Kwa nini na a kwa njia gani tunavyosherehekea meza ya Bwana

Lakini katika kuagiza haya siwasifu ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa hasara. 18 Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki 19 Kwa maana lazima kuwapo na uzushi kwenu ili waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu 20 Basi mkutanikapo pamoja haiwezekani kula chakula cha bwana. 21 Kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula: hata huyu ana njaa na huyu amelewa. 22 Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! 23 Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate. 24 Naye akiisha kushukuru akaumega akasema, “Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” 25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe akisema, “kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho wangu.” 26 Maana kila mwalapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. 27 Basi kila aulaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. 28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe ni hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. 29 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. 30 Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala. 31 Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa. 32 Ila tuhukumiwapotwarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pammoja na dunia. 33 Kwa hivyo, ndugu zangu mkutanikapo mpate kula, mngojaneni. 34 Mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake, msipate kukutanika kwa hukumu. Na hayo yaliosalia nijapo nitayatengeneza.

Kabla ya kurejea Warumi wiki ijayo (Bwana akipenda) nafikiri ni vyema kwetu tuweke chakula cha Bwana Kibibilia na kuelekeza mtazamo wetu kwa nini na jinsi gani tunavyohifadhi utawazo huu. Leo tutaweka ujumbe kwanza hatimaye kuwaelekeza kwenye chakula cha Bwana kwa mafundisho.

Baada ya Bibilia, ambayo ni msingi wenye hakika katika maisha yetu na kanisa letu; mmoja ya stakabadhi muhimu katika maisha ya kanisa letu ni (Bethlehem Baptist Church Elder Affirmation of Faith). Ninahimiza kila mmoja wenu kuisome. Unaweza kuiona katika Mtandao wa kanisa au mtandao wa Desiring God. Aya ya 12.4 inapeana muhtasari ya mafundisho wa kile tunacho amini na kufunza kuhusu chakula cha Bwana.

Tunaamini kuwa chakula cha Bwana kimetawazwa na Bwana ambacho mkusanyiko wa Waumini hula mkate, kufananisha mwili wa Kristo uliopewa kwa watu wake, na kunywa kwa kikombe cha Bwana, kufananisha agano jipya katika damu ya Kristo. Tunafanya haya kama ukumbusho wa Bwana, na hivyo kutangaza kifo chake hadi atakaporudi. Wanaokula na kunywa kwa njia inayostahili hushiriki mwili wa Kristo na damu yake, sio kimwili bali kiroho, ili kwamba kwa imani, wanastawishwa kwa fadhili alizopokea kupitia kifo chake na hivyo kukua kwa neema.

Nitajaribu kupeana msingi wa kibibilia kwa ajili ya kufahamu chakula cha Bwana kwa vichwa sita: 1) Asili ya kihistoria; 2) Wanaoshiriki wanaoamini; 3) Tendo la kimwili; 4) Tendo la kimawazo; 5) Tendo la kiroho; 6) Maanani kiwakfu.

1) Asili ya kihistoria ya karamu ya Bwana

Injili ya Mathayo (26:26ff), Mariko (14:22ff) Na Luka (22:14ff) zinatoa habari kuhusu Karamu ya Mwisho ambayo Yesu alikula pamoja na wanafunzi wake usiku kabla ya kifo chake. Yote inaeleza Yesu kushukuru au kubariki mkate na kikombe, na kuwapa wanafunzi akisema kuwa mkate ni mwili na kikombe ni damu ya agano au agano jipya katika damu yake. Katika Luka 22:19 Yesu anasema, “fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Injili ya Yohana haijatoa habari kuhusu kukula na kunywa bali mafundizo na matendo ambayo yalijawa kwenye jioni hiyo.

Ijapokuwa umbali gani tunaweza sema kwa rekodi za kale kanisa lilifanya kile Yesu alisema: waliitekeleza karamu kama ukumbusho wa Yesu na kifo chake. Nyaraka za Paulo ndizo ushuhuda wa kwanza kabisa tulizo nazo na katika I Wakorintho 11:20 anamaanisha tukio katika uzima wa kanisa liitwalo “Karamu ya Bwana.” huitwa “Karamu ya Bwana.” kwa sababu ulianzishwa na kutawazwa na Bwana Yesu na aana yake halisi ni kusherehekea ukumbusho wa kifo cha Bwana. Paulo anasema kwenye I Wakorintho 11:23-24 “Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliowapa nanyi ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliyosalitiwa alitoa mkate, naye akisha kushukuru akaumega, akasema “Huu ndio mwili wangu uliyo kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu” “Mimi nalipokea kwa Bwana . . . ” Pengine inamaanisha kwamba Bwana mwenyewe alimdhibitishia Paulo (ambaye hakuwa mmoja wa wanafunzi siku hiyo ya Pasaka) kwamba kile wengine waliripoti kuhusu Pasaka hakika kilitendeka.

