Ushindi wa injili katika mbingu mpya na ulimwengu mpya

Katika mlango wa kwanza mstari wa kwanza wa Bilbilia unasema “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” Katika mstari wa 27, Mungu aliumba Adamu kama mume na mke kwa mfano wake na anasema kwenye mstari wa 31 na akaona ni chema sana. Kwenye mlango wa 3 Adamu na Hawa walimuasi Mungu kama kiongozi mwenye hekima, uzuri na wa kutamanika na hii ikaleta laana ya Mungu kwao, vizazi vyao,na mpangilio wa kimaumbile. ”Akamwambia  Adamu ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako.” (Mwanzo 3:17).

Mwanzo 3:15 Inadidimiza matumaini kwamba laana hii haitakuwa neno la mwisho la mungu kwa Viumbe vyake. Mungu anasema kuwa joka muharibifu wa nafsi na viumbe.’Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake, huo atakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino.Mtume Paulo anaona tumaini hili katikati ya laana hii na kufafanua hii kwenye Warumi 8:20-21 “Kwa maana viumbe vyote vilitishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.”

Mateso ya kuonekana yasiyovumiliwa

Sasa picha kubwa kwa mfano uliowazi:Mungu aliziumba Mbingu na nchi bila chochote. Ikawa vyema sana alivyofanya bila mawaa, mateso,uchungu,kifo au maovu.Adamu na Hawa wakafanya kitendo moyoni mwao ambacho kilikuwa cha maovu ya kuhofisha yasiyosemwa yaani kuchagua tunda la mti kuliko ushirika pamoja na Mungu. Kwamba Mungu Hakuwapa  adhabu ya kifo tu (Mwanzo. 2:17) bali viumbe vyote vilitiishwa ambayo Paulo anaita”ubatili” na  “utumwa” wa ufisadi. (Warumi 8:21-22).

Kwa njia nyingine, mahali ambapo hapakuwa na mateso,uchungu na kifo, lakini sasa kila binadamu anafa, huteseka, viumbe wanateseka, mito hupita kingo zake ghafla na hufagia vijiji, theluji huanguka na hufurikia mastakimu, Volkano huaribu miji,Tsunami huua watu 250,000 kwa usiku mmoja, dhoruba kuzamisha firiza za Ufilipino na abiria 800 wakiwa wameiabiri, malaria, Ukimwi na saratani na maradhi ya moyo huua milioni ya watu wakubwa kwa wadogo, jinamizi tornado kufagia mji wote wa Mid Western, ukame na njaa husukuma watu mamilioni kwenye ukingo wa—au zaidi kwenye utapiamlo. Ajali zisizo kawaida hutendeka na mwana wa rafikiyo kwenye kambarau na kufa. Mwengine hupoteza jicho. Na mtoto kuzaliwa bila uso. Kama tungeona moja kwa elfu ya mateso ulimwenguni kwa wakati mmoja tungezimia kwa ajili ya hofu ndani yake. Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kustahimili kuona na kuendelea.

Hofu ya dhambi kwenye picha ya ubatili ya uumbaji

Kwa nini Mungu aliutiisha mpangilio wa maumbile kwenye Ubatili kwa sababu ya dhambi ya wanadamu? Mpangilio wa Maumbile haukutenda dhambi watendaji ni wanadamu.Paulo alisema. “Viumbe vilitiishwa chini ya ubatili” viumbe walitiwa kwenye “ufungwa na ufisadi.”Kwa nini? Mungu alisema “Ardhi imellaniwa kwa ajili yako” (Mwanzo 3:17). Lakini kwa nini? Kwa nini kuna kuna majanga katika maumbilekwa mujibu wa upungufu wa kimadili wa binadamu? Kwa nini kusiwe kifo tu kwa vizazi vyote batili wa Adamu tu? Kwa nini damu hii uwe mfululizo wa mateso ya kuhofisha  karne baada ya karne? Kwa nini watoto wawe na ulemavu wa  kuogofya? Jawabu langu ni kwamba, Mungu aliuweka dunia mzima aliyoumba chini ya laana ili mambo haya ya kutia hofu kama maradhi na majanga yawe wazi kama picha ya kuonekana wazi kuwa dhambi ni ya kuogofya. Kwa maneno mengine,maovu asilia ni bango la kuashiria mshtuko wa kutotajika wa maadili mabovu.

