Kwa nini mahubiri ya ufafanuzi inamtukuza Mungu hasa

Kuna sehemu nne wa ujumbe huu. Kwanza nitatafakari juu ya aina ya mahubiri ambaye natumahi kuona Mungu akiinua wakati huu—aina ambayo umeumbwa kwa uzito wa utukufu wa Mungu. Pili, nitajaribu kuonyesha utukufu wa Mungu, ambayo huakikisha kuhubiri kwa njia hii. Tatu, nitatoa ufahamu wangu wa bibilia jinsi watu huamkia kwa utukufu huu na jinsi wanavyobadilishwa kuipitia. Hatimaye, nitaeleza jinsi hayo yote hutoa mwito kwa aina ya mahubiri ninayoita ufafanuzi wa shangwe.

Tafakari juu ya aina ya mahubiri iliyotolewa na uzito wa utukufu wa Mungu

George Whitefield aliamini katika kuhubiri na alitoa maisha yake kwa hiyo. Kwa mahubiri aina hii Mungu alifanya kazi kuu yawokovu kwa pande zote za Atlantiki. Mwandishi wa habari ya maisha yake, Arnold Dallimore, alitunga matokeo ya kushangaza na ambazo mahubiri ya Whitefield yaliweza kutekeleza nchini Uingereza na Marekani katika karne ya kumi na nane. Ilikuja kama mvua juu ya nchi kavu na kufanya jangwa kuinuka na maua ya haki. Dallimore aliinua mayo yake katika nyika yaliogeuzwa katika nyakati za Whitefield na kudhihirisha hamu yake kuwa Mungu atafanya hivyo tena. Maneno yake yananisaidia kueleza yale ninayotamani katika vizazi zijazo vya wahubiri nchini Marekani na katika dunia kote. Alisema,

Naam . . . kwamba tutaona mkuu mkubwa wa Kanisa mara nyingine tena . . . akiinua kwake vijana Fulani ambao atawatumia katika huu jukumu wenye utukufu. Na hao watakuwa watu wa aina gani? Mashujaa katika maandiko, ambao maisha yao yanaongozwa na hisia ya ukuu, utukufu na utakatifu wa Mungu, na akili zao na mioyo zinan’gaa kwa ukweli mkubwa wa mafundisho ya neema. Nao watakuwa watu ambao wamejifunza nini maana ya kufa kwa ubinafsi, kwa malengo ya binadamu na matarajio ya binafsi; watu ambao wako tayari kuwa ‘wapumbavu kwa ajili ya Kristo’, ambao watabeba [na kuvumilia] lawama na uwongo, ambao watafanya kazi na kuteseka, ambao hamu yao kuu itakuwa, si kwa ajili ya kupata sifa za dunia, lakini kushinda kibali ya Bwana wakati watakapojitokeza mbele ya kiti cha hukumu ambayo inatisha. Watakuwa watu ambao wanahubiri kwa mioyo iliyovunjika na macho yalijawa na machozi, na mbao katika huduma wao Mungu atatoa mwagiko wa ajabu wa Rogo Mtakatifu, na ambao watashudia ‘ishara na maajabu zikifuata’ katika ubadilishwaji wa umati wa maisha ya binadamu.1

Hodari katika maandiko, kun’gaa katika ukweli mkubwa wa mafundisho wa neema, kifo kwa ubinafsi, ambao wana nia ya kufanya kazi na hata kuteseka, wasiopenda heshima za binadamu, kuvunjika kwa ajili ya dhambi, na kuongozwa kwa hisia za ukuu, na uwezo mkuu, na utakatifu wa Mungu. Dallimore, kama Whitefield, aliamini kwamba kuhubiri ni kueneza neon la Mungu kupitia katika moyo wa aina hiyo. Kuhubiri sio mazungumzo. Kuhubiri sio mjadala. Kuhubiri sio majadiliano wa kawaida kuhusu mambo ya dini. Kuhubiri sio tu kufundisha. Kuhubiri ni uenezo wa ujumbe iliyopenywa na hisia ya ukuu na utukufu na utakatifu wa Mungu. Mada inaweza kuwa chochote chini ya jua, lakini daima inaletwa katika mwanga mkali wa ukuu wa Mungu na utukufu wa neon lake. Hivyo ndivyo Whitefield alivyohubiri.

