Uasi wa kufisha wa Adamu na ushindi wa utiifu wa Kristo

Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja na kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi. 13 Kwa maana kabla sheria haijatolewa, dhambi ilikuwepo ulimwenguni. Lakini dhambi haihesabiwi wakati hakuna sheria. 14 Hata hivyo, tangu wakati wa Adamu hadi wakati wa Mose, mauti ilitawala watu wote hata wale ambao hawakuvunja amri kama alivyofanya Adamu, ambaye alikuwa mfano wa yule atakayekuja.  15 Lakini ile karama iliyotolewa haikuwa kama lile kosa. Kwa maana ikiwa watu wengi walikufa kwa sababu ya kosa la mtu mmoja, zaidi sana neema ya Mungu na ile karama iliyokuja kwa neema ya mtu mmoja, yaani, Yesu Kristo, imezidi kuwa nyingi kwa ajili ya wengi. 16 Tena, ile karama ya Mungu si kama matokeo ya ile dhambi. Hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu, bali karama ya neema ya Mungu ilikuja kwa njia ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. 17 Kwa maana ikiwa kutokana na kosa la mtu mmoja, mauti ilitawala kupitia huyo mtu mmoja, zaidi sana wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na karama Yake ya kuhesabiwa haki, watatawala katika uzima kwa njia ya huyo mtu mmoja, yaani, Yesu Kristo.  18 Kwa hiyo, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa watu wote, vivyo hivyo pia kwa tendo la mtu  mmoja la haki huleta kuhesabiwa haki kule kuletako uzima kwa wote. 19 Kwa maana kama vile kwa kutokutii yule mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki.  20 Zaidi ya hayo, sheria ilikuja, ili uvunjaji wa sheria uongezeke. Lakini dhambi ilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi. 21 Ili kwamba kama vile dhambi ilivyotawala kwa njia ya mauti, vivyo hivyo neema iweze kutawala kwa njia ya kuhesabiwa haki hata uzima wa milele katika Yesu Kristo Bwana wetu.

Yesu ni mtawala mkuu

Lengo kuu la toleo hili ni kutilia mkazo mawazoni mwetu ukweli ya kwamba Yesu ndiye mtu muhimu zaidi ulimwenguni—si kuliko Mungu Baba wala Mungu Roho. Kwa hawa utatu wako sawia kwa thamani, hekima, haki, upendo aidha nguvu. Lakini ana thamani zaidi ya watu wengine wote—wawe malaika au mapepo au wafalme au makamanda au wanasayansi au wasanii au wana falsafa au wanariadha au wanamuziki au watendaji—wale ambao wanaishi sasa, awliyeishi hata watakayeishi, Yesu ni mtawala mkuu.

Mambo yote ya Yesu—hata kwa uovu

Kwa toleo hili aidha imekusudiwa kuonyesha kwamba kila kitu kilichopo—hata uovu— imeamuriwa na Mungu Mwenye Utakatifu na Mwingi wa hekima ili kuhakikisha utukufu wa Kristo uangaze hata zaidi. Wiki hii baadhi yetu wamesoma katika mpango wetu wa usomaji wa Biblia: Mithali 16:4 “Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake. Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.” Mungu amefanya haya kwa njia zake zisizofahamika ili kuhifadhi jukumu la wabaya na watakatifu katika moyo wake. Wiki mbili zilizopita tuliona kwamba vitu vyote viliumbwa kwa Yesu Kristo na katika Kristo (Wakolosai 1:16). Na hii inajumuisha, asemavyo Paulo, “enzi, utawala, watawala na wamiliki” ambao walishindwa na Kristo msalabani. Waliumbwa kwa ajili ya “siku ya ubaya.” Siku hiyo nguvu, haki na ghadhabu, na upendo wa Kristo ulidhihirishwa. Bila kukawia, kila uasi dhidi yake utaharibiwa.

