Mawazo ya Uchungaji kuhusu mafunzo ya kidini kuhusu Uchaguzi

Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, kunao mabaki waliyochaguliwa kwa neema. 6 Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema tena. 7 Imekuaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata. Lakini wale wateule walikipata na wengine walitiwa ugumu.

Ni navyo waza kuhusu athari ya uchungaji ya kuhubiri kupitia mafunzo ya kidini nzito hivi kama Warumi 11, ilionekana nzuri kwangu kuwa pengine kila wiki chache hivi tungetulia ndani ya mtiririko wa uchambuzi, tufikirie na tuzungumuze kuhusu athari ya wazi kwa yale tumekuwa tukiona. Yale tumekuwa tukiona wiki chache hivi karibuni kutoka Warumi 11:1-10 (Jinsi tulivyofanya kwa Warumi 8:29-33 na Warumi 9:10-24) ni mafunzo ya dini ya kibibilia kuhusu uchaguzi bila vikwazo.

Hii ndiyo mafunzo ambayo Mngu aliuchagua, Kabla ya msingi ya dunia (Waefeso 1:4). Nani angeamini na basi kuokolewa bila kustahili bila kuzingatia dhambi zao, na ninani angeendelea katika uasi na basi kustahili kuangamia kwasababu ya dhambi zao. Kwa maneno mengine, hekima na haki na neema ya mapenzi ya Mungu ndio ufafanuzi wa mwisho ya yale yanayo tendeka  ulimwenguni kwa ujumla. Wanadamu si Mungu. Hatuwezi sababisha matukio patupu. Sisi viongozi wa Bethlehemu, tushikilie, sana utatanshi na bibilia (sio upingaji) yenye kwa upande mwingine, Mungu ni mtawala pekee na upande huo mwingine sisi wote tumejumuika na tu wenye hatia kwa sababu ya dhambi zetu na tunastahili Hukumu. Ikiwa Mungu alituchagua ili tuje kwa Imani na tuokolewe kutoka kwa hali ya hatia, haitugharimu chochote. Hii ndio tumeona katika Warumi 8 na 9 na sasa tena kwa Warumi 11:1-10. Hiyo ndio na maanisha kwa kusema uchaguzi bila vikwazo.

Basi leo tunageuka mafikira ya kichungaji kuhusu sheria ya uchaguzi.

1. Sio vitu zote nzuri kwetu kujua, na basi Mungu hajatuonyesha; na kuna vitu vingine vizuri kwetu kujua. Hata kama hatuwezi kuyafafanua kikamilifu.

Naweka msingi huu kidogo kwa Kumbukumbu la torati 29:29. Mahali Musa alisema. “Mambo ya siri ni ya Bwana Mungu wetu; Lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu  milele.” Kunayo vitu Mungu hajapanga ili sisi kuya kujua. Huenda ikawa sio nzuri kwetu. Mfano katika Matendo ya mitume 1:7, Yesu anasema “Si kazi yenu kujua misimu au majira ambayo Baba aliyoweka katika mamlaka yake mwenyewe.” Kujua zaidi kuhusu mambo ya usoni hauwezi kuwa nzuri kwetu. Kwa hakika huenda hatujui chochote au twajua kidogo sana kuhusu yatakayo tendeka kesho. Waraka wa Yakobo 4:14 yasema, “Walakini hamjui yatakayo kuwa kesho.” Mfano mwingine utakuwa Zaburi 131 mahali Daudi akasema “Moyo wangu hauna kiburi, wala macho yangu hayainuki; wala si jishughulishi na mambo makuu, wala na mambo yashindayo nguvu zangu.” Kuna mambo mengine ambayo yamo mbali nasi.

Vitu vingine tunavijua, kwa sababu Mungu ametufunulia sisi, lakini tunavijua tu kwa visehemu. Basi ni vyema kwetu kuvijua. Lakini ni lazima tujitosheleze na kujua tu sehemu kidogo tu, kama Paulo asema katika 1 Wakorintho 13:12 “Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; Wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; Wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.” Hii ni kweli kabisa kuhusu mafunzo ya uchaguzi. Tunamazoea ya kuuliza maswali mengi sana zaidi ya yale Mungu anachagua kujibu. Kuna hatari kubwa sana kwa kuwa maswali huenda yakapita kuwa lawama.