Katika karne iliyopita hakuna aliyekuwa na mtazamo huo bora kuliko Martin Lloyd-Jones, ambaye alihudumu katika Chapel ya Westminster kule London kwa miaka 30. Wakati J.I. Packer alipokuwa mwanafunzi mwenye miaka ishirini—na—miwili, alimsikia Lloyd-Jones akihubiri kila jioni ya Jumapili katika London wakati wa mwaka wa shule wa 1948-1949. Alisema kwamba “kamwe hakuwa amewahi sikia mahubiri kama hayo.” (Hiyo ndio maana watu wengi husema mambo mengi yanayokanusha na wenye ujinga mwingi kuhusu kuhubiri—maanake hawajawahi sikia mahubiri ya ukweli. Hawana msingi wa kufanya uamuzi kuhusu umuhimu wa mahubiri ya ukweli) Packer alisema ilikuja kwake “kwa nguvu ya mshtuko wa umeme, ikileta . . . zaidi ya hisia ya Mungu kulik mtu mwingne yeyote” aliyekuwa amejua.2 Hiyo ndio Whitefield alimaanisha. Oh, kwamba Mungu atainua wahubiri wachanga ambao watawaacha wasikilizaji wao na hisia ya mshtuko wa kiroho kwa kuhisi Mungu—kiasi cha hisia wa uzito wa ukweli wa Mungu usiopimika.

Hiyo ndiyo hamu yangu kwa siku zetu—na kwenu pia. Kwamba Mungu atainua maelfu ya mahubiri waliovunjika moyo, walioloweka na bibilia na utakatifu wa Mungu, uliofunuliwa katika injili ya Kristo aliyesulubiwa na kufufuka na anatawala kwa mamlaka kamili juu ya kila taifa na kila jeshi na kila dini na kila gaidi na kila tsunami na kila kiini cha saratani, na kila 'galaxy' katika ulimwengu.

Mungu hakuagiza msalaba wa Kristo au kuunda ziwa la moto3 ili kuwasilisha udhaifu wa kumwasi utukufu wake. Mauti wa Mwana wa Mungu na hukumu wa wale wasiotubu ndio sauti kubwa zaidi chini ya mbingu kwamba Mungu ni takatifu, na dhambi ina vikwaso mengi, na gadhabu ni haki, na neema ni ya thamani kubwa, na maisha yetu fupi—na maisha ya kila mtu katika kanisa au jamii yako—inaelekeza katika furaha ya milele au mateso ya milele. Ikiwa mahubiri yetu hayabebi uzito wa mambo hayo kwa watu wetu, ni nini itazibeba? Veggie tales? Redio? Televisheni? Vikundi vya majadiliano? Mazungumzo yanayoibuka?

Mungu alipanga kusulubishwa kwa Mwana wake (Ufunuo 13:8; 2 Timotheo 1:9) na jehanamu kuwa mbaya (Matayo 25:41) ili kwamba tuwe na ushahidi wazi uwezekanavyo ya yaliyo hatarini tunapo hubiri. Kinachopatia mahubiri uzito wake ni kwamba vazi ya mhubiri imeloweka katika damu ya Yesu na kutoteketezwa na moto wa Jehanamu. Huo ndio joho ambao hubalisha waongeaji kuwa wahubiri. Hata hivyo inasikitisha kwamba baadhi ya sauti ya wainjilisti maarufu wa wakati huu hupunguza hofu wa msalaba na hofu wa Jehanamu—mojawapo ambao umeviliwa uwezo wake wa kubeba adhabu yetu, na wengine hudanganywa katika mambo maovu na taabu za kijamii katika dunia hii.4

Oh kwamba vizazi vijavyo viweze kuona kwamba dunia haujapitwa na hisia za uzito kuhusu Mungu. Hakuna mfuririko wa hali ya utukufu wa Mungu kanisani. Hakuna ziada ya bidii kanisani kuhusu bingu, na jehanamu, na dhambi na wokovy. Hivyo basi furaha ya wakristo wengi una wembamba wa karatasi.