Mungu aliusambaratisha ulimwengu asilia kwa sababu ya kusambaratika kwa maadili ya ulimwengu wa kiroho—yaaani, kwa sababu ya dhambi.Katika hali yetu ya upungufu sasa, kwa nyoyo zetu kupofuka kwa uovu wa dhambi uliyoenea hatuwezi kuona au kuhisi uharibifu wa dhambi. Ni nadra kwa mtu yeyote ulimwenguni kuhisi mchecheto wa maovu ya dhambi zetu. Karibu hakuna hata mtu yeyote anayegadhabishwa au kuchukizwa kwa njia yoyote—vile anavyoidunisha utukufu wa Mungu.Wacha  miili yao iguzwe kwa uchungu, na Mungu huitwa ili aeleze kuhusika kwake. Hatukasirishwi kwa njia ambayo tunaiumiza utukufu wake, lakini wacha aumize kidole chake ndipo hisia zetu za ghadhabu hupanda. Hii huonyesha vile tunavyojiinua na kumsusha Mungu.

Mpulizo wa tarumbeta wa maumivu ya kimwili

Maumivu ya kimwili ni mpulizo wa Mungu na tarumbeta wa kimwili ili kutuambia kuna jambo mbaya kimaadili na kiroho. Magonjwa na uharibifu ndiyo majivuno ya shetani. Lakini katika Mungu kukataa upeanaji ni taswira ya Mungu kuonyesha mfano dhambi katika hali ya kiroho. Hii ni kweli, ingawa wengi wa wa Watumishi wa Mungu wamebeba uharibifu huo. Majanga ni maonyesho ya Mungu mbele kuwa dhambi inahitaji hukumu, na kuwasiku moja atapokea kwenye hukumu mara elfu mbaya zaidi. Ni tahadhari.

Ole wetu tungeuona na kuhisi jinsi ilivyo hali ya kukataliwa, kuudhi, mwiko kuwasilisha chochote kwa muumba, kumpuuza, kutomwamini, kumdunisha na hata kutompa nafasi ndani ya mioyo yetu kuliko vile tunavyofanya kwa zulia lililo sebuleni. Sharti tuyaone haya la sivyo, hatutarudi kwa Kristo kwa wokovu wa dhambi zetu na hatutahitaji mbingu kwa sababu yoyote ila afueni. Na kwa kuhitaji mbinguni kuwa mpumziko ni kuachwa nje.

Amka! Dhambi ni taswira hii!

Sasa basi Mungu kwa rehema anatupasia sauti kupitia magonjwa, uchungu na majanga: Kuwa macho! taswira ya dhambi ni hii! dhambi hutuelekeza kwa vitu kama hivi. tazama (Ufunuo 9:20, 16:9, 11) Kutegemea runinga dhidi ya kushiriki na Mungu ni mfano huu. Kutamani nafuu kule Mbinguni lakini kutotamani mkombozi ni mfano huu.Ulimwengu asili hupenyezwa kwa vitisho na majanga ambayo yana nia ya kutuamsha sisi kutoka kwa ulimwengu ya fikira kuwa kumdunisha Mungu si jambo kubwa. Ni jambo la kutisha tena kubwa.

Nilihubiri ukweli huu Bethlehemu kwenye ukumbusho wa nne wa  (Nine-Eleven) nikiujua kuwa kuna watu mle kanisani mwetu wanaokabiliana na mateso makubwa.Wiki mbili au tatu baadaye nilikuwa kwenye mkutano wa maandalizi wa maombi pamoja na wapendwa na mmoja wa akina mama wadogo aliye na mtoto aliyelemaa vibaya akaomba.  “Bwana mpendwa nisaidie ni hisi tisho la dhambi kama vile ninavyohisi tisho la ulemavu wa mwanangu.” Wapendwa ninapenda kuwa mchungaji—mtume anayetetemeka kwa neno la Mungu.

Sasa turejelee ufafanuzi wa picha kamili: Mungu aliziumba mbingu na nchi kutoka kwa patupu. Ulikuwa vyema sana alivyofanya. Ulikuwa bila mawaa, uchungu,kifo au uovu.hatimaye Adamu na Hawa wakakifanya kitendo cha maovu ya kuogofya moyoni mwao ambacho Mungu hakuadhibu tu kufa (Mwanzo 2:17) bali pia viumbe vyote vikawekwa chini ya  “ubatili” na “ ufungwa wa uharibifu” (Warumi 8:21-22).

