Tutapendaje jirani wetu ambaye ni Muisilamu?

Article by

Founder & Teacher, desiringGod.org

Kuna majibu mengi kwa swali hili vile ilivyo njia nyingi ya kutenda wema badala ya maovu. “Upendo hautendi maovu kwa jirani” (Warumi 13:10.) “Upendo huvumilia kila kitu, huamini kila kitu, hutumaini kila kitu, huvumilia kila kitu” (Wakorintho 13:4). Haya ni vitu, ambavyo kwangu vyaonekana, vinastahili kutiliwa mkazo katika nyakati zetu.

[Jambo jipya: Kusema tupende maadui yetu haijakusudiwa kumaanisha kuwa Waisilamu wote wanahisi ama wanatenda mambo kwa njia ya kiadui kwa Wakristo. La! Hasha. Mara nyingi ni wakarimu na wanajali. Jambo ni kwamba hata kama mtu anatuchukua kwa njia ya kiadui (haijalishi ni wa dini ama si wa dini), inatupasa tuendele kupenda.

Maelezo mengine yahitajika katika hali yetu ya sasa. Ninaposema kuwa upendo unatihimiza kutenda wema katika njia zinazoonekana ya kukimu mahitaji yetu ya kimwili si maanishi kuwa usaidizi huu upeanwe tu wakati Muislamu amekuwa Mkristo. Upendo wa kudhihirika ni ushuhuda wa upendo wa Kristo. Mshuhuda hafichwi pahali anahitajika zaidi. Gumzo ambazo zimeshurutishwa kwa nguvu ama kwa fedha zinaenda kinyume na umbile wa imani iokoayo. Imani iokoayo ni kuukumbatia Yesu kama mwokozi wetu, Bwana wetu, na hazina kuu kwa hiari. Sio njia ya hazina. Yeye ni hazina.]

1. Waombe Baraka zote kutoka kwa Kristo hata kama wanakupenda ama hawakupendi.

 • Luka 6:28 -Wabarikini wale wanaowalaani waombeni wale wanao watendea mabaya.
 • Warumi 12:14 -Wabarikini wale wanaowatesa, barikini na msiwalaani.
 • I Wakorintho 4:12 -Tunapolaani tunabariki.

2. Watende wema kwa njia zinazoonekana ambazo zinatimiza mahitaji yao ya kimwili.

 • Luka 6:27 - Wapendeni adui zenu .Watendeni wema wanaowachukia.
 • Luka 6:31 - Watendeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi.
 • I Wathesolanika 5:15 - Angalieni kuwa mtu asilipe uovu kwa uovu, bali siku zote tufuateni kutendeana mema.
 • Warumi 12:20 - Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula, akiwa na kiu, mnyweshe. Maana ukifanya hivyo, utampaalia makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.

3. Usilipize uovu kwa uovu ukiwa umetendewa mabaya.

 • I Petero 3:9 - Msilipe uovu kwa uovu, au jeuri kwa ujeuri, bali barikini, kwa maana hili ndilo mliloiitiwa ili mpate kuridhi Baraka.
 • Warumi12:17, 19 - Msilipe mtu yeyote ovu kwa ovu . . . Wapendwa msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa, asema Bwana.”

4. Kaeni nao kwa amani ikiwezekana kwa kuwa inakutegemea wewe

 • Warumi 12:18 - Kama inawezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote.

5. Watafutie furaha ya uhuru kutoka kwa dhambi na hukumu kwa kuwaambia ukweli wa Kristo.

 • Yohana 8:31-32 - Kisha Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkihudumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli. Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.”

6. Kwa hakika tamani kuwa wajiunge nawe mbinguni kwa Baba kuwaonyesha njia, yaani Kristo Yesu.

 • Warumi 10:1 - Ndugu zangu, shauku ya moyo wangu . . . kwao ni kwamba waokolewe.
 • Yohana 14:6 - Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.
 • Yohana 3:16 - “Yeyote amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

7. Tafuta kufahamu yale wanayoyasema, ndipo unayokubali ama kukaripia yanatokana na kuelewa kwa kweli, sio mkanganyiko ama picha tatanishi.

