Kwa Nini Yesu Aliwawa na Kufufuka Tena?

Hii ndio sababu, “ilihesabiwa kwake kuwa haki.” 23 Maneno haya, “Ilihesabiwa kwake kuwa haki,” hayakuandikwa kwa ajili yake peke yake, 24 bali kwa ajili yetu sisi pia, ambao Mungu atatupa haki, kwa ajili yetu tunaomwamini Yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu kutoka kwa wafu. 25 Alitolewa afe kwa ajili ya dhambi zetu, naye alifufuka kwa ajili yetu ili tuhesabiwe haki.

Maswali Matatu za Wiki Ijayo

Hapo awali nilipanga kuhubiri ujumbe mmoja katika haya mistari nne ndogo, 22-25. Lakini nilipotafakari zaidi, hata katika uhusiano na Jumapili ya ushirika, hasa katika mtazamo wa kuja kwa aina ya kilele katika mwisho wa sura hii, niliona ni vyema tu tumie Jumapili miwili katika nakala huu muhimu. Hivi ndivyo maswali ningependa kuuliza, moja leo na tatu Jumapili ijayo.

1) Kwa nini imani imehesabiwa kwa Abrahamu  na sis kama haki? Ni nini maana ya "kwa sababu hiyo" katika mwanzo wa sungu la 22: "Hii ndio sababu, “ilihesabiwa [imani] kwake [Abrahamu] kuwa haki.”

2) Ni aina gani ya imani iliyohesabiwa kwa Abrahamu na sisi kama haki? Je, ilikuwa tendo ya kwanza ya imani wakati Mungu alimwongelesha [Abrahamu] mara ya kwanza na kumwambia kuondoka Uru wa Wakaldayo, au ni imani ya Mwanzo 15:6 wakati Mungu aliahidi kufanya vizazi wa Abrahamu kama nyota, au ni imani ya Mwanzo 17 wakati Mungu aliahidi [Abrahamu] mwana  katika mwaka ujao licha ya umri wake na utasa wa Sara, au imani wa Mwanzo 22 wakati Abrahamu alitoa mwanawe Isaka? Je, tunafanyika wenye haki katika ufumbo wa kwanza kabisa ya imani au kwa maisha ya imani?

3) Ni jinsi ipi Abrahamu [pamoja na sisi] anahesabiwa mwenye haki? Je, kuhesabu imani kama haki inamaanisha kuwa imani yenyewe ndio aina ya haki tufanyalo na ambao Mungu anaihesabu kama nzuri ya kutosha usahihi wa haki—ni kama kuhesabiwa haki ina gharimu dola milioni tano na ninaweza kuja na dola milioni moja, kwa hivyo Mungu kwa rehema husema atahesabu hiyo milioni moja kama milioni tano na kufuta hizo zingine? Au kuhesabiwa haki, kweli, ni kuwekwa kwangu haki ya Mungu mwenyewe katika Kristo, na kama hivyo, ina maana gani kusema kwamba imani inahesabiwa kama haki?

Hayo yote ni ya wiki ijayo.

Ni Nani au Nini Tunapasa Kuamini ili Tuhesabiwe Haki?

Lengo langu la wiki hii ni kuuliza: Ni nani au nini tunapasa kuamini ili tuhesabiwe haki? Hivyo tutaanzia katikati wa mstari 24. Mistari 23-14 husema kuwa sababu imeandikwa katika Mwanzo 15:6 kwamba imani ya Abrahamu ilihesabiwa haki ilikuwa kwa ajili yetu, si tu kwa ajili yake. "Hayakuandikwa kwa ajili yake peke yake, bali kwa ajili yetu sisi pia." Usikose hii. Huyu ni mtume wa Yesu Kristo anayetuambia kuwa Mungu alikuwa nasi katika fikira zake wakati alipo mwongoza Musa kuandika maneno "Ilihesabiwa kwake kuwa haki." Mungu anataka uyachukuwe maneno haya kama yako binafsi. Anataka uyasome na usikie, na ujue kwamba anakuhutubia wewe mwenyewe.

Mungu anakuambia hivi sasa: "Imani itakuweka haki na mimi. Niamini. Nitahesabu imani yako kama haki. Je unamsikiza? "Niamini. Nitegemee. Itakuwa sawa. Nina haki kwa ajili yako. Hauna lolote kwa ajili yangu. Nina yangu kwa ajili yako. Niamini. Itahesabiwa kama haki yako.

