Mungu aliwahesabu haki waovu

Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirishwa pasipo sheria, ingawa sheria na manabii wanaishuhudia, haki ya Mungu kupitia imani katika Yesu Kristo kwa wote wanaoamini. Maanake hakuna tofauti; kwa vile wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wanahesabiwa haki kwa neema yake kama kipaji, kupitia ukombozi ulio katika Kristo Yesu, ambayo Mungu aliweka mbele kama kafara kwa damu yake, ili ipokolewe kwa imani. Hii ilikuwa ili ionyeshe haki ya Mungu, kwa vile katika uvumilivu wake wa, kiungu alikuwa amepita dhambi za kale; ulikuwa ya kuthibitisha kwa wakati huo kuwa yeye mwenyewe ni mwenye haki na kuwa anawahesabu haki walio na imani katika Yesu. Hivyo basi nini itafanyika kwa fahari yetu? Imefungiwa nje. Kwa kanuni gani? Kwa kanuni ya matendo. Hapana, lakini kwa kanuni ya imani. Maanake tunashikilia kwamba mtu huhesabiwa haki pasipo matendo ya sheria. Au Mungu ni Mungu wa wayahudi pekee? Si yey ni Mungu wa Mataifa yote pia? Naam, wa Mataifa mengine pia, maanake Mungu ni Mmoja; na atawahesabu haki waliotahiriwa kupitia msingi wa imani yao na wasiotahiriwa pia kupitia imani yao. Je, tunapindua sheria kwa imani huu? La hasa! Ilhali, tunazingatia sheria. Ni nini basi tutakachosema kuhusu Abrahamu, babu wetu kwa jinsi ya mwili? Kwa maana ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa kupitia matenda, basi ana kitu cha kujivunia, lakini si mbele ya Mungu. Kwa maana hi Maandiko matakatifu yasemaje? "Abrahamu alimwamini Mungu, na ikahesabiwa kwake kuwa haki." Sasa kwa yule afanyaye matendo, mshahara yake haihesabiwi kama kipaji bali ni mapato yake. Na kwa yule ambayo haja fanya matendo lakini ana mtumaini yule anaye hesabu haki waovu, imani yake inahesabiwa kama uadilifu. Hivyo pia Daudi anatangaza baraka kwa yule ambaye Mungu amehesabu kuwa haki pasipo matendo: "Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimefunikwa. Heri mtu yule ambaye Bwana hamwesabii dhambi na ambaye rohoni mwake hamna udanganyifu."

Utetesi wa haki ya Mungu

Wiki iliyopita nilijaribu kuonyesha kwamba tatizo kamili iliotatuliwa katika kifo cha Kristo ilikuwa tatizo kwamba Mungu mwenyewe alionekana kuwa mwovu kwa kupitia dhambi nyingi zilizostahili hukumu. Kwa jumla, Agano la Kale ni ushahidi kwa ukweli kwamba Mungu " ni mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi" (Kutoka 34:6-7).

Pia nilisema kuwa hatuwezi hisi kamwe tatizo hili hadi wakati tutamweka Mungu mbele katika fikira zetu kuhusu dhambi na haki.

Dhambi (Warumi 3:23) kwa hakika si hatia dhidi ya binadamu. Ni hatia dhidi ya Mungu. "Wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu." Dhambi daima ni kuthamini choche duniani kuliko Mungu. Ni kudharau utukufu wake. Ni kutoheshimu jina lake.

Lakini haki ya Mungu ni ahadi yake kutenda yale ambaye hatimaye ni wa haki—yaani, kuzingatia heshima ya jina lake na thamani ya utukufu wake. Haki ni kinyume wa dhambi. Dhambi hudharau thamani ya Mungu kwa kuchagua dhidi yake; haki (uadilifu) hutukuza thamani ya Mungu kwa kuchagua kwa ajili yake.