Mamilioni ya watu wanajifurahisha hadi kifo kupitia DVD, televisheni wenye skirini wa inchi 107, na michezo katika simu za rununu, na ibada wenye umbo wa michezo wa kuigiza, wakati wasemaji wa dini kubwa duniani wanaandika mabarua Magharibi katika machapisho makuu wakisema, “Jambo la kwanza tunalowaitia ni Uislamu . . . ndio dini ya kuunganisha mema na kupiga marufuku maovu kwa mkono, ulimi na moyo. Ni dini ya jihadi katika njia za Allah, ili Neno la Allah na dini utawale zaidi.” 5Na kisha wasemaji hao huwabariki hadharani walipuaji wa kujiua ambao hulipua watoto mbele ya maduka ya Falafel na kuiita njia ya paradise. Hiyo ndiyo dunia ambayo tunahubiri ndani yake.

Na bado, kwa njia isiyoeleweka, katika huu enzi wa udunishaji wa Kristo, uharibifu wa mioyo, vitabu na semina na shule za uungu na wataalamu wa ukuaji wa kanisa wanazidi kuambia wachungaji wachanga, “jifurahishe.” “Chekesha watu.” “furahisha watu.” Kwa hayo ninauliza, Wapi roho ya Yesu? “Mtu ye yote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe na auchukue msalaba wake, anifuate. Kwa maana ye yote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata” (Matayo 16:24-25). “Jicho lako la kuume likikufanya utende dhambi, ling'oe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jehanam” (Matayo 5:29). “Vivyo hivyo, ye yote miongoni mwenu ambaye hawezi kuacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi Wangu” (Luka 14:33). “Mtu ye yote anayekuja kwangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto, ndugu zake na dada zake, naam, hata maisha yake mwenyewe” (Luka 14:26). “Nifuate, nawe waache wafu wazike wafu wao.” (Matayo 8:22). “Na ye yote anayetaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa mtumwa wa wote” (Mariko 10:44). “Mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanam” (Matayo 10:28). “Mtasalitiwa hata na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki na baadhi yenu watawaua. Mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu. Lakini hapatakuwa na unywele mmoja wa kichwa chenu utakaoangamia. Kwa kuvumilia mtaokoa roho zenu” (Luka 21:16-19).

Je shauri kwa Yesu kuhusu ukuaji wa kanisa inaweza kuwa, “jifurahishe, Yesu. Fanya mambo yenye vichekesho.” Na kwako wewe mchungaji mchanga: “Lolote ufanyalo, usiwe kama Yesu wa Injili. Jifurahishe.” Kwa mtazamo wangu, ambao unajiskia kuwa karibu na milele siku hizi, ujumbe huo kwa wachungaji inazidi kuonekana kama wazimu.

Dhihirisho wa utukufu wa Mungu

Unachoamini juu ya umuhimu wa kuhubiri na asili ya kuhubiri unaongozwa na hisia wako kuhusu ukuu na utukufu wa Mungu na unachoamini kuhusu jinsi watu huamshwa kwa huo utukufu na kuiishia huo utukufu. Hivyo sehemu inayofuata inatoa igizo ya utukufu wa Mungu, na wa tatu utashughulikia jinsi watu huamkia utukufu huo na kabadilishwa nayo.

Kuanzia mwanzo hadi mwisho hakuna chochote katika Biblia ambayo imo katika mawazo na moyo wa Mungu kuliko utukufu wa Mungu—uzuri wa Mungu, mng’ao mbalimbali wa ukamilifu wake. Kwa kila hatua katika matendo ya Mungu uliofunuliwa, popote anapobainisha kwa wazi lengo lake kuu wa tendo huo, lengo huo huwa sawa: kuzingatia na kuonyesha utukufu wake.

  • Alituteua awali kwa ajili ya utukufu wake (Waefeso 1:6).

  • Alituumba kwa ajili ya utukufu wake (Isaya 43:7).

  • Alichagua Israeli kwa ajili ya utukufu wake (Yeremia 13:11).

  • Aliwaokoa watu wake kutoka Misri kwa ajili ya utukufu wake (Zaburi 106:8).

  • Aliwaokoa kutoka uhamishoni kwa ajili ya utukufu wake (Isaya 48:9-11).

  • Alimtuma Kristo ulimwenguni, ili watu wa mataifa mengine wangemsifu Mungu kwa ajili ya utukufu wake (Warumi 15:9).

  • Anaamuru watu wake, wawe wanakunywa au kula, kufanya mambo yote kwa ajili ya utukufu wake (1 Corinthians 10:31).

  • Atamtuma Yesu mara ya pili ili kwamba wote waliokombolewa watastaajabishwa na utukufu wake (2 Wathesalonika 1:9-10).

