Yesu ndiye kikomo cha Jumuiko la Kikabila

Yesu akarudi kwa nguvu za roho, akaenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando. 15 Naye alikuwa akifundisha kwa masinagogi kama ilivyokuwa desturi Yake, akitukuzwa na watu wote. 16 Akaenda Nazareti, hapo alipotelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, 19 na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. 22 Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu? 23 Akawaambia, Hapana shaka mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe. 24 Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe. 25 Lakini, kwa hakika nawaambia,, palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; 26 wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. 27 Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu. 28 Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo. 29 Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini; 30 lakini yeye alipita katikati yao akaenda zake.

Jumapili uliopita nilijaribu kupuliza baragumu kwa ono nililoliita kupanda Ari. Je tunaweza kuja pamoja kama washirika na kujumuisha kengele pamoja katika ndoto na kuweka kanisa katika mwaka wa 2002 pahali pengine katika mji wa Twin Cities—ama mbali zaidi (kama Charlotte, NC ili iwe sawia na kuenda kwa BGEA huko)? Niliita kupanda Ari ndipo iwe wazi kuwa hili ni lengo la kipekee la neno la huduma ya kanisa letu: Tupo kueneza Ari kwa ajili ya ukuu wa Mungu juu ya vitu vyote kwa furaha ya watu wote kupitia Yesu Kristo. Lakini niliiweka wazi kuwa lengo si tu kuanzisha kanisa ya aina yoyote. Niliweka mambo ya kipekee kulihusu. Lililozungukiwa na Mungu, linaloinua Kristo, lililojawa Bibilia linaloeneza huduma, lavuta moyo, linalotafuta haki, n. k.

Harakati za kufuata haki

Nilipotumia neno “ufuataji wa haki,” mawazoni nilikuwa na hoja zaidi ya mbili: Mtazamo wa jumapili hii ni utangamano wa tabaka na wa Jumapili ujao na utakatifu wa Uzima. Maswala mawili makuu yanayohusu nchi yetu hapa mwanzoni mwa karne ya 21 ni maswala ya haki ya kitabaka na haki ya wasiozaliwa. Ninaamini kuna uhusiano kati ya kuwa Kanisa linalotafuta haki na kudumu ndani ya Mungu, kuinua Kristo, na lililojawa Bibilia.

Tunahitajika kuwa wanaodumu ndani ya Mungu, kutukuza Kristo na waliojawa Bibilia zaidi.

Sababu mojawapo kanisa ya kievanjelisti—hasa kanisa ya Evanjelisti ya Uzungu (hata hilo jina halifai kama vile jina “Kanisa la Weusi”) — Sababu mojawapo ya kutotafuta haki ya kitabaka na ya wasiozaliwa kwa ari zaidi jinsi tunapaswa ni kuwa hatujadumu ndani ya Mungu na kutukuza Kristo na kujawa kibibilia jinsi tunavyofikiri tumekuwa.

Tunaposema,”Tunaendelea kueneza shauku kwa ajili ya ukuu wa Mungu katika mambo yote kwa ajili ya furaha ya watu wote.” Je, tushafikiria kwa undani vile Mungu anafanywa kuwa mkuu katika ushirikiano wa Tabaka? Je, tumeuliza vile Bibilia inajawa katika fikira mwetu, na hisia na matendo yetu juu ya uhusiano ya kikabila na maswala ya tabaka katika masomo, na kuishi, na uchumi, na uwepo wa mwili wa Kristo? Je ukuu wa Mungu na utukufu wa Kristo na ujumbe muhimu wa Bibilia unatengeneza fikira na hisia na matendo yetu katika “vitu vyote kwa ajili ya furaha ya watu wote?

