Kuitwa kuteseka na kufurahi: Kwa ajili ya utakatifu na tumaini

Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na niwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa yeye tunapata njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake;na kufurahia katika tumaini la utukufu wa Mungu. Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti na moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini halitahayarisha; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kuaminiwa katika mioyo yetu na Roho mtakatifu tuliyempata sisi. Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotumia Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida vitu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Natumaini katika majuma manne yajayo kuwasaidia kujiandaa kuteseka kwa ajili ya Kristo. Moja ya sababu kwamba naamini tunafaa kujianda kutesekea Kristo ni kwamba Bbilia inasema tunafaa, na lingine ni kwa sababu hali ya kisasa inasema tunafaa.

Kujiandaa kuteseka

David Barret Mmishonari msomi aliyaandika kitabu chenye maelezo ya nyanja zote na mafunzo au masomo tofauti tofauti yaani Encyclopedia cha Wakristo ulimwenguni cha Oxford (Oxford World Christian Encyclopedia), huchapisha habari za hali ya Jamii ya Wakristo kote ulimwenguni ni kila mwaka akijaribu kutabiri jinsi mambo yatakvyokuwa mwaka wa 2000. Nakala ya mwaka huu aliripoti kuwa mwaka 1980 kulikuwa na waliouwawa kwa ajili ya Kristo kama 270,000. Mwaka huu huenda wakafika 308,000 na mwaka 2000 anakadirisha kuwa 500,000.1 Hawa ni watu wanao kufa zaidi, moja kwa moja kwa sababu ni Wakristo.

Kule Somalia leo kumi ya maelfu ya Wakristo wanatengwa ki makusudi na kuachwa wafe kwa njaa na vitengo hasimu. Tumbo joto kati ya Waisilamu na Wakristo kule Nigeria ni ya makali hatari. Na mamilioni ya Wakristo kule Uchina na nchi zingine nyingi wanaishi katika hatari ya kusumbuliwa na kuhangaishwa na kufungwa gerezani.

Katika nchi yetu yenyewe jamii ya wasioamini kwa ujumla haswa wanahabari na viongozi wasioamini wanazidisha uhasama na ukali wao dhidi ya kanisa za Uinjilisti na maono ya Kibiblia kuhusu haki na mema ambazo ndizo msingi tunazosimamia. Marekebisho ya kwanza ya katiba yamesababishwa ili kutumikia jamii ya wasioamini hivi kwamba haitakuwa jambo ngumu tena kwa wakili fulani kuwasilisha kesi kwamba upeanaji wa huduma za maji na umeme na mabomba ya vyoo na umma kwa majumba ya makanisa ya Kikristo unaruhusu rasilmali na masharti ya Serikali kuimarisha dini, kinyume na katiba

Waandamanaji kwa amani wanaotetea maisha ya mwanadamu ambao wanaomba tu katika sehemu ya mali ya umma wanaweza kudhulumiwa kimabavu na hata kupigwa na wanaotetea uayaji au utoaji mimba kama ilivyofanyika kule Buffalo, New York na wasipokee ulinzi wa polisi bali wapate kushtakiwa na hatia kortini.

Jina la Yesu linadharauliwa na kudhihakiwa wazi na watumbuizaji wakuu kwa kiwango kwamba katika karne zilziopita wangekaripiwa na na kuonekana kutokuwa na nidhamu machoni pa umma, lakini leo inaruhususiwa au inaendelezwa na watu wengine.

Gharama ya wito mkuu

Haya yote yanafikia kwamba, kuwa Mkristo itakgharimu zaidi miaka zijazo. Na kumaliza mwito mkuu itagharimu wengine wetu hata maisha yetu—kama jinsi tayari imekwisha kufanya, na imekuwa ikifanya mara na mara. Miaka elfu moja mia nane iliyopita Tertullian alisema. “sisi [Wakristo] ni mbegu (Apologetius,50), Kisha miaka 200 baadaye Jerome Mtakatifu alisema, “Kanisa la Kristo limewekwa msingi kwa kutiririsha damu yake yenyewe, wala sio ile ya wengine; kwa kustahimili maajabu wala sio wao kuyafanya maajabu hayo. Mateso yameiwezesha kuwa, na kuendelea; Waliouwawa kwa sababu ya kueneza na kutetea injili kwa dhati nao wakaiwekea taji” (Barua 82).

