Kutafuta furaha

Ukweli sita za kibiblia

Article by

Founder & Teacher, desiringGod.org

Je, unajua kwamba Mungu anatuamrisha tuwe na furaha?

“Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako.” (Zaburi 37:4)

1. Mungu alituumba kwa ajili ya utukufu wake

“Walete wana wangu kutoka mbali na binti zangu kutoka miisho ya dunia… niliyemuumba kwa utukufu Wangu.” (Isaya 43:6-7)

Mungu alituumba kwa ajili ya kutukuza ukuu wake - vile darubini huadhimisha ukuu wa nyota. Atuumba kuweka uzuri wake, ukweli, urembo, hekima na haki kwa tamasha. Onyesho kuu la utukufu wa Mungu huja kwa kupendezwa kindani kwa vyote vile alivyo. Hii ina maana ya kuwa Mungu hupata sifa nasi twapata furaha. Mungu alituumba ili atukuzwe zaidi ndani yetu tunaporidhishwa zaidi ndani yake.

2. Kila mwanadamu anafaa kuishi kwa ajili ya kumtukuza Mungu

“Basi, lo lote mfanyalo, kama ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.” (1 Wakorintho 10:31)

Ikiwa Mungu alituumba kwa utukufu wake, ni dhahiri kwamba ni sharti tuishi kwa utukufu wake. Wajibu wetu unatoka kwa uvumbuzi wake. Hivyo sharti la kwanza nikuonyesha thamana ya Mungu kwa kutosheka na yote aliye kwa ajili yetu. Hii ndiyo kiini cha kumpenda Mungu (Mathayo 22:37) na kumwamini (1 Yohana 5:3-4) nakumshukuru yeye (Zaburi 100:2-4) Ni mzizi wa utiifu wa kweli, hasa kuwapenda wengine (Wakolosai 1:4-5).

3. Sisi sote tumeshindwa kumtukuza Mungu tunavyopasa

“Kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” (Warumi 3:23)

Ni nini maana ya kupungukiwa na uukufu wa Mungu? Ina maanisha kuwa hakuna kati yetu aliyemwamini na kumthamini Mungu jinsi tupasavyo. Hatujaridhishwa na ukuu wake wala kutembea kwa njia zake. Tumetafuta kutoshelezwa kwa vitu vingine na kuzithamanisha zaidi ya Mungu, ambayo ni kiini cha kuabudu sanamu (Warumi 1:21-23). Tangu dhambi ilipoingia ulimwenguni sote tumefanya upinzani mkuu dhidi ya Mungu kuwa hazina ambaye huturidhisha kwa yote (Waefeso 2:3). Hili ni kosa la kutisha kwa ukuu wa mungu (Yeremia 2:12-13).

4. Sisi sote tumo chini ya hukumu/laana ya Mungu

“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…” (Warumi 6:23)

Sisi tumepujua utukufu wa Mungu. Vipi? Kwa kutanguliza vitu vingine juu yake. Kwa kukosa shukran, kutoamini na wasi. Hivyo Mungu yuko katika hali ya kutufungia nje ya starehe ya utukufu wake wa milele. “Wataadhibiwa kwa uangamivu wa
milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza Wake.” (2 Wathesalonike 1:9)

Neno "kuzimu" limetumika katika Agano Jipya mara kumi na mbili – kumi na moja na Yesu mwenyewe. Si hadithi zilizoundwa na wahubiri waliokufa moyo na wenye hasira. Ni onyo nzito kutoka kwa mwana wa Mungu aliyekufa ili akomboe wenye dhambi kutokana na laana zake. Kuipuuza ni hatari kubwa.

Ikiwa bibilia ingemalizia hapa uchambuzi wa hali ya binadamu, tungekwama kwa hatma ya kutokuwa na tumaini ya siku za usoni.

5. Mungu alimtuma mwanawe wa pekee Yesu ili atupatie uzima wa milele na furaha

“Kusudi la maagizo haya ni upendo, utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli…” (1 Timotheo 1:15)

Habari njema ni kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya wenye dhambi kama sisi. Na akafufuka kutoka kwa wafu ili adhibitishe nguvu za ukombozi kwa kifo chake na kufungua milango ya uzima wa milele na furaha (1 Wakorintho 15:20). Hii ina maana Mungu anaweza kuwasamehe wenye dhambi na bado kuwa mwenye haki (Warumi 3:25-26). "Kwa maana Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi mara moja tu, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki, ili atulete kwa Mungu" (1 Petro 3:18). Kuja nyumbani kwa Mungu ambako kunapatikana kuridhika unadudumu.

6. Faida ilionunuliwa kutokana na kifo cha Kristo ni kwa wale waliotubu kumwamini

“Tubuni basi mkamgeukie Mungu, ili dhambi zenu zifutwe” (Matendo ya Mitume 3:19). “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka,” (Matendo ya Mitume 16:31).

