Hapo Mwanzo, Alikuwako Neno

Hapo mwanzo alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye neno alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. 3. Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.

Habari ya Yohana Mtakatifu ni picha ya Kristo Yesu na kazi zake za kuokoa. Inaongea kuhusu miaka mitatu ya mwisho ya maisha ya Yesu—na hasa juu ya kifo na ufufuo wake. Jukumu lake ni wazi katika Yohana 20: 30-31: “ Yesu alifanya Miujiza mengine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki. Lakini haya yameandikwa ili muweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu na kumwamini mpate uzima katika Jina lake.” Kitabu hiki kimeandikwa kusaidia watu kuamini Kristo na kupokea uzima wa milele.

Kimeandikwa kwa Wakristo na wasio Wakristo

Usifikiri kuwa kitabu hiki kimeandikwa tu kwa wasioamini. Waaminiyo Yesu lazima waendelee kuamini ndipo wapate waokolewe mwishoni. Yesu alisema katika Yohana 15:6. “Mtu yeyote asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi kama hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea.” Na katika Yohana 8:3, Alisema, “Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli.”

Sasa wakati Yohana anasema kwamba, “Haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye kristo, Mwana wa Mungu na kumwamini mpate uzima katika jina lake.” Alimaanisha kuwa alikuwa anaandika kuamsha imani kwa wasioamini na kudumisha imani kwa wanaoamin—na katika njia hiyo aelekeza wote uzimani milele. Na huenda kuwa hakuna kitabu kingine kizuri zaidi katika biblia ambacho kitakusaidia kuendelea kuamini na kumdhamini Kristo Yesu juu ya yote.

Neno la Shahidi

Picha hii ya Yesu imeandikwa na shahidi ambaye aliyashuhudia matukio haya makuu. Mara tano  katika Injili hii takatifu tunakumbana na maneno matano yasiyo ya kawaida. “mwanafunzi aliyependwa na Yesu.”(13:23; 19:26; 20:2,7, 21:20). Kwa mfano, mwishoni inasema katika Yohana 21:20 “Petro akageuka akamwona mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata.” Mistari minne baadaye (21:240 inasema, “Huyu ndiye Yule mwanafunzi anayeshuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi.” Ni yule anaitwa “mwanafunzi aliyependwa na Yesu” ambaye alikuwa ameegema kifuani Mwake walipokula naye chakula cha mwisho (13:23)—Aliandika kitabu hiki kwa uweza wa Mungu ili iwe kama kumbukumbu la matukio ya maisha ya Yesu na yale  yalimaanisha kwetu sisi.

Kupewa ari ya Kiungu

Sababu mmoja ya kufanya uiseme imepewa ari ya kiungu ni kuwa haya ndiyo Yesu aliahidi kutenda. Alisema katika Yohana 14:26, “Lakini huyo msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia. Katika Yohana 16:13, alisema, “Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonyesha mambo yajayo.”

Kwa neno lingine, Yesu aliteua mitume wake kama waakilishi wake, akawaokoa, akawafundisha, akawatuma, na akawapeana kupitia Roho Mtakatifu, mwongozo wa kiroho katika kuandika nyaraka kwa msingi wa kanisa/jiwe la pembeni (Waefeso 2:20). Tunaamini kuwa Injili ya Yohana ndilo neno lililopewa ari ya Mungu.

Mistari Mitatu ya Utangulizi Katika Yohana Mtakatifu

Maneno hayo—“Neno la Mungu”—yanatuleta katika maneno ya kwanza ya Injili ya Yohana. Yohana 1:1-3, “Hapo mwanzo, Alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2. Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. 3. Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. Mistari hii ndio tutaangalia kwa leo.

“Neno”: Yesu

Kwanza tunatazama tamshi Neno “Hapo mwanzo, Alikuwako Neno” jambo la muhimu zaidi ya kujua juu ya hili Neno linapatikana katika aya ya 14: “Na Neno likafanyika mwili, akakua miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na Kweli.” Neno inamaanisha Kristo Yesu.

Yohana anajua yale anataka kuandika katika milango hii 21. Anaendelea kutuambia hadithi kuhusu kazi za Yesu Kristo na huduma yake. Hiki ni kitabu kuhusu maisha na huduma ya Yesu Kristo—mtu ambaye Yohana alimfahamu, akamwona, akamsikikiza na kumguza na mkono wake (1 Yohana 1:1). Alikuwa na nyama na damu. Hakuwa pepo ama kiumbe pepo linaloonekana na kisha kutoweka. Alikuwa anakunywa na kuchoka na  Yohana alimjua kwa undani. Mamake Yesu aliishi na Yohana sehemu za mwisho ya maisha yake (Yohana 19:26).