 • I Wakorintho 3:16 - Upendo haufurahii mabaya bali hufurahia pamoja na kweli.

8. Wakanye kwa machozi kuwa wale ambao hawatapokea Kristo Yesu kama mwokozi aliyekufa na kufufuka ambaye anaondoa dhambi za ulimwengu, wataangamia kwa ghadhabu za Mungu.

 • Yohana1:12 - Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu, walioamini jina lake.
 • Warumi 10:9 - Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba “Yesu ni Bwana.” Na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka.
 • Wafilipi 3:18 - Kama nilivyokwisha kuwaambia mara nyingi kabla, nami sasa nasema tena hata kwa machozi watu wengi wanaishi kama adui wa msalaba wa Kristo.

9. Usiwaelekeze kwa njia mbaya ama kuwapa tumaini lisilo la kweli kwa kusema “Waisilamu wanamwabudu Mungu wa kweli.”

Neno hili linaonyesha karibu kila mtu taswira sahihi ya moyo wa Muisilamu ujuao, upendao na kumcha Mungu wa kweli. Lakini Yesu anafanya jibu la kibinafsi ya mtu mwenyewe kama jaribio la uhakika wa mtu katika kumcha Mungu. Na  yeye ni wazi kuwa mtu akimkataa kama mtauwa apeanaya maisha yake kama fidia kwa ajili ya dhambi na amefufuka tena—Huyo mtu hajui, wala kupenda ama kumcha Mungu wa kweli.

 • Yohana 8:19 - Ndipo wakamuuliza [Yesu], “Huyo Baba yako yuko wapi?” yesu akawajibu, “Ninyi hamnifahamu mimi ni nani, wala hamfahamu Baba yangu. Kama mngenifahamu mimi, mngefahamu na Baba Yangu.”
 • Yohana 5:23 - Ili wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Yeyote asiyemheshimu mwana, hamheshimu aliyemtuma.
 • Yohana 5:42-43 - [Yesu akasema], “Lakini mnajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu. Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei.”

Upendo hautaelekeza Waisilamu, ama wale wanaowajali kwa njia mbaya, kwa kusema kuwa ‘wanamjua’ ama ‘kumcha’ na ‘kumpenda’ Mungu wa kweli kama hawatampokea Yesu vile alivyo. Hatuwezi kuiona mioyo ya watu. Tunajuaje kama wanamjua na kumcha Mungu wa kweli? Tunaweka chini uhai wetu ili kuwapa Yesu. Wakimpokea, wanajua na kupenda na kumcha Mungu. Wasipompokea Yesu, naye Mungu pia hawajampokea. Yesu ndiye jawabu.

Hilo ndilo hoja katika neno la Yesu katika Luka 10:16’ “Yeye amkataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.” Na katika Mathayo 10:40, “Yeyote atakaye nipokea mimi atakuwa amepokea Yeye aliyenituma.” Na katika Yohana 5:46, “kama mngelimwamini Musa, mngeliniamini Mimi.”

Kitu cha kupendeza ambacho tunaweza kuwafanyia Waisilamu ama mtu yeyote Yule, ni kuwaambia ukweli kamili kuhusu Yesu, kwa njia ya tunzo la kidhabihu kwao na kuwa tayari kuteseka kwa ajili yao badala ya kuwaacha, na halafu kuwasihi kuacha “kuabudu isiyo faida” (Mariko 7:7) na kuupokea Kristo kama mwokozi aliyesulubishwa na kufufuka  kwa ajili ya msamaha wa dhambi zao na tumaini ya uzima wa milele. Hii ingekuwa furaha yetu kuu—Kuwa na ndugu na dada kutoka kwa Waisilamu ulimwenguni.