Mahubiri ya mafanikio: Udanganyifu na hatari

Article by

Founder & Teacher, desiringGod.org

Nisomapo kuhusu makanisa yanayohubiri utajiri, jibu langu huwa: “Nisingalikuwa ndani ya ukristo, singalitaka kuingia ndani.” Maanake, kama huo ndio ujumbe wa Yesu, basi ikae.

Kuelekeza watu kwa Kristo kwa ajili ya kupata utajiri ni udanganyifu na pia hatari. Ni udanganyifu kwa sababu Yesu alipotuita, alinena mambo kama: “Vivyo hivyo, basi, hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa mwanafunzi wangu kama asipoachilia kila kitu alicho nacho” (Luka 14:33). Na ni hatari kwa sababu kutaka kutajirika huvuta “watu kwenye uharibifu na maangamizi” (Timotheo 6:9). Kwa hivyo huu ni ombi langu kwa wale wanaohubiri utajiri.

1. Usijenge filosofia ya huduma ambaye hufanya iwe ngumu kwa watu kuingia mbinguni.

Yesu alisema, "Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!" Wafuasi wake walishangazwa, kama vile wengi waliomo katika chama cha “utajiri” wangeshangazwa. Naye yesu akaendelea kuwashangaza zaidi akisema, “Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu." Wakajibu kwa kutoamini: "Ni nani basi, atakayeweza kuokoka?" Yesu akawaambia, "Kwa binadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungu mambo yote huwezekana"(Mariko 10:23 -27).

Swali langu kwa wahuibiri wa utajiri ni: Kwa nini unataka kujenga huduma ambaye inaifanya kuwa ngumu kwa watu kuingia mbinguni?

2. Usijenge filosofia ya huduma ambaye inaleta maafa kwa watu.

Paulo alisema, “Kweli dini humfanya mtu awe tajiri sana, ikiwa anatosheka na vitu alivyo navyo. Maana hatukuleta kitu chochote hapa duniani, wala hatutachukua chochote. Kwa hiyo basi, kama tunacho chakula na mavazi, tunapaswa kuridhika navyo.” Lakini alikanya majaribio ya kutaka utajiri. Vile vile, alikanya kuhusu wahubiri ambao wanaubiri kuhusu utajiri badala ya kusaidia watu kulikwepa. Alisema, Lakini wale wanaotaka kutajirika huanguka katika majaribu, na kunaswa katika mtego wa tamaa nyingi mbaya za kipumbavu, ambazo huwavuta mpaka kwenye uharibifu na maangamizi. Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi” (1 Timotheo 6:6-10).

Kwa hivyo swali langu kwa wahubiri wa utajiri ni: Kwa nini mnataka kujenga huduma ambaye inaelekeza watu kudunga mioyo yao kwa huzuni nyingi na kuwavuta kwenye maharibifu na uhangamizi?

3. Usijenge filosofia ya huduma ambaye inaendeleza uwezekano wa kuharibiwa kwa nondo na kutu.

Yesu alikanya katika juhudi za kujiwekea hazina hapa duniani. Anatuhimiza kuwa wapeaji, wala si wawekaji. "Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba. Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba” (Mathayo 6:10).

Ndio, sote tunaweka vitu. Lakini kwa vile kuna, ndani yetu maelekezo kwenye choyo, haja gani kutoa darubini kwake yesu na kuibadilisha juu chini?

4. Usijenge filosofia ya huduma ambaye inafanyisha bidii iwe njia ya kujijengea mali.

Paulo alisema hatufai kuiba. Maana yake ilikuwa kufanya kazi kwa bidii tukiwa tukitumia mikono yetu. Lakini sababu hasa haikuwa kujiwekea au kuhifadhi. Sababu ilikuwa “kuweza kupeana.” “Aliyekuwa akiiba, asiibe tena, bali na aanze kufanya kazi njema kwa mikono yake, apate kuwa na kitu cha kumsaidia mtu aliye maskini.” (Efeso 4:28). Hili sio changamoto kwa wale wanaotaka kutajirika kwa ajili ya kuweza kupeana zaidi. Hakuna sababu ambaye inamfanya Yule anayetengeneza $200,000 kuishi tofauti na Yule ambaye anayetengeneza $80,000. Tumia fedha vizuri; na upeane mengine kule.

