Kazi yako kama huduma

Hoja kuu ya ujumbe wangu asubuhi hii yaweza tajwa kama tangazo na kama ombi. Kama tangazo ingekuwa: Vile utatimiza matakwa ya likizo ni pande muhimu ya uanafunzi wa Ukristo. Ama iweke kwa njia nyingine: Vile unafanya kazi yako ni pande kubwa ya utiifu wako kwa Yesu. Itajwapo kama ombi, hoja kuu leo ni: Baba, utupe neema yote ya kutambua uwepo wako kazini mwetu na kuzitii amri zake zako katika uhusiano wetu wote wa likizo. Naamini neno hili ni la Mungu kwetu sisi leo, na nataka kulifunua kwa madakika machache kutoka 1 Wakorintho 7:17-24.

Wacha kila mtu abaki pahali alipoitwa

Kabla tuisome, wacha tujifahamishe na muktadha ya hapo awali. Mojawapo ya shida katika kanisa la Korintho ili kuwa hali ya kutoelewa vile imani katika Kristo inafaa kuathiri uhusiano wa kawaida ya maisha ya mwanadamu. Kwa mfano, katika1 Wakorintho 7 swali laibuka kama imani katika Kristo inamaanisha kuwa mke na mume wanafaa wakomeshe uhusiano wa kimapenzi. Paulo anasema la kwa hali ya juu katika mstari wa 3. Mfano mwingine katika mistari 12-16 ni swali kwamba, ni nini kinafaa tufanye kama mchumba mmojakama mchumba mmoja ameweka imani yake kwa Kristo na mwingine hajafanya hivyo? Je, anayeamini anafaa kutoka kwa ndoa ili ajiweke safi? Tena Paulo anajibu, la. Baki katika uhusiano uliokuwa kwao Mungu alipokuita kwa imani. Imani kwa Kristo kama Bwana na Mwokozi haitaharibu agano la ndoa la ndoa ambalo Mungu aliteua wakati wa kuumba. Lakini baada ya kusema hayo katika mistari 12 na 13, mtume haruhusu hiyo, iwapo mchumba asiyeamini ataacha anayeamini hajafungwa milele kwa uhusiano huo. Kwa maneno mengine, kuja kwa imani ndani ya Kristo haifanyi mtu kuachilia uhusiano ulioteuliwa na Mungu, ilhali kuwatakasa. Kwa mateso marefu na maombi na tabia ya unyenyekevu na ya mfano, mchumba anayeamini anatamani kushinda dhidi ya asiyeamini. Lakini inaweza kuwa, vile Yesu alitabiri katika Mathayo 10:34 na kuendelea, kuwa uasi na kutoamini kwa mchumba asiyeamini utageuza Ukristo kuwa upanga ukatao, badala ya dawa la imani ya kusugua linaloponya. Basi maadili ambayo mtume anafuata ni: kaa katika uhusiano wako ulioteuliwa na Mungu. Usijaribu kuuharibu au kuuacha. Lakini anaacha nafasi kuwa iwapo uhusiano umeachiliwa ama kuvunjiliwa mbali kutoka kwa tamaa ama uwezo wako na mchumba asiyeamini, basi wacha liwe. Yule amwaminiye bila tashwishi hajafungwa na yule anayetoroka.

Hapa andiko letu linaanza katika 1 Wakorintho 7:17. Baada ya kujadili maadli ya kuishi katika uhusiano wa ndoa ulioteuliwa na Mungu unapokuwa Mkristo, Paulo sasa anajadili maadili haya kwa miungano miwili zaidi. Wacha tusome 1Wakorintho 7:17-24.

Lakini kila mtu na aishi maisha aliyopangiwa na Bwana, yale Mungu aliyokuitia. Hii ni sheria yangu kwa makanisa yote. 18 Je, mtu alikuwa ametahiriwa alipoitwa? Asijifanye asiyetahiriwa. Je, mtu alikuwa hajatahiriwa alipoitwa? Asitahiriwe. 19 Kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu. Lakini kuzitii amri za Mungu ndilo jambo muhimu. 20 Basi kila mmoja wenu na abaki katika hali aliyoitiwa nayo. 21 Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Hata kama unaweza kupata uhuru, tumia nafasi uliyo nayo sasa kuliko wakati mwingine wowote. (Ama: lakini, hata kama unaweza kuwa huru, basi tumia hali yako ya sasa). 22 Kwa maana yeyote aliyeitwa katika Bwana kama mtumwa yeye ni mtu huru kwa Bwana, kama vile yeyote aliyekuwa huru alipoitwa yeye ni mtumwa wa Kristo. 23 Mlinunuliwa kwa ghrama, ili msiwe watumwa wa wanadamu. 24 Ndugu zangu, kama kila mtu alivyoitwa, akae katika mwito wake aliyoitiwa na Mungu.

