Jitolee kwa maombi

. . . iweni na furaha katika tumaini, katika dhiki iweni na saburi, dumuni katika maombi . . .

Lengo langu rahisi na ambalo kwa mwanadamu haliwezekani asubuhi hii katika ujumbe huu ni kuwa ninyi nyote mtadumu katika maombi katika mwaka wa 2003. Hili ndilo lengo langu kwa sababu hili ndilo Bibilia anatuhimiza tufanye. Andiko langu ni Warumi 12:12 ambayo ni sehemu ya msururu mrefu wa himizo. Inasema inafaa “kufurahi katika tuamini katika dhiki, kudumu (proskarterountes) kwa maombi.”

Tafsiri yako inaweza sema “maombi bila kukoma” ama “mwaminifu katika maombi.” Haya yote yaelekea kwa neno hilo. “ Kudumu “ Nitafsiri mufti. Neno hilo latumika katika Marko 3:9 ambapo linasema, “Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, (Yesu) aliwaambia wanafunzi wake waweke tayari (proskartere) mashua ndogo kwa ajili yake ili kuwazuia watu kumsonga.” Mashua ilitengwa- ya kudumu- kwa ajili ya kumpeleka Yesu mabali ikiwa umati wangemsonga “ya kudumu”-Ilio tengwa kwa jukumu iliyoteuliwa kwake.

Sasa, mashua zinakuwa tu pale. Lakini watu hawajajitenga hivyo. Kama neno likitumika kumaanisha mtu linamaanisha kudumu au kutengwa si tu kwa njia ya hadhi ama uteuzi bali ya kitendo katika jukumu lililotendwa na kulisisitiza. Hivyo basi kwa mfano katika Warumi 13:6 Paulo anaongea kuhusu jukumu la Serikali hivi, “Kwa sababu hii mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala.” Ni kusema, si tu eti wameteuliwa na Mungu kwa jukumu, bali wamejitolea kwalo.

La muhimu katika neno hili ni kuwa matumishi matano kati ya kumi ya Agano Jipya yanatumiya maombi.

Sikiza, ukiacha Warumi 12:12 kunayo:

  • Matendo ya Mitume 1:14 (Baada ya kupaa kwa Yesu kwenda mbinguni wakati Wanafunzi walikuwa wakiongojea kuvuviwa Roho mtakatifu huko Yerusalemu), “Hao watu wote waliungana pamoja katika maombi. Pamoja nao walikuwa wanawake kadha wa kadha na Maria mama yake Yesu na ndugu zake Yesu.

  • Matendo ya Mitume 2:42 (Kwa waliomgeukia Yesu hapo awali jijini Yerusalemu), “Nao wakawa wanadumu katika mafundisho ya Mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali.”

  • Matendo ya Mitume 6:4 (Mitume wansema), “Wakati sisi tutatumia muda wetu mrefu kuomba na kulihudumia lile neno.”

  • Wakolosai 4:2 (Paulo anatuambia sisi wote). “Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru.”

Basi tunaweza sema kutoka kwa maandiko ya Agano Jipya kwamba maisha ya Kristo ya kawaida ni maisha ya kudumu katika maombi. Na basi inafaa ujiulize unapotoka kwa mwaka wa 2002 na kuingia katika mwaka wa 2003, “Je ninadumu katika maombi?”

Si kumaanisha kwamba maombi pekee ndicho kitu unachokifanya- kuliko kuwa pamoja na bibi kunamaanisha kuwa kile Bwana anafanya ni kuenenda tu kwa pamoja na bibi yake. Lakini kudumu kwake kunabadilisha vyote maishani mwake na kumfanya kumpeana kwake kwa njia nyingi tofauti. Basi kudumu kwa maombi hakumaanishi kuwa yote ufanyayo ni kuomba (Ingawa Paulo asema katika pahali pengine, “Omba bila kukoma.” 1 Wathesalonika 5:17). Inamaanisha kuwa kutakuwa na mtindo wa kuomba unaokaa kama kudumu katika maombi. Hautakuwa sawa kwa watu wote. Lakini utakuwa kitu chenye umuhimu. Kudumu katika maombi inakaa tofauti na kutodumu katika maombi. Na Mungu anajua tofauti. Atatuita tutoe ushuhuda: Je, tumedumu katika maombi? Je, kuna mtindo maishani mwako ambao unaweza kuitwa, “kudumu katika maombi?”