Kisha katikati wa mstari 24 yeye huanza kutuambia ni nani lazima tumwamini. " . . . Yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu kutoka kwa wafu. 25Alitolewa afe kwa ajili ya dhambi zetu, naye alifufuka kwa ajili yetu ili tuhesabiwe haki." Huyu ndiye ambaye tuna imani ya kufanyiwa haki ndani mwake. Paulo anamtambulisha Mungu tunaye tumaini kwa yale [Mungu] aliyoyafanya. Hivyo anaposema, Imani inahesabika [na Mungu] kama haki," na kusema hayo yaliandikiwa sisi tulio na imani, alafu anatuambia yale ambayo Mungu amefanya, tunahitajika kujifunza misingi na maudhui ya imani yetu.

Basi wacha tuijumuishe pamoja katika kauli tatu kuhusu Mungu. 1) Mungu ambaye tunamtumaini hufanya nguvu usizoweza kueleweka . 2) Mungu ambaye tunamtumaini hufanya ukombozi wa rehema. 3) Mungu ambaye tunamtumaini hufanya haki ya ushindi. Huu sura wote umekuwa juu ya njia [maana] ya kuhesabiwa haki, si msingi wa kuhesabiwa haki kwa imani. Lakini sasa, katika sentensi ya mwisho katika sura huu, Paulo anarudi kwenye msingi (ambapo alikuwa awali katika Warumi 3:24-26) wa kuhesabiwa haki kwa imani. Msingi wa kuhesabiwa haki ndio Mungu alifanya katika kazi ya Kristo katika historia. Njia ya kuhesabiwa haki ni vile tunaunganishwa  na huo kazi kubwa kupitia imani. Zote ni muhimu mno ingawaje msingi ni muhimu zaidi ya yote.

John Murray, ambayo yuko na Bwana sasa, lakini ambaye alikuwa mkufunzi katika Westminster Seminari, aliandika kitabu ndogo muhimu ambayo inaitwa Ukombozi: Yametimia na Kutumika [Redemption: Accomplished and Applied]. Nili isoma miaka 25 iliyopita. Natamani kila mtu aisome. Itaweka kitembwe ya nguvu katika mti wa imani wako. hayo maneno mawili, "yametimia na kutumika," yana rejea kwa msingi na njia [maana] ambazo ninaongea kuhusu hapa. Ukombozi yametimia—huo ndio msingi wa yale ambaye Mungu alifanya katika Kristo; imekamilishwa, mbali na sisi na nje yetu. Ukombozi kutumiwa huo ndio Mungu hufanya kutuunganisha na kazi kubwa, na uliokamilika wa ukombozi—kitu yeye hufanya kwetu na ndani yetu.

Paulo anamaliza sura huu na taarifa kali kuhusu ukamilifu wa ukombozi—asili, msingi wa sura nzima, ambayo imekuwa kuhusu utumiaji wa ukombozi katika imani. Yule tunayemwamini ndiye aliyetimiza ukombozi kwa ajili yetu hata kabla ya kuwepo kwetu. yeye ndiye tunayemwamini, tunayeweka tumaini yetu kwake.

Kwa hivyo huu ndo tutauangalia kwa ufupi: Yeye ndiye afanyaye nguvu tusizoweza kuelewa, ukombozi wa rehema na haki ya ushindi. Wacha tuziangalie moja kwa moja na kuzitazama katika maandishi na kupendezwa nazo katika akili na mioyo yetu.

1. Tunamwamini Yule Ambaye Hufanya Nguvu Tusizoweza Kuelewa

Msitari wa 24b inasema kwamba “tunaomwamini Yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu kutoka kwa wafu.” Sababu ya kuweka ufufuo wa Yesu mbeleni ni kwamba inaungana na nguvu ilitumiwa kuzalisha Isaka katika mstari 17. Tazama tena maneno haya: “ . . .ambaye [Abrahamu] alimwamini, Mungu awapaye ahadi waliokufa na kuvitaja vile vitu ambavyo haviko kana kwamba vimekwisha kuwako.” Abrahamu alimwamini yule ambaye huwapa wafu uzima na kuvitaja vile vitu ambavyo haviko kana kwamba vimekwisha kuwako. Kwa Abrahamu, lengo kuu ilikuwa katika ahadi ya Mungu kuzalisha Isaka wakati Abrahamu alikuwa na umri wa miaka 100 na mkewe akiwa tasa. Hii ilikuwa jambo lisilowezekana. Na hiyo ndiyo ilifanya imani ya Abrahamu iwe mfano. Mstari wa 19: "hakuwa dhaifu katika imani hata alipofikiri juu ya mwili wake, ambao ulikuwa kama uliokufa, kwani umri wake ulikuwa unakaribia miaka mia moja, au alipofikiiri juu ya ufu wa tumbo la Sara."