Basi, wakati Mungu anapopita dhambi na kuwaacha waovu bila kuwaadhibu katika haki, yeye huonekana kama ambaye hana haki. Huonekana anasema: mzaha kwa thamani yangu si muhimu; kudharauliwa kwa utukufu wangu si hoja; kufedheheshwa (kuchafuliwa) kwa jina langu haijalishi. Ikiwa hayo ni kweli,

Mungu angekuwa mwovu. Nasi tungekuwa bila matumaini. Lakini Mungu hakuiruhusu iwe kweli. Alimweka mbele mwanawe, Yesu Kristo, ili kupitia kifo chake angefahamisha kuwa Mungu ni mwadilifu. Kifo cha mwana wa Mungu ni onyesho wa thamana ambao Mungu huweka katika utukufu wake, na jinsi anvyochukia dhambi, na mapenzi yake kwa waovu.

Kuhesabiwa Haki kwa waovu

Neno nyingine kuhusu huu kupita kwa dhambi ambayo ulimfanya Mungu kuonekana mwovu ni "kuhesabiwa haki"—kuhesabiwa haki kwa wasiomcha Mungu (Warumi 5:4). Hiyo ndio ninalotaka kuongea juu yake leo. Na si to kwamba Mungu aliyapita dhambi zilizotendwa zamani za kale, lakini kwamba aliyapita dhambi za watu wake - tulizotenda jana na leo asubuhi na tutakazotenda hata kesho.

Mstari wa 26 inasema kwamba wakati Yesu alikufa, mambo mawili yalitokea, si moja tu. "Alifanya hivyo [kifo cha Kristo] ili kuonyesha haki Yake wakati huu, ili Yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Yesu."

Sitaki kuelekeza nguvu leo katika tendo la nafsi ya imani ambalo kwalo tunapokelea uhesabiwaji wa haki. Bali nataka kutuelekeza kwa makusudi ya Mungu katika kuhesabu haki. Maanake natumai kwamba tukielekeza katika hii kazi kuu—kwa yale ambao Mungu hufanya badala ya tunayofanya—tutaupata imani ya kuipokea ikienea katika miyo yetu.

Hebu tutazame mambo manne ambazo kuhesabika haki yanamaanisha kwa wale wanaopokea kipaji kwa kumtumaini Yesu.

1. Kusamehwa dhambi zote

Kwanza, Kuhesabika haki inamaanisha kusamehewa dhambi zote.

Dhambi zote—za kale, wa sasa, na yajayo

Tazama Warumi 4:5-8 amabapo Paulo anafunua ukweli wa kuhesabika haki kwa kunukuu Agano la Kale.

Lakini kwa mtu ambaye hafanyi kazi na anamtumaini Mungu, Yeye ambaye huwahesabia waovu haki, imani yake inahesabiwa kuwa haki. 6) Daudi pia alisema vivyo hivyo anenapo juu ya baraka za mtu ambaye Mungu humhesabia haki pasipo matendo: 7) "Wamebarikiwa wale ambao uovu wao umesamehewa na ambao dhambi zao zimefutwa. 8) Amebarikiwa mtu yule ambaye Mungu hamhesabii dhambi zake."

Huu ni ndani katika moyo wa kuhesabika haki. Thamini haya maneno matatu mkuu kutoka mistari wa 7–8: “uovu wao umesamehewa,” “dhambi zao zimefutwa,” “Mungu hamhesabii dhambi zake.”

Tazama kwamba Paulo hajakomesha msamaha kwa dhambi tulizotenda kabla ya kuamini - kana kwamba dhambi zako za kale yamesamehewa lakini yale yajayo yatahesabiwa. Kizuio kama hicho hayajatajwa. Baraka ya kuhesabiwa haki ni kwamba maovu yana samehewa na dhambi zina futiliwa na "Bwana hatahesabu dhambi juu yetu." Imetajwa kwa njia usioweza kupingwa au kujadiliwa kwa vyovyote.