Ni nini sasa kitakachotutendekea sisi na viumbe ambao mungu ameviweka chini ya ubatili? Utawaambia nini wazazi ambao watoto wao hawatakuwa kamwe na uwezo wa kufikiria zaidi ya mtoto wa miezi sita? Mwasomee kwa machozi na furaha ya tumaini (“Ni ya kuhuzunisha bali furahini wakati wote”) Sehemu iliyobaki ya ufahamu huu kutoka kuanzia Warumi 8:18-25.

Nina mtazamo kuwa mateso ya sasa hayafai kulenganishwa na utukufu ambao tutafunuliwa.Viumbe wanangojea kwa hamu kufunuliwa kwa mwana wa Mungu,kwa sababu viumbe havikutiwa chini ya ubatili, kwa hiari,bali kwa sababu ya Yule aliyewatia kwa matumaini kuwa viumbe wenyewe watawekwa huru kutoka utumwa wa uharibifu na kupokea uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. Kwa kuwa tunajua kuwa viumbe vyote vimekuwa vikiugua pamoja kwa uchungu wa kite wakati wa kuzaa,hadi wa leo. Si tu viumbe bali hata sisi, [ambao wana uzao wa kwanza wa Roho,tunaugua kindani tukisubiri kwa hamu kuchuliwa kama wana, ukombozi wa miili yetu. Kwa tumaini hili tuliokolewa.Tumaini kwa yanayoonekana si tumaini.  Anayetumaini anayoona ni nani? Lakini tukitumaini tusiyoyaona tunayangojea kwa utulivu.

Kwa wachungaji wadogo, kuna maandiko kadhaa ya muhimu ili kupata ufafanuzi zaidi.Mojawapo za ibada zangu niliyo hubiri miaka ishirini na saba iliyopita baada kuja Bethlehemu ilikuwa "Kristo na Saratani." Nilitaka watu wangu wafahamu elimu yangu ya bilbilia kuhusu maradhi na mateso. Nilihitaji wafahamu kwamba nikija kuwatembelea hospitalini  sitakuwa nadhania tu kuwa wakiwa na imani tosha Mungu hakika angewaponya. Nilitaka waone mstari wa 23. “Si kwa viumbe tu bali sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu tukikutazamia kufanywa wana yaani, ukombozi wa miili yetu.” Waliojazwa roho huugua, wakiutazamia ukombozi wa mwili wao. Ufahamu huu ndio wa muhimu zaidi kwa kuhusika na uumbaji na yenye maana na kiuchungaji ni wa thamani katika Bibilia. Unatupeleka kwa mbingu na ulimwengu mpya kwa mwili mpya na kutupa ukamilifu na ukweli wa picha ya kuugua kwetu sasa katika umri huu na inatukirimisha na tumaini ya ambalo tuliokoka kwayo.

Sasa basi nijaribu kuufungua kwa mitizamo minne:

1. Mungu anaahidi kuwa kutakuwa na ukombozi wa viumbe kutoka kwa ubatili na utumwa wa uharibifu.

Mstari wa 21a: “Kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu.” Ulimwengu asilia—vifaa, ulimwengu wa kimwili—vitawekwa chini ya utumwa na uharibifu. Hii ni njia Paulo anavyoeleza Mbingu na Ulimwengu mpya. Ulimwengu na anga hii itawekwa huru. Ulimwengu  huu utakuwa mpya.

Isaya 65:17: Tazama mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya na mambo ya kwanza hayatakumbukwa wa hayataingia moyoni.

Isaya 66:22: Kama vile mbingu mpya na nchi mpya nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu aseme bwana,ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.

2 Petero 3:13: Lakini ,kama ilivyo ahadi yake mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.

Ufunuo 21:1, 4: Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, na bahari haikuonekana tena . . . Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwepo tena wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Matendo ya mitume 3:19-21: Tubuni basi, mrejee,ili dhambi zenu zifutwe zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana,apate kumtuma Kristo yesu mliyewekewa tangu zamani ambaye ilipasa kupokewa mninguni hata zije zamani za kufunywa upya vitu vyote zilizoneuwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.

Maneno ya Paulo katika Warumi 8:21 ni ushuhuda wazi kuendelea kati ya ulimwengu wa kwanza na ulimwengu mpya: “Viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu. Sasa anaelewa “mpya” kumaanisha “kuwa upya” bali si kubadilishwa. Si sawa na kusema,  “ Nimepata gari jipya.” Kitu kikiwe kwa huru hakitoweki au kuwachwa. Inaweza badilika lakini bado kiko na ni huru.

