Kuuzwa kwa Yusufu na Mwana wa Mungu

Maneno ya kushangaza kwa Abramu

Kabla niwambie hadithi ya Yusufu na dhambi ya asili ya ndugu zake, lengo lake duniani kwa utukufu wa Kristo Yesu, wacha tuiambatanishe na Mwanzo 12. Abramu ameteuliwa na Mungu miongoni mwa watu wa ulimwengu kupitia neema ya bure na tena bila kumdai kitu chochote. Katika kitabu cha Mwanzo 12:2-3, Mungu anampa ahadi: “mimi nitakufanya taifa kubwa na nitakubariki, Nitalikuza jina lako, nawe utakuwa Baraka.3 Nitabariki wale wanakubariki, yeyote akulaaniye nitamlaani na kupitia kwa mataifa yote duniani yatabarikiwa.” Huu ndio mwanzo wana wa Israeli kupitia kwao, Yesu Kristo Mwana wa Mungu atakuja ulimwenguni kutuokoa kutoka dhambi zetu.

Katika mstari wa kumi na tano, Mungu anafanya agano la dharura na Abramu. Anatumia matendo ya kudhihirika na maneno mengine ya kustaajabisha. Anamwambia Abramu katika Mwanzo 15:13-16, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo sio yao wenyewe, nao watakuwa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne. Lakini nitaliadhibu taifa lile wanaolitumikia kama watumwa, hatimaye watatoka huko na mali nyingi. Wewe, hata hivyo utakwenda kwa baba zako kwa amani na kuzikwa katika uzee wema. Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana dhambi ya Waamori bado haijafika kipimo kilichojaa.”

Miaka mia nne!

Mwanzoni mwa uhusiano wake wa Agano na watu wake wateule, Mungu anatabiri kuishi kwao kwa miaka 400 Misri na kurudi kwa nchi ya ahadi. “Watateseka kwa miaka 400” Yuko na sababu zake zizizoeleweka, ya kuwafanya watoroke kwa karne 4 (tafakari) kabla ya kuridhi nchi ya ahadi sasa, anasema katika mstari 15. “dhambi ya Waamori bado haijafika kipimo kilichojaa.” Wakati wana wa Israeli watakaporudi kunyakua nchi ya ahadi kupitia uongozi wa Yoshua, katika miaka 400, wataharibu mataifa haya. Tunaweza kuelewaje haya? Kumbukumbu la Torati 9:5 inatupatia jibu la Mungu. “Si kwa sababu ya haki yenu na uadilifu wenu kwamba nitamiliki nchi yao, lakini kwa sababu ya uovu wa mataifa haya, Bwana Mungu wenu atawafukuza mbele yenu, lile aliloapa kwa baba zenu, kwa Abrahamu, Isaki, na Yakobo.” Unyakuzi wa nchi ya ahadi ni uamuzi wa Mungu kwa ukamilifu wa karne ya uovu.

Watu wa Mungu wanaingia kupitia majaribu mengi

Kwa sasa, Mungu asema kuwa watu wake watakuwa wageni katika nchi ambayo sio yao na watateseka kwa miaka 400, hii ni katika nchi ya Misri. Basi kuna mpango wa Mungu kwa watu wanaoenda katika haji – picha ya maisha yako duniani hadi mbinguni. Kama Mungu anapanga miaka 400 ya mateso kwa watu wake (Mwanzo 15:13) mbele ya nchi ya ahadi, tusishtuke wakati anatuambia, “kupitia mateso mengi ni hakika utaingia katika ufalme wa Mungu” (Matendo ya Mitume 14:22).

Utabiri uliotimika kutokana na dhambi ya asili

Swali kwetu leo ni: Itawezekanaje watu wa Mungu wakusanyike Misri? Na Mungu anataka kutufundisha nini juu ya njia zake na Mwanawe kupitia kwa kuishi kama wageni katika nchi ya Misri? Jibu ni kwamba Mungu anatimiza utabiri wake kupitia dhambi ya asili. Kupitia dhambi hizi, anahifadhi, sio tu agano lake hai lakini pia uhai wa wana wa Israeli, na pia jamii ambayo Simba wa Yuda atakuja kupitia ili aokoe na kutawala juu ya watu. Hivyo mambo makuu yamo katika hadithi hii ya Yusufu.