Hivyo basi utume wa kanisa ni: “Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote" (Zaburi 96:3).

Haya na maeneo mengine zaidi ya mia hutuelekeza hadi ukingoni mwa utii kwa Mungu. Hakuna chochote kinachoathiri kuhubiri kwa undani kuliko karibu kuwa bubu—karibu —kwa shauku ya Mungu kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Ilioko wazi katika uzima wa ufunuo mbalimbali wa biblia ni kwamba hatimaye utii wa Mungu ni kujijua mwenyewe kikamilifu, na kujipenda mwenyewe bila kikomo, na kushirikishana uzoefu huu, jinsi inavyowezekana, pamoja na watu wake. Juu ya kila tendo la Mungu kunapepea bendera huu: “Kwa ajili yangu mwenyewe, kwa ajili yangu mwenyewe, nafanya hili. Kwa jinsi gani niliache jina langu lichafuliwe? Sitautoa utukufu wangu kwa mwingine" (Isaya 48:11; cf. 42:8).

Tangu milele yote, Mungu aishie milele, ambaye kamwe hakuwi, na ambaye daima ni kamilifu, amejijua na kupenda kile ambacho ajuayo. Milele ameuona uzuri wake na kuonja yale aonayo. Kuelewa kwake kwa kuwepo kwake ni kamili na uchangamfu wake katika kufurahia haina kipimo. Yeye hana mahitaji, maanake hana dosari. Hana upendeleo kwa maovu kwa sababu hana upungufu ambao unaweza kumletea jaribio la kutenda uovu. Yeye basi ni umbe kilicho takatifu sana na chenye furaha zaidi ambayo inaweza kufikiriwa. Hatuwezi fahamu juu ya furaha ulio kuu kuliko furaha ya uweza usiokoma unaofurahisha bila kikomo katika uzuri wa ushirika wa kibinafsi ya utatu.

Kushiriki katika hali hii—hali ya kufahamu na kufurahia utukufu wake—ndiyo sababu Mungu aliuumba dunia. Atatufanya tumjue na kumfurahia jinsi alivyojijua na vile anavyojifurahia. Kwa kweli lengo lake ni kuwa huo ufahamu aliyo nayo kwaye na furaha aliyo nayo ndani mwake itakuwa ufahamu wetu na furaha yetu, ndipo tumjue kwa ufahamu wake na tumfurahie katika furaha yake. Hii ndio maana kamili ya ombi la Yesu katika Yohana 17:26 pahali anamuuliza Babake “ili upendo ule unaonipenda Mimi uwe ndani yao na Mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.” Ufahamu wa Baba na furaha katika mng’ao wa utukufu wa Mwana—ambaye Jina Lake na Yesu Kristo (Waebrania 1:3)—atakuwa ndani yetu kwa sababu Yesu yu ndani mwetu.

Na ukiuliza, Mungu anapanga kushiriki aje hali hii (ya kujifahamu na kujifurahisha), linganisha na *upendo *wa Mungu, jibu ni: Lengo lake la kushiriki tukio hilo ni upendo Wake. Upendo wa Mungu ni juhudi yake ya kushiriki ufahamu na furaha ya utukufu wake pamoja nasi. Yohana anaposema Mungu ni upendo (Yohana 4:8, 16), anamaanisha kuwa ni umbile wa Mungu kushiriki furaha ya utukufu wake, hata kama inamgharimu uhai wa Mwanawe.

Hii inamaanisha kwamba kusudio la Mungu kuonyesha utukufu wake na furaha yetu katika utukufu huo yanaambatana. Huwezi kumcha kabisa kile ambacho hukifurahii. Mungu hatukuzwi kwa yote kwa kujulikana tu; anatukuzwa kwa kujulikana na kufurahiwa kwa undani sana mpaka maisha yetu inakuwa onyesho la thamani yake.

Yesu alisema vitu viwili ili kisisitiza jukumu lake katika kutupatia ufahamu na furaha ya Mungu. Alisema “Hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anampenda kumdhihirishia Baba kwake” (Mathayo 11:27). Na akasema, “Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili” (Yohana 15:11) kwa maneno mengine tunamjua Baba kupitia ufahamu wa Mwana, na tunafurahia Baba kupitia furaha ya Mwana. Yesu alitufanya washiriki wa ufahamu na furaha wake kwa Mungu.