Maadili ambayo Paulo tayari amefundisha kulingana na ndoa hapa imetajwa  wazi wazi  mara tatu. Tazama mstari 17, “Lakini kila mtu na aishi maisha aliyopangiwa na Bwana, yale Mungu aliyokuitia.” Halafu mstari wa 20, “Basi kila mmoja wenu na abalki katika hali aliyoitwa nayo.” Halafu mstari wa 24 Ndugu zangu, kama kila mtu alivyoitwa, akae katika mwito wake alioitiwa na Mungu.” Haya matamshi matatu ya kimaadili ya Paulo yanagawanyisha andiko katika sehemu mbili. Inaweza saidia ukitafakari haya kama pande tatu za mikate kwenye mkate ulio na sehemu ya juu na chini (kama Big Mac). Kati kati ya pande mbili za juu ni mstari wa 18 na 19 ambapo maadili yatumika kwa jambo la kutahiri na kutotahiri.” Kati ya pande mbili za chi kuna mistari 21-23 ambapo maadili yametumika kwa utumwa na kuwa huru. Lakini kabla tufahamu matumishi haya, tunafaa tueleze kinaga ubaga neno kuu katika maadili yenyewe.

Je, ni mwito wa aina gani unaoangazwa?

Neno ambalo linapatikana katika kila tamshi la kimaadili na mara tisa katika aya hii ni neno “mwito.” Paulo anaposema katika mstari wa 17, “Lakini kila mtu na aishi maisha . . ., yale Mungu aliyokuitia,” na anaposema katika mstari wa 24, “Ndugu zangu, kama kila mtu alivyoitwa, akae katika mwito wake alioitiwa na Mungu.” Anaongea kuhusu mwito wa kiungu ambao tulivutwa nayo kumwamini Kristo. Kila mara tunalitumia neno “mwito” kumaanisha kazi yetu. Mwito wangu ni kuwa mhifadhi wa boma; mwito wangu ni kuwa mchukuzi; na kadhalika. Lakini hiyo sio vile Paulo ameutumia mara nane kati ya tisa vile inavyoonekana katika aya hii. Wakati mmoja analitumia neno “mwito” Kwa hali hii ya kazi, ambayo iko, katika mstari wa 20. Kwa ukawaida mstari huu unasema, “Kila mtu na abaki katika “mwito” (si hali) wake aliyoitwa nayo.” Neno “mwito” hapa linamaanisha kazi ama kituo katika maisha. Na katika kazi ama kituo katika maisha mwito mwingine huja kutoka kwa Mungu. Mwito huu ni mvuto wa Roho Mtakatifu katika ushirika na Kristo. Kwa kifupi mwito wa Mungu unaomjia mtu katika kazi yake ni uweza wa Mungu kubadilisha moyo kupitia Injili.

Hii yote iko wazi katika 1 Wakorintho 1. Katika sura ya kwanza, fungu la 9, Paulo anasema, “Mungu ni mwaminifu ambaye mmeitwa naye ili muwe na ushirika na Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.” Basi wakristo wote, na Wakristo pekee, wameitwa katika hali hii. Mwito huu wa Mungu ni tofauti, kwa upande mwingine na “mwito” kutoka kwa kazi yetu na pia kwa upande mwingine, tofauti na mwito wa dharura ya toba ambao huenda kwa watu wote. Wakati Yesu alisema katika Mathayo 22:14 kuwa “Wengi wameitwa bali wachache wamechaguliwa,” alimaanisha mwito wa ulimwengu wote ya injili ambao wengi husikia na kukataa na kuangamia. Lakini hiyo sio mwito Paulo alikuwa nao mawazoni mwake. Mwito wa Mungu unaotufanya tuamini, kuwa na ushirika wa kupendeza na Yesu ni yenye nguvu sana, mwito wenye uweza wa kutuelekeza hadi kwa Mwana (Yohana 6:44, 65). Hii inaonekana dhahiri shahiri katika 1 Wakorintho1: 23, 24, pahali Paulo anasema, “Lakini sisi tunamuhubiri kristo aliyesulubiwa, ambaye kwa Wayaudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuuzi, lakini kwa wale Mungu amewaita, yaani Wayahudi na Wayunani, Kristo ni nguvu na hekima ya Mungu.” “Walioitwa” si wote wanaosikia mahubiri, lakini wanaoyapokea kama hekima. Tunaweza kunukuu mafungu haya kuonyesha tofauti kati ya mwito wa dharura na mwito sahihi: Paulo asema,”Tunamwita kila mmoja kuamini Kristo aliyesulubiwa, lakini Wayaudi wengi wanauona mwito huu kama kikwazo, na Wayunani wengi wanauona kama upuuzi. Lakini kwa wale ambao wameitwa (kusema, kuitwa kwa nguvu na usahihi sana kwa Kristo) wanapata mwito wa injli kuwa nguvu na hekima ya Mungu.”