Nadhani wengi wetu wanaweza kukubaliana juu ya baadhi ya aina fulani ya maombi ambayo hayawezi itwa “Kudumu katika maombi.” Kuomba tu wakati shida inapoingia maishani mwako, hautakuwa mtindo wa kudumu katika maombi. Kuomba wakati wa mlo ni mtindo, lakini je inalingana na vile Paulo anavyohimiza Kanisa “kudumu katika maombi?” Changamoto, “Sasa najilaza ili nilale” maombi mwishoni mwa siku yawezakuwa ni “kutodumu katika maombi.” Kulenga na kukosa “Nisaidie, Bwana” ndani ya gari ukihitaji pahali pa kuliegeza si “kudumu katika maombi.” Hayo yote ni mazuri. Lakini sisi sote tutakubaliana kuwa Paulo anahitaji kitu zaidi na tofauti kutoka kwa Wafuasi wa Kristo anaposema “Mdumu katika maombi.”

Tusije tukasahau katika haya yote, vile tulivyoona wiki uliopita, kuwa msalaba wa Kristo- kifo chake kwa ajili ya wenye dhambi- ni msingi wa maombi yote. Hakungekuwa na jibu mwafaka kama KWA NINI ama VIPI tunaomba kama Kristo hangekufa kwa ajili yetu. Ndio maana tunaomba “katika jina la Yesu.”

Vile nimepima vizuizi katika maombi naweza kuviongelea, baadhi ya vizuizi vimeandikwa chini ya swali, KWA NINI uombe? Na baadhi yao chini ya swali JINSI ya kuomba. Asubuhi hii nataka kuangazia juu ya JINSI. Si kwamba swala la KWA NINI si muhimu, lakini inaonekana kwamba tunaweza kuwa na jibu lote la kitaaluma la kidini ya KWA NINI inafaa tuombe na bado wapuuzi na wasiojali katika maisha ya maombi. Basi nitawapa jibu fupi kwa swali KWA NINI, na baadaye kuangazia maswali ya kawaida kuhusu kwa njia gani ambayo naomba utakuinuwa kubuni hatua mpya ya “kudumu katika maombi” katika mwaka wa 2003”.

Kwa nini kuomba?

Naanza na majibu matatu mafupi juu ya KWA NINI tunafaa kudumu katika maombi.

1) Bibilia inatuambia kuomba na tunafaa kufanya yale Mungu anayoyasema. Andiko hili pamoja na mengine linasema, “Dumu katika maombi.” Tusipofanya hivyo, hatuko watiifu kwa maandiko. Hiyo ni upumbavu na hatari. Kama maombi hayaji kwa urahisi kwako, jichukuwe kama mtu wa kawaida ambaye ameanguka na mtenda dhambi pamoja na wengine wetu. Halafu pigana. Jihubirie. Usiache dhambi zako na udhaifu wako na vitu vya dunia vikutawale. Mungu asema “Dumu katika maombi.” Pigania hii.

2) Mahitaji maishani mwako, na katika familia yako, na katika Kanisa hili na makanisa mengine, na katika hatima ya huduma ya ulimwengu, na katika utamaduni wetu kiujumla ni kubwa mno na yana hitaji. Katika hali nyingi mbingu na kuzimu yaning’inia, kuamini ama kutoamini, uhai ama mauti. Kumbuka huzuni na hofu wa Paulo kwa ajili ya watu wa ukoo wake wanaoangamia katika Warumi 9:2 na ukumbuke katika Warumi 10:1 anawombea kwa dhati, “Ndugu zangu, shauku ya moyo wangu na maopmbi yangu kwa Mungu ni kwa ajili ya Waisraeli kwamba waokolewe.” Wokovu waning’inia tunapoomba. Hutajua ni nini haja ya maombi hadi utakapojua kuwa maisha ni vita.Mojawapo ya vizuizi kuu kwa maombi ni kuwa maisha kwa kawaida sana sana huwa nyororo kwa wengi wetu. Uwanja wa vita ndiyo njia hapo nje, lakini hapa katika donge langu ndogo la amani na kutosheleka yote ni vyema.Lo! Mungu na atufumbue macho ili toune na kuhisi mahitaji yanayotuzingira na uweza mkuu wa maombi.