"Toba "yamaanisha kuacha ahadi zote za uongo za dhambi. "Imani " yamaanisha kutosheka na yeyote ambayo Mungu anaahidi kukuwa kwetu tukiwa ndani ya Yesu. "Yeye aniaminiye mimi," Yesu asema "hataona kiu kamwe" (Yohana 6:35). Hatuwezi kupata wokovu wetu. Hatuwezi sifa yake (Warumi 4:4-5). Ni kwa neema kupitia Imani (Waefeso 2:8-9). Ni zawadi ya bure (Warumi 3:24). Tutaupata iwapo tutauthamini zaidi ya mambo yote (Mathayo 13:44). Tunapofanya hivyo, kusudi wa Mungu kwa uumbaji unatekelezwa: Anatukuzwa ndani yetu nasi tunaridhishwa ndani yake - milele.

Je, unafahamu mambo haya?

Je, unatamani furaha ambalo huja kutokana na kuridhishwa na yote ambaye Mungu aliye kwa ajili yako ndani ya Yesu? Ikiwa hivyo, basi Mungu anafanya kazi katika maisha yako.

Unapaswa kufanya nini?

Toka kwa ahadi za uongo za dhambi. Mmuite Yesu akuokowe kutoka kwa hatia, adhabu na utumwa. “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokoka.’’ (Warumi 10:13). Anza kuweka tumaini yako kwa yote ambayo Mungu amekuwa kwa ajili yako, ndani ya Yesu. Vunja nguvu za ahadi za dhambi kwa imani na utoshelezwe na ahadi kuu za Mungu. Anza kusoma Biblia na utapata ahadi yake ya thamani kubwa mno, ambazo zinaweza kukuweka huru (2 Petro 1:3-4). Tafuta kanisa linaloamini biblia na uanze kuabudu na kukua pamoja na watu wengine ambao wanaomthamini Mungu zaidi ya mambo yote (Wafilipi 3:7).

Habari njema zaidi duniani ni kwamba hakuna mvutano yeyote kati ya furaha zetu na utakatifu wa Mungu. Kuridhishwa na yote ambaye Mungu amekuwa kwetu ndani ya Yesu inamdhihirisha kama mwenye thamana

“Umenijulisha njia ya uzima, utanijaza furaha katika uwepo wako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kuume” (Zaburi 16:11).


Mwonekano wa Neno "Kuzimu" katika Agano Jipya

Yesu mwenyewe alinena juu ya kuzimu katika vifungu vifuatavyo:

“Yeyote atakaye mkasirikia ndugu yake wa kiume au wa kike, atapasiwa hukumu. Tena, Yeyote atakayemwambia ndugu yake wa kiume au kike, 'Raca,' yaaani kumdharau na kumdhihaki, atapasiwa kufanyiwa baraza. Lakini yeyote atakayesema 'We mpumbavu alaaniwe! Atapasiwa hukumu ya moto wa jehanum.” (Mathayo 5:22)

“Jicho lako la kuume likikufanya utende dhambi, likoe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jahanum.” (Mathayo 5:29)

“Kama mkono wako wa kuume ukikufanya utende dhambi, ukate uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jahanum.” (Mathayo 5:30)

“Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho afadhali mwogopeni Yeye awezeye kuiangamiza roho na mwili katika jahanum.” (Mathayo 10:28)

“Nalo jicho lako kama linakusababisha utende dhambi likoe, ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili ukatupwa katika moto wa jahanum.” (Mathayo 18:9)

“Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Ninyi mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu moja ageuke na kuwafuata ninyi, lakini baada ya kumpata, mnamfanya mwana wa jahanum mara mbili kuliko ninyi!.” (Mathayo 23:15)

“Ninyi nyoka, ninyi uzao wa nyoka wenye sumu! Mtaiepukaje hukumu ya jahanum?” (Mathayo 23:33)

“Kama mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja kuliko kuwa na mikono miwili ukaingia jahanum mahali ambako moto hauzimiki.” (Marko 9:43)

“Kama mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa kilema kuliko kuwa na miguu miwili ukaingia jahanum mahali ambako moto hauzimiki.' (Marko 9:45)

“Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, lingo'e. Ni afadhali kuwa chongo ukaingia katika ufalme wa Mungu kuliko kuwa na macho mawili na ukatupwa jahanum.” (Marko 9:47)

“Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: 'Mwogopeni yule ambayye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia mwogopeni huyu!.” (Luka 12:5)

“Kule kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Abrahamu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa karibu yake.” (Luka 16:23)

Yakobo naye alisema, “Ulimi pia ni moto, ndiyo ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili yetu. Ulimi hutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa jahanum.” (Yakobo 3:6)

Petro naye alisema, “Kwa maana kama Mungu hakuwasemehe malaika walipotenda dhambi, bali aliwatupa kuzimu, katika vifungu vya giza wakae humo mpaka ije hukumu.” (2 Petro 2:4)