Mungu ambaye yuko

Toleo hili pia inasisitiza na kudhibitisha kuhukumika kwamba Ukristo si tu mpangilio wa mawazo, desturi, na hisia zinazoegemea maslahi yetu kimaumbile—iwe chanzo chake ni Mungu au mwanadamu. Hii si Ukristo vile ulivyo. Ukristo huanza na imani kuwa Mungu ni uhakika na anakusudi nje ya sisi wenyewe. Hatuwezi kumfanya awe alivyo kwa kufikiria kwa jinsi Fulani kumhusu. Kama vile Francis Schaefer alivyosema: Yeye ni Mungu ambaye yupo. Hatumtengenezi. Anatutengeneza. Kwa vyovyote vile hatuwezi kubashiri atakavyo fanana. Yeye huamua jinsi tutakavyokuwa. Aliumba ulimwengu, na ina maana aliyoipatia, si tunayoipatia. Tukiipatia maana yeyote tofauti na iliopewa na Mungu, sis huwa tu wapumbavu. Hatima ya maisha yetu yatakuwa hatarini. Ukristo si mchezo wala tiba. Kila funzo lake yatiririka kutoka kwa vile Mungu alivyo na kile alichotenda kihistoria. Zinalingana na hoja ngumu. Ukristo ni zaidi ya pendekezo. Kuna imani, tumaini na upendo. Haya yote hayaelei tu angani. Yanakua kama mti mkuyu uliopandwa kwenye mwamba wa ukweli wa Mungu.

Sababu ninayotoa, hapa ni lengo letu kwa toleo hili hakikisho ni kwamba ndani yangu nimesawishika katika Biblia kuwa furaha, nguvu na utakatifu wa milele umeegemea uthabiti wa maoni ya kilimwengu ya kuweka azimio tosha kwa imani ambayo ni  uti wa mgongo. Maoni ya uoga hufanya Wakristo waoga. Wakristo waoga kamwe hawawezi kuendelea siku za usoni. Hisia zisizo na mzizi ambazo zimegubika ukristo kama chaguo la tiba zitafagiliwa mbali siku za mwisho. Watakao salia wakidumu ni wale tu ambao wamejenga nyumba zao kwenye jabali kuu, kusudi la ukweli katika Kristo Yesu, kama chanzo, kitovu na madhumuni wa mambo yote.

Utukufu wa Yesu ulipangwa katika dhambi ya Adamu

Mtazamo wake leo ni kwa dhambi ya mvuto wa binadamu wa kwanza Adamu, na vile ilivyoandaa jukwaa zaidi kwa makabiliano hatimaye ushindi wa mvuto wa Yesu Kristo. Tuelekee Warumi 5:12-21. Kwa majira ya kiangazi ya 2000, tulitumia wiki tano kwa mistari hii. Leo mtazamo wetu ni tofauti na yote tuliyoangazia katika wiki hizo.

Ningetaka kuangazia utukufu wa Kristo kama kusudi kuu ambalo Mungu alinuia alipopanga na kuruhusu tendo dhambi ya Adamu, na pamoja naye, kuanguka kwa wanadamu wote katika dhambi. Kumbuka nililosema wiki iliyopita: Chochote Mungu ameruhusu ina sababu, na sababu hizi huwa zenye hekima na kusudu wa kupindukia. Haikumbidi kukubalisha upungufu kufanyika. Angeukomesha vile tu angekomesha kuasi  kwa shetani (kama tulivyoona wiki jana). Kwa kutokomesha ina maana kwamba alikuwa na sababu na kusudi. Mungu hafanyi mipango yake kadiri mambo yanavyoendelea. Kile anachofahamu ni cha hekima, daima afahamu kuwa na hekima. Hivyo, dhambi ya Adamu na pia uasi wa wanadamu wote pamoja, naye katika dhambi na mateso hayakumshtua Mungu, bali ni uendelezaji wa mipango na udhihirishaji wa ukamilifu wa utukufu wa Yesu Kristo.

