Mungu hakuyaachia Mwanawe mwenyewe

Nasi  twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapa mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. 29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu sili wapatanishwe na mfano wa mwana wake, ili yeye awe mwana wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi; 30 na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki, hao akawatukuza. 31 Basi tuseme nnini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? 32 Yeye asiyemwachilia mwana wake mwenyewe bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?

Ukweli zingine hutusababisha kushangaa; Warumi 8:28-30 ulimshangaza Paulo. Yote yanatendeka kwa wema—Mungu hufanikisha, kwa sababu alikujua tangu asili, alikuchagua kwa utukufu wa Kristo, kakwita ukiwa mfu kwa uasi na dhambi. Akakutukuza polepole mpaka wakati wake wa kuja. Wakati utakapo badilishwa mwili kama wa Kristo uliofufuliwa.

Jambo hili karibu linamshangaze Paulo. Anasema, “Tusemeje basi kuhusu mambo haya?” N’naya sikia mambo mawili kwa maneno hayo kwa Paulo na kwetu sisi. N’nasikia, “ Ni vigumu kupata maneno kwa mambo haya makuu.” N’nadhani wakati Paulo asemapo, “Tuseme nini kuhusu mambo haya?” Jiba u lake ni: Ni lazima tuiseme tena kwa njia nyingine. Ni lazima tupate maneno tofauti ya kuisema tena. Haya ndiyo anayofanya na maneno, “Kama Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye juu yetu?” Maneno haya amekuwa akiyasema. Lakini ni sharti ayaseme kwa tafsiri  nyingine.

Na basi hata nasi ni lazima. Kama umewahi kushiriki injili tukufu na mtoto au mzazi ama rafiki mara nyingi, ni laima ufanye vile tena, linene tena kwa njia ingine. Ni lazima tuandike barua nyingine pepe, andika barua ingine kwa imla, tufundishe mafunzo mengine, tengeneza mabango mengine, andika shairi lingine na uimbe wimbo mwingine, mwambie babaa fulani mwenye afya mbovu, kando ya kitanda chake. “Basi tuseme nini kuhusu mambo haya?”  Tuyaseme  kwa njia ingine, mara na mara mpaka kifo kisha kwa milele yote. Hapatakoma kuwa njia inayostahili kuwa njia linguine la kueneza injili tukufu.

Mungu yu kwetu

Wakati huu Paulo asemaje katika mlango 31? Anasema “Kama Mungu akiwa upande wetu ni nani atakaye kuwa juu yetu ama atakaye tupinga?” Na lengo lake ni kujumlisha na yale yaliokuwa mbele: Mungu ni wetu, basi hakuna awezaye kutupinga. Mungu alitujua tangu asili, alitufanyia hatima ya kuwa wana tangu asili, akatuita toka kwa wafu, akatuita haki, na atendakazi ndani yetu kutoka kwa kiwango kimoja cha  utukufu hadi kingine mpaka siku ile kuu na wenye furaha, siku ya Kristo. Tutalisemaje tena? Tutasema, “Mungu ni wa upande wetu.”

O maneno haya mawili ni ya dhamani kiasi gani, “upande wetu.” Hakuna maneno mengine ulimwenguni ambyo ni ya kutisha kiasi ya, “Mungu yu kinyume chetu.” Kama ghadhabu kuu isio na kipimo ikiwa kinyume chetu, basi kufagiliwa au kuondolewa kabisa ulimwenguni itakuwa ni dhawabu tamu ya neema. Ndiposa wanaojaribu kutuhawishi kuwa kuondolewa ulimwenguni kabisa ndio maana ya hukumu, wala sio jehanamu, wameacha njia pakubwa. Kuondolewa kabisa ulimwenguni kwa sababu ya ghadhabu ya Mungu sio hukumu, ni ukombozi na msaada (ona Ufunuo 6:16). Hapana. Hakuna kuondolewa kabisa utakaotendekea mwanadamu tena. Milele tuaishi pamoja na Mungu akiwa kinyume chetu au akiwa wa  upande wetu. Na wote walio ndani ya Kristo watasema wakiwa karibu na (!) furaha isio na kifani, “Mungu ni  wa upande wetu.” Yu upande wetu.

Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu (Warumi 8:1) Mungu yu kwa vyote, upande wetu wala kamwe hatakuwa kinyume yetu. Hakuna moja ya magonjwa yetu yatakuwa ni adhabu ya hukumu kwetu kutoka kwa hakimu asiyesamehe. Magari yetu yalio haribika au mashine zilizo haribika nazo sio ishara ya adhabu ya Mungu. Tofauti za ndoa sio ishara ya ghadhabu yake. Wala kazi tulizofutwa sio kichapo kwa sababu ya dhambi. Hapana watoto wsio na nidhamu ambao ni adhabu kwa hasira  ya Mungu. Tukiwa ndani ya Kristo. La. Mungu ni wa upande wetu wala sio kinyume yetu, kwa na katika mambo yote—yawe mepesi au machungu.

Ni nani aliye dhidi yetu?

Maana yake ni, kuisema tena kwa njia tena ingine, “Ni nani aliye kinyume yetu?” Tungali katika mlango wa 31: “Kama Mungu ni wa upande wetu ni nani atakayetupinga?” Ambapo tuna mazoea yakusema, “Kweli?” Hiyo ina maana gani? Mlango 35 inasema kwamba kutakuwa na mateso na mahangaiko na kuuawa kwa upanga. Mlango 36 inasema kwamba waKristo wanauawa mchana kutwa, wanahesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa. Paulo alisema hayo. Basi maana ya kusema, “Ni nani aliye kinyume yetu?” Ninafikiri ana maanisha hakuna atakayefaulu kutupinga.

Sheitani na wenye dhambi wanaweza kukufanya kuwa mgonjwa, waweza kuibagari lako, wanaweza kupanda mbegu ya uhasama katika ndoa yako au kukunyang’anya kazi au mtoto wako. Lakini mlango wa 28  unasema kwamba Mungu anatenda haya yote pamoja kwa ajili ya wema wako kama wampenda. Na kama yakitendeka hatimaye kwa wema wako, mitindo ya adui yanavunjiliwa mbali na lengo lake la kukupinga linageuzwa likawa la kuinua jina la Kristo, kutakasa nafsi, kuongeza imani, manufaa machungu. Kama mungu ni wa upande wako, hatakuzuia vitu hivi.Lakini anakuundia mema mahali naye adui anapopanga maovu (Mwanzo 50:20; 45:7). Mambo yalio kinyume chako anayaunda yakawa ya upande wako. Hakuna atakayefaulu kuwa hasimu wako.

Litakuwa na kishindo kikuu kiasi gani jambo hilikatika maisha yetu! Hatustahili kuwa kama ulimwengu kama mambo yakiwa hivi. Wengi ulimwenguni wanchagua njia ya maisha yao wenyewe kwasababu wanaogopa ugonjwa na wizi na ugaidi na ukosefu wa kazi na mengine mengi. Lakini kwa mfuasi wa Yesu, Bwana anasema, “Mataifa wanaytafuta haya yote. Ninyi tafteni kwanza ufalme kanza" (ona Mathayo 6:32-33). Mungu atawapeeni mahitaji yenu. Na kile mpotezach au kukosa katika huduma ya ufalme wa upendo na dabihu na mateso itakutendea kwa wema na kukurudia, katika njia mojawapo ya muundo wa Mungu, mara mia.

Kwa hivyo simama mbele ya hasimu wako na uinene injili, uwe Kankan, Guinea, au Istanbul, Uturuki, au Tentara, Indonesia, au Minneapolis, Minnesota. Na uyaseme maneno hayo kwa wale waliopanga hata kuondoa uhai wako: “Fanya yanayokulazimu kufanya, lakini hatimaye maneno yako yote na majeraha yako yote yatanoa imani yangu, yataongeza dhawabu yangu, na kunipeleka Paradiso pamoja na Yesu Kristo aliyefufka.” O tofauti ulioje kama tukiamini kuwa Mungu akiwa upande wetuhakuna atakaye simama kinyume chetu.

Makuu ya maana kule mbinguni

Na sasa tusemje kwa hiyo? Mtume Paulo ataongeza nini kwa jambo hilo? Atalisema bado kwa tena njia lingine. Katika mlango wa 32 kwamba sio tu ahadi kwamba hapana mahasimu bali tena ameahidi ukarimu kamilifu, kwa utele wake kutoka kwa Mungu; na yote hayo kwa msingi imara wa kifo cha mwanawe kwa ajili ya wenye dhambi. “Hakumzuia mwanawe mwenyewe, lakini alimtoa kwetu kwa ajili ya sisi sote, atakosaje pia pamoja naye kutupa—vote! Ukweli dhabiti wa Mbingu.