Basi, yale Yohana anafanya katika Yohana 1:1-3 ni kutambua mambo ya hakiaka kuhusu Yesu vile anaweza. Ilimchukua Yohana zaidi ya miaka tatu kufahamu ukamilifu wa vile Yesu yupo. Lakini hataki wasomaji wake wachukue zaidi ya mistari mitatu kuelewa yale yaliyomchukua muda mrefu kufahamu. Anataka mawazoni mwetu tuwe, wazi na kudumu, kuanzia mwanzo wa injili yake, utukufu wa milele, mkimo wa Mungu na haki ya muumbaji wetu yesu Kristo.

Yesu katika Utakatifu Wake

Hilo ndilo jambo katika mstari 1-3. Anatuhitaji tusome injili hii kwa kuabudu, kwa kunyenyekea, kwa unyofu, kwa uoga, kuwa kijana harusini na kisimani na milimani ndiye muumba wa dunia. Je unasikia na kuhisi haya. Huu sio mpango wangu. Huu sio mpangilio yangu ya mafundisho. Ni muundo wa kitabu hiki.  Yohana aliandika hivi—jinsi Mungu alikusudia aiweke pamoja. Wewe pamoja nami tungeliandika kwa njia ya kufanya kitambulisho ya Yesu ikue pole pole kwa wasomaji ili washangae, Huyu Mtu ni nani?

Lakini Yohana anakataa. “katika neno langu la kwanza, nitakushtua, na kukupoteza na kitambulisho cha huyu Mtu ambaye alifanyika nyama na kuishi miongoni mwetu. Basi hakuna kukosea.” Yohana anatuhitaji tusome neno la Injili hii kwa uwazi, umoja na maarifa kwamba Yesu kristo alikuwa pamoja na Mungu na alikuwa Mungu na akatoa uhai wake kwa ajili Yetu (Yohana 15:13) aliumba dunia. Yohana anataka ujue na kuamini Mwokozi mwema. Chochote ambacho unaweza kufurahia juu ya Yesu, Yohana anataka ufahamu na kuthamini Yesu katika utukufu wake mkuu.

Kwa Nini “Neno”?

Lakini yafaa tuulize tena, kwa nini aliamua kuita Yesu “Neno”? “Hapo mwanzo alikuwako Neno.” Jibu langu kwa hili swali ni hili: Yohana anamwita Yesu Neno kwa sababu alikwisha kuona maneno ya Yesu kama ukweli wa Mungu na maumbile ya Yesu kama ukweli wa Mungu katika njia ya kijumla mpaka Yesu  mwenyewe—katika kuja kwake, na huduma yake, mafundisho yake, kifo chake na kufufuka—alikuwa Neno la mwisho na uamuzi wa Mungu. Ama liweke hivi: yale Mungu alikusudia kutuambia sio tu yale Yesu alisema, lakini yule Yesu alikuwa na yale aliyoyatenda. Maneno yake yalimweleza wazi na huduma yake. Lakini Yeye mwenyewe na huduma yake ndio ukweli kamili Mungu alikuwa anadhihirisha. Mimi ni kweli Yesu akasema (Yohana 14:6)

Alikuja kushuhudia ukweli (Yohana 18:37) na Yeye ndiye kweli (Yohana 14:6). Ushuhuda Wake na maumbile Yake yalikuwa Neno la kweli. Alisema, “ Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu wa kweli” (Yohana 8:31), na akasema, “Kaa ndani yangu (Yohana 15:7). Tunapodumu ndani ya Yesu, tunadumu ndani ya Neno lake. Anasema kazi zile afanyazo, “zinashuhudia” juu yake.(Yohana 5:36; 10:25). Kwa maneno mengine, katika huduma yake alikuwa Neno.

Yesu: Ujumbe wa Mungu Dhahiri na wa Mwisho

Katika Ufunuo 19:13 (lililoandikwa na mwandishi mmoja na Injili), anafafanua kurudi kwa Yesu kwa utukufu, “Alikuwa amevaa vazi lililochovywa kwenye damu na jina lake ni Neno la Mungu.” Yesu anaitwa Neno la Mungu, wakati anaporudi duniani. Mistari miwili baadaye Yohana anasema “Kinywani mwake mlitoka upanga mkali” (Ufunuo 19:15). Maanake, Yesu anayaangusha mataifa kwa nguvu za Neno la Mungu analolinena—upanga wa Roho mtakatifu (Waefeso 6:17). Lakini nguvu za neno hili limeunganika na Yesu mwenyewe na Yohana anasema kuwa hana tu upanga wa Neno la Mungu litokalo kinywani mwake, lakini Yeye ndiye Neno la Munugu.