Kwa sababu Kristo alibeba dhambi zetu, na hatia

Anawezaje kuyafanya hayo? Warumi 3:24 inaeleza kwamba tunahesabiwa haki "bure kwa neema Yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu." Neno "ukombozi" ina maana ya kuachilia au kuweka huru, au kufungulia mtu kutoka kwa utumwa au kifungo. Hivyo hakika ni kwamba wakati Yesu alikufa kwa ajili yetu, alituweka huru kutoka jela ya dhambi zetu. Alivunja kifungo cha hatia uliotuweka chini ya hukumu.

Paulo anasema katika Wagalatia 3:13 kwamba "Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti." Petero asema (katika 1 Petero 2:24), Kwamba Kristo "alizichukua dhambi zetu katika mwili wake, juu ya mti." Isaiah alisema, "Bwana aliweka juu yake maovu yetu sisi sote" (53:6).

Hivyo kuhesabiwa haki—msamaha wa dhambi—huja kwetu kwa sababu Kristo alibeba dhambi zetu, akabeba lawama zetu, hivyo akatufungulia kutoka hukumu. Hii ndio maana ya kuhesabiwa haki "kwa njia ya ukombozi katika Kristo Yesu."Tunaondolewa katika adhabu kwa sababu aliubeba adhabu yetu.

Kristo Aliteseka mara Moja tu

Elewa hivi: aliteseka mara moja tu. Yeye si dhabihu kila mara katika meza ya Bwana au Misa kana kwamba dhabihu yake ya kwanza haikutosha. Waebrania 9:26 inasema kwamba: "Kristo... ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aindoe dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu" (cf. Waebrania 7:27). Na pia inasema katika 9:12, "Yeye aliingia Mahali Patakatifu mara moja tu, tena hakuwa amechukua damu ya mbuzi wala ng'ombe, bali aliingia kwa damu yake yeye mwenyewe, akatupatia ukombozi wa milele."Hii ni muhimu kabisa ili kufahamu utukufu wa kile Mungu alifanya kwa ajili yetu pale msalabani.

Je waona uhusiano uliopo katika kifo cha Kristo uliofanyika mara moja na ujumla wa dhambi zako na dhambi za watu wote wa Mungu? Si baadhi ya dhambi, au aina fulani ya dhambi, au dhambi za zamani tu, bali ni dhambi - dhambi kamili ambazo Kristo aliondoa mbali kwa ajili ya watu wake.

Hivyo, msamaha wa kuhesabiwa haki ni msamaha wa dhambi zote zilizopita, za sasa na zijazo. Hiyo ndiyo iliyotendeka wakati Kristo alipokufa.

2. Haki ilio kubaliwa na haki ilio geni

Kuhesabiwa haki ina maana ya kuvikwa haki ya Mungu tuliowekewa, au iliohesabiwa kama yetu.

Hatujasamehewa tu na kuachiliwa bila msimamo mbele ya Mungu. Mungu haweki tu kando dhambi zetu, lakini pia hutuhesabu kama wenye haki na kutuweka katika msimo imara na yeye. Anatupatia haki ambaye ni yake mwenyewe.

Haki ya Mungu kupitia imani katika Yesu

Tazama mistari ya 21-22. Paulo amemaliza tu kusema katika mstari 20 kwamba hakuna binadamu anayeweza kuwa mwadilifu kwa matendo ya sheria. Huwezi kamwe kuwa na msimamo sawa mbele ya Mungu kwa kupitia msingi wa jitihada za utimilifu wa sheria. Kisha anasema (kuonyesha jinsi haki inavyopatikana), "Lakini sasa, haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa pasipo sheria, ambayo Torati na Manabii wanaishuhudia. 22) Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Yesu Kristo kwa wote wamwaminio."