Abrahamu, Isaki na Yakobo

Tukirudi kwake Abramu, wacha tulete hadithi hii hadi kwake Yusufu. Abramu ana mwana aitwaye Isaki. Isaki ana mwana ambaye ni Yakobo (kwa jina lingine Israeli), na Yakobo ana wana kumi na wawili ambao ni baba ya makabila kumi na miwili ya Israeli. Mojawapo ya wanawe kumi na miwili, mabayeni Yusufu, anazo ndoto mbili. Kwa ndoto zote mbili, ndugu zake kumi na mmoja na wazazi wake wanamwinamia, Mwanzo 37:8 inasema ndugu zake walimchukia kwa sababu ya ndoto hizi. Na mstari wa 11 inasema walishikwa na wivu.

Kuangamiza muotaji

Siku ilitimia kwao kudhihirisha hasira yao dhidi ya ndugu yao. Babake anamtuma kwenda kuhakikisha kuwa ndugu zake wako katika hali nzuri. (Mwanzo 37:14). Wanamwona akija na kusema katika mstari wa 19 hadi 20. “Yule mwota ndoto anakuja! Njooni sasa, tumwue na kumtupa katika shimo mojawapo na tuseme kwamba mnyama mkali amemrarua. Kisha tutaona matokeo za ndoto zake.” Reubeni anajaribu kumwokoa Yusufu lakini kujaribu kwake kunafaulu tu kwa kiasi kidogo wakati ndugu zake wanauza Yusufu kama mtumwa kwa msururu wa Waishmaeli waliokuwa wakielekea Misri (Mstari 25). Wanaliweka joho lake lililorembeshwa vizuri, kulichovya katika damu la mnyama, na babake anafikiria kuwa ameraruliwa na mnyama mkali. Ndugu zake wanafikiria kuwa huo ndio mwisho.

Mkono usioonekana imo kazini

Lakini hawatambui yale yanayotukia. Hawatambui mkono wa Mungu usioonekana katika matendo yao. Hawajui kuwa katika jitihada zote za kuangamiza mwota ndoto huyu, wanatimiza ndoto za Yusufu. Kweli, kwa mara ngapi Mungu hufanya kazi sawa na  hii! Anachukua dhambi za waharibifu wenyewe na kuzifanya njia za kukomboa waharibifu.

Potifa, gereza na riziki

Katika nchi ya Misri, Yusufu ananuliwa na Potifa, afisa wa Farao na Mkuu wa ulinzi (Mwanzo 37:36). Hapo Yusufu ananyenyekea katika riziki usioeleweka wa Mungu na anamtumikia Potifa kwa uaminifu.Anainuka kwa uaminifu na umarufu dhidi ya nyumba ya Potifa. Na unaweza kufikiria kuwa watu wa haki wataendelea. Lakini inakaa kinyume. Bibiye Potifa anajaribu kumtongoza Yusufu. Yusufu anahepa uzinifu. Na mwanamke aliyekataliwa anapandwa na mori na kudanganyana juu ya Yusufu. Ijapokuwa ni mwenye haki, anawekwa korokoroni.

Humo korokoroni, tena, bila kufahamu yale Mungu anafanya katika mapito haya yote, anamtumikia tena mhukumu kwa uaminifu na anapatiwa jukumu na kuaminika. Kupitia kwa kufasiri ndoto ya mnyweshaji na mwokaji wa Farao, Yusufu hatimaye anatolewa korokoroni kufasiri mojawapo ya ndoto za Farao. Ufasiri wake unatimia kuwa kweli na hekima yake yasisimua Farao na Yusufu akafanywa kuwa msimamizi wa jumba la kifalme,” Farao asema, “na watu wangu wote watatii amri zako. Ni kuhusu kiti cha ufalme tu nitakuwa mkuu kuliko wewe” (Mwanzo 41:40).