Mwanawe mwenyewe

Tafakari kwanza sehemu za maneno. Kwanza maneno “Mwana wake mwenyewe.” Yesu Kristo hakuwa mwanadamu ambaye Mungu alibuni na kumfanya awe wake duniani. Yesu Kristo ni Yule aliyekuwa tangu asili; kwa kweli alikuwepo, amekuwepo mileleyote, ambaye hakuumbwa, wa milele pamoja na Baba (Mungu), akiwa na umbo la kiungu na Baba ambaye kwake, ukamilifu wa Ufalme unadumu (Wakolosai 2:9) Kumbuka kutoka kwa Warum 8:3 kwamba Mungu alimtumia mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwili wenye dhambi.” Kwa tafsiri linguine Mwana alikuwepo kabla ya kuichukua mwili wa mwanadamu. Yeye siye tu nabii bali ni Mungu Mwana.

Na mlango wa 32 unapomwita Mwana “wake mwenyewe”, sababu ni kuwa hakuna wengine na kuwa ni yeye wa dhamana kuu kwake Baba. Yesu akiwa ulimwenguni Mungu alisema mara mbili, “Huyu ndiye Mwanangu nimpendaye” (Mathayo 3:7: 17:15). Katika Wakolosai 1:13 Paulo anamwita Mwana Mpendwa wa (Mungu). Yesu mwanyewe alitoa fumbo waliokodisha shamba la mizabibu nao watumishi wa Bwana walipigwa na ku uawa walipoenda kuchukua matunda. Kisha Yesu anasema kuwa alikuwa na mwingine bado ambaye ni Mwana mpendwa (Marko 12:6). Baba alikuwa tu na mwana mmoja ambaye alimpenda kwa dhati. KIsha akamtuma mwanawe huyo wa pekee

Nina wana wane. Hakuna upendo mwingine ufananao na ule kati ya baba na  mwana. Usinielewe vibaya. Nampenda mke wangu  na hata binti yangu vile vile. Kisha nampenda baba yangu na wenzangu kazini, hapa kanisani na hata wewe. Hivi simaanishi kwamba aina hizi za upendo hazina uzito kama upendo ule kati ya baba na mwana, bali upendo huu  wa baba na mwanawe ni tofauti. Zote hizo pia ni tofauti lakini niruhusu niseme tu kuhusu upendo huu: Hakuna upendo kama ule wa baba na mwanaye.

Maana ya mlango wa 32 ni kuwa upendo huu wa Mungu kwa mwanawe wa pekee ulikuwa kamakizuizi kikubwa kama mlima Everest uliosimama kati yake na wokovu wetu. Hapa kuna kizuizi kilicho kigumu kuondoa. Je, Mungu angeweza, angefanya kuushinda upendo wake mkuu, wa kutamanika, na wenye joto jingi na uzito mkuu kwa mwanawe ili apate kulawitiwa na kusalitiwa, kisha kukataliwa na kudhihakiwa, apigwe mijeledi, atemwe mate na kusulubuwa msalabani na kuchomwa mkuki kama mnyama anayechinjwa. Angefanya hivyo kweli? Je angemtoa mwana wake wa upendo? Kama hivyo hakuna kingine ambacho kingezuiwa kama akitaka kulitenda. Kama kizuizi kikuu zaidi kilishindwa katika ari  yake ya kutenda wema kwa watu wake, kila kizuizi hakika kitashindwa.

Je, alifaulu?  Jibu la Paulo ni ndio, kisha anaiangalia kwa mitazamo miwili, hali ya kuridhisha na kutoridhisha: ”Hakumzuia lakini alimtoa.” Kwa maneno haya, “hakumzuia,” tunasikia uzit wa hali hiyo ngumu na kizuizi. Mungu hakufurahia uchungu na dharau kwa mwana wake. Jambo hili lilikuwa lenye uchungu sana kwa Mwana wa Mungu akitendewa. Dhambi ilikuwa imefika kilele chake wakati huo. Asili yake ilifunuliwa—kwamba ni uvamizi dhidi ya Mungu. Dhambi zote—zilizo zetu—ni uvamizi dhidi ya Mungu. Kukataliwa kwa Mungu uvamizi wa haki yake na kweli na wema wake. Lakini Mungu hakumzuia Mwana wake hata kutendewa maovu haya.