3) Sababu ya tatu ya kuomba ni kuwa Mungu anatenda tunapoomba. Na Mungu anaweza kuyatenda mengi katika sekunde tano kuliko yale tunaweza kufanya kwa miaka tano. Na ni vipi nilivyo jivunza hivi kwa miaka. Ni jambo la ajabu kuungama mara kwa mara na kumsihi Mungu wakati wa kutayarisha mafunzo, ama wakati mwingine katika ushauri juu ya shida ama baadhi ya gumzo ya ushuhuda ama baadhi ya mkutano wa mpango, na kuwa na upenyo baada ya upenyo ambao haukuja hadi nilipoomba. Ni funzo muhimu kuhisi ukiwa na uwoga na kuwa na hamu ya kuanza kazi mara moja kwa sababu nina mengi ya kufanya na sijui vile nitayamaliza yote, lakini kujilazimisha kuwa kulingana na Bibilia na kujali na kuchukua muda ya kuungama chini kabla ya kufanya kazi na nikiwa nimeungama chini ili niwe na mawazo akilini ama kutengeneza ujumbe ama kukabiliana na janga ama kusuluhisha shida ya kidini-na hivyo basi kujiokolea masaa kadha wa kadha ya kazi na shida ya kugonga kichwa changu ukutani nikijaribu kufahamu kilichotukia katika sekunde tano ya kuangaziwa! Simaanishi kuwa Mungu anatuondoa katika kazi ngumu. Namaanisha kuwa maombi yanaweza kufanya kazi yako izalishe matunda mara 5000 kuliko vile unaweza kufanya pekee yako.

Kuna mengi, lakini haya ndiyo majibu ya swali KWA NINI kuomba: 1) Mungu anatuamrisha tuombe; 2) Mahitaji ni makuu na vitu vya milele viko taabani: 3) Mungu anatenda tunapoomba na kila mara anatenda mengi zaidi kwa masekunde kuliko vile tungeweza kufanya kwa masaa ama wiki ama wakati mwingine miaka.

Kuna maswali mengine mengi ya kujibiwa kuhusu maombi ambayo sitayashughulikia hapa. Ndio maana kuna sura ndefu juu ya maombi katika Kutamani Mungu na Starehe za Mungu na Wacha Mataifa Wafurahie na sababu ya kuwa na kitabu nzima kiitwacho: Njaa kwa Mungu: Kumtamani Mungu kupitia Kuomba na Kufunga. Sana sana ikiwa unang’ang’ana na vile kuomba kwa wokovu wa watu unavyolingana pamoja na kuchaguliwa bila masharti enda moja kwa moja hadi ukurasa wa 217-220 ama Starehe za Mungu.

Jinsi ya kuomba

Lakini kwa wakati wetu uliobaki asubuhi hii twataka kuongea kuhusu JINSI ya maombi. Nataka kuwapa motisha na mambo yanayoonekana, uweza wa kibibilia ambayo hujawahi kudhani, ama labada kujaribu na baadaye kushindwa kuyastahimili- kukosa “kudumu katika maombi.”

Hii ni jitihada yangu kuchora kinachomaanisha kudumu katika maombi bila kufanya njia yangu nyembamba ama fikira kama ya njia kuu. Si sote ni tofauti. Mipangilio yetu ni tofauti. Familia zetu ni tofauti. Tuko katika hatua tofauti za kimaisha zilizoko na mahitaji tofauti za nyakati zetu. Tuko katika viwango tofauti ya ukomavu wa kiroho na hakuna anaye komaa kwa usiku mmoja. Yale ambayo unaweza kuyafanya kwa miaka mitano katika kudumu kwako kwa maombi yaweza kukufanya uwaze nyuma na kushtuka vile ulivyostahimili nyakati za ukavu. Lakini sote twaweza songa mbele. Paulo anapenda kuandikia makanisa yake na kusema, “Mnaendelea vizuri, lakini mkizidi kuyatenda mengi hivyo zaidi” (Wafilipi 1:9; 1 Wathesalonika 4:1, 10). Na kama kuna mahali popote ambapo “kutenda hivyo zaidi na zaidi” pametumika, ni katika kudumu kwetu katika maombi.