Madhara moja kuhusu pointi hii ni kuwa hatutakuwa tukijua jinsi mafunzo ya kidini mengine katika Bibilia ni nzuri kwetu. Sisi wa Amerika sana sana huwa watu wa kuchukuwa hatua na kutaka vitu vifanywe kikamilifu. Tusipoona malipo ya mafunzo ya kidini kwa haraka, huwatuna mazoea ya kupuuza. Sisi tuu kama watoto wapumbavu tufanyapo hivyo. Kila mzazi anajua watoto ni lazima wafanywe kujifunza mambo bila kujua jinsi yatakuwa ya maana baadaye. Tunawafunza mambo kuhusu maadili mezani wakiwa wachanga, Kwa mfano. Ili badaye wataweza kupitia kila hali na watu kwa neema. Na hawana fahamu kwa nini unawaambia washike kijiko kwa njia fulani na kutoweka kumbo zao mezani wakila. Ni lazima waliamini neno lako kuwa jua limesimama tisti, Ulimwengu ni mviringo, mboga hukufanya uwe mwenye afya, na begi ndogo ya sumu ya panya huuwa. Kama watoto ni lazima wajue mambo haya kabla wajue kwa nini au kwa njia gani. Basi waza hatua kati yetu na Mungu na kiasi gani tunapaswa kujuwa bila kujuwa ni jinsi gani jambo hilo litatusaidia.

Madhara katika maisha yetu kwa ajili ya yale tunajuwa, huwa ni nyingi kuliko tujuavyo au tunavyo weza kufafanua. Wakati mwingine, ni lazima tujifunze jambo kwa sababu Mungu anasema hio jambo ni kweli kisha hapo baadaye twaweza ona jinsi gani maarifa hiyo imetulinda au imetutia nguvu au imetunyenyekeza, au imetutakasa, au imetuongoza au imetusababisha kuona mambo mengine kwa ukweli. Jambo kuu linatiririka kupitia tumaini. Je tunatumaini kuwa Mungu ametufunulia yale mazuri ilitupate kufaham?

Na mafunzo ya kidini kuhusu uchaguzi, hatujui njia zote zile nzuri kwetu. Lakini twajua mengine baadhi yao. Ambayo inaongoza kwa fikira ya uchungaji ya pili kuhusu madhara ya kujua mafunzo ya kidini kuhusu uchaguzi.

2. Mafunzo ya kidini mara kwa mara ina nguvu ya kufanya kanisa iwe makini kuhusu ukweli na kuhusu maandiko ya Biblia, na basi kulizuia kupotoka na kuingia kwenye mafunzo ya kidini ya kupotosha na kufuata namna ya utamaduni.

Mafunzo ya kidini mara kwa mara huwapa msimamo dhabiti na mzizi wale wenye akili nyororo. Huwa inatoa rutuba, Wakristo wenye kufikiria na wale wasio enenda na mitindo, mawazo ya ubinafsi. Inayo nguvu ya kutunza ya kushangaza ambayo inafanya kazi ya kuzuia mafunzo mengine ya kidini isichanganywe na kupotea. Kwa ujumla huwa inajaribu kusisitiza akilini mwetu ilituwe na mtazamo wa kiMungu ambayo imejengwa kwa ukweli yenye manufaa.

Hapa kuna maonyesho kwanini hiyo ina maana. Katika uchapishaji wa hivi karibuni sana, ya Ukristo Leo Chuk Colson anajadili “maisha baada ya maendeleo ya sasa” — “ Filosofia ambayo inasema kuwa hakuna ukweli usiokuwa na mpaka." Anapatiana alama nne au tano kutoka kwa utamaduni yakuwa, maisha baada ya maendeleo ya sasa ina ishiwa nguvu na basi itakuwa bila mvutio wa watu mkubwa. Lakini hata hivyo sikiza mwito anayeambia makanisa.