Alimpeana

Badala yake ”alimpeana.” Usikose kupata hili. Karibu kila kitu ulimwenguni kilicho cha dhamana na umuhimu kinakutanika hapa wakati huu usio wenye matukio yasio na kifani. Upendo wa kiungu kwa mwanadamu, na chuki cha kiungu kwa dhambi, zinakutana hapa. Hekima isio na  mwisho na nguvu zinakutana hapa. Uhuru timilifu na wa kiungu na uzito wa milele kwa mwanadamu wa kujitolea hesabu na matendo ya kibinadamu yanakutana hapa. Hekima isiyo na mwisho na nguvu zinapatana hapa— Mungu alipomtoa mwana wake mwenyewe ili afe.

Biblia yasema Yuda alimsaliti (Marko 3:19), naye Pilato alimpeana (Marko 15:15) na Herode na Wayahudi na mataifa walimtoa (Matendo 4:27-28), na sisi tulimtoa (1Wakorintho 15:3; Wagalatia 1:4; 1Petro 2:24). Inasema hata kuwa Yesu alijitoa (Yohana 10:17; 19:30). Lakini Paulo anasema jambo la muhimu hapa katika mlango wa 32. Katika, nyuma ya, chini ya na kupitia yote haya ukombozi wa mwanadamu, Mingu alikuwa anamtoa mwana wake ili afe. “Mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa na kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulubisha msalabani kwa mikono ya watu wabaya, wakamwua” (Matendo 2:23). Katika Yuda, Pilato, Herode, vikundivya Wayahudi, askari wa mataifa na dhambi zetu, na unyenyekevu wa kusadiki kwa Yesu, Mungu alimtoa Mwana wake. Hakuna kikuu zaidi ya hiki kimewahi kutendeka.

Kama haya ni kweli, kisha?

Tusemeje kuhusu haya? Tutasema, “Makuu ya maana mbinguni ni mazito!” Kama kweli Mungu alimtoa Mwana wake, basi . . . nini? Jibu:   Basi pamoja naye atatukirimia na mambo yote. Kama Mungu hakumzuia Mwana wake mwenyewe, hatatuzuia chochote kizuri. Ni ununuzi wa mwisho na utimilizaji wa  Zaburi 84:11, “Hatatunyima kilicho chema waendao kwa ukamilifu.” Hii ahadi katika msingi wa 1 Wakorintho 3:21-23, “Basi mtu yeyote na asijifie mwanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu; kwamba  ni Paulo au Apolo, au Kefa; dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwepo; vyote ni vyenu; nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.” Huu ndio muhuri wa ahadi ya Waefeso 1:3, “Atukuzwe Mungu, Baba ya Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubarikikwa baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa roho ndani yake Kristo.” Huu ndio kuweka salama ahadi zake Yesu kwa maneno, “Msisumbuke basi mkisema, “Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?”…Kwasababu Baba yenu wa Mbinguni anajua yakuwa ni mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake na hayo yote mtazidishiwa” (Mathayo 6:31-33).

Kwa maana hakumzuia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu, kwa hakika ya nidhamu yote, atatukirimia yote naye. Kweli? Yote? Je na mateso au fadhaiko au hukumu au njaa au dhiki au uchi au upanga” (Warumi 8:35)?  Jibu ni matamshi haya ya ya ajabu ya John Flavel kutoka miaka 350 iliyopita:

Hakumzuia Mwanawe mwenyewe, bali alimtoa kwetu sote; Atakosaje kutukirimia mambo yote pamoja naye?” (Warumi 8:32). Itawezekanaje kwamba mungu atunyime, baada ya haya, mambo ya roho au kimwili sisi watu wake? Atawezaje kukosa kuwaita moja kwa moja, awafanye haki bure, awatakase kabisa na kuwatukuza milele? Atakosaje kuwavisha, kuwalisha kisha awalinde na kuwakomboa? Kwa kweli hangemzuia mwanawe mwenyewe kichapo kimoja, mchipuko mmoja, kilio kimoja, hali moja ya fedheha, haitafikiriwa kuwa angeweza, baada ya haya, kutunyima aukuzuia watu wake, ambao kwa ajili yao mateso hayo yakaja, rehema zozote, faraja zozote, fursa yoyote, ya roho au mwili, ambayo ni zuri kwao.

Kila wakati Mungu anatutendea mema. Kama unaamini kwamba alimtoa mwana wake kwa sababu yako, basi hivi ndivyo unavyoamini. Maisha yote ya uKristo ni matunda ya imani hiyo. Mtazame Kristo. Tazamia upendo wa Mungu. Ishi kwa upendo. Usiogope tena.