Hivyo Yohana anapoanzisha Injili yake, anayo dhihirisho yote ya ufunuo, ukweli yote, ushuhuda yote, utukufu yote, nuru yote, maneno yote yatokayo kwa Yesu kupitia kuishi kwake, mafundisho yake, kifo chake na kufufuka kwake, anajumulisha ufunuo yote ya Mungu kwa jina: “Yeye ndiye Neno”—mwanzo, mwisho, wakipekee, bila pingamizi, kweli mtupu na Neno la kuaminika. Maana yake ni sawa na Waebrania 1:1-2: “Zama za kale, Mungu alisema na babu zetu kwa njia ya Manabii mara nyingi na kwa njia mbali mbali, lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe.” Mwana wa Mungu aliyefanyika binadamu ni uhondo wa Mungu na Neno lake kwa ulimwengu.

Maelezo Manne kuhusu Yesu

Sasa ni jambo gani ya kwanza ambayo Yohana anataka kutuambia kuhusu Yesu kristo ambaye matendo yake na maneno yake yanajaza nakala za injili hii? Anataka kutueleza mambo manne kuhusu Kristo Yesu: 1) wakati wa kuwepo kwake 2) maana ya kitambulisho chake 3) uhusiano wake na Mungu 4) uhusiano wake kwa walimwengu.

1) Wakati wa Kuwepo Kwake

Mstari 1: “Hapo mwanzo alikuweko Neno.” Maneno “Hapo mwanzo” yanafanana kwa kigiriki na maneno mawili ya kwanza katika agano la kale la kigiriki: “Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia.” Sio ajali, kwa sababu jambo la kwanza Yohana anaenda kutuambia kuwa yesu alifanya ni kuumba dunia. Hilo ndilo anasema katika mstari wa tatu. Sasa maneno “Hapo mwanzo” yanamaanisha: Kabla ya kiumbe chochote, alikuwako Neno, ambaye ni Mwana wa Mungu.

Kumbuka: “Haya yameandikwa ili mpate kuamini kuwa Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu” (Yohana 20:31). Yohana anaanzisha Injili yake kwa kumtambua Yesu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, kulingana na kuwepo, yaani kabla ya wakati. Yuda anafurahia katika ukweli huu kwa sifa kuu: “Yeye Mungu pekee, mwokozi wetu kwa Yesu Kristo Bwana wetu, utukufu, ukuu, uweza, na mamlaka vina Yeye tangu milele, sasa hata milele. Amina” (Yuda 1:25). Paulo anasema katika 2 Timotheo 1:9 kuwa Mungu alitupatia neema kupitia Kristo Yesu “kabla ya wakati wa jadi.” Sasa kabla ya wakati wowote ama kiumbe chochote Alikuwa Neno, Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Yey ndiye tutakutana naye katika Injili hii.

2) Kiini cha Utambulisho Wake

Mstari 1, mwishoni: “Neno alikuwa Mungu.” Alama mojawapo katika Injili hii ni kuwa mambo yenye uzito mkuu yanaletwa kwa maneno rahisi sana. Haingeweza kuwa rahisi zaidi ya hii—na haingekuwa na uzito zaidi. Neno, ambaye alifanyika kuwa nyama anaishi kati yetu, Yesu Kristo, alikuwa, na bado ni Mungu.

Wacha ijulikane kwa sauti kuu na iwe wazi kuwa katika mji wa Bethlehemu—hakika , katika makanisa yote ya Kristo ya kweli—tunaabudu Yesu kristo kama Mungu. Tunaanguka chini na Thomasi mbele ya Yesu katika Yohana 20:28 na kukiri kwa furaha na mshangao, “Bwana wangu na Mungu wangu!”

Wakati tunasikia viongozi wa Kiyahudi wakisema katika Yohana 10:33, “Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyoyatenda, bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ingawa ni mwanadamu unajifanya kuwa Mungu,” Tunalia tukisema, “La hii sio kufuru. Ndiye Yeye, mwokozi wetu, Bwana wetu, Mungu wetu.”

Je, unaona kile hiki kinamaanisha katika msururu wetu juu ya Injili ya Yohana? Inamaanisha kuwa tutachukua wiki baada ya wiki tukitafuta kujua Mungu, vile tunaendelea kumjua Yesu. Je unataka kumjua Mungu? Njoo nasi, na ualike wengine, waje wakutane na Mungu, tunapokutana na Yesu.

Iwapo Mshahidi wa Jehova ama Muislamu atakuambia: “Hii ni tafsiri isiyo ya kweli. Halingelisoma, “Neno Alikuwa Mungu.” inafaa isome “neno ilikuwa mungu” Kuna njia hapa ya katika andiko ambalo inaweza kufanya ujue lililo uwongo hata kama hufahamu kigiriki. Nitawaonyesha baada ya muda si mrefu kama neno la mwisho. Lakini kwanza tuangalie uhusiano wake na Mungu.

