Kuvumiliana, kusemesana ukweli, urugu, na sheria

Article by

Founder & Teacher, desiringGod.org

Tangu Septemba 11, 2001 Swali kuhusu jinsi gani wakristo na Waislamu wanashirikiana imekuwa ya dharura sana. Swali hili limekuwa sehemu ya swala kuu kuhusu jinsi gani Wakristo wameitiwa, Kuishi katika ulimwengu ulio na tabaka na tamaduni tofauti tofauti. Haswa zaidi, vipi Wakristo wa hapa Marekani, tunavyofikiria na kutenda kuhusu uhuru wa dini katika muktadha wa tabaka na tamaduni tofauti, tofauti ikielezwa na maoni ya wanao tuwakilisha ki demokrasia? Hasa, tutashudiaje ukuu wa Kristo ulimwenguni palipo na tamaduni na dini yenye nguvu na ambazo hazishiriki upendo wa uhuru au maoni ya demokrasia?

“Wazee wa Kanisa la Bethlehem Baptist, Agosti 26, 2002, walikubaliana juu ya sheria (ishirini) 20 kama mwongozo wa kibibilia kwa Wakristo. Tunawashukuru, kwanza kisha kanisa ilio chini ya ulinzi wetu kwa mwongozo wao. Pia tunawashukuru Wakristo wote kwa ujumla kwa kuwaza kimakini na faida na latatu kwa watu wasio Wakristo kwa kuelewa kwenu. Juhudi zetu kuu ni kusaidia Wakristo kushukuru upekee na ukuu wa Yesu Kristo kwa unyenyekevu na ujasiri ili wengine wapate kumtukuza kwa imani na wapate uzima wa milele."

1. Iwe tume kubalika au tumekataliwa na wengine tunafaa kuwa shukran na furaha kushikilia kabisa ukweli wa kuelewa Mungu kibibilia na njia ya wuokovu ambayo amepeana na maisha ya upendo na usafi na haki ambayo Kristo amefanya na kufunza. (1 Wakorintho 15:2; Waebrania 3:6; 4:14; 6:18; 10:23 Ufunuo 2:13, 25; 3:11)

2. Kanisani pia ulimwenguni tunafaa kufanya wasia wa Mungu kuonekena wazi na usawa inavyo funuliwa katika neno lake, Biblia—kwa upande zote ambazo wasio Wakristo wana kubali na pande wanazo pinga. Hatufai kuficha ishara ya imani yetu ili kuhepa kukashifiwa na kukataliwa. (Mathayo 10:27-28: Waefeso 6:19-20; 2 Wakorintho 4:2; Wagalatia 1:10)

3. Ni upendo kuonyesha makosa na madhara ya Imani zinazo mkataa Kristo. Madhara inajumuisha sio tu athari ya muda mfupi, lakini sana sana uchungu wa milele inayo sababishwa na kukataa ukweli wa Kristo. Onyo hili linapaswa kupeanwa kwa bidii na kwa kumaanisha na kwa kutamani uzuri kwa wale walio katika hatari ya ghadhabu ya kutomtumaini Kristo. (Luka 6: 31-32; Warumi 13:10; 1Timotheo 4:8; 2 Wathesolanika 1: 8-9; 2 Wakorintho 5:20)

4. Sisi wakristo tunafaa kukubali dhambi zetu na kwa njia yoyote ile wuokovu kupita mokozi aliyesulubiwa na aliye fufuka ili tusijiweke kama wanaostahili wuokovu kanakwamba tuna nguvu kuu ya akili inayo tuwezesha kufikiria na kujifunza au maarifa au uzuri. Sisi ni fukara na waombaji ambao ni kwa neema tu ndio tumepata mkate wa uzima wa ukweli, msamaha, na furaha. Tunakusudia kuipeana yote, ili watuunge kwa kutamani na kufurahia ukuu wa Kristo milele. (1 Wakorintho 1:26-30; 4:7; 1 Petero 5:6; Yakobo 4: 8-10; Luka 18:13-14; Mathayo 10: 8b)

5. Tunafaa kumwonyesha Kristo sio kama aliye shinda ubishi kati ya dini, bali kama mwaminifu na msema kweli sana, Mrembo, muhimu, na mtu mwenye kutamanika katika historia, na kama hitaji letu na upendo mbadala kwa njia mbili: 1) Alichukua kwa kuteseka na kwa kifo chake, ghadhabu ya Mungu badala yetu na 2) Alikuwa utakatifu wetu mbele ya Mungu mtakatifu zaidi kwa kuishi maisha bila dhambi iliyo tafsiriwa kama utakatifu kwetu tunapo mwamini Yesu. (1Wakorintho 2:1-2; 2 Wakorintho 4:4; 1 Petero 2:6-7; Warumi 3:24-26; 5: 18-19: Wagalatia 3: 13; 2 Wakorintho 5:21)