Nitaweza maoni mbili mbili kwa mara tano nikitumia herufi tofati tofauti ambayo kwa pamoja itasomeka kama “FADES.” Hakuna umuhimu kwa neno “fades.” Lakini ni vile tu inavyosomeka. Lakini ukijaribu kuilazimisha, unaweza sema kwamba bila haya , kudumu kwa maombi kunatoweka (fades).

F - Free and Formed (Huru na yaliyoumbwa)

Hapa ninayo mawazoni tofauti kati ya ombi lilopangwa na lisilopangwa. Kudumu katika maombi kutamaanisha kwamba yale unasema katika muda wako wa maombi yatakuwa ya huru na yasiyopangwa na kila mara yaundwa na kupangwa. Unapokuwa huru tu katika maombi yako utakuwa juu juu na bila mpango. Kama umeumbika tu katika maombi yako, labda utakuwa kama mtambo na mviringo. Njia zote za maombi ni muhimu. Si mojawapo, bali yote na.

Kwa kuwa huru namaanisha kila mara utahisi kumwaga roho yako kwa Mungu na utaufanya. Hatuhitaji maandishi ama mwongozo ama jarida ama vitabu. Utakuwa na mahitaji mengi amabayo yatatoka tu kwa huru bila mpangilio wowote wa kabla. Hii ni nzuri. Bila hii ni shaka kwamba tuna uhusiano wa kweli na Kristo. Hebu tafakari juu ya ndoa bila urafiki ambapo mawasiliano yote yatoka kwenye vitabu ama majarida ama yatamkwa kutoka kwa maandiko yaliyotiliwa akilini. Hiyo itakuwa ya kibinadamu sana.

Kwa upande mwingine nakusihi kutodhani kuwa uko ndani ya roho sana ama una njia ama tajiri ama una nidhamu kiasi kwamba unaweza kuendelea bila usaidizi wa miundo. Ninayo akilini aina ya miundo minnne ambayo natumai mtaitumia.

Muundo #1. Bibilia. Omba kibibilia. Omba maombi ya kibibilia. Wiki hii tunajenga maombi yetu katika ombi kwenye Waefeso 3:14-19.

Kwa sababu hii naungama mbele ya Baba, 15 Ambaye kwa yeye ubaba wote wa kila jamaa za mbinguni na za duniani unaitwa. 16. Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kwa njia ya roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu Wake, 17 Ili kwamba, Kristo apate kukaa mioyoni mwenu kwa njia ya imani. Nami ninaomba kwamba nanyi mkiwa wenye mizizi tena imara katika upendo. 18 muwe na uwezo wa kufahamu pamoja na watakatifu jinsi ulivyo upana na urefu na kimo na kina upendo wa Kristo. 19 Na kujua upendo huu kwamba unapita fahamu ili mpate kujazwa na kufikia kipimo cha ukamilifu wa Mungu.

Litafakari na liombe kila mara. Omba ombi la Bwana na unapoomba weka kila sentensi kwa maneno yako na kulitumia kwa watu ambao una mizigo kwao. Omba amri za bibilia: “Nisaidie- msaidie bibi yangu, watoto wangu, wazee, upendo wetu wa huduma wako, ewe Mungu, kwa moyo wangu wote na roho yangu yote na nguvu zangu zote.” Omba ahadi za kibibilia: “Ewe bwana chukua mamlaka yote, iliyo yako juu mbinguni na duniani na uwafanye wahudumu wetu kuhisi utamu wa ahadi ya kuwa utakuwa nao hadi mwisho wa dahari. Omba maonyo ya Bibilia: “ama Bwana ,Ni ruhusu kupigana dhidi ya tamaa kwa njia ya dharura ambayo ulifundisha uliposema, ng’oa jicho lako na upate kuridhi ufalme wa mbingu kuliko kuliacha na kuenda jehanamu.” Fungua Bibilia mbele zako na uweke kiniko kimoja kwa upande mmoja na kingine upande mwingine na kuomba ile aya yake kwa kuabudu ama kusifu ama kwa kushukuru ama kuamrisha.