Njia hii inadhihirika katika dunia si tu sana kupitia matendo ya ukakamavu ya ibada ya kijumla ya Jumapili asubuhi—vile nyakati hizo ni za thamani—lakini kupitia mabadiliko zinazoleta maishani mwetu. Yesu alisema, “Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele za wa watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (Mathayo 5:16). Nuru inaoangaza kupitia matendo yetu na kufanya watu kumwona Mungu wala si sisi, ndiyo thamani itosheleshayo ya utukufu wake.

Inafanya kama hii: Wakati utukufu wa Mungu ni hazina ya maisha yetu, hatutahifadhi hazina katika dunia, lakini kuzitumia kwa kueneza utukufu wake. Hatutakuwa na tamaa, lakini kutiririshwa na uhuru. Hatutatamani sifa za wanadamu, bali kujisahau tukimsifu Mungu. Hatutashikwa na uzuri wa kihisia yenye dhambi, lakini kung’oa mizizi yao kwa nguvu ya ahadi ishindayo yote. Hatutauguza tamaa iliyo na vidonda ama kushiriki kinyongo ama kuwa na roho ya kulipiza kisasi, bali tutayaachilia yote kwa Mungu na kubariki wote wanaotuchukia. Dhambi yoyote inatiririka kutoka kwa kukosa kuuthamini utukufu wa Mungu juu ya vyote. Basi njia mojawapo muhimu na inayoonekana ya kuonyesha ukweli na thamani ya utukufu wa Mungu ni kupitia maisha ya unyenyekevu na kujikana ya huduma inayotiririka tu kutoka kwa kidimbwi cha utukufu wa Mungu unaotoshelesha yote.

Jinsi watu wanavyoinukia utukufu huu na kubadilishwa nayo

Tunageukia sasa kwa swali la vile watu wanainukia katika utukufu wa Mungu na kubadilishwa nao. Pande mmoja muhimu la jibu limepeanwa na mtume Paulo katika 2 Wakorintho 3:18-4:6. Anasema, “Nasi sote, tukiwa na nyuso zilizotiwa utaji tunaakisi utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.” Tukiakisi utukufu wa Bwana, tunabadilishwa toka utukufu hadi utukufu. Hii ni njia ya Mungu ya kubadilisha watu katika mfano wa Mwanawe ndipo wang’ae nuru ya utukufu wa Bwana. Kubadilishwa katika njia inayotukuza Mungu, tunaweka macho yetu kwa utukufu wa Bwana.6

Hii inafanyika kwa njia gani? (Na hapa tunasogea karibu kwa athari za mahubiri). Paulo anaeleza katika 2 Wakorintho 4:3-4 vile tunaakisi utukufu wa Bwana.

Na hata kama Injili yetu imefunikwa, inafunikwa tu kwa wale wanaoangamia. Katika hali yao mungu wa ulimwengu huu amepofusha fikira za wasioamini, ili kuwazuia kuona [hapa ni timilizo ya 2 Wakorintho 3:18] nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano wa Mungu.

Tunaakisi utukufu wa Bwana kwa uwazi zaidi na kwa umuhimu kuu katika Injili. Kwa wingi mpaka Paulo anaiita “Injili ya utukufu wa Kristo.” Ambayo inamaanisha—ni hii ina athari kubwa kwa mahubiri—kuwa katika hali hii, hatuwezi kuona utukufu wa Bwana moja kwa moja kama vile tutauona wakati atakaporudi mawinguni, tutauona kwa wazi sana kwa njia ya Neno Lake. Kuwa Injili ni ujumbe kwa maneno. Kwa kawaida, maneno husikizwa na utukufu huonekana. Hivyo basi Paulo anasema kwamba tunaona utukufu wa Kristo si mara mingi kupitia macho yetu bali kupitia masikio yetu. “Imani yaja kwa kusikia na kwa kusikia tu neno la Kristo” (Warumi 10:17), kwa sababu kuona utukufu wa Kristo huja tu kwa kusikia na kusikia tu Injili ya Kristo.