Hivyo sasa, Paulo asema, leo tunamtumaini huo mungu mmoja, na imani ambao Mungu amekubali kuwa haki ni imani katika Mungu mwenye kuwafufua wafu, yaani Bwana wetu Yesu Kristo. Ndiye tunaye amini, yeye aliyemfufua Bwana wetu Yesu kutoka wafu.

Ninaiita "nguvu isiyowezakueleweka," si kwa sababu hamuwezi kuielewa, lakini ni kwa sababu tunakariabia mwisho wa karne ambayo imekuwa ikiendeshwa na filosofia ya kiulimwengu—maoni, au imani, ya kwamba hakuna ukweli ambayo si sehemu ya maumbile—imani kwamba hakuna ukweli kawaida. Wanasema haieleweki. Imani hii imeenea zaidi katika fomu ya mageuzi ya kiulimwengu—jitihada za kueleza asili ya mambo yote bila kuwa na imani katika Muumba asiyeonekana nje ya maumbile.

Jambo nyingine ambayo imeenea katika karne hii ni usomaji wa historia kwa njia ya kimaumbile. Katika masomo ya Biblia, imanii hii ina uharibifu mno. Moja ya kauli maarufu wa imani hiyo ilitolewa na Rudolf Bultmann ambaye alisema, "Ukweli wa kihistoria ambayo inahusisha ufufuo kutoka kwa wafu haieleweki kamwe" (Imenukuliwa katika Carl F.H. Henry, God, Revelation, And Authority, Vol. IV [Wheaton: Crossway Books, 1999, orig. 1979], p. 333). Hapo ndipo nimetoa neno "haieleweki."

Imani ambayo Mungu anatuhesabia kama haki ni imani katika yule ambayo anafanya nguvu usioeleweka. Anafanya tu yale ambayo Bultmann alisema kwamba "haieleweki"—anafufua wafu. Anafanya mambo ambayo watu wanasema haiwezekani kufanyika. Alileta Isaka kutoka tumbo iliokufa la mwanamke wa miaka 90. Naye akamleta Kristo kutoka kaburini siku ya tatu na kumfanya Bwana wa ulimwengu. Hivyo Mungu anaweza kutimiza kila ahadi. Ndio maana tunamwamini.

2. Tunamwamini Anayefanya Ukombozi wa Rehema

Tazama sehemu ya kwanza ya mstari wa 25: "Alitolewa afe kwa ajili ya dhambi zetu." Jambo la kuzingatia hapa ni kwamba kifo cha yule Mungu alimfufua ilikuwa katika mipango. Mungu hakunuia tu kuonyesha nguvu yake isioeleweka hivyo akampata tu mto mmoja aliyeuawa ili amfufue kutoka wafu. Mungu mwenyewe alipanga kifo hiki na pia kupanga sababu yake.

Waweza kuona hili katika maneno mawili muhimu za mstariwa 25a: "(1) Alitolewa afe (2) kwa ajili ya dhambi zetu." Yesu "alitolewa afe"—na nani? Na maaskari? Na Pilato? Na Herode? Na kundi ya Wayahudi? La, hatimaye, si yeyote kati yao maanake inasema alipeanwa afe "kwa ajilu ya dhambi zetu. "Maaskari na Pilato na Herode na Wayahudi hawakumpeana Yesu "kwa ajili ya dhambi zetu."

Matendo ya Mitume 2:23 inatupa jawabu wazi ambaye pia ni kweli: "Huyu mtu akiisha kutolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa kwa kujua kwake Mungu tangu zamani. " Mungu alimpa kwa kifo. Warumi 8:3 inasema, "Mungu alimtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi." Warumi 8:32 inasema, ". . . Mungu hakumhurumia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote." Hivy kifo cha Yesu Kristo ilikuwa katika mpango wa Mungu. Mungu alipanga kifo chake. Haakufa tu hivyo. Alipeanwa mikononi mwa kifo na Mungu.

Na huo mpango ulikuwa na nia (msitari wa 25a): “kwa ajili ya dhambi zetu.” Mpango wa Mungu ilikuwa kukabiliana na uhalifu wetu. Alitaka kufanya kitu kuhusu uhalifu wetu. Nini? Alitaka kufa badala yetu ili tusije kufa kwa ajili ya uhalifu  wetu. Na kifo ambacho kinge fanya hiyo ni kifo cha Mwanawe. Hivyo Warumi 8:23 inasema, "Mungu kamtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi, Yeye aliihukumu dhambi katika mwili." Hivyo uhalifu [dhambi] wetu hazifagiliwi chini ya mkeka, wala kupuuzwa. Zina hukumiwa. Zinasababisha unyongwaji.Lakini si kwetu, bali ni kwa kristo.