Tunazungumuza sana kuhusu nchi zilizo fumbwa leo kiwango kwamba karibu tupoteze mtazamo wa Mungu kuhusu huduma- kana kwamba alimaanisha huduma itakuwa rahisi na salama. Hakuna nchi zilizofumbwa kwa wale wanaodhania ya kuwa dhiki, kufungwa jela, na kifo ni mojawapo ya uwezekano kwa ajili ya kueneza injili. Naye Yesu alisema wazi kwamba hayo ni mambo yanayowezekana. “Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki nao watawaua; na ulimwengu utawachukia kwa sababu yangu.” (Mathayo 24:9). “Kama walinidhikisha nanyi watawadhikisha” (Yohana 15:20).

Mpaka turejee mtazamo wa Mungu kuhusu mateso na kueneza injili, hatutafurahia ushindi wa neema anayopanga.

Utiifu katika ma misheni na haki ya kijamii daima imekuwa ya gharama kubwa, na itakuwa kila mara. Katika kijiji cha Miang’o, Nigeria, kuna chumba cha wageni cha SIM na kanisa ndogo pale liitwalo Kanisa la Kirk. Nyuma ya kanisa hili kuna makaburi 56. Kati ya yale makaburi thelathini na tatu yamebeba miili ya watoto ma mishenari. Majina kwenye makaburi haya yameandikwa “Ethyl Arnold: Septemba 1, 1928–Septemba 2, 1928.” “Barbara J. Swanson: 1946–1952.” “Eileen Louise Whitmoyer: Mei 6, 1952 – Julai 3, 1955.” Hii ilikuwa ndio gharama ya kupeleka injili Nigeria kwa familia nyingi miaka hizi za karibuni. Charles White alihadithia kuhusu ziara yake katika makaburi haya na kamaliza kwa sentensi moja yenye nguvu kuu. Alisema, “Njia ya pekee ya kuelewa makaburi ya Mihang’o ni kukumbuka kuwa Mungu pia alimzika mwanawe katika uwanja wa umishenari.”2

Na alipomfufua kutoka kwa wafu, alilialika kanisa kumfuata katika uwanja ule hatari uitwao “ulimwengu wote.” Lakini je unahiari ya kufuata?

Je Unafanyia Nini Timotheo wa Pili 3:12?

Miaka miwili iliyopita, ule Ermelo, Uholanzi, Ndugu Andrew alinihadithia jinsi alivyoketi kule Budapest, Hungary, na wachungaji kama kumi na wawili hiviwa mji huo akiwafundisha kutoka kwa Biblia. Kisha akaingia mchungaji mmoja mzee, rafiki yake wa kutoka Romania na ambaye hivi karibuni alikuwa amefunguliwa kutoka gerezani. Ndugu Andrew akasema alikoma kufundisha maana alifahamu ilikuwa wakati wa kusikiliza.

Baada ya kimya kwa muda Yule mchungaji Mromania akasema, “Andrew, je, kunao wachungaji wowote katika magereza Uholanzi?” “La,” akasema. “Kwa nini hawapo?” Mchungaji Yule akauliza. Ndugu Andrew akawaza kwa muda mfupi kasha akasema, “Nafikiri ni kwa sababu hatutumii fursa zote ambazo Mungu anatupatia.”

Kisha akauliza swali ngumu kabisa. “Andrew, mnafanyaje kuhusu Timotheo wa Pili 3:12?” Ndugu Andrew akafungua Biblia yake mpaka kwa andiko hilo kasha akasoma kwa sauti, “Wanaotamani kuishi maisha ya kiungu katika Yesu Kristo atadhikishwa.” Akafunga Bibilia yake pole pole na kusema, “Ndugu, tafadhali nisamehe. Hatuifanyii chochote fungu hilo.”3

Ninatoa hofu kuwa ,tumebinafsisha sana dhana ya uungu kwa kiwango cha kukosa makali ila ikawa kama hali ya ki nidhamu ya ki wastani na uhifadhi sheria mapka 2 Timotheo 3:12 ikawa yenye maana duni kwetu. Ninafikiri kuwa wengi wetu hawajajiandaa kuteseka kwa ajili ya injili. Ndio sababu naahisi wito ili nichukue majuma manne ya kushughulika na Bibilia jinsi inavyosema kuhusu jambo hili na Mungu anachotuitia leo.

