Ari ya ukuu wa Mungu, sehemu ya 2

Mungu ni Mungu mwenye ubinafsi wake

Jana, katika jaribio la kuchoma jiwe la barafu na kueneza ari ya ukuu wa mungu katika vitu vyote, kwa furaha ya watu wote, nilijaribu kusema kuwa  mungu afanya yote afanyalo kwa sababu ya utukufu wa jina lake. Mungu  amtukuza Mungu. Moyo ulio na ari zaidi ulimwenguni kote kwa  ajili ya mungu ni moyo wa mungu. Hiyo ndio ulikuwa jambo muhimu. Ari ’97, ninavyo u elewa, ni kuhusu ari ya Mungu kumhusu Mungu. Yote afanyalo, kuanzia uumbaji mpaka kuufanya kamilifu anaufanya  kwa nia ya kuuonyesha na kuinua utukufu wa jina lake.

Ubinafsi wa Mungu sio kutokuwa na Upendo

Jambo muhimu ya pili kutoka jana lilikuwa kwamba, hii sio kukosa upendo. Sababu sio kukosa upendo ili Mungu ajitukuze kwa njia hii, Kwa sababu kumjua Mungu na kumezwa ndani ya sifa zake ndio inatosheleza moyo wa binadamu. “Utanijulisha njia ya uzima; mbale ya uso wako ziko furaha tele; Na klatika mkono wako wa kiume mna mema ya milele.” (Zaburi 16:11) Kwa hivyo ikiwa Mungu anajitukuza mwenyewe . . . Kiwango cha sisi kumwona jinsi alivyo . . .. Inatutosheleza nafsi, Basi Mungu tu ndie kiumbe ulimwenguni kote ambapo kujitukuza kwake ndio kiwango kikuu cha utu na msingi wa upendo.

Huenda hautamiigaa kwa hili. Hadi kiwango cha kujitukuza mwenyewe ili mtu mwengine afurahie. Hio itakuwa ni chuki . . .. Wala sio upendo . . .. Kwa sababu unapotosha mawazo yao kutoka kwa yule anayeweza kutosheleza nafsi zao. Basi huenda hatuta iga Mungu katika uungu wake. Mungu tu ndie kiumbe cha kipekee zaidi ulimwenguni kote mwenye kujitukuza ndio msingi wake wa upendo. Ni lazima iwe hivyo ikiwa yeye ni Mungu

Huenda tukamhitaji apende jinsi mwanadamu anavyo penda kwa kuwafanya wengine kuwa muhimu; Lakini hawezi fanya hivyo na awe Mungu. Yeye ni wa thamani milele ndani yake. Hakuna mwingine  kando yake. Kwa hivyo yeye yupo—kuiweka wazi—amebaki nautukufu, awezae yote, na mwenye yote, bila kukuhitaji wewe kwavyovyote ile. Kwa ukweli: Kwa mtukufu zaidi na mkuu zaidi na anyetutosheleza zaidi na anyejitosheleza bila kukuhitaji kwavyovyote vile. Hii ndio msingi wa neema. Ukijaribu kujiweka katikati ya neema basi haiwi neema tena. Neema ya Ubinafsi wa Mungu ni Neema ya kibibilia.

Furaha yangu sio kwa Mungu kunifanya niwe muhimu ulimwenguni. Furaha yagu ni kwa Mungu kuwa muhimu ulimwenguni milele na kunichukua katika ushirika wake, ili nimwone, nimjue, nimfurahie, nimthamini, nitosheleke ndani yake, milele na milele.

Hayo yalikuwa ujumbe wa jana.

Kidokezo cha ubinafsi wa Mungu kwa mwanadamu

Sasa leo . . . ikiwa yale nishasema ni kweli, ikiwa ni ya kibibilia, basi kuna athari wazi maishani mwako. Ni hivi: Utokapo hapa na kurudi makanisani mwenu au vyuo vyenu, yale unapaswa kutenda ni kufanya jukumu lako kuwa mwenye furaha jinisi uwezavyo . . . ndani ya Mungu. Mwito wangu kwenu sasa, kwa jina la Mungu mkuu ni ili uufanye jukumu lako milele na milele kutafuta mema yako kwa nguvu zote Mungu amechochea ndani yako.