Hivyo asili ya historia ya Karamu ya Bwana ni hicho chakula cha mwisho ambayo Yesu na wanafunzi walikula usiku kabla ya kusulubishwa. Maana na kitendo hiki kina shina kwa kile Yesu alisema na kufanya katika usiku huo wa mwisho. Yesu mwenyewe ndiye chimbuko cha chakula cha Bwana. Aliamuru kwamba kiendelee na yeye ndiye tegemeo na muhusika ndani yake.

2) Washiriki wanachokiamini chakula cha Bwana

Chakula cha Bwana ni kitendo cha mkusanyiko wa familia ya walioamini Yesu, yaani Kanisa. Si kitendo cha wasioamini. Wasioamini wanaweza kuwepo—kwa kweli, tunawakaribisha—hakika hakuna kilichositirika kuhusu chakula cha Bwana. Hufanyika hadharani. Ina maana dhahiri. Si la siri, tambiko uliojawa nguvu za uganga. Ni kitendo cha hadharani cha kuabudu kwa mkusanyiko wa kanisa. Hakika katika I Wakorintho 11:26 Paulo anasema, “Maana kila mlapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.” Sasa basi kuna hali ya kutangaza hadharani kwa chakula hicho. Kutangaza hadharani, si kwa siri ni barua ya onyesho.

Hatukatazi kushikiri chakula cha Bwana kwa mtu yeyote kwenye chumba cha uuguzi au hospitalini lakini sherehe hiyo ya ubinafsi ni ya aina yake, si maadili ya kibibilia. Mara tano katika I Wakorintho 11, Paulo ananena kwa kanisa, “Kujumuika pamoja” wanaposhiriki meza ya Bwana. Mstari wa 17b “Mnapokusanyika si kwa faida bali kwa hasara.” Mstari wa 18: “Kwa maana kwanza mkutanikapo kama kanisa nasikia kuwa kuna faraka kati yenu.” Mstari wa 20 “Basi mkutakinapo haiwezekani kula chakula cha Bwana” Mstari wa 33 “basi mkutanikapo kula mngojane.” Mstari wa 34 “Mtu akiwa na nja na ale nyumbani mwake,msipatane kukutana kwa hukumu.”

Kwa maneno mengine ni ya kuwa walikuwa wakidunisha chakula cha Bwana kwa kukiunganisha kwa Karibu na chakula chao cha kawaida. Wengine walikuwa na chakula kingi bali wengine hawakuwa nacho. Basi akasema Kuleni chakula chenu nyumbani na mje pamoja kula chakula cha Bwana.

Tazama neno "Kanisa" katika mstari wa 18: “Kwa maana mkutanikapo kama kanisa." yaani mwili wa Kristo mkutano wa wafwasi wa Yesu. Walioacha na vinyago na kumtumaini Kristo pekee yake, kwa msamaha wa dhambi, tumaini la uzima wa milele na faraja ya nafsi zao. Wao ndio Wakristo. Basi washirikio chakula cha Bwana ni waumini waliokusanyika katika Yesu.

3) Matendo ya kimwili ya Chakula cha Bwana

Tendo la kimwili la chakula cha Bwana si kula Chakula aina ya nyingi. Ni rahisi sana. Ni kula mkate na kunywea kikombe mstari wa 23b-25. “Alitwaa mkate naye akisha kushukuru akaumega akasema.“ huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Vile vile akakitwaa kikombe akasema kikombe hiki ni agano jipya katika damu fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho wangu.

Hakuna kitu kilichotengwa maalum kuhusu aina ya mkate au jinsi ya kuumega. Maelezo ya pekee kuhusu kilichokuwa kwenye kikombe yapatikana katika kila mstari mmoja wa Mathayo, Mariko na Luka “nawaambieni sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa upya, pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu” (Mathayo 26:29); cf. Mariko 14:25; Luka 22:18). Basi unaitwa (uzao wa mzabibu). Sidhani yafa a kushughulika kuwa ilikuwa sharubati au kileo kilichotumika. Hakuna chochote kwenye aya hii kinachoamrisha au kukataza kimoja au kingine.

Kinachofaa kushughulikiwa ni kuhusu mabadiliko ya kimzaha—tuseme mkate umbo pete na kinywaji cha (coke) Kando ya moto uliowashwa kambini. Chakula cha Bwana si cha kuchezea. Yafaa kuisherehekea kwa hisia dhabiti ambayo—ambayo tutanena kwayo hivi punde.