Kupooza wa kutokamilika

Basi tunapowaza juu ya upandaji wa kanisa, si kwamba tumewasili na hivyo basi tuko tayari kujizalisha wenyewe. Tukingojea hadi tukiwa tumewasili ndipo tujaribu kitu kama hicho, hatutaifanya—na hutaoa hata, ama kubaki kama uko katika ndoa, ama kuchukua kazi yako ya kwanza ama kuihifadhi, ama kuenda katika huduma ama kuishi huko ama kuamua kuwa na watoto ama kuanzisha huduma. Mambo machache yanalemeza watu wazuri zaidi ya kutokamilika kwao. O kuwa Mungu atawainua watu ambao watasikiza na kuelimika na kuachilia ukashifu unaolemeza wa watu wanaoonge kando kando. Hatulengi kupanda kanisa kwa sababu tumekamilika bali kwa sababu tuko na ndoto au nia: Kuwa kanisa jipya, katika mahali mpya na viongozi tofauti watafanya mambo mengine vizuri sana kuliko vile tunayafanya hapa, wakivutwa na maono hilo sawa ya kibibilia.

Ishi kwa ajili ya sababu kuu, sio starehe kuu

Njia mojawapo ninavyofikiri kuhusu kupanda Ari ni kuwa tunapanda watu ambao wamejiweka kuishi kwa nia kuu, wala si starehe kuu. Nimehubiri hapo mbeleni chini ya kibango: Kuwa, Mkristo ni kusogelea kwa hitaji wala si atarehe. Kuamka asubuhi na kujilaza kitandani usiku bila kuota vile ninavyoweza kuendelea kwa starehe zangu, bali jinsi ya kuendeleza nia ya kuzingirwa na Mungu iliyo kuu. Kupanda Ari kuna maanisha kupanda watu ambao hawashughuliki usiku na mchana wakitafuta kujihifadhi kwao na kujitukuza kwao na kujivinjari kwao, bali wanaotafuta kitu kikubwa na kikuu kuwaliko ama kuliko familia zao ama kanisa lao.

Ni nini nia kuu unayoishia? Jumapili huu na ule ujao nauliza, Je, kutakuwa na baadhi yenu—mamia kati yenu—wanaosema, ‘Ni nia kuu ya maisha yangu kumtukuza Kristo Yesu kupitia kuzingirwa na Mungu, haki na utangamano wa kutabaka iliyojawa Bibilia?” Ama Yule asemaye, “Ni nia kuu ya maisha yangu kumtukuza Yesu Krsito kupitia kuzungukwa na Mungu, haki ya asiyezaliwa iliyojawa Bibilia.” Na Mungu akawainua, dhidi ya kujipendekeza yote na unyenyekevu ya muda na kujikabidhi usio na nidhamu, wake kwa waume ambao wanahifadhi nia kuu, sio vile pumzi inavyofanya bali vile moyo hufanya! Pumzi huleta kiwango cha nguvu inayoitajika halafu hufanya mwili kuanguka. Moyo huendelea kuleta uhai mwilini katika nyakati nzuri na nyakati ngumu, msimu wa baridi ama kiangazi, kwa furaha ama huzuni, kwa udhaifu na kukiwa na nguvu, kwa furaha ama huzuni, kwa udhaifu na kukiwa na nguvu, ugonjwa na uzima! Lo! Kwa Wakristo wenye mioyo sana katika nia ya haki ya kitabaka, Si tu Wakristo wa pumzi!

Tunawahitaji William Wilberforces

Na kina nani kati yenu ambao ni William Willberforces kwa wakati wetu? Alikuwa Mkristo wa ndani, mhubiri ambaye sifa zake zilienea na mwenye ari katika safari ndefu katika nia ya haki ya kitabaka kule Uingereza. Mnamo Oktoba 28, 1787, akiwa na umri wa miaka 28 aliandika katika kitabu chake cha kumbukumbu,” “Mungu mkuu ameniweka mbele ya vitu viwili vikuu, kumalizwa kwa Biashara ya Watumwa na Mageuzi ya [maadili]”  (John Pullock, Willberforce, p. 69) Vita baada ya vita katika Bunge alishindwa kwa sababu Biashara ya Watumwa kutoka Afrika ilikuwa imekita mizizi sana katika mambo ya kifedha ya taifa. Lakini hakukata tamaa wala kukaa chini. Hakuwa Mkristo wa Pumzi, bali Mkristo wa Moyo. Mnamo Febuari 24, 1800 saa kumi alfajiri, miaka ishirini baada ya kuandika katika jarida lake, kura ya uamuzi ukafanywa na Biashara ya Watumwa ukapigwa marufuku. Bado kazi haikukamilka baada ya miaka 20 ya uvumilivu. Je, inakuwaje mtumwa akijishikanisha? Mnamo Julai 26,1833, miaka 16 baadaye, na siku tatu kabla afe, kura ukapigwa na utumwa ukapigwa marufuku nchini Uingereza na katika nchi zote chini ya Ukoloni wake.