Muundo #2. Orodha. Orodha ya kuomba. Akilini ninayo orodha ya watu ya kuombea na orodha ya mahitaji ya kuombea. Kama unaweza kukumbuka watu wote na mahitaji ya kuombea yafaa uombe bila orodha, wewe ni Mungu. Lazima niwe na orodha zingine akilini mwangu na zingine kwenye karatasi. Nimeweka akilini karibu watu 70 ambao nawaombea kwa majina kila siku. Lakini hiyo haijumulishi orodha ya watu waliokuja kwa huduma katika ukumbi ambao Noeli pamoja nami wanawaombea kila siku kutoka kwa orodha ulioandikwa. Haijumlishi orodha ya wahudumu wetu ninayosoma kutoka kwa orodha. Na hiyo ni watu tu, bila kutaja mahitaji ambayo yabadilika ndani ya moyo wangu na katika familia na kanisa na ulimwengu wiki baada ya wiki. Basi nakuhimiza kutumia orodha ya watu na mahitaji. Hifadhi aina fulani ya mfuko wa maombi ama kijitabu ama hifadhi katika tarakilishi yako ya mkono. Kumbuka naongea tu juu ya nusu moja ya haya mawili: Uhuru na muundo. Usisahau thamani ya uhuru. Ni yote mbili si moja wapo.

Muundo #3. Vitabu. Omba kupitia vitabu kama Dunia ya Operesheni- taifa tofauti na Nia ya Kristo ndani yake, Kila siku ama kwa siku mbili.Ni njia yenye nguvu ya kupata moyo kiasi cha ulimwengu na maono ya ukuu wa Mungu! Omba kupitia kitabu kama Kudumu kwa Undani- Mtazamo wa haraka wenye ukurasa mmoja kuhusu mateso, kanisa linaloteswa kwa kila siku ya mwaka. Chukua kitabu changu Wacha na Dunia ifurahi, na ufunguwe ukurasa 57-62 na uombe juu ya vitu 36 ambavyo kanisa la kwanza waliviombea moja kwa mwingine. Chukua bonde la maono, Kitabu cha maombi cha Waumini cha wanaofuata mafundisho ya Yesu, na uombe yale wataua wakuu wa zama wameyaombea. Sisi ni wapumbavu kufikiri kuwa tukiwachwa pekee yetu tutaona yote Bibilia inafaa iseme na mahitaji yote ambayo inafaa tuombe bila usaidizi wa vitabu.

Muundo #4. Mitindo. Tengeneza mitindo ya maombi ambayo inakupatia mwelekeo fulani ya kufanya ya kwanza na ya pili na ya tatu unapoungama chini. Mtindo mmoja vile nimetaja, ni kutengeneza maombi yako kupitia wosia za ombi la Bwana. Mtindo ninaoptumia kila siku ni mtindo wa miduara dufu. Nikiaanza na moyo wangu mwenyewe-ambao unahisi dhambi na mahitaji kwa ustadi sana- na baadaye kwa familia yangu na baadaye kwa wafanyikazi katika kitengo cha uchungaji na wazee, halafu wafanyikazi wote katika kanisa, halafu huduma wetu, halafu mahitaji ya dharura katika mwili wa Kristo na nia ya Kristo katika huduma na tamaduni. Bila muundo au mitindo fulani kama huu nashikwa na baridi na siendi popote.

Basi mbili za kwanza ni huru na yaliyoumbwa. Yasiyo tengenezwa na yaliyo na mahitaji yatiririkayo na shukrani na sifa; na yaliyotengenezwa na usaidizi kama Bibilia, nakala, vitabu na mitindo. Kama “unadumu katika maombi” utatafuta uhuru na muundo katika maombi.

A - Alone and Assembled (Pekee na ulio kusanywa)

Kudumu katika maombi kutamaanisha kuwa kila mara utaomba pekee yako na kila mara katika mkusanyiko wa Wakristo wengine.