Hivyo, Paulo anaposema katika 1 Wakorintho 7:17, 20 na 24 kuwa inafaa tubaki na kuishi na Mungu katika hali tuliyoitiwa, anamaanisha: Baki katika hali ulivyokuwa wakati ulipobadilishwa, ulipovutwa na Mungu kwa ushirika na Mwanawe  ya kuamini na ya kupenda.

Maadili yanayotumika kwa Wayaudi na Wayunani

Sasa yafa yuone vile Paulo alivyotumia maadili haya kwa wakati wake, na yale yanamaanisha kwetu sasa. Tunapoendelea, sababu yake ya kithiolojia itachipuka pia. Matumizi ya kwanza ya Paulo ya maadili si kazi, lakini kwa kutahiri na kutotahiri. Anaitumia hivi: kama uliitwa ukiwa Myunani, usijaribu kuwa Myahudi. Kama uliitwa ukiwa Myahudi usijaribu kuwa Myunani. Vivyo hivyo ndivyo kutotahiriwa na kutahiriwa kulimaanisha. Hii ina maadhara ya kitamaduni kwa hali ya juu. Kama wewe ni mtu mweusi, usijaribu kuwa mweupe; ukiwa mweupe usijaribu kuwa mweusi. Kama wewe ni mtu wa asili ya Mexico, usijaribu kuwa Mmarekani; ukiwa Mmarekani usijaribu kuwa mwenye asili ya Mexico. Halafu Paulo anapeana sababu ya kithiolojia kwa hali hii. Fungu la 19 lasema hadharani, “Kutahiriwa na kutotahiriwa si kitu. Lakini kuzitii amri za Mungu ndilo jambo muhimu. Na kama tunaelewa athari zake za kitamaduni kwa upana, itatuudhi sisi sote. Lakini ni kweli. Tazama vile ni tofauti sana umuhimu wa Paulo kuhifadhi hadhi yako ya kitamaduni kuliko vile ilivyo sasa kwa wakati wetu. Tunasema ueupe unapendeza, ueusi unapendeza, uekundu unapendeza, unjano unapendeza; basi usijaribu kubadilisha tamaduni. Paulo anasema, ueupe ni bure ueusi ni bure, uekundu ni bure, unjano ni bure, lakini kuzitii amri za Mungu ndilo jambo muhimu; hivyo basi, usijaribu kubadilisha tamaduni. Baki pahali ulivyo na kumtii Mungu. Paulo ni mwenye fikira asiye na ustadi, kwa hivyo anaumuhimu wa milele. Anaegemea Mungu sana. Kila kitu, kila kitu kinaanguka mbele ya matakwa ya Mungu.