Ndoto zilizotimilika

Miaka saba ya neema ukifuatwa na miaka saba ya njaa yalikuwa juu ya nchi, jinsi Yusufu alivyosema. Yusufu anajiandaa kwa njaa juu ya nchi ya Misri kwa kuhifadhi nafaka nyingi katika miaka saba za neema. Hatimaye, nduguze Yusufu wanasikia kuna nafaka katika nchi ya Misri na wanaenda kutafuta msaada. Mara ya kwanza hawamtambui Yusufu, lakini mwishowe Yusufu anajitambulisha kwao. Alikuwa na umri wa miaka kumi na saba wakati aliuzwa kama mtumwa. (mstari 37:2) na wakati anajitambulisha kwao yuko na umri wa miaka thelathini na tisa (41:46,53; 45:60). Miaka ishirini na mmoja ilikuwa imepita. Wanapatwa na hofu kuu. Walijaribu kumwondosha mwota ndoto na katika hiyo hali ya kumwondosha, walitimiliza ndoto yake. Ndugu wa Yusufu mwishowe wanamwinamia.

Anawaalika kuja kuishi naye katika nchi ya Misiri kuokoa maisha yao, na utimilizo wa utabiri wa jadi kuwa uzao wa Abramu wataishi kama wageni kwa nchi isiyo yao unaanza. Itawezekanaje kuwa watu wa Mungu walijipata Misiri kulingana na mipango yake? Na Mungu anataka kutufundisha nini kuhusu njia zake na za Mwanawe katika kuishi usiotarajiwa katika nchi ya kigeni ya Misri?

Maelezo mawili kutoka kwa Biblia kuhusu utimilizo huu

Jibu la vile watu walijikuta wamejumuika katika nchi ya Misri unajidhihriisha kwa hatua mmoja. Walifika huko kupitia dhambi ya asili ya kujaribu kuua, kuuza kama mtumwa kwa ulafi, na uwongo wa kutofikiria kama ya mzee ambaye ana moyo wa uchungu. Je, Biblia inasemaje kuhusu utabiri huu wa Mungu ulivyotimilika? Kwa njia mbili.

1) Mungu alituma Yusufu kuokoa maisha

Kwanza, katika Mwanzo 45:5, Yusufu anasema kwa ndugu zake wanaomwogopa. “Sasa msihuzunike wala msijichukie wenyewe kwa kuniuza huku, kwa sababu Mungu alinituma niwatangulie ninyi.” Njia ya kwanza Biblia inaeleza juu ya dhambi ya asili ya nduguze ni kuwa ilikuwa njia ya Mungu kumtuma Yusufu nchini Misri ili apate kuokoka maisha ya wale waliojaribu kumua. “Mungu alinituma mbele yenu.”

Tusije tukafikiri kuwa ni neno tu ambalo halina maana, tumesoma yaya haya katika Zaburi 105:16-17—ni kiwango tu ndicho kimepandishwa juu. Mungu hakuwa akitawala tu matendo ya nduguze kupeleka Yusufu katika nchi ya Misri, bali alikuwa akitawala hata njaa pia. “Akaamrisha njaa juu ya nchi na kuharibu chakula chao chote, naye akatuma mtu mbele yao, Yusufu, aliyeuzwa kama mtumwa.” Basi toa mawazoni mwako kuwa Mungu tayari alishaona mbeleni njaa ikizuka kivyake ama ikiwakumba kutoka kwa shetani. Mungu aliamrisha njaa na akatayarisha ukombozi.

2) Kilichoumbwa na mwanadamu kwa ajili ya uovu, Mungu aliumba kwa mema

Njia ya kwanza Biblia inafafanua utimilizo wa utabiri wa Mungu kuwa watu wake watakuja Misri ni kusema Mungu alituma Yusufu mbele yao. Njia ya pili biblia inafafanua utabiri huu ni ya kupenyeza na ya kufagilia. Nduguze Yusufu wanakuja mbele zake tena, wakati huu, baada ya kifo cha babao, na wana uoga kuwa atalipisha kisasi dhidi yao. Katika Mwanzo 50:19-20, Yusufu anasema, “Msiogope. Je, mimi ni badala ya Mungu? Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema ili alitie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya wengi.”

Njia ya pili biblia inaeleza njia ya Mungu kutimiliza utabiri wake ni: Nduguze Yusufu walikusudia kuuzwa kwake kwa uovu lakini Mungu kusudi lake lilikuwa kwa wema. Tazama haisemi kuwa Mungu alitumia uovu wao kwa wema baada yao kuikusudia kuwa uovu, Inasema kwamba katika hicho kitendo chenyewe kiovu, Mungu alikuwa akiunda wema.