Siwezi kufikiria wakati wa dharura sana kwa wachungaji, wasomi, na viongozi wa makanisa kuchunguza na kufundisha ukweli wa Bibilia na kupigania kwa usawa ili kusaidia walio na njaa ya kujua ukweli.

Lakini, je tuko tayari kwa changamoto kiasi hii? George Barna karibuni alimaliza safari ya makanisa ya Amerika na akaja na ripoti inayo huzunisha yakwamba, makanisa mengi na viongozi wa makanisa—asilimia 90, kulingana na utafiti moja—hawana ufahamu na mtazamo wa ulimwengu. Je, tutabishanaje na filosofia ambazo tunapingana nazo ikiwa sisi hatuja imarika katika njia ya ukweli yetu sisi wenyewe?

Chakushangaza ni hili, panapo kuwa na dalili ya kutia moyo katika utamaduni, kunayo pia dalili ya kuwa, kanisa ina kosa nguvu ya ushawishi, na kusonga kutoka kwa ujumbe ambao una msukumo wa neno hadi kwenye ujumbe unao lenga urembo na umbo la mtu na hisia za watu (chunguza, ni redio stesheni ngapi hivi karibuni zimegeuka kutoka kwa mazungumuzo na mahubiri hadi kucheza tu mziki pekee).

Itakuwa kejeli kwa kiwango kikubwa—na ajali mbaya zaidi—ikiwa tumejipata tukitekeleza ndani ya maisha baada ya maendeleo ya sasa na tupate kuwa watu na mitindo ya sasa wamegunduwa kuwa hapo mbele ni ukingo. (“Ufa unajitokeza kwa maisha baada ya mendeleo ya sasa,” ndani ya Ukristo leo Desemba, 2003 toleo la 47 nambari 12 kurasa la 72).  

Mafunzo ya dini kuhusu uchaguzi ni ya kupendeza na iko na athari ya kuamsha watu ambao wamesongelea mto wa upuuzi waliorithi bila ya kuhusisha akili. Kwa ghafla wanaumizwa nyoyo na ubinafsi wa mungu na ukamilifu wa Bibilia na ubinafsi wa mwanadamu inayo shtua ambayo imo ndani ya moyo zao. Kwa hali ya kutafuta njia ya kuwa na hali ya kufikiria kibiblia kumhusu Mungu na ulimwengu iliwapate kuhepuka ajali. Colson aonya kuhusu: mfano, Dunia kuvumba hatimaye ya kuwa, ukweli ni ya umuhimu sana, wakati tu kanisa imeamua katika jina la utamaduni wa kisasa na mafunzo hayo ya kidini haina umuhimu. Mafunzo ya kidini kuhusu uchaguzi ni nzuri kwetu na pia kuna wajukuu wetu kwa njia yenye hatuwezi kueleza.

3. Mawazo ya tatu ya uchungaji kuhusu mafunzo ya dini kuhusu uchaguzi ni kwamba ni njia moja nzuri zaidi ya kubaini ikiwa tumebadilisha sehemu yetu na Mungu.

Hii ni shida isiyo kuwa na wakati, lakini zaidi kwa ulimwengu wa sasa ambayo umechukuwa mkondo wa kuto taka uongozi  kwa wanadamu na kushuku mamlaka yote na kuchukuwa kiti cha hukumu kutathmini iwapo Mungu yupo.

Paulo alisuluhisha jambo hili kwa kutumia nguvu sana katika Warumi 9:6-23. Alipokuwa akifanya hayo, alisikia upingaji wa wakati wa kale na wa sasa, “Kwa nini (Mungu) bado anapata kosa? Kwani nani awezaye kuzia mapenzi yake? Jibu lake kwa hayo ilikuwa, “Lakini wewe ni nani, E mwanadamu, kumjibu Mungu? Je kinacho finyangwa kinaweza ambia mfinyanzi, “kwanini umenifinyanga hivi?” (Warumi 9:19-20). Aidha, sio vizuri kwako kubadilisha sehemu yako na Mungu. Yeye ni mfinyanzi. Mafunzo chache ya kidini yanajaribu kwa usawa ikiwa tunamhukumu Mungu au Mungu anatuhukumu.