O! ni muhimu sana tunapokutana na Mungu pekee kupitia kwa Yesu Kristo. Hakuna Ukristo bila kujiamini kwako na kupatana na Mungu kupitia Yesu. Yote ni Sarakasi na mabaki na kujidanganya bila hii. Sussana Wesley pamoja na watoto wake 16 alikuwa anafunika kichwa chake katika chumba cha kupikia na watototo wote walijifunza kuwa hii ilimaanisha kimya katika chumba cha kupikia. Watoto wanafaa kujifunza kuwa Baba na mama wana wakati na Yesu ambayo ni tukufu na ambayo haifai itatanishwe. Pata pahali, panga wakati, fundisha watoto wote nidhamu.

Lakini nadhani kuomba katika mkusanyiko wa waumini wengine kunapuuzwa sana kuliko kuomba pekee. Pekee na yaliyokusanywa. Agano Jipya limejawa na mikutano ya jumuiko ya maombi. Yamkini maombi mengi katika Agano jipya yawezekana yamefikiriwa kwa njia ya mkusanyiko wa maombi. Matendo 1:14, “Hawa wote waliungana pamoja katika maombi. Pamoja nao palikuwa wanawake kadha wa kadha na Maria mamake Yesu pamoja na ndugu zake Yesu.” – Hiyo ni mfano ya kile utapata. Matendo 12:12, wakati Petro alipotoka kwenye jela, “alikwenda nyumbani kwa Maria mamake Yohana aliyeitwa pia Mariko, ambako watu wengi walikuwa wamekutana kwa maombi.” Mikutano ya maombi ilikuwa kawaida na nadhani ilikuwa kitendo cha kawaida kwa Kanisa la Kwanza.

Kudumu katika maombi katika Agano Jipya ilijumulisha kuomba pamoja na watu wa Mungu. Je, unafanyaje hili? Hii si ukristo ulioendelea sana. Hii ni Ukristo wa kimsingi Wiki hii tuko na mikutano ya maombi 12 ya muda wa dakika 30 iliyopangwa pamoja na maombi ya masaa 8 usiku kucha ya ijumaa. Yote ni kwa ajili ya kukufanya uwe na upenyo mpya. Katika muda uliosalia ya mwaka kuna mikutano ya maombi ya dakika 30 kwa asubuhi 6 kila wiki, Siku ya Jumatano jioni saa 12 na mbili kasorobo kule jijini. Halafu kuna vikundi vidogo wanao kutana kwa maombi na huduma. Halafu kuna Jumapili asubuhi ambayo inajumuisha maombi kupitia nyimbo na njia nyinginezo. Kama kusanyiko ya maombi si pande ya kudumu kwako kwa maombi, fanya mwaka wa 2003 uwe mwaka wa upenyo: Uhuru na Ulioundwa, pekee na ulio wa mkusanyiko.

D - Desparate and Delighted (Yenye hitaji na furaha)

Kudumu katika maombi kutamaanisha kuwa unamjia Mungu katika maombi kila mara ukiwa na hitaji na kila mara ukiwa na furaha. Kwa urahisi ninamaanisha kuwa ombi ni pahali pa kukutana na Mungu kwa furaha zako kuu zaidi na Shukrani. Kama tandiko ulitumialo kwa kiniko chako unapoungama mbele za Bwana litakuwa tandiko lililorarulika. Na hata hivyo kwa vile Mungu ni Yule asikiaye maombi, Utasema pamoja na mtume Paulo, “Nina huzuni bali kila mara nafurahi.” (2 Wakorintho 6:10) na kila mara nafurahi hiyo itashinda mizigo yote ya Ulimwengu huu iliyoanguka- vile inafaa- na ikufanye utake kuruka kwa furaha. Mungu anataka kukutana nawe hata katika nyakati kama hizo. Dumu katika maombi ya hitaji na kwa furaha- kwa kufunga na kusheherekea. Si kwa mojawapo bali yote na.