Kuelekeza, dhambi zinazookoa maisha

Hiki ndicho tumekiona na tutakiona tena na tena. Kile mwanadamu anakiunda—ama miundo za kishetani—kwa uovu, Mungu anakiunda kwa ajili ya wema wa ajabu. Wema kuu umetajwa katika Mwanzo 45:5 ni “kuhifadhi maisha.” Na wema kuu ambao umetajwa katika Mwanzo 50:20 ni “alikusudia mema ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi.” Lakini katika maneno hayo, hadithi yote ya vile Mungu anaokoa watu wake ni viegemeo vya lengo la dhambi hii—dhambi hii ya kuokoa—kwa utukufu wa Yesu Kristo.

Viegemeo vitatu vya utukufu wa Yesu

Wacha tuyaangalie mambo matatu katika hadithi hii yanayotutayarisha kuona utukufu wa Yesu na vile Yeye alivyo.

1) Wokovu unakuja kupitia dhambi na mateso

Kwanza, tunaona mtindo unaojirudia rudia katika biblia, uitwalo, ushindi wa Mungu unaookoa watu wake mara kwa mara huja kupitia dhambi na mateso. Nduguze Yusufu walitenda dhambi dhidi yake na akateseka kwa ajili yake. Na katika haya yote, Mungu yu kazini kuokoa watu wake—wakiwemo wale wanajaribu kuangamiza mwokozi. Kuja kwa Yesu kwa njia hii haingeshangaza watu wengi vile ilivyofanyika.Kuwa dhambi ilitendeka dhidi yake na  akapitia mateso katika harakati ya kuokoa watu wake ndio inastahili tutarajie kupitia mtindo huu unajirudia rudia.

Katika hadithi ya Yusufu na dhambi asili ya ndugu zake, tutaandaliwa kuona utukufu wa Kristo—Uvumilivu wake na kunyenyekea kwakena kutumika kwake, wakati huu woteakiokoa wale waliokuwa wakijaribu kumwondosha.

Alikufa kwa ajili Yangu, ambaye alisababisha  uchungu wake—kwa ajili yangu ambaye katika kifo nilifuata?Upendo wa ajabu, inawezekanaje kuwa wewe, Mungu wangu, ufe kwa ajili yangu?

2) Yule anateseka ni mwenye haki

Ya pili, hadithi ya Yusufu na dhambi ya asili ya ndugu zake inatuandaa kuona Yesu sio tu kwa sababu ni mtindo wa kawaida  kuwa ushindi wa Mungu unaookoa kwa watu wake kila mara huja kwa mateso na dhambi, lakini katika hali ya kipekee, kwa sababu Yule anateseka na dhambi inatendwa dhidi yake ni mwenye haki sana. Yusufu anajidhihirisha kwa kusimama wima kwake wa ajabu na uaminifu wake katika kila uhusianio. Hata katika utumwa isiyostahili, anakuwa mwaminifu kwa Potifa na msimamizi wa gereza Mwanzo 39:22: “kwa hiyo msimamizi wa gereza akaweka Yusufu awe mkuu wa wafungwa pamoja na kusimamia yote ambayo yalitendeka mle gerezani.”

Na ni nini iilikuwa dhawabu ya Yusufu? Mke wa Potifa alisema uongo juu yake, na Mnyweshaji wa Farao ambaye Yusufu alifasiri ndoto yake, bila shukrani alimsahau akiwa gerezani muda wa miaka mbili baada ya ndoto zake. Jambo la kujifunza kutoka kwa haya matukio sio tu kuwa kuna dhambi na mateso na kuwa Mungu anafanya jitihada ya kuokoa watu wake. Hakika ni kuwa mwenye haki, na wale wanateswa kwa muda mrefu, mwishowe wanaokolewa na Mungu. Ingawa wengine wamemkataa huu jiwe wa haki, Mungu anamfamya jiwe kuu la pembeni (Mathayo 21:420). Kuachiliwa kwake unakuwa njia ile ya kuokoa watesi wake.