Madhumuni nne za biblia za kuteseka

Kila ujumbe unaoambatana na mojawapo ya kusudi za kuteseka. Na twaweza kuzungumza kuhusu kusudi za kuteseka kwa sababu ni wazi kuwa ni kusudi la Mungu kwamba wakati mwingine tuteseke kwa sababu ya haki na vile vile injili.Kwa mfano, “Basi hao wateswa kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kwa Muumba mwaminifu (Waraka wa kwanza wa Petero 4:19; Waraka wa Waebrania 12:4-11).

Kusudi nne za kuteseka nilizo nazo wazoni ni

  1. Kusudi ya nidhamu, kwa sababu mateso hufisha utakatifu na matumaini yetu (Warumi 5:1-8)
  2. Kusudi ya usuhuba, kwa sababu katika mateso uhusiano wetu na Kristo unazidishwa na unakuwa mtamu zaidi (Wafilipi 3:7-14)
  3. Kusudi za misheni, kwa sababu Mungu anatuita kukamilisha maudhui ya Kristo tunapoendeleza gharama yake kupitia ile ukweli wetu (Wakolosai 1:24)
  4. Na kusudi la utukufu, kwa sababu wakati huu mdogo wa maudhui unatutenda kuwa na uzani wa utukufu wa milele. (2 Wakorintho 4:16-18)

Kusudi ya kinidhamu (kiroho) za kuteseka

Leo hii tunaangaliza kusudi za nidhamu (kiroho) za kuteseka. Mungu anateua kwamba kuteseka kwa ajili ya injili na kwa haki kwa sababu ya athari ya kinidhamu na ki Roho juu yetu.

Kutukuka katika matumaini ya utukufu wa Mungu

Na tusome sehemu mojawapo ya maaandishi makuu kwa mada hii: Warumi 5:3-4. Baada ya kuonyesha kwamba tunasimama kwa wema, anasema katika fungu la 2 kwamba sisi Wakristo “tufurahi katika matumaini ya Utukufu wa Mungu. “Sababu kuu ya furaha katika maisha ya Mkristo ni tarajio kwa hamu kwamba tutaona na kushiriki katika utukufu wa Mungu. Tumaini katika utukufu wa Mungu ndio moyo wa furaha yetu.

Sasa kama hiyo ni kweli, basi Paulo anaendelea katika utimilifu wa kusema katika kifungu cha 3 na cha 4 kuwa pia tutafurahia katika vitu vinavyo sababisha ongezeko ya matumaini yetu. Huu ndio mstari wa kuwazia hapa: tunaanza na matumaini ya utukufu wa Mungu katika mwanzo wa fungu la 2, kisha ndipo tunamaliza na matumaini mwisho wa fungu la 4. Cha muhimu ni kama tukifurahia matumaini, tutafurahia kinacholeta matumaini hayo.

Nini kinacholeta matumaini

Kwa hivyo katika vifungu vya 3 na vya 4 hebu eleza ni nini hii. “Wala sivyo tu [Si tu kwamba tufurahi kwa matumaini ya Utukufu wa Mungu] ila na mfurahi katika dhiki pia, mkijua kuwa dhiki kazi yake ni kuleta saburi, na saburi [hudhihirisha] kazi yake ni kuleta uthabiti wa moyo [tabia iliyothibitika]; na kazi ya uthabiti wa moyo ni kuleta [kudhihirisha] tumaini.”

Kwa hivyo sababu za sisi kufurahi katika dhiki si kwa sababu tunapenda uchungu au mashaka au ukosefu na staarabu au taabu (sisi sio machoists) Lakini kwa sababu dhiki huleta yale tunayopenda, yaani hisia za matumaini zilizo na nguvu zaidi na zaidi zinazokuja kupitia ile hali tupitiayo ya kuwa na uvumilivu kwa muda na hisia za kuthibitika.