6. Inafaa tuweke wazi ya kuwa imani ya Kikristo inayo tupatanisha na Kristo na fadhili zake zote za kutuokoa, ni kama mtoto mchanga, tumaini ipotezayo taraji katika thamani na kazi ya Kristo na sio kazi yetu tuliostahili sisi. Mwito wetu kwa wengine kuwa Wakristo sio mwito wa kufanyia Mungu kazi au kupata kibali chake kwa kufanya matendo ya utakatifu au upendo. Tunawaita watu ili waache kujitegemea na kutegemea maisha ya kufa na kufufuka ya Yesu Kristo inayo okoa. (Waefeso 2:8-9; Tito 3:5; Warumi 4:4-5; Warumi 10:1-4; Wafilipi 3:9)

7. Tunamini ni haki na jambo la upendo kuonyesha makosa ya hayo imani mengine adharani, iwapo tu, hili litafanywa kupitia ushahidi wa kutosha yakuwa maandiko ya kanisa au mwakilishi mnenaji wa imani hizi ameashiria  makosa hayo. Na ya dharura  tung’ang’ane ili tusije tukaonyesha imani mengine vibaya kwa sababu hayo sio tu kukosa heshima bali pia inashusha ukweli wetu. (Matendo ya Mitume 6:8-7:53; Mariko 12:24; Mariko 8:33; Matendo ya mitume 3:15; 5:30; Kutoka 20:16; Waefeso 4:25)

8. Tunapoweka wazi makosa ya dini mengine, tunafaa kuhisi na kuonyesha huzuni na huruma kwa wale wasio kubali Kristo ili waokoke. (Luka 19:41-42; Wafilipi 3:18; Warumi 9:3; 10:1)

9. Tunafaa kuweka wazi kuwa sisi ni Wakristo kwanza kisha wa Amerikani. Sisi ni wageni hapa ulimwenguni na uraia wetu wa kindani na wa ukweli zaidi uko mbinguni. Bwana wetu  mkuu na kiongozi ni Yesu Kristo wala sio rais wa Amerika. Hili kwanza na uhusiano wetu wa kindani sana una tuunganisha na Wakristo wa mataifa tofauti, tofauti kwa nguvu sana kuliko uraia wetu wa kidunia unavyo tuunganisha na wa Amerika wengine.Tukizingatia maadili na tabia za Wa Amerika wengi sisi ni raia walio keuka. Tamaduni ya ki Amerika sio Ukristo. Tunaamini kuwa, sio uzalendo mbaya kukashifu maovu na matendo yasiyo ya ki Mungu katika tamaduni yetu. (Wafilipi 3:20; 1Petero 2:11; Mathayo 22:21; Matendo ya Mitume5:29; 1 Timotheo 6:14-15; Ufunuo 17:14; Waefeso 5:11)  

10. Tusitarajie “vita vya adili” katika ulimwengu wa kidunia ambayo ni uadui kwa Mungu na haina starehe karibu na ukweli wa Kristo. Kwa hivyo, majibu yetu kwa matusi au kubadilishwa kwa ukweli, au kusemwa vibaya, haifai kuwa hasira lakini ku shuhudia ukweli wa uvumilivu, kwa tumaini na kwa maombi kwa kurudisha mema kwa mabaya yaweza fungua nyoyo kwa ukweli. Kushuhudia kwetu hautaendelea mbele kwa hasira na kutangaza juu haki yetu. Itaendelezwa na “Mateso lakini tunafurahia kila wakati” na kwa kushinda uovu kwa uzuri na kwa maneno yaliyo dhabiti na kulinda ukweli kwa njia ifaayo. (Matahyo 5:43-45; Warumi 12:17-21; 1Wakorintho 4:12-13; 1 Wathesolanika 5:15; 2 Timotheo 3:12; 1 Petero 2:15, 19-24; 3:9; 4:12)

11. Tunafaa kukataa dhuluma zote kama njia mojawapo ya kueneza imani yetu. Wakristo wa kibiblia hawajaribu kutumia siasa au dhuluma ya kibinafsi ili kueneza imani yao. Wakristo wanaeneza imani yao kwa kuteseka, wala sio kwa kusababisha mateso. Ukristo wa Asili hauwezi kulazimishwa kwa nguvu au kutumiwa kwa njia ya uwongo. (Luka 10:3; 2 Wakorintho 5:11; Wakolosai 2:24; 1Petero 2:19-24; Ufunuo 12:11)  