Hii ni muhimu sana kushikilia tusije tukaleta hali mpya za kisheria. Sheria ya awali ilisema, “Lazima utahiriwe ndipo upate kuokoka” (Matendo 15: 1). Lazima uwe mweupe ndipo upate kukubalika. Sheria mpya yaweza kusema, “Hufai kutahiriwa kama unataka kuokoka. Hufai kuwa mweupe kama unataka kukubalika.” Tutadunisha mafunzo ya Paulo na kukosa kusudio lake tukiuchukua sentensi, “Wacha wasiotahiriwa wasitahiriwe” (mstari 18), na kulifanya jambo la kukataliwa katika hali ya kitamaduni. Paulo hatangazi hukumu unaofunika juu ya wale wote wanaochukua baadhi ya mambo katika tamaduni zingine na kuacha zao. Hii ni wazi kutokana na kuwa alifanya Timotheo kutahiriwa (Matendo ya Mitume 16:3), na kutokana na neno lake mwenyewe kuwa anafanyika mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia yoyote aweze kuokowa baadhi yao (1 Wakorintho 9:22). Kile Paulo alikuwa akidhihirisha ni kwamba kutii amri za Mungu ni muhimu zaidi kuliko dhihirisho za kitamaduni, na kwa kubadilisha tu hizi dhihirisho za kitamaduni haifahi iwe na umuhimu yoyote kwa Mkristo. Kwa maneno mengine, usitaabike sana kama umetahiriwa ama hujatahiriwa, ama kama wewe ni mweupe ama mweusi ama mwekundu ama mtu wa asili ya Uswidi. Lakini fanya utiifu kuwa jambo kubwa; fanya lengo lote la maisha yako liwe kutii amri za kiadili za Mungu. Hapo ndipo kutahiri (vile 3 Paulo anakusudia kusema katika Warumi 2:25) na mambo mengine yote ya kitamaduni yanayotenganisha yatakuwa ya kupendeza, kwa njia ya ziada na ya kuvutia kama onyesho la utiifu kwa imani. Kwa neno mmoja, matumizi ya maadili ya Paulo kwa tofauti za kitamaduni ni hili: Usiogope wala kuringa kuhusu hali yako ya sasa ya tofauti za kitamaduni; yana umuhimu mdogo kwa Mungu ukiilinganisha na vile unajitolea wewe mwenyewe, moyo na fikira na mwili, kuzitii amri zake ambazo zatimilizwa katika hii: “Mpende mwenzako vile unavyojipenda” (Warumi 13:8-10; Wagalatia 5:14)

Maadili yanayotumika kwa watumwa na walio huru

Halafu Paulo anageukia mistari 21 hadi 23 kutumia maadili yake kwa hoja ya kama mtu ni mtumwa ama huru. Shida ya ufasiri katika fungu la 21 ni mgumu mno. Tafsiri za kisasa kabisa zasema, “Je, uliitwa ukiwa mtumwa? Usijali. Lakini kama unaweza kupata uhuru wako, jiweke tayari kwa nafasi hiyo” (RSV). Hii inaweza kuwa kweli, lakini naipata kuwa ngumu kukubali kwa kuwa maadili ambayo anayaangazia yameelezwa katika mstari wa 20 kama, “Basi kila mmoja wenu na abaki katika hali alioitwa nayo,” na katika mstari wa 24 kama, “Kama kila mtu alivyoitwa, akae katika mwito wake alioitiwa na Mungu.” Inaonekana yote ni kama isio na haja kati ya haya kusema, “Kama unaweza pata uhuru wako, ifanye.” Si tu hiyo, lakini tafsiri hi halitendi haki kwa maneno yote ya Kigriki (“hata” na “afadhali”) ambayo yanatokea katika tafsiri badala. “Je, uliitwa kama mtumwa? Usiache hiyo ikujalishe; lakini, hata kama unaweza kuwa mtu huru, afadhali tumia (hali yako ya sasa).” Tofauti ya hakika, inaonekana kwangu, yafaa kusisitizwa kama: “Usiruhusu utumwa wako ukuweke katika hali ya wasiwasi, afadhali uitumie.” Uitumie kumtii Kristo na hivyo basi “vaa maadili ya Mungu wetu mkuu na mwokozi” (Tito 2:10).

Nadhani ni kweli katika mtazamo wa mwisho kuwa hii siyo makataa kabisa ya kukubali uhuru, kuliko vile mstari wa 18 ulivyokuwa makataa kwa kutahiri. Lakini ukiitafsiri kama amri ya kutafuta uhuru, hoja ya kweli ya aya hii inapoteza maana. Hoja ni: unapoitwa katika ushirika wa Kristo, unapokea aina mpya ya nafasi iliyozingirwa kwa Yesu; kwa wingi kwa kiasi kwamba ikiwa wewe ni mtumwa, haifai kukuhuzunisha. “Je, ulikuwa mtumwa ulipoitwa? Usijali.” Je, kazi yako ni ya mkono? Usijali. Je, ni kazi isiochukuliwa kwa hali ya juu kama taaluma zingine? Usijali. Hii ndiyo hoja sawia aliokuwa akisema kwa tofauti za kitamaduni kama kutahiri: Je, ulikuwa hujatahiriwa? Usijali. Je, ulikuwa umetahiriwa? Usijali.