Mungu anakusudi katika mateso ya watu wake

Kwa hivyo somo la muhimu hapa ni kuwa Mungu ana kusudi katika mateso ya watu wake. Na kusudi hilo mara nyingi huwa tofauti na lengo na huduma ambalo wanalifanyia kazi. Lengo la huduma huenda ni kuwahubiri wale wasio na kanisa ilhali pia wako katika hali ya upweke kwa hali ya uchumba na ndoa, katika Twin Cities, au hata wataalamu katika miji ya kitajiri, au Waisilamu wa Uturuki. Lakini kusudi la Mungu liweze kuzaa matumaini zaidi katika huduma na Wamishonari kwa kuwaweka katika magereza. Kila mara Mungu anatenda zaidi ya hayo (Kama tutakavyo ona katika majuma yajayo), lakini hayo yatatosha.

Kwa maneno mengine Mungu huenda hatazungumza kuhusu kuzaa na utenda kazi kwa ubora wa huduma kila hatua kama sisi tuwezavyo. Tena na tena Paulo alikumbana na kazi ya Mungu ya ajabu katika kutiwa kwake gerezani na kupigwa chombo kikazama majini na mipango yake yalioharibika. Ingekuwaje kwamba Mungu asifanye juhudi ila akamwacha ili misheni yake iweze kuzuiliwa hivi mara na mara tena? Jibu ya maandishi haya (sio tu jibu) yatakuwa : Mungu amejihusisha katika kuongeza matumaini na utakatifu na watu wake katika harakati ya kuwafikia waliopotea. Na Mungu pekee ndiye ajuaye jinsi ya kuzifanya hizo na kuzisababisha kutimia katika njia bora zaidi.

Athari tatu za dhiki

Sasa hebu tuangalie athari hizi za dhiki kwa makini haswa. Kuna athari tatu haswa zilizotajwa katika fungu la 3 na 4.

1) Kustahimili

Kwanza dhiki huleta kustahimili au uvumilivu katika saburi. Paulo hamaanishi kuwa hii ni jambo la kweli ulimwenguni kote. Kwa wengi, dhiki hufungulia chuki na uchungu na hasira na manung’uniko na dharau. Lakini hii sio athari inayoendelea kwa wale walio na Roho wa Kristo. Kwao athari hiyo ni uvumilivu katika saburi, kwa sababu tunda la Roho ni uvumilivu.

Kwamba jambo kuu ni mpaka magumu yaje maishani mwetu, sana ugumu kwa sababu ya Kristo na haki yake,hatuoni ukuu na undani wa kujitoa kwetu kwa Kristo. Mpaka nyakati yawe magumu, hatuonji na kufahamu kweli kama sisi ni Wakristo wepesi- kama wale Yesu anaoeleza katika fumbo la udongo katika Mariko 4:16-17.

Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye miamba ambao kwamba wakiisha kuhisikia lile neno, mara hulipokea kwa furaha; ila hawana mizizi ndani yao bali hudumu muda mchache; kisha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno mara hujikwaa.

Kwa hivyo, Paulo anasema kuwa mojawapo wa athari ya dhiki ni kuwa inalete uvumilivu, kustahimili na saburi katika maisha ya watu wa Mungu, kwa hivyo wanaweza kuona uaminifu wa Mungu katika maisha yao na kujua kuwa wao kweli ni wake.

2) Asili ya Kuthibitika

Hiyo ndiyo dhana ya athari ya pili ambayo imetajwa (fungu la 4). “Na (hii ) saburi kazi yake ni kuleta uthibiti wa asili.” Kwa maana ya juu neno dokimen lamaanisha “hali ya kujaribiwa na kuthibitiwa. Tunaweza sema uthabiti au kuthibitika.”