3) Uhusiano Wake na Mungu

Mstari 1, katikati ya mstari: “Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.” “Hapo mwanzo alikuwa Neno, na huyo neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.” Huu ndio moyo wa torati kuu la Utatu. Siku moja ninaweza kuhubiri ujumbe kuhusu torati hii mbali na Yohana na maandiko mengine.

Lakini kwa sasa wacha tu neno hili la wazi likadumu ndani ya akili yako na moyoni mwako. Neno, Yesu Kristo alikuwa pamoja na Mungu, na Alifanyika Mungu. Naye ni Mungu, na ni mfano wa Mungu, anadhihirisha kikamilifu yale ambayo ni Mungu na Anasimama wima kutoka milele kama ukamilifu wa hali mmoja ya kiungu na watu watatu—jopo tatu la ufahamu. Mbili kati yao yametajwa hapa. Baba na Mwana. Tutajifundisha majina hayo baadaye katika kitabu hiki. Roho mtakatifu atazungumziwa baadaye.

Ingawa tunaona taswira kama ya kwenye kioo na tunamfahamu kwa sehemu (1 Wakorintho 13:9, 12), usishangae kama haya yanabaki yasijulikane. Lakini usiitupilie mbali. Kama Yesu kristo si Mungu, hangeweza kutimiliza wokovu wako (Waebrania 2:14-15). Na utukufu wake haungetosha kusababisha tamaa yako ya milele ya uvumbuzi mpya wa urembo. Ukitupilia mbali, uungu wa Yesu Kristo, unatupilia roho yako na furaha yako ya miaka ijayo.

Tumeona 1) wakati wa kuwepo kwake (kabla ya nyakati zote), 2) maana ya utambulisho wake (neno alikuwa Mungu), na 3) uhusiano wake na Mungu (Neno alikuwa pamoja na Mungu).  Sasa tunamalizia na uhusiano Wake na ulimwengu.

4) Uhusiano Wake na Ulimwengu

Mstari 2-3: “Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.” Neno akafanyika mwili na kukaa ndani yetu, akatufundisha, akatuponya, kutukemea, kutulinda, akatufilia, aliumba Dunia. Kumbuka kuhifadhi fumbo [siri] kwa Utatu kuanzia msitari wa 1. Usiiachilie mara tu utakapofika katika mstari wa tatu. “Vyote viliumbwa kwa Yeye” Kweli, mwingine alikuwa akitenda kupitia Neno. Mungu alikuwa. Lakini Neno ni Mungu. Basi, usijiruhusu kuzima ukuu wa kazi ya Kristo kama Muumba. Alikuwa mwakilishi wa Baba, ama Neno, katika uumbaji wa vitu vyote. Lakini katika kuifanya, Alikuwa Mungu. Mungu Neno , Aliumba dunia. Mwokozi wako, Bwana wako, Rafiki yako—Yesu ni muumbaji wako.

Yesu Hakuumbwa

Sasa, ikiwa Muislamu ama Mshahidi wa Yehova ama mtu wa dhehebu lolote la Ariania (neno la zama za kale la karne ya nne ambalo haliambatani na imani) akisema, “Yesu hakuwa Mungu, hakuwa wa milele—si asiyeumbwa—bali Yesu aliumbwa. Alikuwa wa kwanza katika maumbile. Mkuu wa malaika wakuu” ama vile waarania walivyosema kuwa, “Kulikuwa wakati hakuwa.” Yohana ameandika mstari 3 kwa uwazi ambao umeifanya hiyo iwe wa kutowezekana.

Hakusema tu, “Vitu vyote viliuimbwa kwa Yeye.” Unaweza kufikiri kuwa hiyo inaweza kuikamilisha. Yeye sio kiumbe; aliumba viumbe. Lakini mwingine anaweza kusema kwa kuashiria kuwa, “kweli, lakini ‘kila chochote’ hakimjumulishi hata Yeye. Inajumulisha kila kitu ila tu Yeye. Basi aliumbwa na Baba, lakini pamoja na Baba akaumba vitu vingine vyote.

Lakini Yohana hakuiachilia hapo. Kwa kuongezea, alisema (katika sehemu ya mwisho wa mstari wa 3), “ . . . wala pasipo Yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.”  Maneno ya mwisho yanasemaje “ambacho kimeumbwa” ukiongeza na maana ya “wala pasipo yeye hakuna chochote kilichoumbwa?” “wala pasipo yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa” wanaongeza hili: Wanakifanya kionekane na kijidhihirishe kuwa chochote katika kikundi hiki cha kuumbwa, Kristo alikiumba. Hivyo basi, Kristo hakuumbwa. Kwa sababu kabla ya kuwepo, huwezi ukajileta kuwa.

Kristo hakuumbwa. Hilo ndilo linamaanisha kuwa Mungu. Na Neno alikuwa Mungu.

Bwana na atusaidie tuone utukufu wake. Na tumwabudu. Amina.