Yesu Kristo ndiye mwisho na wa kipekee na Mwenye haki kamilifu. (Matendo 7:52). Ilionekana kwa wengine kana kwamba maisha yake ulikuwa umechukua mwelekeo mbaya na hakika alikuwa mtenda dhambi. Lakini mwishowe, uovu juu yake, na mateso aliyoyavumulia katika haki kamilifu, ikaelekeza kwa ukombozi wake na kwa ajili ya hiyo wokovu wetu. Kama Yusufu ni wa kustajabisha katika kusimama kwake, Yesu ni wa kustajabisha mara elfu kumi, kwa sababu alipitia mateso mara elfu kumi na hakuistahili mara elfu kumi, na alisimama wima kwa ukamilifu na uaminifu, na haki katika haya yote.

3) Fimbo la ufalme halitaondoka kwa Yuda

Kuna mambo sambamba katika hadithi kati ya Yusufu na Yesu, lakini tunaegemea kwa jambo muhimu zaidi katika hadithi hii ya Yesu na si sambamba na ile ya Yusufu. Ni utabiri kuhusu kuja kwa Yesu, ambalo halingefanyika kama wana waovu wa Yakobo wangekufa katika janga hili la njaa. Dhambi ya asili ya hawa ndugu ilikuwa njia ya Mungu ya kuokoa kabila la Yuda kutoweka ili kwamba Simba wa Yuda, Yesu Kristo, akazaliwe, afe, afufuke na kutawala juu ya watu wote wa ulimwengu.

Hapa yanadhihirika katika Mwanzo 49:8-10. Yakobo, baba, anakaribia kufa na kabla ya kuaga, anatamka Baraka uliotabiriwa juu ya wana wake wote. Hivi ndivyio asema kuhusu mwanawe Yuda:

Yuda, ndugu zako watakusifu, mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakusujudia. Ee Yuda, wewe ni mwana Simba, unarudi toka mawindoni, mwanangu. Kama simba humnyemelea na kulala chini, kama simba jike, nani adhubutiye kumwamusha? Fimbo la ufalme haitaondoka kwa Yuda wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake, ambaye miliki ni yake, ambaye utii wa mataifa ni wake.

Hii ni utabiri wa kuja kwa mfalme wa Israeli, Simba wa yuda, mesia. Tazama. katika mstari wa 10 kuwa fimbo ya ufalme—fimbo ya mtawala, mfano wa mfalme—itakuwa katika ukoo wa Yuda mpaka aje mfalme asiye wa kawaida, kwa sababu watu wote, sio tu Israeli, watamtii. Mstari 10b:  “Ambaye utii wa mataifa ni wake.”

Inatimilika katika Yesu. Sikiza vile Yohana anasema kuhusu jukumu la Yesu mbinguni baada ya kusulubishwa na kufufuka kwake: “Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa uzao wa Daudi, ameshinda, ili kwamba aweze kukifungua hicho kitabu na kuvunja hizo lakiri zake saba . . . Nao wakaimba wimbo mpya wakisema “wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri zake, kwa sababu ulichinjwa na kwa damu Yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa. Kumtumikia Mungu wetu, wewe umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani kumtumikia Mungu wetu, nao watamiliki katika dunia” (Ufunuo Wa Yohana 5:5; 9-10).

Simba wa Yuda ndiye kondoo aliyechinjwa

Jambo la kustajabisha sana kulihusu Simba kutoka kabila la Yuda katika utimilizo wa ubashiri wa Yakobo ni kuwa anajidhihirisha katika unyenyekevu wa watu wote ulimwenguni sio kwa hila na kushurutishwa kujisalimisha, lakini kubeba shauku zetu na kutukomboa ili tumpende na kumsifu na kumtii kwa furaha milele. Simba wa Yuda ndiye kondoo aliyechinjwa. Anashindia utiifu wetu kwa kutusamehe dhambi zetu na kufanya utiifu wake, kwa ukamilifu wake kama mwenye haki, msingi wetu wa kukubalika kwa Mungu. Na hakika hali hii ya ulinzi usio kifani na furaha- hii yote ni kupitia mateso yake na haki na kifo na ufufuo—anashindania uhuru na utiifu wetu wa furaha.

Hadithi ya Yusufu ni hadithi ya mwenye haki ambaye ametendewa uovu na anateseka ndipo kabila la Yuda ihifadhiliwe na Simba azaliwe, na atadhihirisha kuwa kama Simba aliye kama kondoo, kupitia kwa mateso yake na kifo chake, kununua na kuhimiza furaha ya kutii katika mataifa yote—hata kwa wale wanaomtia hata kifoni.

Je ana chako?