Naweza pia kutaja tu kwa kupitia kwamba hakuna chochote katika agano jipya kuhusu mara ngapi yafaa chakula cha Bwana. Wengine huamini ni vyema kushiriki kila wiki, wengine washiriki katika robo ya mwaka, n. k. Sisi kwetu tu katikati na kwa kawaida tunasherehekea katika Jumapili ya kwanza ya kila mwezi. Nafikiri tuko huru katika jambo hili; na swali linaloibuka ni mojawapo 1) Je mara ngapi yalengana na umuhimu wake hasa kwa uhusiano katika huduma ya neno la Mungu? 2) Mara ngapi hutusaidia tuhisi umuhimu wake kwetu bila kutukwaza kwa kukosa maana? Haya si maamuzi rahisi kufanya na makanisa tofauti tofauti hufanya kwa njia tofauti tofauti.

4) Tendo la kufikiria (Hisia) la chakula cha Bwana

Mawazo ya wanaoshirikli chakula cha Bwana ni kulenga fikira za  kwa Yesu na haswa kazi yake ya kihistoria kwa kutufia dhambi zetu. Mistari ya 24 na 25: “Yafanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Tunavyotenda tendo la kimwili ya kula na kunywa lazima pia kufanyike tendo la kufikiria. Yaani kihisia, yafaa tutafakari kwa urazini mawazoni mwetu utu wa Yesu kama vile alivyoishi, na kazi yake, alivyokufa na kufufuka tena, na kile kazi yake inamaanisha katika msamaha wa dhambi zetu.

Chakula cha Bwana ni ukumbusho dhabiti kila wakati kwamba ukristo si roho wa kisasa. Haipatani na utu wako wa ndani. Si dhamani ya kiroho. Shina yake ni katika uhakika wa kihistoria kuwa Yesu aliishi, akawa na mwili, na moyo wa kupiga damu na ngozi ya kufunika. Alikufa hadharani kwa msalaba wa Waroma kwa ajili ya wenye dhambi. Yeyote amwaminiye aokolewe kutokana na ghadhabu ya Mungu. Hii ilitendeka mara moja tu katika Historia

Basi tendo la kifikira ya chakula cha Bwana ni kumbukumbu la kimsingi bali si kwa ubunifu tu wala ndoto, wala kuelekeza, wala kusikia wala bila kuwa na msimamo. Ni ya kuelekeza mawazo nyuma kwenye historia ya Yesu na tunachokifahamu kumhusu katika Bibilia. Chakula cha Bwana kinatudhibitisha kila wakati kwenye uhakika wa kimsingi kihistoria. Mkate na kikombe. Mwili na Damu. Mateso na Kifo

5) Tendo la Kiroho ya chakula cha Bwana

Hiki ni cha muhimu. Sababu ni kwamba wasioamini wanaweza fanya kila kitu nilichofafanua hadi sasa. Kwa kweli kama shetani angevaa mwili angeweza fanya. Kula, kunywa na kumbuka. Hakuna chochote kinachohusiana na rohokuhusu hayo. Basi kwa chakula cha Bwana kuwa vile Yesu alivyokusudia, jambo la ziada  lazima liwe likitendeka kuliko tu kula, kunywa na kukumbuka. Jambo ambalo haliewezi kutendwa na wasioamini wala shetani.

Wacha nisome sentensi ya maelezo katika (Elders Affirmation of Faith ). Baadaye niwaonyeshe katika bibilia mahali uliotolewa, “Wanaokula na kunywa kwa njia inayostahili hushiriki mwili wa Kristo na damu Yake, si kimwili bali kiroho kwa hiyo imani wanastawishwa kwa fadhili alizopokea kwenye kifo chake na hivyo  kukua na kuimarika kwa imani.”

Mawazo haya ya “Kushiriki mwili wa Kristo na damu . . . kiroho . . . kwa imani” yametoka wapi? Kifungu cha karibu zaidi kuhimiza haya ni katika sura inayotangulia: I Wakorintho 10:16-18 Ninapokisoma jiulize “Ni nini maana ya ‘kushiriki’?” “Kikombe cha baraka tukibarikicho, Je! Si ushirika wa damu ya Kristo?

(koinonia estin tou haimatos tou Christou)? mkate ule tuumegao si ushirika wa mwili wa Kristo? (Ouchi koinonia tou somatos tou Christou estin)? Kwa kuwa mkate ni mmmoja sisi tulio wengi tuu mwili mmoja kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. Zingatieni  wana wa Israeli, si ni waulao  madhabihu ya washiriki kwenye madhabahu? (Koinonia tou thusiasteriou)?

Hapa pana jambo la ndani kuliko ukumbusho. Hapa pana waaminio—wanaotumaini na kuthamini Yesu Kristo-Na Paulo anasema kwamba wanashiriki mwili wa Kristo na damu yake. Kiwazi wanapitia ushirika (koinonia) kwa mwili wake na damu yake wanashuhudia ushirika katika kifoo chake.