Paulo angepeana sababu hio hio ya kithiolojia kwa hali hii vile alivyofanya katika mstari wa 19. Angesema, “Kwani kuwa mtumwa ni bure, na kuwa mtu huru ni bure, lakini kutii amri za Mungu ni kila kitu.” Hii ni kweli. Lakini Paulo anaimarisha kuelewa kwetu na sababu mpya ya kithiolojia. Sababu mtu anaweza kusema, “haijalishi” hata kama yeye ni mtuwa, ni hii katika mstari 22, “Kwa maana yeyote aliyeitwa katika Bwana kama mtumwa yeye ni mtu huru kwa Bwana.” Na sababu ya kufanya mtu aliye huru kusema, “Haijalishi,” ni sawia. “Yeyote aliyekuwa huru alipoitwa yeye ni mtumwa wa Kristo.” Napenda kutazama Paulo akiweka theolojia yake kufanya kazi kwa njia hii. Anasema katika lnjili kuna dawa ya kukata tamaa katika kazi za mikono na dawa ya kiburi katika kazi zilizo na hadhi ya juu. Anamtazama mtumwa ambaye anaweza kuhisi kukata tamaa na kusema, “Kwa Kristo wewe ni mtu huru. Ulinununuliwa kwa gharama. Wacha mtu yeyote asije akafunga moyo wako. Furahi katika Bwana na uwe na tumaini ndani yake na utakuwa huru zaidi kuliko wakuu waliojawa na wasiwasi.” Halafu anatazama wakuu walio huru na kusema, “Msiwe na kiburi kwa kuwa ndani ya Kristo ninyi ni watumwa. Kunaye aliye na mamlaka zaidi juu yenu, na lazima muwe wanyenyekevu na watiifu.”

Chanzo cha hiki ni kwamba hata kama mtu ni mtumwa au huru, haifai iwe sababu ya kukata tamaa kwake ama kiburi yake. Anafaa aweze kusema, “usijali.” Hafai kuringa kama yeye ni daktari ama wakili ama afisa mtendaji, na hafai kujihurumia ama kuhuzunika kama yuko na kazi ambao jamii wanaidunisha. “Basi ndugu zangu,” Paulo anatamatisha katika mstari wa 24, “Kama kila mtu alivyoitwa, akae katika mwito wake aliyoitiwa na Mungu.” Na Mungu! Huo ndio msemo muhimu sana. Hoja sio kwamba eti kazi zetu ni ya ngazi ya juu ama ya chini machoni pa mwanadamu. Cha muhimu ni kama tunahimizwa na kunyenyekezwa katika uwepo wa Mungu

Kuweka matumizi mawili ya Paulo pamoja, mafundisho yanaonekana kuwa haya: Kutii amri ya Mungu (mstari 19) na kufurahia uwepo wake (mstari 24) yana umuhimu zaidi kuliko yale tamaduni ama kazi yako ilivyo ambapo unafaa kutohisi kikwazo chochote kubadilisha msimamo wako. Usivutwe kwa mtu kwa sababu ya uoga ama kukata tamaa, wala kuvutwa na mwingine kwa sababu ya mali au kiburi. Unafaa kusema kwa msimamo wako, “Haijalishi. Wewe si maisha yangu. Maisha yangu ni kumtii Mungu na kufurahia uwepo wake.”

Athari nne za dharura

Wacha nitamatishe sasa na baadhi ya athari za dharura. Kwanza, Mungu anajali sana vile unavyofanya kazi ulio nayo sasa kuliko vile alivyo juu ya kama utapata kazi mpya. Katika umati huu tunao; wauguzi, walimu, maseremala wasani, makatibu, makarani, mawakili, wapokezi, maasibu, wafanyikazi wa jamii, waundaji wa kila aina, waandisi, mameneja wa ofisi, wahudumu wa hoteli, mafundi wa aina mbalimbali, wachukuzi, seremala, walinzi, madaktari, wafanyi kazi katika jeshi, washauri, wahudumu wa benki, maafisa wa polisi, wapambaji, wanamuziki, wapakaji rangi, wapiga deki, viongozi wa shule, wake nyumbani, wachungaji, watengenezaji wa vifaa vya kuhifadhi stakabadhi na wengine wengi. Na yote tunayofaa kusikia ni kuwa kile kilichoko sana ndani ya moyo wa Mungu si eti tunatoka kwa kazi moja hadi nyingine, bali kama katika kazi zetu za sasa tunafurahia uwezo wa Mungu ulio aidiwa na kuzitii amri zake kwa  ile njia tunavyofanya kazi zetu.