Hivyo ingawa hakuna anayeweza kuhesabiwa haki kupitia matendo ya sheria, kuna haki ya Mungu ambayo unaweza pokea kupitia imani katika Yesu Kristo. Hii ndyo ninacho maanisha nisemapo kuhesabiwa haki in maana ya kutambuliwa kuwa mwenye haki. Haki ya Mungu inahesabiwa kama yetu kupitia imani yetu.

Yesu anapokufa kuonyesha haki ya Mungu tulivyoona wiki iliyopita kutoka mistari 25-26, yeye hufanya huo haki kupatikana kama kipaji kwa waovu. Ikiwa Kristo hangekufa kuonyesha kwamba Mungu ni mwenye haki katika kupita dhambi zetu, njia moja pekee ambao haki ya Mungu ingejionyesha ingekuwa kwa kuhukumu sisi. Lakini Kristo alikufa. Na hivyo sasa haki ya Mungu si hukumu lakini zawadi ya uzima kwa wote wenye wanaamini.

2 Wakorintho 5:21

2 Wakorintho 5:21 ni moja wa vifungu vinavyo sisimua zaidi kuhusu hii zawadi kubwa ya haki tuliohesabiwa. "Kwa maana Mungu alimfanya Yeye [Kristo] asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu katika Yeye."

Kristo hakujua dhambi. Alikuwa mtu kamili. Hakutenda dhambi. Aliishi kikamilifu kwa ajili ya utukufu wa Mungu katika maisha yake yote na katika kifo chake. Alikuwa mwenye haki. Sisi, kwa upande mwingine, sote tumetenda dhambi. Tuna fedhehesha utukufu wa Mungu. Sisi ni waovu.

Lakini Mungu, ambaye alituchagua katika Kristo Yesu kabla ya kuumbwa ulimwengu, aliteua kuwa kungekuwa badilisho maridadi: Angefanya Kristo kuwa dhambi—si mwenye dhambi, lakini dhambi - dhambi zetu, hatia yetu, adhabu yetu,utengano wetu na Mungu, uovu wetu. Na angechukua haki [uadilifu] wa Mungu, ambayo Kristo alikwisha thibitisha kwa ajabu, na kutufanya kuivaa na kuimiliki vile Kristo alivyofanya na dhambi zetu.

Suala hapa si kwamba Kristo, kwa adili, huwa mwenye dhambi nasi tunakuwa waadilifu. Suala ni kwamba kwamba Kristo hubeba dhambi geni na anateseka kwa ajili yake, nasi tunabeba haki ambao ni geni na tunapata kuishi kwa hilo.

Kuhesabiwa haki inatangulia utakaso

Kuwa na hakika kwamba unaweza kuona hali halisi ya lengo hii nje ya sisi wenyewe. Hii bado si ukweli wa utakaso - taratibu halisi ya kukomaa kimadili katika jinsi tunavyo fikiri, kuhisi na kuishi. Hiyo pia ni kipaji (tutaona hayo katika wiki tatu ijayo). Lakini imewekwa katika msingi huu. Kabla mtu yeyote anaweza fanya maendeleo kweli kwa injili katika kuwa haki hata kwa sehemu tu, lazima tuamini kuwa tumehesabiwa haki kabisa. Au tuweke kwa njia nyingine, the peke ambayo tunaweza kushinda kwa hakika kwa uwezo wa Mungu ni dhambi iliosamehewa. Zawadi kuu ya kuhesabiwa haki hutangulia na huwezesha utaratibu wa utakaso.

3. Kupendwa na Mungu na kutunzwa kwa neema

Kuhesabiwa haki ina maana ya kupendwa na Mungu na kutunzwa kwa neema.

Kristo anathibitisha kipimo cha upendo wa Mungu kwetu

Ikiwa Mungu hakukupenda, kakungekuwa shida ya kutatua kwa kupitia kifo cha Mwanawe. Ilikuwa upendo wake kwako uliomfanya kupita dhambi zako na kumfanya kuonekana mwovu. Kama hangependa wewe, angesuluhisha tatizo la dhambi kwa kulaani sisi hadi maangamizi. Hiyo ingethibitisha haki yake. Lakini hakufanya hivyo. Na sababu ni kwamba anakupenda.