Tafakari vile hii ilidhihirishwa katika maisha ya nabii Samueli. Wakati wa Samueli hapakuwa na maono nyingi ya bwana (1 Samueli 3:1)—vile tu sasa wakati ambapo kuna ukame wa kuona na kutamani utukufu wa Mungu. Lakini Mungu alimwinua nabii mpya. Na Mungu alijitokeza kwake kwa njia ipi? Vile atakavyojitokeza kwako na kwa watu wako. 1 Samueli 3:21, “Bwana akaenmdelea kutokea huko Shilo na huko kujidhirisha kwa Samueli kwa njia ya neno lake.” Alijidhihirisha kwa njia ya neno. Hivi ndivyo watu wetu wataakisi utukufu wa Bwana, na kubadilishwa kama aina ya watu wanaofanya utukufu wake kujulikana. Na Paulo anatuambia sasa kuwa neno ambalo ladhihirisha utukufu wa Mungu kwwa uwazi zaidi na kwa kina ni Injili (2 Wakorintho 4:4).

Mwito wa dharura wa hitapo la kudhihirisha

Hii hatimaye inanileta kwa hoja ya kutamatisha juu ya mahubiri kama hitapo la kudhihirisha. Kama ni kusudio la Mungu kuwa tudhihirishe utukufu wake kwa ulimwengu, na tukiudhihirisha kwa sababu tumebadilishwa kwa kujua na kuufurahia kwa kuuakisi utukufu wa bwana, na tukiuakisi huo utukufu kwa uwazi na kwa kina katika Injili ya utukufu wa Kristo, na kama Injili ni ujumbe uliopelekwa kwa njia ya maneno kwa ulimwengu, basi kile kinachofuata ni kuwa Mungu anakusudia ili wahubiri wafunue maneno haya na kuyatukuza—ndicho ninachokiita hitapo la kudhihirisha.

Maneno yote yana umuhimu. Ni ya kudhihirisha kwa sababu kuna mengi katika Injili yanayohitaji kudhihirishwa (kufunguliwa, kufunuliwa, kufanywa wazi, kufafanuliwa, kuelezwa, kuonyeshwa). Tutaona hii tunapoangazia pande tano muhimu ya ujumbe wa Injili.

  • Injili ni ujumbe kuhusu matukio ya kihistoria: maisha na kifo na kufufuka kwa Kristo—unatuamrisha kuyafungua kwa dhihirisho sahihi ya maandiko.

  • Injili ni ujumbe kuhusu matukio hayo yaliyoafikiwa kabla tuhisi chochote ama hata kuwa: ukamilifu wa utiifu kamili, malipo ya dhambi zetu, kutolewa kwa ghadhabu ya Mungu, kuitwa kwa Yesu kama Masiya na mfalme wa Mbingu na nchi aliyesulubishwa na kufufuka, kuwanyang’anya silaha watawala na mamlaka yote, kuharibu kifo—haya yote yanatuamrisha kuyafungua kwa dhihirisho sahihi ya maandiko.

  • Injili ni ujmbe kuhusu kutoa haya mapokezi kutoka kwa Kristo hadi kwa watu fulani kupitia muungano wetu na Kristo kupitia imani pekee mbali na kazi—ambayo inatuamrisha kufungulia watu wetu umbile na njia za imani kwa dhihirisho sahihi ya maandiko kadha.

  • Injili ni ujumbe kuhusu vitu vyema ambavyo sasa ni kweli kutuhusu kama vile mapokeo ya msalaba yanatumika kwetu kupitia Kristo: kuwa Mungu anatuneemesha tu sasa badala ya kuwa mwenye ghadhabu, ndiyo maana tunahesabiwa haki katika Kristo sasa, tumewekwa huru kutokana na maovu na nguvu za dhambi (kukombolewa), kwa kuwekwa kwa nafasi, na kwa hatua tumefanywa takatifu (kutakaswa)—yote yanatuamrisha tuufungue hakika hizi tukufu kwa watu wiki baada ya wiki kwa dhihirisho sahihi ya maandiko kadha wa kadha.