Shida yangu maishani, na shida yako maishani sio kuwa unatafuta mema yako wakati unge faa kufanya jukumu lako. Hiyo sio angalisho yangu au ya Mungu au ya Bibilia ya shida yako. C.S. Lewis aliupata vizuyrikatika ujumbe wakeunaobadilisha unao itwa “Uzito wa utukufu” Wakati anasema yakuwa shida zetu ni kuw atunafurahishwa kwa urahisi sana, sio eti tunatafuta mema yetu kwa pupa sana. Anasema sisi tu kama watoto wachanga ambao wanacheza na matope kwenye vitongoji duni kwa sababu hatujui jinsi wakati wa mapumziko kule baharini ikoje. Shida yetu ni kuwa atumeshikilia miungu ya mabati wakati ukweli wa dhahabu umesimama mbele yetu. Tunafurahishwa kwa urahisi sana. Shida ya dunia sio raha; ni upungufu war aha kutoendea yale ambayo yana tutosheleza kabisa. Hiyo ndio jambo kuu leo asubuhi.

Na kidokezo hicho; kama ni kweli, ni kwamba unafaa kuamka asubuhi na kama George Muller asemavyo kabl, a atoke nje na kutenda chochote, “Ni lazima nifanye moyo wangu iwe na furaha kwa Mungu la sivyo sitakuwa na manufaa kwa mtu yeyote. Nita watumia na nijaribu kuwafanya wanitosheleze tamaa yangu na utupu wangu.” Ikiwa unataka kuwa mtu wa upendo, ikiwa unataka kufunguliwa ili uweke maisha yako chini kwa ajili ya wengine, lazima ufanye jambo kuu kwa mwenye furaha ndani ya Mungfu. Hiyo ndio ujumbe wa leo. Tunafurahishwa kwa urahisi sana.

Tumechukua vitu vidogo, visivyo chukua muda mrefu, visivyo tutosha, visivyotosheleza mema yetu, hadi kiwango chetu cha furaha kime punguza kiwango cha kufanya majukumu yetu bila furaha msingi wa utu ili kuficha nyoyo zetu ambazo hazijabadilishwa na haziwezi kupata uguso wa Mungu. Waona jinsi ya kuhepuka ilioko? Niko katika hali ya kupiga debe dhidi ya wanao teseka bila kulalamika na dhidi ya Immanuel Kant, Mfilosofia wa Uhamisho aliyesema, kiwango cha wewe kujitafutia wema wako kwa njia yoyote ya maadili njema, una dunisha utu wema. Hili sio Bibilia . . . na inaharibu maabudu, utu wema, ujasiri na ubinafsi wa Mungu kila mahali, Inamwinua mwanadamu, mtu mwenye maadili njema afanyae jukumu lake bila kuzimngatia Mungu kutosheleza nafsi yake. La hasha! Na iwe mbali na nyoyo zetu milele.

Niko kwa hlai ya kupiga debe dhidi ya yale yanayo ninginia katika hewa ya mahubiri. Nilianza kupiga debe karibu miaka Ishirini na tano iliyopita, na sija wahi rudi nyuma tangu wakati huo, ’najaribu kulkea familia yangu kwayo, kujenga kanisa kwayo, kuandika vitabu kuihusu, najaribu kulishi, kwa kidogo kidogo upingaji uja. Hivyo ndivyo una kuwa. Wengi wenu wameni eleza yakuwa mnahisi kuwa dunia yenu unageuzwa na kongamano hili.   Yana tikiswa. Na hivyo ndivyo unaanza kubadilika. Yaweza kuchukua miaka . . . upingaji baada ya upingaji. Mwaka wa 1968 nilianza kuona mambo haya nikisaidiwa na Dan Fuller, na C.S. Lewis na Jonathan Edwards, na Mfalme Daudi, na mtakatifu Paulo na Yesu Kristo, na kwwa njia ambayo akili yangu inafamnya kazi ni kuwa upingaji moja baada ya nyingine ikija na aibika, kisha naenda kwenye Bibilia na naomboleza na kulia nanangananga na nauliza na naomaba na naongea kasha kidogo kidogo upingaji huo unachgunga maono hiyo.  