Sasa jambo la kumwambia huyo mama wa huyo mtoto mlemavu: Unajua, Bibilia inafunza kuwa ijapokuwa mtoto wako amenyimwa kuruka na  kukimbia maisha yake yote kwa dunia hii kwa utukufu wa Mungu, bado kuna ulimwengu mpya unakuja ambao hakutakuwa na magonjwa wala ulemavu. Hatakuwa nayo tu kwa maisha yake yote bali milele kukimbia na kuruka kwa utukufu wa Mungu.

2. Ukombozi huu wa mpangilio wa kimaumbile kutoka kwa utumwa wa uharibifu utakuwa wa ushirikishaji wa uhuru tukufu wa wana wa Mungu.

Mstari wa 21: “Kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.” Mpangilio hapa ni dhahiri kama vile viumbe vilivyofuata binadamu aliyeasi katika uharibifu, vivyo hivyo watafuata ukombozi wa binadamu katika utukufu.

Mmoja aweza kujaribu kumwambia mteule anayeteseka (mzazi wa mtoto anayeteseka) “Unaona  Bibilia inavyosema;mpangilio wa maumbile—viumbe watawekwahuru kutoka kwa utumwa wa uharibifu—basi mwili wako—au wa mtoto wako—ni sehemu ya mpango. Je, ni hivyo? Ndiyo. Sasa basi hata wewe—naye pia—utashuhudia utukufu huu wa kuwekwa huru kutoka kwa uharibifu na kuwa ni ufufuo wa mwili mpya,kwa kuwa wewe ni sehemu ya kinacho wekwa huru.”

Hii siyo njia ya mkazo Paulo anavyoona mambo. Ni hakika mwili wetu  utakombolewa kwenye mpangilio mpya. Mstari wa 23b. “Tukitazamia kufanywa wana , yaani ukombozi wa mwili wetu.” Lakini mwili wetu haujaorodheshwa kwa upya huu kwa kuwa sehemu ya viumbe. Ni kwa mtazamo tofauti viumbe vimeorodheshwa katika “uhuru wa utukufu wa wana wa Mungu.” Mstari wa 21: Kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingine katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.

Uhuru wa utukufu wa wana wa mungu ni ya Kwanza. Baada ya kutukuza wana wake katika miili mipya yenye utukufu—Yesu akasema itang’aa kama jua katika ufalme wa baba yetu (Mathayo 13:43) hatimaye viumbe vyote vitafanywa na Mungu kuwa makao salama ya familia tukufu.

Sasa unaweza kumwambia mzazi wa mtoto mlemavu kuwa “Mwanao hatabadilishwa kuingia katika utukufu wa ulimwengu mpya, ulimwengu mpya utabadilishwa wa kutosha mwanao na wewe mliotukuzwa..” Cha muhimu kwenye Mstari wa 21 ni kuwa Mungu anawapenda watoto wake na amejua kilicho bora kwao. Chunguza msemo huu: “Uhuru wa Utukufu wa wana wa Mungu.” Si uhuru wa wateule wala uhuru wa utukufu wa wakkisto wala uhuru wa utukufu wawaliokombolewa. Unaweza kuwa kweli.Lakini ndivyo sivyo Paulo anavyofikiria.

Kilichoko kwenye mawazo ya Paulo hapa ni kama mistari mitano mwanzoni—Warumi 8:16-17 Roho mwenye hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa sisi tu watoto wa mungu na kama tu watoto basi tu warithi, warithi wa Mungu,warithio pomaja na Kristo,na tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Cha muhimu kwenye mstari wa 21 ni kuwa Mbingu mpya na ulimwengu mpya ni za mirathi ya watoto. Mbingu na nchi si za muhimu. Ni  muhimu kama uwanja wa mchezo wa wana wa Mungu, kama hekalu—au konde au karakana. Mungu hajaweka wana kwa ajili ya mbingu na nchi bali ameweka mbingu na nchi kwa ajili ya watoto wake.Hii ilikuwa ukweli tokea mwanzo na ni hakika mwishowe-hasa kwa mwanawe mfano wa binadamu, Mungu—binadamu Yesu kristo. Vyote vilifanyika kwa yeye. Mwanao mlemavu hata hitaji kufanyiwa mwana tena. Mwili wake utakombolewa kikamilifu na upya. Kila kilichoumbwa kitafanyika yake.

3. Kuja kwa viumbe vipya vilivyowekwa huru umelenganishwa na kuzaa ili kwamba kusiwe tu hali ya kuendelea kwenye ulimwengu huu bali pia kuwe mwisho.