12. Tunafaa kukubali na kutangaza yakuwa, Kristo wakati wake wa kuja, atawaadhibu wale ambao wamemkataa. Atawaamrisha kwa hukumu ya milele jehanamu yenye mateso. Walakini tunapaswa kufanya wazi yakuwa dhuluma ya Kristo wakati wa kiama ni sababu kuu ili tusifanye vita na huenda hatuta fanya dhuluma dhidi ya wengine kwa sababu ya Imani yao. Hii ni haki ya Mungu, sio yetu. (Mathayo 25:46; Warumi 12:19; Wathesolanika 1:7-9; 1 Petero 2:20-23; Ufunuo 6:16)

13. Wakati huu wa sasa kabla ya kuja kwa Kristo, yeye binafsi, mamlaka ya kiraia hawafai kutumia nguvu ya kimabavu au kutumda uweza wa lazima au kukwamilia  mapato yaku tunuku au adhibu watu kwa sababu  ya imani yao. (Imesemwa kwa mienendo ya kibiblia ya Imani ya kujitenea inayotafutwa na uwezo wa ushawishi na mfano; na mahitaji ya uungu inayowezesha neema ya kubadilisha. (2Wakorintho 5:11; 1Wathesolanika 1:5-6; Waefeso 2:8-9; Matendo ya Mitume 6:14 Wafilipi 1:29; Timotheo 2: 24-26)

14. Hakuna kulazimishwa kwa kutumia mabavu au kutumia uwezo wa lazima au kukwamilia mapato inafaa kutumiwa na mamlaka ya ki raia ku adhibu watu kwa sababu ya maneno yao au maandishi au pia michoro, isipokuwa tu kama mawasiliano yaweza onyeshwa kupitianjia zote za sheria ili kuonyesha nia ya kutenda maovu au kusaidia wengine kutenda maovu. (Tazama usaidizi wa #13)

15. Tunaamini kuwa Mungu amepatia serikali ya raia wala sio watu binafsi au kanisa jukumu ya “kubeba upanga” ya haki na usalama. (Mathayo 26:52; Warumi 13:1-4; Warumi 12:17-21; 1 Petero 2:20-23; 3:9, 14)

16. Tunafaa kufafanua kati ya vita haki ya kujikinga dhidi ya uadui, na vita vya kidini dhidi ya watu kwa sababu ya yale wanayo amini. Tunafaa ku kubali yakuwa, tofauti hizi huenda hazita tambuliwa na dini zengine ambazo zinaendeleza imani yao kujumuisha haki ya kutawala tamaduni kupitia nguvu. Lakini tunafaa kusisitiza utofauti huu kuliko kukubali madai ya mchokozi ya kuwa, kujilinda kwetu dhidi ya uchokozi wao ni uvamizi wa kidini dhidi ya imani yao. Tutatetea kwamba msingi ya ulinzi wa kitaifa kama hiyo ni haki ya raia kupata uhuru (wa dini na kuongea na utangazaji na mikutano) sio kutokubali hilo dini ambayo inasababisha uvamizi. Hatutakubaliana na dini mengine lakini kutokubaliana huo sio msingi wa upande wa ulinzi wa kitaifa uliojiami. Tunafaa kutofautisha kati ya kundi ya kijeshi isiyo halali inayopigana dhidi ya kundi halali ya kidini, Kwa upande mmoja na kutiwa moyo kwa upingaji wetu kwa upande mwingine, ambao sio kukataa dini lolote lakini huru wa dini zote kupata waamini kwa njia isiyo ya dhuluma ya kushawishi na kuwavutia. (Imechangiwa katika maoni iliyopita)

17. Tunafaa kujua yakuwa imani na tabia haina msimamo sawa mbele ya sheria. Hakuna imani inayofaa kuadhibiwa na mamlaka ya kiraia. Lakini tabia zingine, zilizo na mizizi katika imani, yaweza kuwa nje ya sheria na kwa hivyo yaweza kuadhibiwa na mamlaka ya kiraia. Tabia hizi zaweza kuwa kama kuuwa watu wengine, kuvamia na kupiga watu wengine vibaya, kuiba, aina tofauti ya kukandamiza. Tabia hiz ambazo zimepigwa marufuku kisheria katika makaazi ya watu wakizingatia uhuru wa imani na uhuru wa dini zitaamuliwa katika hali na wakati wa ushawishi wa mjadala na uchaguzi wa wanasheria wanaowakilisha, na wakitazamwa kwa makini na watawala na tawi za mahakama na walindao sheria ili kulinda haki ya walio wachache. Kutoeleweka vizuri umetambulika. (Angalia kiunga mkono ya #13 na maadhara ya maoni mengine yakichukuliwa pamoja)