Wakati kitabu cha ayubu kinamalizika na kinga yote ya Ayubu kukamilika, na ushauri unaopotosha wa Elifazi, Bildadi, na safari kugonga mwamba. Hesabu ya jambo hili ni, “kisha Ayubu akamjibu mungu na kusema: 2 'Najua kwamba waweza yote na hakuna sababu yako yoyote yaweza kuzuiwa . . .. Nimesema yale ambayo sikuelewa, mambo makuu kwangu, yale sikuyajua.“ Mungu anajibu, “sikiza na nitanena; Nitakuuliza maswali, na unifahamishe.” Aidha chukua sehemu yako inayostahili Ayubu, na unisikize. Jifunze kutoka kwangu; usinifunze mimi. Nitumaini mimi, usinilaumu mimi. Kuhusu haya, Ayubu anasema mwishowe, “Nilikuwa nimekusikia tu kwa kusikia kwa sikio, lakini sasa macho yangu yame kuona; kwa hivyo najidharau, na natubu kwa vumbi na majivu.” (Ayubu 42:1-6). Mafunzo ya kidini kuhusu uchaguzi yatuweka kwa majaribu kama mengine machache ili kuona kama tuko kwa hali ya Ayubu anaye laumu, au Ayubu aliyevunjika na kunyenyekea na kutumaini Mungu.

Ni vigumu kwa samaki kujua kwamba amelowa maji. Samaki yu majini. Basi hata afikiri kuhusu kuwa baridi. Kwa hivyo ni vigumu kwa mtu wa kisasa—Mtu anayeishi katika miaka mia mbili za mwisho—kujua kuwa yeye ni shingo ngumu kwake Mungu. Ushingo ngumu kwake Mungu imo ndani ya mtu wa ulimwengu wa sasa. Ndio bahari ambayo tunapiga mbizi kwayo—hewa ambayo tunapumua. Imesukwa kwa mishipa ya akili yetu. Hatujui hata kama ipo hapo. Hatuwezi kuuona, kwa sababu tunautazama ili kuona mambo mengine yote.

Hivi ndivyo C.S. Lewis anaiweka:

Mtu wa kale aliendea kwa Mungu . . . kama mtu aliyestakiwa anavyo songea mhukumu wake. Kwa mtu wa sasa sehemu yao imebadilishwa. Yeye ndiye hakimu: Mungu kizimbani. Yeye ni hakimu mwema: Kama Mungu atakuwa na ushaidi wa kutosha kumkinga kwa sababu ya kuwa Mungu anaye ruhusu vita, ufukara na magonjwa, yeye yuko tayari kusikia. Kesi hiyo dhidi ya Mungu yaweza malizika kwa kutupiliwa mbali. Lakini cha muhimu ni kwamba binadamu ndie hakimu na Mungu yuko kizimbani. ( “Mungu kizimbani,” katika maandishi ya ed., C.S. Lewis: mkusanyiko wa insha na maandishi mengine fupi [London: Harper Collins mchapishaji, 2000], Ukurasa 36)

Hiyo ndio maana hasa ya kuwa wa kisasa: Hali ambayo hatuwezi hisi—Kiwango ya ubaya hatujui hata kama tunayo—Ambayo inatosha sisi kumshuku na hata kumhukumu Mungu. Mafunzo ya kidini kuhusu uchaguzi ni njia moja yenye manufaa ya kujua kama unakombolewa kutoka kwa bahari la sasa la shingo ngumu katika ulimwengu wa sasa au bado umelowa mpaka kwenye mfupa. Ni vyema kwetu kujaribiwa katika hali fulani ya utawala wa Mungu, ili tuweze kusema pamoja na Ayubu: “Nalikusikia kwa masikio, lakini sasa macho yangu yanakuona; Kwahivyo najidharau, na natubu kwa vumbi na majivu” (Ayubu 42:6).