Hii sio ugumu kuelewa kama, dhiki zikija unafanya kuwa na saburi katika kujitoa kwa Kristo. Na usimpe mgongo, basi unatoka katika mapito hayo na hisia yenye uzito kuwa wewe ni wa kweli, thabiti, sio mnafiki. Mti wa kuaminika ulikunjwa wala hakumvunjika. Ukweli wako na uaminifu zilipitishwa katika majaribu nayo yakapita. Sasa zina “asili ya kithibitika.” Dhahabu ya imani yako iliwekwa motoni nayo ikatoka imeoshwa, wala haikuchomwa.

Katika majaribu ya moto njia zako nitalala,
Neema yangu, inatosha yote, nitakuwa mpaji wako
Moto hautakuchoma, naliunda tu mema yako
Kuyala na dhahabu yako kusafisha.

Hiyo ndio athari ya pili ya dhiki: Uthabiti na kuosha dhahabu ya uaminifu wetu kwa Kristo. Saburi huleta hakikisho ya uthabiti.

3) Matumaini

Athari ya tatu yaja kutoka katika hisia ya kuwa umejaribiwa na kuthabitika na kuoshwa. Fungu la 4b. “Na uthabiti (unaleta) kazi yake ni kuleta matumaini.” Hii inaturejesha nyuma mpaka kwa fungu la 2: “Tunafurahi katika matumaini ya utukufu wa Mungu.” Maisha ya Ukristo unaanza na matumaini katika ahadi za Mungu katika Injili nayo inasambaa na kuingia katika dhiki na zaidi ya matumaini.

Uthabiti unaleta matumaini zaidi kwa sababu matumaini yetu yanakuwa wakati tunapitia ule udhahiri wa uhalali wetu kupitia kujaribiwa. Watu wanaomfahamu Mungu vyema ni wale wanaoteseka na Kristo. Watu ambao daima hawabanduki katika matumaini yao ndio wale ambao wamejaribiwa kwa urefu wale wanao tazamia na shauku kuu na bila kuchoka matumaini ya utukufu ndio wale ambao wamepata faraja ya maisha haya yakiwa yametandazwa katika dhiki.

Furaha katika matumaini ya utukufu wa dhiki

Kwa hivyo jambo la kwanza tunasema kuhusu mateso na dhiki katika nakala hii ni kuwa Mungu ana kusudi kwayo na kusudi hilo ni kuchipua ule uvumilivu na saburi ya watu wake kwa ajili ya jina lake; na kupitia hiyo kujaribu na kufanya thabiti na kusafisha udhahiri wa imani na uaminifu kwa Kristo; na kupitia hiyo hisia ya kuthabitika kutia nguvu na kimo zaidi na kutia nguvu matumaini yetu.

Tuna malengo ya huduma kama kanisa (Kufanya wanafunzi katika miji, uchungaji wa vikundi vidogo, kufanya uinjilisti ya mitandao, kutetea watoto ambao hawajazaliwa; kukusanya vijana na watoto); Tuna maono makuu ya kimishonari ya kutuma 2000 kufikia mwaka wa 2000; tuna jengo la kulipia na makadirio ya kuifadhili kifedha haya yote kwa ajili ya Kristo na Ufalme wake. Zaidi kiasi gani ya ukuu wa uweza wake ambayo atasababisha kuja kutimia, sijui. Lakini nafahamu kuwa katika kutii kwetu kufuata malengo haya Mungu ana kusudi lake kwa kila kizuizi na kila wakati tunapohangaishwa na kila uchungu tunayopata na kiladhiki tunayopitia, na kusudi hilo ni la muhimu kama vile malengo hayo yenyewe- saburi yako, uthabiti wako wa asili, na matumaini yako kwa utukufu wa Mungu.

Kingine chote ambacho Mungu anaweza kuwa anafanya katika kiwango cha kupangia maisha yetu, haya yeye hufanya katika kimo cha moyo wa maisha yako. Na basi pamoja na Paulo hebu tufurahi katika matumaini ya utukufu na pia katika dhiki zijazo.


1 International Bulletin of Missionary Research, vol. 16, no. 1, January 1992, p. 27.

2 Charles White, "Small Sacrifices," Christianity Today, vol. 36, no. 7, June 22, 1992, p. 33.

3 Taken from the foreword to Herbert Schlossberg, Called to Suffer, Called to Triumph, (Portland: Multnomah Press, 1990), pp. 9–10.