Picha nzuri ya tendo hii inapatikana katika Warumi 5:6-8.

Tulipokuwa bado wanyonge, Kristo, wakati ulipotimia, alikufa kwa ajili yetu sisi waovu. Si rahisi mtu kufa kwa ajili ya mtu mwadilifu; labda mtu anaweza kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema. Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda, maana wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.

Kile Mungu anathibitisha katika kifo cha Mwanawe si tu ukweli wa haki yake, lakini pia kipimo cha upendo wake.

Zawadi ya bure kutoka kwa Mungu

Katika Warumi 3:24 Paulo anasema kuwa tunahesabiwa haki "bure kwa neema kama zawadi." Upendo wa Mungu kwa waovu hufurika kwa zawadi za neema—maanake, zawadi zinazotokana na ukarimu wa wema wa Mungu, wala sio kwa matendo au thamani yetu.

Msamaha wa dhambi na haki ya Mungu ni zawadi ya bure. Hii ina maana kuwa haitugharimu chochote kwa sababu zilimgharimu Kristo kila kitu. Haziwezi kununuliwa kwa matendo au kurithiwa kwa wazazi au kufyonzwa kwa njia ya sakramenti. Ni za bure, na zinapokelewa kwa imani.

Warumi 5:17 husema hivi:

Kwa maana ikiwa kutokana na kosa la mtu mmoja, mauti ilitawala kupitia huyo mtu mmoja, zaidi sana wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na karama Yake ya kuhesabiwa haki, watatawala katika uzima kwa njia ya huyo mtu mmoja, yaani, Yesu Kristo.

Msamaha wa dhambi na haki ya Mungu ni zawadi za bure za neema zitokazo katika upendo wa Mungu.

Kuhesabiwa haki ina maanisha kusamehewa, kukubaliwa kuwa haki, na kupendwa na Mungu.

4. Kulindwa na Mungu milele

Hatimaye, kuhesabiwa haki ina maana ya kulindwa na Mungu milele.

Huu ndio utimiligu wa baraka. Paulo anatangaza katika Warumi 8:30. "Nao wale Mungu aliotangulia kuwachagua, akawaita, wale aliowaita pia akawahesabia haki, nao wale aliowahesabia haki, pia akawatukuza."

Kama umehesabiwa haki, utatukuzwa. Utafika utukufu wa miaka zijazo na kuishi milele na Mungu kwa furaha na utakatifu. Kwa nini kuna uhakika kwa hayo?

Ni hakika kwa sababu matokeo ya kifo ya Mwana wa Mungu ina lengo halisi na ni kweli na ni hakika na haushindwi kwa ajili ya watu wa Mungu. Chochote kitakachofaulu kitafaulu milele. Matokeo ya damu ya Kristo si geugeu—Hivi sasa yaokoa alafu tena yashindwa, kuokoa na vile vile kushindwa.

Hii ndio lengo la mstari wa 32, "Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote, atakosaje basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu pamoja Naye?"—yaani, si nasi pia atatutukuza! Ndiyo! ule dhabihu unaotupa haki ndiyo pia ambayo hutupa utukufu.

Ukiwa umehesabiwa haki asubuhi hii, umepita mashtaka na hukumu. Mstari 33: "Ni nani atakayewashtaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni Mungu mwenyewe ndiye mwenye kuwahesabia haki." Je waona lengo: ikiwa Mungu amekuhesabu haki kupitia kifo cha Mwanawe, hakuna mtu—si mbinguni au katika nchi, wala chini ya nchi—hakuna anayeweza kufanya mashtaka kusimama juu yako. Utatukuzwa.

Kwa nini? Je ni kwa sababu hauna dhambi? La. Ni kwa sababu umehesabika haki kwa damu ya Kristo.