Mojawapo ya njia wazi kuonyesha haya katika Biblia—Na hatutafafanua zaidi hapa—ni kutazama sehemu ambazo dhabihu ya Kristo ya kushinda dhambi yanaonyeshwa katika mawazo ya Mungu kabla ya uumbaji wa ulimwengu. Kwa mengi zaidi tazama ujumbe, “Mateso ya Kristo na utukufu wa Mungu.” Kwa mfano Ufunuo 13:8. Yohana anaandika kuhusu “kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo aliyechinjwa; kwa hivyo kulikuwa na kitabu kabla msingi wa ulimwengu, kiitwacho. “Kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo aliyechinjwa.” Kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, Mungu tayari alikuwa amepanga kwamba Mwanawe atachinjwa kama mwana kondoo ili aokoe wote walioandikwa kwenye kitabu.  Tunaweza kudusu maandiko kadhaa kama vile: Waefeso 1:4-5, 2 Timotheo  1:9, Tito 1:1-2, 1 Petro 1:20. Ili tuone maoni ya kibiblia ya kwamba masaibu na kifo cha Kristo kwa ajili ya dhambi hayakupangwa baada ya kuasi kwa Adamu walakini kabla. Kwa hivyo, wakati dhambi ya Adamu ilipotendeka, Mungu hakushangazwa, bali alishaifanya kama sehemu ya mpango wake—yaani, mpango wa kudhihirisha ghadhabu, uvumilivu, neema na haki yake ya kushangaza katika historia ya ukombozi, hatimaye, kwa wakati, kudhihirisha utukufu wake kwa mwanawe kama Adamu wa pili mkuu katika njia zote kuliko Adamu wa kwanza.

Tutazame Warumi 5:12-21, wakati huu tia mawanzoni kwamba mbali na dhambi ya Adamu kutobatili madhumuni ya kuinua Kristo, bali zilizitimiza kusudi na kuyakamilisha. Mtazamo wetu katika mstari huu ni kwamba, kuna maelezo bayana matano kuhusu Kristo. Mmoja wao inaandaa jinsi Paulo anavyofikiria kuhusu Kristo na Adamu. Mengine yanaonyesha vile Kristo ni mkuu kuliko Adamu. Mawili yana   husiana, na hivyo tutayaambatanisha pamoja. Inamaanisha kwamba tutaangalia mambo matatu kuhusu ukuu wa Kristo.

Yesu, “ambayo yuaja”

Kwanza tutazame maelezo kuhusu Yesu katika mstari wa 14 halafu tusome mistari ya 12-13. Kwa yaliomo “Kwa hivyo kama  kwa mmoja dhambi iliingia ulimwenguni na kwa dhambi hiyo mauti, na hivyo mauti ikafikia watu wote, kwa sababu  walifanya dhambi. 13 Maana kabla ya sheria dhambi ilikuweko ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria. 14 Walakini dhambi ilitawala tangu Adamu  mpaka Musa nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. Hapa kuna asilia ya Kristo: “Yeye atakayekuja.”

Mstari wa 14 inafafanua mkondo wa fikira za Paulo katika ufahamu unaofuata.
Adamu anaitwa “yeye” atakayekuja. Yaani, Yeye Kristo. Kwanza gundua kilicho bayana hapa. Kristo alikuwaje tangu mwanzo. Kristo ndiye alikuwa anayekuja. Paulo anaonyesha kwamba Kristo si fikira ya baadaye. Paulo hasemi kwamba Kristo alishikiwa mimba yake kama mfano wa Adamu. Anasema Adamu alikuwa aina ya Kristo. Mungu alimuadhibu Adamu kwa njia ambayo ingemfanya asilia ya mpango wake kumtukuza Mwanawe. Asilia ni onyesho la jambo ambalo litatokea baadaye na litakuwa hivyo- nit u lenye utukufu. Sasa Mungu aliadhibu Kristo kwa njia ambayo ingemfanya asilia ya Kristo.

Chunguza kwa makini wapi, mtiririko wa mawazo Paulo anasema Adamu ni asilia ya Kristo. Mstari 14: Walakini mauti ilitawala tangu Adamu hadi Musa nayo ilitawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu,  aliye mfano wake yeye atakayekuja. Anachagua kutuambia kwamba Adamu ni mfano wa Kristo baada ya kusema hata wao ambao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa lake bado watajumulishwa kwenye hukumu sawa na Adamu. Kwa nini Paulo katika sehemu hii anasema Adamu ni mfano wa Kristo?

Yesu,  msimamizi wetu

Kwa sababu ya kile alichosema kinabainisha uhusiano na tofauti kati ya Kristo na Adamu. Hapa ndipo inashangaza: Watu wasiofanya dhambi kama ya Adamu walikufa kama Adamu. Kwa nini? Kwa sababu ya uhusiano kati yao na Adamu. Yeye ndiyealikuwa msimamizi mbele ya mwanadamu na dhambi zake zinahesabika kama ya wote kwa ajili ya uhusiano pamoja naye. Hii ndiyo sababu Adamu anaitwa mfano wa Kristo- na kwa sababu utiifu wetu si kama wa Kristo na bado tuna uzima wa milele pamoja na Kristo. Kwa nini? Kwa sababu tumeunganishwa na Kristo kupitia imani. Yeye ndiye msimamizi mbele ya kila mwanadamu na haki na ukamilifu wake unahesabiwa kwetu kwa ajili ya kuunganishwa naye (Warumi 6:5).