Basi ninapofikiri juu ya kupanda Ari, nafikiri juu ya kupanda au kuanzisha kanisa ya kukuza ari ya aina hii—Ari  kama ya moyo, si kama ya pumzi. Iliyozungukwa na Mungu, unaotukuza Kristo, iliyojawa Bibilia, inayotafuta haki, kutia bidii usiokata tamaa kwa nia kuu, wala si starehe.

Basi tunapotaka kuweka Mungu katikati na kumwinua Kristo na tujawe Bibilia, wacha tuende katika Injili na tumsikize na kumtazama Yesu anapomaliza jumuiko la kikabila—Jumuiko la kikabila—shauku ama hisia kwamba kundi langu la kikabila linafa litumikiwe ama kuchukuliwa kama ya juu ama waliojaliwa.

Luka 4:16-30: Ufalme ni tofauti sana kikabila kuliko vile unavyofikiri  

Tunaanza katika Luka 4:16-30. Hapa ni kijana aliyekuzwa nyumbani anayerudi jijini mwake, Nazareti, baada ya kuwa maarafu Kapenaumu. Anaenda katika Sinagogi siku ya Sabato na umati wa watu unamkaribia. Na yale anatenda katika ujumbe huu ni karibu na yasiyo ya kujulikana. Karibu anachochea ghasia. Na analitenda kimakusudii kwanza wakampa kitabu cha nabii Isaya ili apate kusoma kwacho, anachagua mlango wa 61. Ni juu ya mkombozi ajaye ambaye atafungua waliofungwa na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika (Mistari 18b-19); na anasema kuwa inatimia wakisikia. Mstari 21: “Na ndipo akaanza kuwaambia, “ Leo maandiko haya yametimia mkiwa mnasikia.” Hiyo ilikuwa ya kustajaabisha. Kilichogonga habari: “Kijana aliyelelewa nyumbani anadai kuwa Masia.” Lakini hii haingezua ghasia. Mstari 22: “Wote waliokuwako wakimsifu na kuyastajaabia maneno yake yaliyojaa neema.” Hadi hapo ni vyema.

Lakini tazama kile anasema baadaye. Yasiyotarajika kabisa! Yasioelezeka kama kile unataka ni ufuasi. Yasiyoelezeka kama kile unataka ni kua kwa Kanisa. Anaamua  kusimulia hadithi kutoka kwa Agano la kale unaoenda kinyume na kusanyiko la kikabila la jiji lake. Hangeweza kuepuka maudhi zaidi. Anajua vile jibu lao litakavyokuwa kwa sababu anasema katika mkstari wa 24, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika kwenye mji wake mwenyewe.” Kwa maneno mengine, Kweli mnaongea vyema juu yangu sasa (mstari 22) Bali mna hisia yenu wenyewe vile Masiya atakayoyatenda, na vile uifalme wake utakavyokuwa. Lakini ngojeni hadi niwaambie kile niko karibu kukifanya na vile ufalme wangu utakavyokuwa.

Halafu anawasimulia hadithi ya kwanza. Mistari 25-26, iliyotolewa kutoka kwa 1 Wafalme 17: “Lakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati Eliya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nch nzima. (26) Lakini Eliya hakutumwa hata kwa mmoja wao, bali kwa mjane mmoja wa Sarapeta katika nchi ya Sidoni (Fonekia) “Bila kutarajiwa anasimulia hadithi vile Mungu anapita juu ya kabila yote ya Wayahudi kuleta Baraka ya kimiujuiza kwa Myunani mgeni kutoka kwa nchi ya Sidoni (Fonekia). Na anafanya hii kwa uwazi na kwa nguvu na bila ulegevu ama masimulizi: Kulikuwa na wajane wengi katika Israeli, Na mungu alibariki mgeni.