4. Mawazo yauchungaji ya nne kuhusu mafunzo ya kidini juu ya uchaguzi ni hili: kuukumbatia kwa unyenyekevu—sio kuujadili; sio hata imani ya wasomi katika, lakini kukumbatia kwa unyenyekevu—ukweli yenye thamani  juu ya uchaguzi na neema yenye utawala wa Mungu, kuzalisha msimamo mkali, upendo, huduma bila uwoga na huduma wa nje.

Mfano mmoja, (Na kuna uwezekano wa kuwa na mengine kutoka kwa William Carey na Adoniram Judson na David Livingstone and John Patton na George Mueller na Charles Spurgeon na Johnathan Edwards na zaidi): Kristine Clarson amekuweko kule Zambia kwa karibu miaka mmoja akifanya kazi na chokoraa  na action international. (Pata kuwa juwa; ningeweza kunakili mkurugenzi, Doug Nicholas, miongoni mwa wakristo wenye msimamo mkali walioenda kule Rwanda akiugua saratani ya matumbo kwa sababu yeye kwa unyenyekevu wake alikumbatia ukweli wa uchaguzi). Haya ndio yale Kristin alitutumia kwa mtandao asubuhi ya kutoa shukrani:

Kwanza kabisa, nashukuru Mungu kwa neema yake isiyo na kipimo kwa kunichagua mimi. Sijafanya lolote kustahili hii, na kila mara na shangazwa na uzuri wa baba yangu kwangu. Sababu ya kuwa mwenye shukrani kwa kuchaguliwa ni kwa sababu na juwa ni kwa kazi gani nimechaguliwa. Nimechaguliwa ili nieneze uzuri usiokuwa na kipimo wa Mungu: Nimechaguliwa ili nitosheleke milele ndani ya Mungu kupitia Yesu; Nimechaguliwa ili niishi ndani ya nuru na sio gizani;Nimechaguliwa ili nionje ili nione kuwa yeye yumwema.

Usikose haya. Wengine wenyu hawana ufahamu ya yale Kristin asemalo, kwa maana mmefunzwa ya kuwa mafunzo ya dini kuhusu uchaguzi aidha si ukweli au si yenye manufaa. Kila wakati umesimama nje ukiangalia ndani na kushuku au kukashifu. Sasa unausikia katika barua pepe hili barua kutoka ndani—kutoka kwa mtu anyejua jinsi inavyo hisi kukumbatia na kukumbtiwa ndani ya mafunzo ya kidini kuhusu uchaguzi bila vikwazo. Athari sio yale huwenda umefunzwa. Sikiza athari ya yale umefunzwa. Anaendelea kusema:

Ninashukran kuwa Mungu alimchagua Vasco, mtu mgumu, asiye elimika, chokoraa aliyemuasi, kutoka gizani hadi kwenye mwangaza wake nzuri zaidi. Na matunda tayari na uona katika maisha ya Vasco ni ushuhuda kwa Vasco kubaki kushikilia ndani ya Yesu, ambaye ni mzabibu.

Ninashukran kwa uzuri wa Mungu uliobubujika mwak uliopita . . . Ni kazi nzuri ilioje kuwa mmoja wapo—kuwa marafiki na chokoraa na kushiriki tumaini la milele nao. Na kwa kuongoza hapa, Nina shukran kwa moyo ambayo Munguamenipa kwa watoto hawa. Kwa hakika, najua sio “kawaida”  KU PENDA kupitia juu ya taka na kukalia mbao iliyo sitiriwa na chuma pamoja na watoto wachafu na wenye uvundo, lakini hivi ndivyo ipo na naupenda.

Kukumbatia na kukumbatiwa na mafunzo ya kidini ya neema huru—Kuanzia uchaguzi bila vikwazo—Kwanza ina zaa aina hiyo ya msimamo mkali, hali ya kutochukua tahadhari na dhabihu ya upendo; na baadaye inatu nyenyekeza kufurahia katika ukweli ya kuwa hatukuzalisha urembo huu ndani yetu, Mungu aliufanya. Kisha tunampa utukufu.