Mstari wa 22: Maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja navyo vina utungu (sunodivei) pamoja hata sasa. Mtoto anapozaliwa ni binadamu si farasi. Kuna hali ya kuendelea. Bali  mtoto si yule yule aliyemzaa. Nadhani hatuwezi kulazimisha istiara kama hii—kuja kwa ulimwengu mpya ni kama kupokea mtoto—kumaanisha kwamba ulimwengu mpya kwa uhakika una uhusiano wa ulimwengu wa kwanza kama vile mtoto na mama.Hii itafanya maneno haya yabebe zaidi. Walakini yanaibua maswali ya uwezekano wa kikomo na kutulazimu kutafuta zaidi fahamu (maandiko) ili tuone kikomo cha aina gani kinaweza kuwa. Hakika funzo la wakati huu lasema: Mwili utawekwa huru kutoka kwa ubatili na uharibifu lakini kuna zaidi.

Kwa hakika tunapata mazuri na mwelekeo wa hali ya kuendelea na hali ya kikomo. Kwa Paulo mwelekeo safi ni katika 2 Wakorintho 15. Anaibua swali kwenye mstari wa 35: “lakini labda mtu atasema, wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani? Halafu anajibu kwa maneno haya kwenye mistari ya 37-51:

Nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa ila chembe tu, ikiwa ni wa ngano au nyingineyo, lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo na kila mbegu mwili wake, Hii inasikika kama muumba si mkombozi tu ambaye inafajiri unapofikiri kuwa miili ya babu zenu sasa umeoza na chembechembe zilizotengeneza miili yao sasa ziko kwa maelfu ya watu na mimea na wanyama . . . . kinachopandwa huaribika na kinafufuliwa hakiharibiki.hupandwa katika aibu hufufuliwa katika utukufu. Hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu. Hupandwa mwili asili,hufufuliwa mwili wa Roho. [Aghalabu anasema: hupandwa na hufufuliwa. Hii ni kuendelea]. Kama kuna mwili asili, basi kuna mwili wa kiroho [Sasa neno mwili unamaanisha kuendelea na neno asili na Roho lina maana ya Kikomo] . . . ” Na kama tulivyoichukua sura yake Yule wa udongo kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni. [Sura hizi hazifanani; kuna kikomo na kuendelea.] Ndugu zangu nisemayo ni haya: nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu. Wala uharibifu kurithi kutokuharibika. Angalieni nawaambia ninyi siri.

Hakika ni siri.Sote tutabalishwa. Lakini vile Yohana anavyosema, ”Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutavyokuwa" (1Yohana 3:2). Yesu alisema,”Kwa maana kiama hawaoi wala koulewa, bali huwa kama malaika mbinguni.” (Mathayo 22:30). Mambo yatakua tofauti. Petero kwa mfano katika barua wa pili haoni urejesho au uimarishaji wa ulimwengu wa sasa. Anasema katika 2 Petero 3:7. ”Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo zikilindwa hata siku ya hukumu na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. Yohana mtume anasema. “Mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.” (Ufunuo 21:1). “Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuangaza kwa utukufu wa Mungu huutia nuru na taa yake ni mwana-kondoo" (Ufunuo 21:23). ”Na hapatukuwa na usiku tena.” (Ufunuo 22:5).

Hapana usiku wala jua wala mwezi wala bahari wala ndoa. Mwili wa kiroho katika ulimwengu uletwao kupitia moto. Kungali uhakika wa kuendelea—Wafilipi 3:21: Atakeyeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitisha vitu vyote viwe chini yake. Naye Yesu alikuwa na mwili wa aina gani? Mwili unaofufuka ambao wetu utauchukua? Umetambulikana. Ilikuwa kidogo haielezeki, kujitokeza na kutoweka kwa njia ya ajabu. Na bado tazama maneno haya ya kushangaza na muhimu katika Luka 24:39-43:

Tazameni mikono yangu na miguu yangu ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishike nishikeni mwone. Kwa  kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyo niona mimi kuwa nayo. Baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha huku wakistaajabu aliwaambia, ”Mna chakula chochote hapa?” Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. Akakitwaa akala mbele yao.