  • Na ya mwisho Injili ni ujumbe kuhusu Mungu mwenye utukufu mwenyewe kama ya mwisho, milele, hazina itosheleshayo yote. “Tuna . . .fyurahi katika Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa kupitia kwake tumepata upatanisho” (Warumi 5:11). Injili tunaohubiri ni “injili ya utukufu wa Kristo ambaye ni mfano wa Mungu”. Injili yetu isipofikia lengo hili—kumfurahia Mungu mwenyewe, si tu thawabu zake za msamaha na kuokolewa kutoka jehanamu na uzima wa milele—basi hatuhubiri “Injili ya utukufu wa Mungu usoni mwa Kristo” (2 Wakorintho 4:6). Lengo letu kuu ni kujua na kumfurahia Mungu. Vile tulivyoona mwanzoni mwa sura hii, hiyo ndiyo sababu tuliumbwa—kuwa Mungu atashiriki nasi ufahamu na kufurahi kwake mwenyewe. Hii ndiyo inamaanisha kwake kutupenda. Huu ndio msalaba ulitimiliza kwa ajili yetu. Na hii pia, kutoka kwa kila neno la andiko—yote yametiwa nguvu na Mungu ili iamshe tumaini katika utukufu wake7—lahitaji dhihirisho lenye rotuba ndipo watu wetu wakalishwe vyakula vizuri zaidi na vya juu zaidi vya mbingu.

Ufafnuzi wa maandiko ni muhimu kwa sababu injili ni ujumbe ujao kwetu kwa maneno na Mungu ameteua kwamba watu wauone utukufu wa Kristo—utajiri usiopimika wa Kristo (Waefeso 3:8)—katika maneno hayo ya Injili. Huu ni mwito wetu: kuyafungua maneno na sentensi na aya ya andiko na kuonyesha “utukufu wa Kristo ambaye ni mfano wa Mungu.”

Ambayo inatuelekeza hatimaye hadi kwa neno la pili katika tamshi ufafanuzi wa kujitapa. Ole wetu tunapofanya dhihirisho yetu ya Injili kama hii bila hitapo—ni kusema, bila kusherekea juu ya ukweli tuufunuao. Paulo anaposema katika 2 Wakorintho 4:5, “Kwa maana hatujihubirii sisi wenyewe ila tunamhubiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana.” Neno ambalo analitumia kwa “kutangaza” ni kerussomen—tunamhubiri Kristo kuwa ni Bwana, tunamtangaza Kristo kuwa ni Bwana. Mhubiri—mtangazaji, “mhubiri” (1 Timotheo 2:7); 2 Timotheo 1:11)—itapaswa kueleza yale anayoyasema watu wasipoelewa (mafundisho yaweza kuhitajika). Yanayotenganisha mhubiri kando na mwanafalsafa, na mwandishi na mwalimu ni kuwa yeye ni mtangazaji wa habari—na katika hali yetu, habari njema zizisokoma. Habari zenye thamani zisizokoma. Habari kuu zaidi kuliko zote ulimwenguni.

Muumba wa mbingu na nchi, ambaye ni mtukufu sana na wa kutamaniwa sana kuliko hazina yoyote ulimwenguni, amejidhihirisha kupitia Yesu Kristo ili ajulikane na kufurahiwa milele na mtu yeyote ulimwenguni ambaye ataweka chini silaha za uasi, na kupokea msamaha wake ulionunuliwa kwa damu, na kukumbatia Mwanawe kama Mwokozi, Bwana na hazina ya maisha yao.

Ewe ndugu, usidanganye juu ya thamani ya Injili kwa uhayawani/ubutu wa mwenendo wako. Ufafanuzi wa utukufu hakika zaidi ni hakika tukufu. Ikiwa si ufafanuzi wa kujitapa—halisi litokalo moyoni—uwongo unasemwa kuhusu thamani ya Injili. Usiseme kwa uso wako ama kwa sauti yako ama kwa maisha yako kuwa Injili si Injili ya utukufu wa Kristo utosheleshayo yote. Na Mungu na akawainue kati yenu vizazi vya wahubiri ambao ufafanuzi wao ina thamani ya ukweli wa Mungu na ambao hitapo lao linafaa utukufu wa Mungu.


1 Arnold Dallimore,George Whitefield, Vol. 1 (London: Banner of Truth Trust, 1970), p. 16.

2 Christopher Catherwood, Five Evangelical Leaders(Wheaton: Harold Shaw Publishers, 1985), p. 170.

3 Yesu alisema katika Luka 22:22 kwamba msalaba u”uliamuliwa” [horismenon] na Mungu,” na katika Mathayo 25:41 kwamba mioto za jehanamu vilitayarishwa na Mungu. “Kisha atawaambia wale walio upande Wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ilioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake.’”