Na kama hiyo haikutosha anasimulia hadithi ya pili katika mstari wa 27 kutoka 2 Wafalme 5: “Pia palikuwa na wengi  wenye ukoma katika Israeli katika siku za nabii Elisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyetakaswa, isipokuwa Naamani mtu wa shamu.” Tena hoja ni kati ya watu wote ambao Mungu angechagua kuwatakasa kutokana na ukoma alichagua mfalme mgeni, mtu wa Shamu, si Myahudi.

Hizi hadithi mbili hazikuepuka ukabila wa Galilaya. Mstari wa 28 “Watu wote katika Sinagogi waliposikia maneno haya, wakakasirika sana. 29 Wakasimama, wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hadi kwenye kilele cha mlima mahali ambapo mji huo ulikuwa umejengwa ili wamtupe chini kutoka kwenye mteremko mkali. 30 Lakini Yeye akipita papo hapo katikati ya huo umati wa watu akaenda zake.” Wanaipata, na hawakupendezwa nayo.

Sasa ni nini hoja katika hadithi hii? Hoja ni ufalme auletao Yesu asema ni tofauti kikabila kuliko jinsi mnavyofikiria. Pahali penu palipoteuliwa kama Israeli hapajaleta unyenyekevu na huruma, bali kiburi na kejeli. Yesu ndiye mwisho wa kusanyiko la kikabila. Mnitazame. Mjifunze kutoka kwangu, anasema nimekuja kuwakomboa watu kutoka makabila yote, Si mmoja ama wachache tu. Ole wenu kwa kukosa kwenu kuona katika haki na rehema ya Mungu, shauku yake ya kukusanya kutoka kwa watu ufalme wa makuhani na marafiki.

Mathayo 8:5-13 Imani katika Yesu inaharibu ukabila

Je, nimeenda mbali sana na kutamka ole kwa watu hawa wa Galilaya? Amua unapozingatia hadithi nyingine, mara hii ni katika Mathayo 8:5-13. Yesu anatamatisha mahubiri milimani katika Mathayo 5-7 na baadaye, katika Mathayo 8:1-4, anamgusa mwenye ukoma, yule aliyechukiwa na kutengwa kati ya watu wote katika Israeli, na kumtakasa. Halafu katika Mathayo 8:5 anaingia Kapernaumu anakutana na aina ya mtu wa pili anayechukiwa na wa kuudhi—Jemedari Mrumi. Vile mwanajeshi Mmarekani alivyo kwa mpiganaji wa Taliban. Hoja kuwa huyu jemedari ni mashuhuri kati ya Wayahudi (Luka 7:3-5) umeachwa na Mathayo. Hauhusiki hapa. Mtu huyu ni mgeni, si Myahudi. Hilo ndilo hoja Mathayo anatilia mkazo.

Ni nini hoja katika hadithi hii? Jemedari anamsihii Yesu akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza tena ana maumivu makali ya kutisha.” Bila maswali ama kusita Yesu asema katika mstari 7, “Nitakuja na kumponya.” Halafu jemedari anasema kitu ambacho Yesu anapata ni ya kustaajabisha. Mstari 8: “Bwana, mimi sistahili. Wewe uingie chini ya dari yangu. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona. (9) Kwa kuwa mimi nami niko chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu ‘Nenda’, naye huenda, na mwingine, ‘Njoo’, huja. Nami nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi’ hufanya.

Yesu aliposikia maneno haya, Mstari wa 10 inasema, akashangaa. Halafu na kuichukua hali yote hii ambayo kila mtu alifikiri ilikuwa kuhusu uponyaji na nguvu na mamlaka, na kuigeuza kuwa kitu ambacho ni tofauti kabisa, kiitwacho, hali kuhusu jumuiko la ufalme kutoka kwa wageni na kuhusu hatari ya kutegemea kitambulisho cha kikabila kupokea baraka. Mstari 10b: “Amin, amin nawaaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii. 11 Ninawaambia kwamba wengi watatoka mashariki na magharibi . . . ” Mashariki na magharibi! Nini hiyo? Ni Fonekia (Ukanda wa Gaza), Misri, Ugiriki, Arabia, Pasia (Yorodani, Iran na Irak, Afghanistani, Pakistani, India na China). Na nini kitatukia watakapokuja—hawa wageni wasiotahiriwa, ambao tabia zao za kigeni si kama ya Wayahudi na umbo zao ni za kigeni? Mstari 11b: “ . . . [nao] wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaka na Yakobo katika ufalme wa mbinguni: (12) Lakini warithi wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwa na kulia na kusaga meno.”