Kushiriki katika damu na mwili wa Kristo kiroho kwa imani

 Naje ushirika huu una maana gani? Kushiriki, kugawana, na ushiririkiano yana maana gani? Nafikiri mstari wa 18 unatupa fikira kwa sababu unatumia neno sawa lakini analilenganisha na ninachotendeka katika dhabibu ya Wayahudi. “Waangalieni hao waisraeli: si wale wanaokula dhabibu Washirika ni kama kisawe kwenye madhabahu?” Nini maana ya washirika/washiriki, wanaoshiriki kwenye madhabahu? Ina maana kuwa wanashirikiana katika au wanafaidika kwa kile kinachoendelea katika madhabahuni. Wanafurahia, kwa mfano, msamaha na urejesho wa ushirika pamoja na Mungu.

Basi naichukua mstari wa 16 na 17 kumaanisha kwamba waumini wanapokula mkate na kunywea kikombe kimwili tunatenda aina nyingine ya kula na kunywa kiroho. Tunala na kunywa—yaani tunaingiza katika maisha yetu—Kilichotendeka kwa msalaba. Kwa Imani—kwa kutumaini ndani ya yote ambayo Mungu yu kwa ajili yetu ndani ya Yesu—tunajistawisha kwa fadhili ambazo Yesu aliyotupokeza kwetu alipotiririsha  damu na kufa msalabani.

Hii ndiyo sababu tunawaongoza kwa mtazamo tofauti tofauti kwenye meza la Bwana kila mwezi (amani na Mungu, furaha kwa Yesu, tumaini la usoni, uhuru kutokana na uoga, usalama wakati wa mabaya, muelekeo wakati tumekwama, uponyaji wa magonjwa, ushindi wakati wa majiribio n. k). Kwa kuwa Yesu alipokufa damu yake iliyomwagika na mwili uliovunjika; uliotolewa kwenye kifo chake kwa niaba yetu, alizinunua kila ahadiza mungu. Paulo anasema, “Maana ahadi zote za Mungu zilipo katika yeye ni ndiyo” (2 Wakorintho 1:20) kila kipawa cha Mungu na furaha ya ushirika wetu pamoja na Mungu, tuliupokea kwa damu ya Yesu. Paulo anaposema, “Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuuegemeao si ushirika wa mwili wa Kristo? Anaamanisha: Je, si tunashiriki kwenye meza ya Bwana kiroho kupitia imani kila Baraka ya kiroho uliogharamiwa kwa mwili na damu ya Yesu? Hakuna asiyeamini awezaye kufanya hivyo. Shetani hawezi. Ni karama kwa familia. Tunaposherehekea meza ya Bwana, tunasheherekea kiroho kwa imani katika kila ahadi za Mungu zilizonunuliwa kwa damu ya Yesu.

6) Maanani ya kiwakfu kwa Chakula cha Bwana

Naliunga mkono kile Paulo anasema katika 1 Wakorintho 11: Anawaonya kuwa mkija kwenye Chakula cha Bwana kama shabiki, kwa ghadhabu na bila kujali hii haidhihirishi maanani ya  kilichofanyika msalabani. Unaweza ukiwa mwamini kupoteza maisha yako si kwa ghadhabu bali kama tabia ya Mungu Baba ya kutiwa nidhamu. Wacha nisome polepole 1 Wakorintho 11:27-32 tunavyosogea kwa furaha na kumaanisha meza ya Bwana.

Basi kila aulaye mkate huo na kukinywea kikombe hiki cha Bwana isivyostahili atakuwa amejipatia hatia (kutotumaini na kuweka hazina kwa kipawa cha thamani cha Kristo) ya mwili na damu ya Bwana. 28 Lakini mtu ajihoji alafu (Si kuangalia kama mnastahili bali kuona kama unahiari kughairi ubinafsi na kumtumaini Yesu kwa kile unachohitaji.) hivyo aule mkate na kukinywea kikombe. 29 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa bila ya kujipambanua (yaani, bila kuwa mwangalifu kwa mkate huu si kama samaki na keki vile wengine walivyokuwa katika Wakorintho) hula na hunywa hukumu ya nafsi yake. 30 (hapa ndipo kuna maana) Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala (Si kupelekwa jehanamu) mstari ufuatao unaeleza. 31 Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu tusingehukumiwa. 32 Ila kukihukumiwa na Bwana twarudiwa (Yaani wengineni dhaifu, wagonjwa na wanakufa) isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia (Yaani kuenda Jehanamu)

Usichukulie chakula cha Bwana kiurahisi. Ni mojawapo wa karama za thamani Kristo ameipatia kanisa. Wacha na tule pamoja.