Kuna usambamba unaobainika kwa kuita Adamu mfano wa Kristo:

  • Adamu > dhambi ya Adamu > binadamu kuhukumiwa kupitia yeye > kifo cha milele
  • Kristo > Utakatifu wa Kristo > Utu mpya kupata haki ndani yake > Uzima wa milele

Sehemu ya ufahamu iliyobaki inaeleza ukuu wa Kristo  na kazi yake ya wokovu kuliko Adamu na kazi yake ya uharibifu. Kumbuka kile nilichosema mwanzoni. Tunachoona hapa ni Ufunuo wa Uhakika wa Mungu ambao unatambulisha ulimwengu kwamba kile aishiyekatika sayari hii amejumulishwa hapa kwa sababu Adamu alikuwa baba ya wote. Ina maana kwamba kila mtuunayekutana naye Marekani au nchi yoyote, kabila lolote anahusika kwa kile somo hili lazungumzia. Uzima katika Kristo na mauti katika Adamu. Hili ni somo kwa ulimwengu mzima. Usikose hiyo. Huu ndio ufafanuzi wa ukweli kwa kila mtu atakaye kutana naye. Maoni ya ulimwengu ya uoga huzalisha Wakristo waoga. Hii si maoni ulimwengu ya uoga. Imeenea kote katika historia na ulimwengu mzima.inahuishakwa undani kila mtu katika dunia na ndiyo yaliyomo kwenye mtandao.

Kusherehekea ukuu wa Kristo

Sasa tuangazie vile Paulo anavyosherehekea ukuu wa Kristo na kazi zake dhidi ya Adamu na kazi zake. Yanaweza fupishwa kwa sehemu  tatu: 1) Wingi wa neema 2) Utimilifu wa utiifu 3) Kudumu kwa uzima.

1) Wingi wa neema

Kwanza, mstari wa 15 na wingi wa neema. “lakini karama ya bure [karama ya utakatifu mstari 17] haina kosa. Kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake Yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.  Cha muhimu hapa ni neema ya Mungu lina nguvu zaidi ya kosa la Adamu. Haya ndiyo maana ya maneno haya “kimezidi zaidi. ”yamaanisha. zaidi sana neema ya Mungu . . . kimezidi kwa ajili ya wengi." Kama kosa la mtu mmoja lilileta mauti zaidi kiasi gani neema ya Mungu utaleta uzima.

Paulo analenga hasa kwamba. Neema ya Mungu ni “Neema ya mtu huyo mmoja Yesu Kristo.” Zaidi sana kuwa na neema ya Mungu na karama ya bure. Kwa neema ya mtu huyo mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wengi. Hii si neema aina mbili tofauti. Neema ya mtu huyo mmoja Yesu Kristo ni mantiki ya neema ya Mungu. Hivyo ndivyo Paulo anena kwayo, kwa mfano Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo (Kristo) wanadamu wote imefunuliwa.” Na 2 Timotheo 1:9. “Kwa neema yake ambaye alitupa kupitia Yesu Kristo.” Neema iliyo katika Yesu ni neema ya Mungu.

Neema hii ni tukufu. Ina uwezo wa kushinda vyote katika njia yake. Tutaona kwamba ina nguvu ya mfalme wa mbingu na nchi. Ni  neema inayotawala. Hii ndiyo sherehe ya kwanza ya ukuu wa Kristo dhidi ya Adamu. Kama  kosa la mtu mmoja Adamu na neema ya mtu mmoja Yesu zimekutana, Adamu na kosa lake atashindwa. Yesu na neema atashinda. Hii ni habari njema kwa wao ambao ni milki ya Kristo.