E - Explosive and Extended (Ya kulipuka na kuendelezwa)

Yale ninamaanisha hapa ni fupi na ni refu, ningesema fupi na ndefu, lakini herufi hazingeambatana na tamshi halingemaanisha lolote. Tena ya kulipuka ni wazi mno na ni hakika maombi yanaweza kuwa kutoka muda hadi nyingine. Kama unadumu katika maombi, utalipuka kila mara katika maombi ya sifa na ya shukrani na ya hitaji hayatakuwa kwa nasekunde mengi. Na kama unadumu katika maombi utakuwa na wakati wakening’inia kwa muda mrefu katika maombi kwa Bwana. Saa zingine napiga simu ya haraka kwa Noeli na saa zingine tunakaa pamoja kwa muda wa jioni. Kama unampenda Kristo na kumuegemea kwa vitu vyote na kumthamini kwa vyote vile, utakutana naye kila mara katika maombi ya kulipuka na kila mara kwa maombi ya kuendelezwa.

S - Sponteneous and Scheduled (Mara mmoja na yaliyo ratibishwa)

Ni nini tofauti kati ya hii na “huru na yaliyopangwa” ama “ya kulipuka na yaliyoendelezwa”? Kwa “huru na yaliyopangwa” nilimaanisha yaliyomo katika maombi yetu- yale tunafanya tunapokuja kuomba. Kwa “Yakulipuka na yaliyoendelezwa nilimaanisha muda wa maombi yetu. Kwa mara mmoja na yaliyoratibishwa ninamaanisha tunapoomba.

Ikiwa tunadumu kwa maombi tutaomba kwa mara mmoja katika siku- bila kukoma vile Paulo anavyosema- Roho ya umoja kwa pamoja na Kristo, kutembea kwa roho na kumjua kama kitu kinachoishi kwa kuendelea ndani ya maisha yako. Hakuna mpango utakao tawala unapomuongelesha. Itafanyika kwa mara kadhaa katika siku. Hii ni kawaida na vyema. Hii ni kudumu katika maombi.

Lakini ukiwa tu na hii, hutakuwa nayo kwa muda mrefu. Tunda nzuri ya kweli ya mara mmoja hukua katika shamba lililotunzwa vizuri kwa nidhamu ya mpango. Basi nawasihi, uwe na wakati wako uliopangwa kwa ajili ya maombi. Uipange kwa mwaka wa 2003. Lini utakutana naye kila mara? Muda gani utatenga. Nakuhimiza uanze kwa njia hii. Je, uko tayari kupanga siku moja ama siku mbili na nusu mbali pekee yako ama pamoja na rafiki ama na mchumba- si kusoma kitabu bali kuomba kwa masaa mannne au manane. Vipi? Kwa kusoma tu Bibilia yako na kuigeuza yote kuwa maombi Noeli pamoja nami tumekuwa na siku zetu zilizo na utajiri mwingi kwa kuchukua kitabu kifupi cha Bibilia na kusoma sura na kutuliza na kuiombea sura hiyo kwa familia na kanisa letu. Halafu kusoma sura nyingine na kuomba na mengine mengi. Lakini hiyo haifanyiki tu. Lazima ipangwe. Si kwa ghafla. Ni ya kujengwa. Na ni takatifu.

Basi unayo hapo. Neno la Mungu kwetu leo ni, “Dumu katika maombi.” Kaa ndani yake. Kuwa mwaminifu kwayo. Kwa nini? Mungu anatuamrisha tuwe; mahitaji ni makuu na uzima wa milele u taabani; na Mungu anasikia na kutenda mengi katika sekunde tano yale ambayo tunaweza kufanya kwa miaka tano.

Na je tutadumu aje kwa maombi? Mambo haya. Bila hayo maombi YATOWEKA (FADES). Wacha ombi lako liwe….

*F - Free and formed (Huru na lililopangwa)
A - Alone and Assembled (Pekee na la kusanywa)
D - Desparate and delighted (Lenye Hitaji na Furaha)
E - Explosive and Extended (La kulipuka na la kuendelezwa)
S - Spontenoues and Scheduled (La mara mmoja na lililotayarishwa) *

Na Bwana awape roho ya neema na kuzidishiwa kwa wiki hii ya maombi na Mwaka yote.