Sasa hii inashangaza sana! Lazima uhisi mvuto wa hii. Hapa Yesu anaambia wateule wa Israeli kuwa kwanza Warumi, kama huyu Jemedari aaminiye, na halafu aina yote ya watu. Wa kabila ya Yunani wasio wasafi, wataingia katika ufalme wa mbinguni, lakini ninyi, “Wana wa wafalme,” mtaketi katika giza la nje. Hii ni kama haijasikika, kusema kuongea juu ya kabila teule kwa njia hii. Je anasema nini? Anasema: Yesu ndiye mwisho wa jumuiko ya kikabila.

Ama kuiweka kwa njia inayofaa: Yesu anasema kuwa kwa kupitia kuja kwake, njia mpya ya kipekee ya kutambua watu wa Mungu iko hapa, inaitwa, imani kwake. Imani kwa Yesu huvunja ukabila. Mara kwa mara katika injili hii hufanyika:

  1. Hadithi ya Msamaria Mwema—mgeni ndiye shujaa wa huruma (Luka 10:33).

  2. Kutakaswa kwa wakoma kumi, na mmoja tu anarudi; na yeye ni nani? Msamaria, mgeni anang’aa na unyenyekevu na shukrani (Luka 17:16).

  3. Uponyaji wa binti wa Kisirofainike (Marko 7:26).

  4. Kuabudu kwa Wataalamu wa nyota kutoka Mashariki, Yawezekana Peresi ama Arabia (Mathayo 2:1).

  5. Na mwishowe kifo na kufufuka kwa Yesu ambaye Yeye mwenytewe anatafsiri kabla katrika mfano wa wapangaji waovu (Mathayo 21:33-43). Mwenye shamba la mzabibu anatuma mwanawe kukusanya martuunda kutoka kwa watu wake. Wanamuua. Na Yesu anauliza, “atawafanyia nini hao wakulima?” Mungu atafanyaje wakati mwanawe atakataaliwa na wateule wake? Mstari 43 inapeana jibu: “Kwa hivyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na watapewa watu wengine wawezao kuzaa matunda yake.”

Si rangi, bali imani katika Kristo

Hii ndio Martin Lurther King alikuwa akimaanisha katika hotuba yake maarufu aliposema, “Nina ndoto kuwa wanangu wanne wadogo siku moja wataishi katika nchi ambao hawataonekana kwa rangi ya mwili wao lakini kwa yatokayo kwenye matendo yao.”

Yesu ndiye mwisho wa kusanyiko la kikabila. Si kwa rangi bali kwa imani katika Kristo, hiyo ndiyo alama ya ufalme. Noeli na mimi walikuwa wakinong’oneza kwenye simu jana tulipokuwa tukiongea na mwana wetu Benjamin akiwa Chicago. Tulikumbuka Uribana katika mwaka wa 1967. Warren Webster aliulizwa mbele ya wanafunzi 15,000, Je, itakuwaje iwapo binti wako ataamua kuolewa na Mpakistani wakati unahudumu huko? Neno lake bado lagonga sikioni mwangu hadi wa leo, vile ninatumai ujumbe huu utafanya kwako: Heri Mkristo Mpakistani maskini kuliko tajiri mzungu Mmarekani anayehudumu katika benki asiyeamini. Kwa maneno mengine, Kristo, si rangi ambayo ni hoja. Yesu ndiye tamati ya jumuiko la kikabila.

Kama tutaanzisha kanisa  linalozingatiwa na Mungu, linaloinua Kristo, lililojawa Bibilia, na linalotafuta haki lazima lifikie hapa pia. Na jambo la ajabu kiasi gani inapokamilika na kila kabila na tabaka na watu wanatukuza Kristo kwa pamoja.Ewe Bwana, lifanye litendeke!