2) Utimilifu wa utiifu

Ya pili, Paulo asherehekea vile neema ya Kristo imeshinda kosa la Adamu na mauti, yaani utimilifu wa utiifu wa Kristo. Mstari wa 19: kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja (Adamu) watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja (Yesu) wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki. Sasa neema ya mtu mmoja Yesu Kristo inamuondolea dhambi- inamuhifadhi mtiifu hata kufa, kifo cha msalaba. Wafilipi 2:8 ili kwamba aweze kuwa bilaa mawaa- utiifu timilifu kwa Baba kwa niaba ya wale ambao wameunganishwa kwake kwa imani. Adamu alipungukiwa kwa utiifu wake. Yesu alifanikiwa kikamilifu. Adamu alikuwa chanzo cha dhambi na mauti. Kristo alikuwa chanzo cha utiifu na uzima.

Kristo ni kama Adamu aliyekuwamfano wa Kristo- wote ni wakilishaji wa mbele ya binadamu ya kwanza na binadamu  ya pili. Mungu anaeleza upungufu wa Adamu katika utu wake vilevile Mungu anafafanua ufanisi wa Kristo katika utu wake, kwa sababu hawa wawili wameunganishwa katika utu wao wanaowakilisha. Ukuu wa Kristo ni kwamba sit u kwa ufanisi wa kutii kikamilifu bali vile ili mamilioni ya watu wahesabiwe haki kwa ajili ya utiifu wake. Je! Wewe umeunganishwa na Adamu pekee? Je, wewe ni sehemu ya mtu mpya ambaye amehakikishiwa uzima wa milele?

3) Kudumu kwa utawala wa uzima

Tatu, Paulo hasherehekei tu neema inayounganisha ya Yesu Kristo, na utiifu kamilifu ya Kristo, lakini hatimaye, kudumu kwa uzima. Neema inaongoza kupitia utiifu wa Kristo kufikia ushindi wa uzima wa milele. Mstari wa 21 ili kwamba kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Neema inatawala kwa njia ya haki (hii ni kwa njia ya haki tiimilifu ya Yesu Kristo). Kwa upeo mkubwa na uzima wa milele- Na yote hayo ni kupitia Yesu Kristo Bwana wetu.

Au kwa mara nyingine mstari wa 17, ni ujumbe huohuo. Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana, wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watawala katika uzima kwa Yule mmoja Yesu Kristo. Mtindo huo huo: Neema kwa njia ya kipawa cha haki cha bure, inaleta utawala wa uzima na yote hayo ni kwa njia ya Kristo Yesu.

Nilitaja awali kwamba neema ya Mungu kwa Kristo Yesu ambaye Paulo ataja kwenye mistari hii ni neema tukufu. Hapa ndiposa unaona kuwa inatajwa neno kutawala. Kifo kina utukufu fulani juu ya wanadamu,na inatawala kote. Wote wafa. Walakini neema imeshinda dhambi na mauti. Inatawala katika uzima hata kwa wao waliokufa. Neema ya utukufu.

Utiifu wa mvuto wa Yesu

Hii ni ushindi mkubwa wa Yesu- alimshinda mtu wa kwanza kwa umbali. Dhambi ya mvuto wa Adamu si kuu kama vile mvuto wa neema na utiifu wa Kristo pamoja na karama ya uzima wa milele’ Kwa hakika mpango wa Mungu tokea mwanzo ndani ya haki yake timilifu ilikuwa kwamba Adamu awakilishe mbele wanadamu wote ambao wangekuwa mfano wa Kristo kama mwakilishi mbele ya Adamu mpya. Mpango ulikuwa kwamba kwa kulenganisha usawa na tofauti. Neema ya Kristo ungeng’aa zaidi kote.

Mstari wa 17 unaegemeza ujumbe huu kwako kibinafsi na pia kidharura. Umesimama wapi? “Kwa maana ikiwa kwa kukosa kwa mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema na kille kipawa cha haki watatawala katika uzima kwa Yule mmoja, “Yesu Kristo.” Chunguza maneno haya kwa uangalifu na kibinafsi wao wapokeao wingi wa neema na kile kipawa cha haki.”

Maneno yenye thamani kwa waovu

Maneno haya ni muhimu kwa wenye dhambi: Neema ni  bure, haki ya Kristo ni bure bila malipo. Je! Utaipokea kama tumaini na hazina ya maisha yako? Kama umekubali, “Tawala katika uzima kwa njia ya mtu mmoja Yesu Kristo.” Pokea sasa. Kuwa mshuhudaji kwa njia ya ubatizo. Na uwe sehemu ya Wakristo waliohai.