Kwa njia hii tunakombolewa kwa kifo cha Kristo. Yaani, tunaokolewa kutoka katika dhambi zetu. Tunaokolewa kutoka kwa adhabu ya jahannamu. Tumelipiwa fidia kutokana na hukumu ya Mungu. Na huu ukombozi wote hatukustahili. Tunastahili kufa na kwenda kuzimu na kuvumilia hukumu wa Mungu. Lakini huu ni ukombozi wa rehema. Huyu ndiye Mungu ambayo tunamwamini ili kufanyiwa haki—Mungu afanyaye ukombozi wa rehema. Alipanga kutuokoa kutoka kwa uhalifu wetu katika kifo cha Mwanawe.

3. Hatimaye, Tunamtumaini Yule Ambaye Hufanya Haki ya Ushindi

Tunamtumaini Yule ambaye hufanya nguvu usioeleweka, ukombozi wa rehema na sasa haki ya ushindi. Nina maana gani kusema hivyo, na ninaipata wapi? Nimeipata kutoka katika sehemu ya mwisho wa msitari wa 25. Ni nani huyu Mungu tunayemwamini? Ni Yule aliyemfufua Yesu “kwa sababu ya kutufanyisha wenye haki.” Nitaichukua kama kumaanisha wakati yesu alikufia dhambi zetu, malipo kamili na za kutosha iliwekwa kwa msamaha wetu na hakikisho. Kwa hivyo, haingeuwa haki kumwacha Kristo Kaburini, kwa sababu alikwisha lipa dhambi zetu kwa ukamilifu. Ufufuo wa Yesu ilikuwa azimio kwamba yale aliyetimiza ilikuwa na mafanikio bila tashwishi, yaani, ya ununuzi wa kuhesabiwa haki kwetu.

Pengine tunaweza kusema hivi: Wakati Kristo alikufa na kumwaga damu yake kwa ajili ya uhalifu wetu alifanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zilizomuua. Kwa vile dhambi hizo zimefunikwa na kulipwa, hakuna haja ya Kristo kubaki katika wafu. Kifo chake ilikuwa tu ya kulipia dhambi zetu. Hakuna kibali cha kifo kilichobaki baada ya Kristo kulipa dhambi zetu kwa kikamilifu. Ingekuwa dhuluma kubaki kaburini. Hangeisha kaburini, "haikuwezekana yeye kushikiliwa na nguvu za mauti" (Matendo ya Mitume 2:24).

Hivyo Mungu tunaye amini ndiyo yule afanyaye haki ya ushindi. Ufufuo wa Yesu ni ushindi maanake ina shinda kifo. Ni haki ya ushindi kwa sababu haki ilihitaji kuwa Yesu afufuke kutoka kwenye wafu. Alikuwa amelipia dhambi kamili, yaani dhambi zilizomsababishia maafa. Ikiwa dhambi zilizomeletea kifo—dhambi zetu—zililipiwa kabisa na kwa ukamilifu msalabani, basi sababu pekee ya kifo chake imepita. Tumekwisha hifadhiwa haki kamili (bado haija timizwa kupitia imani, lakini imehifadhiwa na kulipiwa). Hivyo ingekuwa maovu kama Kristo angebaki kwenye wafu. Ingekuwa adhabu bila sababu. Basi, ilikwa sawa na haki kuwa Mungu alimfufua kutoka wafu. Ilikuwa haki ya ushindi. (Tazama Waebrania 13:20).

Ni Nani Ambaye Lazima Tumwamini Ili Kuhesabiwa Haki?

Hivyo ninafunga na swali nililouliza mwanzoni: Ni nani au nini tunapasa kuamini ili tuhesabiwe haki? Jawabi ni kwamba lazima tumwamini Mungu – 1) kwamba alifanya nguvu tusizoweza kuelewa kwa kumfufua Mwanawe kutoka kwenye wafu, 2) alifanya ukombozi wa rehema kwa kupanga kifo cha Mwanawe ili kutuokoa kutoka mautini, na 3) alifanya haki ya ushindi kwa kumfufua Yesu kutoka mautini kuonyesha kwamba msingi wa kuhesabiwa kwetu kuwa wenye haki ilitimizwa kwa kikamilifu kupitia kifo cha Mwanawe.

Hivyo mwamini leo. Fungua roho yako na upokee utukufu wa ukombozi huu: nguvu usizoweza kueleweka, ukombozi wa rehema, haki ya ushindi. Amini haya na Mungu atahesabu imani yako kama haki. Utakuwa salama pamoja naye. Utakuwa na haki ambayo si wako mwenyewe na pia isiyo tingisika, mwamba wa milele wa kusimamia.