Sababu gani unachochea watu kufikiri kwamba wanahitaji kuwa na mali ndiposa waweze kupeana? Kwa nini usiwahimize kufanyisha maisha yao iwe ya kawaida na waweze kutoa hata zaidi? Ingekuwaje kutoa kwao kuwa shuhuda kubwa kwamba Kristo, na sio rasilmali, ndio hazina yao?

5. Usijenge filosofia ya huduma ambaye yanaendeleza kutokuwa na imani katika ahadi za Mungu ili iwe kwetu yale ambaye fedha hayawezi.

Sababu ya mwandishi wa Ebrania kutusawishi kutosheka na tuliyo nayo ni kwamba kinyume yake inamaanisha imani ndogo katika ahadi za Mungu. Asema, “Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: ‘Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.’ Ndiyo maana tunathubutu kusema: ‘Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?’” (Ebrania 13:5-6).

Ikiwa Biblia inatuhimiza ya kuwa kutosheka na tulionayo inaheshimu ahadi ya Mungu kutotupa sisi, ni sababu gani tunafundisha watu kutaka kutajirika?

6. Usijenge filosofia ya huduma ambayo inachangia kwa watu wako kunyongwa hadi kufa.

Yesu anakanya kwamba neno la Mungu, ambaye inafaa kuleta uhai, inaweza kunyongwa na kutolewa uwezo wake na utajiri. Asema ni kama mbegu ambaye inamea kati ya miiba yatakayoinyonga hadi kifo: “Zile zilizoanguka kwenye miti ya miiba ni watu wale wanaosikia lile neno, lakini muda si muda, wanapokwenda zao, husongwa na wasiwasi, mali na anasa za maisha, na hawazai matunda yakakomaa” (Luka 8:14).

7. Usijenge filosofia ya huduma ambao unautoa utamu katika chumvi na kuficha mwangaza kikapuni.

Ni nini hufanya wakristo kuwa chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu? Hakika sio mali. Mapenzi ya utajiri na ufuataji wake inaonja na pia inafanana na ulimwengu. Haipatii dunia chochote tofauti na yale ambaye imekwisha amini. Pigo kubwa kwa mahubiri ya utajiri ni kwamba mtu hapaswi kuwa ameamshwa kiroho ndio aweze kuipokea; mtu anahitaji tu kuwa mchoyo. Kutajirika katika jina la Yesu si chumvi ya dunia au mwanga wa ulimwengu. Katika hayo, dunia huona tu picha yake. Na ikiwa ina maana, wataipokea.

Muktadha wa Yesu, aliponena, hutuonyesha ni nini maana ya chumvi na mwanga. Ni kutaka kwa furaha kuteseka kwa ajili ya Kristo. Yesu alisema, "Heri yenu ninyi watu wakiwatukana, wakiwadhulumu na kuwasingizia kila aina ya uovu kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia maana tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Hivyo ndivyo walivyowadhulumu manabii waliokuwako kabla yenu. Ninyi ni chumvi ya dunia! Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika” (Mathayo 5:11-14).

Kitakachofanya dunia ionje (chumvi) na ione (mwanga) wa Kristo ndani yetu si ya kwamba tunapenda utajiri jinsi wanavyoipenda. Bali, itakuwa matayarisho na uwezo wa wakristo kupenda wengine kupitia mateso, ilhali wakisherekea kwa sababu malipo yao imo na Yesu mbinguni. Kwa kawaida, mambo haya ni magumu kwa binadamu. Ni mambo ya kiroho. Lakini kuvuta watu na ahadi ya utajiri ni jambo la kawaida na sio ujumbe wa Yesu. Yesu hakufa iliwa watu wapate utajiri wa ulimwengu huu.