Ukiuliza; Je huu ndio njia ya bibilia ya kufikiria? Je bibilia kwa kweli unafundisha ya kuwa ukweli wa uchaguzi ni uamuzi wa Mungu ili uwe na athari hizi? Jibu ni ndio. Kwanza zingatia maneno ya Wakolosai 3:12-13, ”Basi kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; Kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo nanyi.” Hapo kuna unganisho. Niya kueleweka na wazi katika akili ya Paulo, ili kujua umechaguliwa kwa neema, yakuwa umetengwa kando kwa ajili ya Mungu, yakuwa umependwa, yakupasa uwe mmoja wa wavumilivu duniani tayari kupitia hali ya kudharauliwa na tayari kusamehe. Kupenda wasio pendeza—kule Zambia na kwengineko.

Hapa kuna ujumbe mwingine jinsi inafanya kazi. Katika Warumi 8:33 Paulo asema “Ni nani atakayewashtaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.” Jibu ni: Hakuna anayeweza kufanya shtaka ibakie dhidi yako ukiwa umechaguliwa na Mungu. Yeye yu upande wako milele. Ni kwa uwazi yakuwa Paulo asema hili kwa sababu anatarajia iwe na athari ya kuonekana kwetu. Anatarajia tuhisi ahadi na furaha na baadaye tuwe wajasiri na wasio waoga. Utakapokuwa unasimama mbele ya uamuzi inayoonekana kuwa nzuri na yenye upend leo, lakini hatari, Je wa hisi athari ya swali: “Ni nani atakaye washtaki wateule wa Mungu?” Je wa hisi hakikisho inayozalisha nguvu ya injili katika neno “wateule”?

Hiyo sio mafunzo ya dini hasa ya kuvutania, lakini funzo ya dini ya kufurahiwa. Haujaundwa ya mzozano; Imeundwa utumishi. Hailengi kugawanya watu (Ingawa ita gawanya); Inafaa Iwafanye wawe na rehema, utu wema wanyenyekevu na wenye msamaha.

5. Nafunga na mawazo ya kichungaji moja ya mwisho. Usiwaze kuhusu uchaguzi pasipo na Yesu Kristo.

Waefeso 1:3 inasema, “(Mungu) alituchagua ndani ya (Kristo) kabla ya msingi ya ulimwengu.” Kwa njia nyingine, Mungu alipoupanga tangu milele kututoa kwenye mzigo ya dhambi zetu. Alikuwa na kristo mawazoni jinsi atakavyo fanya. Mungu aliupanga kabla ya msingi ya ulimwengu kutu okowa kupitia kifo na kufufuka kwa Kristo.

Kwa hivyo yale Mungu amefanya ili kutuokowa na  kutuita kwake, sio kutueleza kabla ya wakati ikiwa tumeteuliwa. Mungu hatufunulii hili ila kwa kupitia uhusiano na Kristo Yesu, ili Kristo awe katikati ya kuchaguliwa kwetu. Badala ya kutueleza ikiwa sisi ni wateule, aliyo ifanya Mungu ni kumtuma mwanawe na kusema “Yeyote amwaminie (Yesu) anauzima wa milele” (Yohana 3:16) “Yeyote amwaminie mwana wa Mungu anaushuhuda ndani yake” (1 Yohana 5:10). Anajua kuwa yeye ni mteule.

Kwa hivyo kwa jina la Kristo nakuita; njoo, mchukue kama mokozi na bwana wako na mwenye hazina ya maisha yako. Hamtupi nje yeyote ajae kwa imani. Anasamehe dhambi. Ana vishana utakatifu. Anapeana Roho mtakatifu. Ata kutunza. “Kondoo wangu husikia sauti yangu, na nawajua, na wananifuata. Nawapa uzima wa milele, na hawata angamia kamwe, na hakuna atakae wachukua mikononi mwangu” (Yohana 10:27). Sikia sauti ya mchungaji mwema na uje.