18. Tunafaa kutofautisha kati ya haki ya kukashifu imani potovu na tabia za dhambi, kwa mkono mmoja, na maoni ya uwongo ambayo wengine huwa nayo kuhusu hili kukashifu yakuwa wanao unga mkono imani inayo kashifiwa wanaweza dhulumiwa kwa haki bila tatizo. Hatufai kukubali madai yakuwa kukashifiwa au kukataliwa kama walio kosewa au kama watenda dhambi ni njia mojawapo ya “kudhulumiwa". Sio uhalifu (Uhalifu wa chuki au chochote kile) Kuwita imani ya mtu adharani kuwa mbaya na hatari, au kuita tabia ya mtu hadharani kuwa dhambi na ya kuangamiza. Sehemu muhimu katika mjadala yote kuhusu imani na tabia na maoni na ubishi yakuwa mengine na mbaya, yamejengwa kwa ila, na yana madhara ya kufufua ukweli. Hivi ndivyo mijadala yote ya wabunge huendelea. Hii ni halali katika ulingo wa dini. Kwa mfano, ikiwa  mbunge wa Amerikani amedhulumiwa kwa kutumia mabavu na mtubarabarani baada ya kukashifiwa bungeni kwa sababu hoja yake ilikuwa na makosa na kwa sababu hakuwa ameshauriwa vizuri na hoja lile linge umiza maskini aidha hatuwezi laumu mbunge aliye kashifu mwenzake kwa sababu ya dhuluma aliyetendewa mbunge Yule na kumshtaki kwa kuchochea dhuluma. Basi ni lazima tu tofautishe kati ya kukashifiwa adharani juu ya dini na tabia kwa upande moja na maoni isiyo halali kuhusu imani na matendo ya dhambi imetosha kudhulumiwa. (Angalia kiunga mkono katika #3 na #7)

19. Tunaamini kuwa imani tofauti, tofauti ya badilisha maana ya ndani ya kuhukumiwa na tabia, lakini hayabadili aina yote ya kuhukumika na tabia. Basi kwamfano, watu wawili waweza kuwa na imani tofauti, lakini wanashikilia hukumu sawa na tabia sawa kuhusu uavyaji wa mimba. Tunatamani kuwa watu wote wangeshiriki imani ya Kristo na wawe na hukumu na tabia ambayo maana yao ya ndani ni yakuwa, Kristo ni Bwana na zawadi ya maisha. Lakin hata hivyo tunafuraha wakati aina ya hukumu yetu na tabia zetu zinashirikwa na wale wana tofautiana nasi katika imani. Tunaamini inawezekana kuwa pamoja nao kwa mambo ya kijamii mradi tu hayo matendo tunayo shiriki pamoja hayadhuru maoni yetu ya hukumu inayo tukuza Kristo. (1 Wakorintho 10:31; Wakolosai 3:17; Warumi 14:23)

20. Tunaamini kuwa kila dini, maono ya ulimwengu, au filosofia ya maisha yaweza  kazana zaidi kutushawishi na kujenga tamaduni yetu. Tunapinga utumizi wa mabavu au hongo au udanganyifu katika hii nia ya kujenga tamaduni. Tunasisitiza kuhubiri injili, uchapishaji wa ukweli, ufinyanzi wa upendo na haki, nguvu ya maombi, utumizi wa ushawishi, na kushiriki katika siasa. Tunatambuwa yakuwa sheria zote “Imesababisha” tabia ya hukumu ya vikundi vingine. Basi sio ukashifu inayopendeza kusema yakuwa sheria inayolinda tabia ni mbaya kwa sababu ina “tawala" utu wa mtu kuhusu uma. Hata hivyo, hii inaifanya muhimu zaidi yakuwa tunaunga mkono maadili, sheria, na aina ya tabia inayo linda uhuru halali ya wachache wasiyo na wakilishi mkubwa wa kubadilisha hatuwa ya kujenga sheria. Kiwango ya uhuru haya unapimwa na sheria yanayo ashiriwa hapo juu sana sana #17. (Imezingatiwa katika sheria na kiunga mkono za hapo awali)