingine ni vya kutokana.

Utakatifu wake basi ni nini? Sikiza haya maandiko matatu, 1 Samueli 2:2 “Hakuna yeyote mtakatifu kama Bwana, hakuna mwingine zaidi yako.” Isaya 40:25, “Utalinganisha Mimi na nani? Na ni nani anayelingana Nami? asema Yeye Aliye Mtakatifu.” Hosea 11:9, “Mimi ni Mungu wala si binadamu, Aliye Mtakatifu kati Yenu.” Hatimaye Mungu ni mtakatifu kwa kuwa Yeye ni Mungu wala si binadamu. (linganisha haya Mambo ya Walawi 19:2 na 20:7. Angalia miundo sambamba ya Isaya 5:16). Hawezi kulinganishwa. Utakatifu wake ni kiini cha uungu wake wa kipekee. Inaamua yote Aliye na afanyaye na haamuliwi na mtu yeyote. Utukufu wake ni vile alivyo kama Mungu ambapo hakuna aliye ama atakayekuwa. Iiite ukuu wake, uungu wake, umarufu wake, thamana yake kama lulu lenye bei ya juu. Mwishowe zinaisha. Katika neno “takatifu” tumesafiri kwa maji hadi pembeni mwa dunia katika kimya kikuu cha uvumilivu na hali ya mshtuko na kushangazwa. Kunaweza kuwa na mengi ya kufahamu kuhusu Mungu, lakini hayo yapita misemo, “Lakini Bwana yuko katika hekalu lake takatifu, Dunia yote inyamaze mbele yake” (Habakuki 2:20).

7. Mungu ni mtukufu

Kabla ya utulivu na kutikisika kwa visingiti na moshi la kufunika tunasoma jambo la saba na la mwisho kuhusu Mungu. Mungu ni mtukufu. “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Bwana wa majeshi, dunia yote imejaa utukufu wake.” Utukufu wa Mungu ni dhihirisho wa utakatifu wake. Utakatifu wa Mungu ni ukamilifu usio  kifani wa maumbile yake ya kiungu; utukufu wake ni onyesho la huo utakatifu. “Mungu ni mtukufu” unamaanisha: utakatifu wa Mungu umekuwa wa dharura. Utukufu wake ni onyesho la wazi ya siri za utakatifu wake. Katika Mambo ya Walawi 10:3 Mungu asema, “Miongoni mwa wale watakaonikaribia nitajionyesha kuwa mtakatifu, machoni pa watu wote nitaheshimiwa.” Wakati Mungu anajidhihirisha kuwa mtakatifu, yale tunayaona ni utukufu. Utakatifu wa Mungu ni utukufu wake uliofichika. Utukufu wa Mungu ni utakatifu wake uliofunuliwa.

Maserafi wanaposema, “Dunia yote imejaa utukufu wake,” ni kwa sababu kutoka umbali wa mbingu unaweza kuona mwisho wa dunia. Kutoka hapa chini mtazamo wa utukufu wa Mungu ni duni. Lakini ni kidogo kwa sababu ya kupendelea visivyo na maana kwa upumbavu. Tukitumia fumbo wa Søren Kierkegaard, sisi ni kama watu wanaoendesha magari yetu usiku katika nchi tukitafuta utakatifu wa Mungu. Lakini juu yetu, pande zote za kiti cha gari, tunawakisha taa. Bora tu vichwa vyetu vimezingirwa na mwangaza wa kibinadamu, mawingu juu yetu ni tupu na bila utukufu. Lakini upepo wa neema ya roho ukivuma kutoka kwa mwangaza wa dunia, basi katika giza yetu mbingu za Mungu zimejawa na nyota.

Siku moja Mungu atavurumisha na kushinda utukufu unaoshindana na kufanya utakatifu wake ujulikane kwa ustarabu kwa viumbe wakarimu. Hakuna haja ya kungojea. Ayubu, Isaya, Charles Colson na wengi wenu wamenyenyekea na kuufuata utakatifu wa Mungu na hivyo wamejiandalia kionjo cha ukuu wake. Kwako na wale wote ambao wanaanza kuihisi, nashikilia ahadi hii kutoka kwa Mungu, ambaye ni hai milele, mwenye mamlaka, mweza yote, wa kungaa wa kusujudiwa, takatifu na tukufu. “Kisha mtaniita na mtakuja na kuniomba, name nitawasikiliza. Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote” (Yeremiah 29:12-13).