Akala Samaki. Sasa  jambo la tatu ni: Katika mbingu mpya na ulimwengu mpya kutakuwa kuendelea kutoka kwa ulimwengu huu-kikomo kwetu ndilo jambo la siri.Bado hakujadhihirika kuwa sisi tutakuwa namna gani? Kuwa kama yeye siku hiyo tunajua. Sasa  wale wazazi wa mtoto mlemavu wanapouliza Je, mwana wetu atakua mkubwa? Je atakula pekee yake bila kusaidiwa? Je, atakuwa na uwezo wa kufanya chochote kutoka kwa maumbile? Tutamjibu Mungu hakuumba dunia na kuihifadhi ili kuharibiwa. Mwanao atala pamoja na Yesu.’ Mungu atampa kiwango cha maendeleo ambayo yatakuwa furaha na utukufu kubwa kwa Mungu. Lakini  bado kuna siri kubwa. Twaona  kupitia dirishani kwa umbali.

Sasa je kuna uhakikisho gani kwao katika nuru ya siri kubwa hivi? Ni nini matumaini yao kuu kwa mwanao—na kwao wenyewe? Hii inatuleta kwenye mtazamo wa nne na wa mwisho kwa injili ya Yesu Kristo.

4. Tumaini ya kuwa na mwili uliokombolewa katika viumbe vipya umelindwa na wokovu wetu ambao twapokea kwa imani kupitia injili, bali hii si tumaini letu bora zaidi.

Chunguza hasa Warumi 8:23b-24. “Sisi pia tukikutazamia kufanywa wana, yaani ukombozi wa mwili wetu. Kwa maana tuliokolewa kwa taraja.” Hii ina maana gani—kwa tarajio hili tuliokolewa? Ni kwa niaba yetu. (te’ gar elpidi eso’themen). Pengine kuwasilisha asilia:kwa mtazamo wa tarijio hili tuliokolewa. Hakika hii itajumuisha maana kwamba, tulipookoka tumaini hili lilihifadhiwa kwetu na kwa kuwa tuliokolewa kwa kutegemea injili ya kwamba yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na akafufuka 1 Wakorintho 15:1-3 tumaini hili limelindwa katika injili. Ushindi wa injili unatuelekeza kwenye tumaini hili (Warumi 6:5, 8:11).

Hatufai kukomea hapo.Injili ni mwamba imara ya uhakikisho kuwa kutakuwa na mbingu mpya na ulimwengu mpya na tutafufuliwa kwenye miili iliyo kombelewa kuishi milele. Injili ya kuwa yesu alisubulishwa kwa ajili yetu huleta msamaha, haki na kudhihirisha kazi hii ni kwa kufufuliwa Yesu kutoka kwa wafu kwa nguvu zaidi ya vitu vyote. Jambo hili ndilo tutakalomwambia wazazi hawa wakitafuta mwamba wa kusimamia katika uoga na masikitiko yao.

Kipawa bora zaidi cha injili: Mungu alidhihirisha ndani ya kusulubishwa kwa Kristo

Lakini kipawa bora zaidi cha injili si mbingu mpya na ulimwengu mpya. Karama nzuri ya Injili hatimaye si ukombozi wa mwili. Hatima ya karama mzuri wa injili si msamaha wa dhambi wala ukombozi wala kushinda upendeleo au kuhesabiwa haki. Vyote hivi ni mbinu za kutuelekeza kwenye  mwisho. Hatimaye uzuri wa injili ambao unaifanya kuwa habari njema, na bila hiyo, hakuna kati ya karama hizi kuwa habari njema ni Mungu Mwenye—aliudhihirisha kwenye utukufu wa kusulubiwa na kufufuka kwa Mwanawe na akafurahia kwa ajili ya uzuri usio na kifani vile vile kuhifadhiwa kwa sababu ya thamani na kuonyeshwa kwetu kwa kuwa tumebadilishwa katika mfano wa Mwanawe.

Injili: Dhihirisho tosha ya utukufu wa Mungu

Sababu kuu ni kuwa kuna mbingu mpya na ulimwengu mpya ni kwa kuwa kristo aliyefufuka hatalaza mwili wake bali kuuhifadhi kama alama ya milele ya kalvari mahali utukufu wa neema ya Mungu ulidhihirishwa kikamilifu. Ulimwengu na mbingu ziliumbwa kwanza, zikapewa umbo mpya, ili Mwana wa Mungu achukue sura ya mwanadamu, ateseke katika mwili asulubiwe, afufuke kutoka kwa wafu, atawale kama Mungu Binadamu akizingirwa na umati wa watu waliokombolewa ambao katika mwili wetu wa kiroho huimba, huongea, hufanya kazi, hucheza na hupenda kwa njia inayodhihirisha bayana utukufu kamilifu kwa kuwa tuna mwili uliojawa utukufu wa Mungu katika ulimwengu asili na wa kiroho.