4 Kutoka eneo Marekani zingatia maoni ya kusisimua ya Joel Green ambayo inapuuza yale ambayo kanisa imeaamini kuwa ni kiini cha injili na imedhubutiwa wazi katika maandiko (Isaya 53:4-6, 8-10; Wagalatia 3:13; Warumi 8:3): “Chochote kinachomaanishwa na upatanisho, itakuwa kosa kubwa kufikiri kwamba inalenga kutuliza hasira ya Mungu au kushindia tahadhari ya huruma ya Mungu. . . . Maandiko kwa ujumla hautoi msingi wa picha ya Mungu mwenye hasira anayehitaji shiba katika dhabihu ya upatanisho . . .. Chochote uwezayo kusemwa kuhusu jinsi Paulo aelewavyo kifo cha Kristo, theolojia yake kuhusu msalaba haina kamwe maana yeyote ya uendeleshaji wa adhabu ya Mungu.” Joel Green, Recovering the Scandal of the Cross: Atonement in New Testament & Contemporary Context (Downers Grove: Intervarsity Pres, 2000), pp. 51, 56. Kutoka eneo la Uingereza Steve Chalke anaita mafunzo ya kuwa Kristo aliubeba gadhabu ya Mungu kwa ajili yetu “unyanyasaji wa kiulimwengu wa mtoto”: Ukweli ni kwamba msalaba si aina ya unyanyasaji wa kiulimwnefu wa watoto—Baba anayelipa kisasi, kwa kumadhiby Mwanawe kwa kosa ambayo hajatenda. Hakika, watu nje na ndani ya kanisa wamegundua huu toleo la tukio uliosongwa kuwa yenye kimaadili ya kutatanisha na pia kikwazo kikubwa kwa imani. Ndani zaidi, hata hivyo, ni kwamba dhana hiyo inasimama kinyume na taarifa kuwa ‘Mungu ni upendo’. Ikiwa msalaba ni kitendo binafsi ya unyanyasaji unaofanywa na Mungu kwa binadamu lakini kubebwa na Mwanawe, basi inafanya kejeli kwa mafundisho ya Yesu mwenyewe kuwapenda adui zenu na kukataa kulipa maovu kwa uovu. The Lost Message of Jesus (Grand Rapids: Zondervan Publishing Company, 2004), pp. 182-183. N.T. Wright anasema kuwa “wingi” (je anaaanisha “wote”?) wa kumbukumbu wa kuzimu katika Agano Jipya hayazungumzi kuhusu pahali pa mateso ya milele katika hali ya ufahamu, lakini kwamba tunahitaji a’ujenzi” au “marudio” ya mafundisho ya kuzimu “katika nyakati za kisasa” 1) Kwa upande wa binadamu kwa kutumia “zawadi yao ya uhuru” “kuharibu uutu wao kabisa,” na 2) katika suala la haki ya kijamii na taabu: “Kuna swala jingine sahihi na ambaye pia ni muhimu zaidi kuhusu mafundisho ya kuzini katika biblia kwa suala la maisha ya binadamu ya kijamii maisha ya kijami ya mashirika katika dunia hii. Following Jesus: Biblical Reflections on Discipleship (Grand Rapids: William B. Eerdmans Publishing Company, 1994), pp. 95-96.

5 Quoted from The Islam/West Debate: Documents from a Global Debate on Terrorism, U. S. Policy and the Middle East, edited by David Blankenhorn in First Things, March 2006, #161, p. 71.

6 Jihadhari katika kusema: “Haifanyi” na kisha kugeukia mbinu nyingine na kuwacha nyuma njia ya Mungu ya kubadilisha watu. Unaweza kuwa na uwezo wa kubadilisha watu kwa njia na mbinu tofauti na utaratibu huu wa kuona utukufu wa Bwana katika ujumbe wa Mungu, lakini, je itakuwa mabadiliko ambayo inatukuza utukufu wa Kristo? Si kwamba mabadiliko yote yanamuheshimu Kristo. Paulo anaonya kwa maneno yaliomo katika 2 Wakorintho 4:3, “Hata nayo Injili yetu kama imetiwa utaji, ni kwa wale tu wanaopotea.” Kwa maneno mengine anakubali kwamba injili yake halibadili kila mtu. “Wa “kuangamia” hawaoni utukufu wa Mungu katika injili. Paulo habadilishi mbinu yake kwa sababu huo. Nasi pia hatufai.

7 2 Timotheo 3:16-17; Warumi 15:4.