Pili, vile tumeona, amri ya kubaki katika mwito uliokuwa kabla ya kuitwa, si halisi. Haikatazi kubadilisha kwote kwa kazi. Tunajua hii si tu kwa sababu ya nafasi Paulo aliacha kwa madili yake hapa katika 1 Wakorintho 7 (mstari 15), lakini andiko pia linaonyesha na kuruhusu mabadiliko kama hayo. Kuna nafasi ya kuweka huru wafungwa katika agano la kale, na tunamfahamu mtosha ushuru aliyefanyika mchungaji na wavuvi waliofanyika wahudumu. Mbali na haya, tunajua kwamba kuna kazi zingine ambazo hungeweza kubakia na kuzitii amri za Mungu; kwa mfano ukahaba, utumbuizaji wa aina tofauti tofauti usio na utu mwema na unaochafua na yale ambayo yatakulazimisha kufunyilia watu. Paulo hasemi kuwa mwizi sugu ama kahaba wa dhehebu la Korintho abaki katika mwito aliyoitiwa. Swali katika Korintho lilikuwa; tunapo kuja kwa Kristo yafaa tuachilie nini? Na jibu la Paulo ni; haufai kuacha mwito wako ukiwa unaweza baki ndani yake na Mungu. Hoja lake ni kwamba asihukumu ubadilishaji wa kazi. Bali kufundisha kwamba unaweza kuwa na utimilifu wa Kristo kwa kazi yoyote. Hili ni fundisho lisilokuwa ya mtindo katika jamii za magharibi wa kisasa, kwa maana inazuia nia zote za kiulimwengu. Yafaa tufikiri kwa urefu na kwa undani juu ya kama yale tunawaambia watoto wetu kuhusu ufanisi ni kulingana na bibilia ama ni ya Kimerekani. Neno la Mungu kwetu sisi sote “wanao tafuta ufanisi” ni hili: Chukua hiyo nia na msukumo wote ambao unaweka katika kuinuka kwako juu na badala yake uimwage katika shauku ya kiroho ili kuleta furaha ya uwepo wa Mungu na utiifu kwa mapenzi yake uliofunuliwa katika andiko.

Ya tatu, kwenu watu chiukizi ambao hawajaingia katika taaluma, maana ya andiko hilo ni hii: Unapojiuliza swali hili, “Ni nini mapenzi ya Mungu katika maisha yangu?” Inafaa upeane jibu mwafaka: “Mapenzi yake ni kuwa niuhifadhi ushirika wa karibu naye na kujitolea kuzitii amri zake.” Mapenzi ya Mungu iliyodhihirishwa kwako (mapenzi peke unayostahili kuyatii) ni utakaso wako (1 Wathesalonike 4:30), si kazi yako. Jitole kwa moyo wako wote na uchukue kazi yote utakayo. Sina shaka kwamba, kama watu wote chipukizi wanafanya kila juhudi kukaa karibu na Mungu na kuzitii amri za andiko Mungu atawasambaza ulimwenguni kwa mahali pa kipekee ambapo anataka usawishi wao uwe kwa ajili yake.

Ya nne, na ya mwisho, hili andiko linamaanisha kwamba kazi ulio nayo sasa, bora tu uwe hapo ni mpango wa Mungu kwako. Mstari 17 inasema, “Lakini kila mtu na aishi maisha yake aliyopangiwa na Bwana.” Mungu ni mtawala. Si ajali kuwa upo pahali ulipo. “Moyo wa mtu huifikiri njia zake bali Bwana huelekeza hatua yake” (Mithali 16:9). “Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama” (Mithali 19:21). “Kura hupigwa katika kufunikwa, lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana” (Mithali 16:33). Upo pahali ulipo kwa sababu ya mpango wa Mungu hata kama umefika hapo kwa kashfa. Kazi yako ni jukumu la kuhubiri, kama vile ilivyo kwangu. Vile unatimiliza mahitaji ya kazi hiyo ni muhimu maishani kama vile unavyofanya siku ya Jumapili. Kwa wengi wetu hiyo itamaanisha kubadilisha ukurasa mpya kuanzia kesho asubuhi. Wacha sote tuombe kabla tuanze kazi: “Mungu, enda nami leo na uhifadhi fahamu yangu kwa uwezo wako. Nihimize wakati nahisi kukata tamaa na uninyenyekeze wakati ninajaribu kuringa. Ewe Mungu, nipe neema ya kuzitii amri zako, ambazo ninajua zimejumuishwa ndani ya hii, kupenda jirani yangu vile ninavyojipenda mwenyewe. Amina.”