Pingamizi

 1. Je Bibilia kwa kweli inafundisha yakuwa unafaa kujifurahia furaha kwa roho yako na akili , nafsi na nguvu yako yote, au ni ujanja wa mahubiri wa John Piper ili kupata wasikilizaji?
 2. Na je kujikana mwenyewe ulikuwaje? Si Yesu alisema, “Ikiwa mtu atanifuata na ajikane mwenyewe?"
 3. Je, si hii hautilii mkazo sana hisia? Je si ukristo sana sana ni mambo ya kupenda kwa mtu. Ambapo tunafanya agano na maamuzi?
 4. Na itatendeka nia nzuri ya kumtumikia Mungu kama jukumu wakati ni ngumu au hisi kulitenda?
 5. Je si hii linaniweka—na sio Mungu—katikati ya mambo?

Majibu ya Upingaji

1. Je, kweli Bibilia inafunza ya kuwa unafaa kufuata furaha yako mwenyewe?

Jibu langu ni ndio na inafanya hayo angalau kwa njia nne:

a) Na amri.

Zingatia Zaburi 37:4. “Jifurahishe kwa Bwana.” Hii sio pendekezo bali ni amri. Ikiwa umeamini, “usizini” ni jambo unapa wa kutii kisha unafaa kutii. “Jifurahisheni kwa Bwana.”

Au Zaburi 32:11 “Mfurahieni Bwana, shangilieni enyi wenye haki; pigeni vigelegele vya furaha, Ninyi nyote mlio wanyofu wa Moyo.” Hadi kiwango yenye hakuna tofauti ikiwa unamtumikia Mungu kwa furaha au la, Wewe nbi Yule Yule mbele ya Mungu. Alikueleza ni lazima umtumikie Bwana kwa furaha. Au Wafilipi 4:4  “Furahini katika Bwana siku zote; tena nasema furahini.”

Yako kila mahali katika Bibilia. Tunaongea kuhusu Amri za Bwana Hiyo ndio nji aya kwanza Bibilia inafunza hii.

b) Na vitisho.

Jeremy Taylor wakati mwingine alisema, “Mungu anatisha maovu ikiwa hatutakuwa wenye furaha.” Nilidhania hiyo ni ujanja nilipo usikia mara ya kwanza. Sio ujanja . . . ni nukuu kutoka  Kumbu kumbu la Torati 28:47 na inaangamiz.” Kwa kuwa hukumu milikia Bwana, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa hivyo utawatumikia adui zako atakao waleta Bwana juu yako.” Mungu anatutisha na mabaya ikiwa hatutakuwa na furaha ndani yake. Je hiyo ni ruhusa ya raha au la? Je hiyo ni ruhusa ya kufanya wajibu wako maishani iwe ni kuutafuta furaha yako ndani ya Mungu kwa nguvu zako zote?

c) Kwa kuonyesha imani inayo okoa kama inayotoshelezwa na yote ambayo Mungu amesimamia katika Yesu.

Kwa mfano, Waebrania 11:6:  “Laikni pasipo na imani haiwezekani kumpendeza Mungfu, Yule amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” Ikiwa ungempendeza Mungu ni lazima uwe na imani. Imani ni nini? Kumwendea Yule.

Au chukua Yohana 6:35 Yesu asema, “Mimi ndimi chakula cha uzima; Yeye ajae kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.” Wekea mstari neno hili: Naye aniaminiye  hataona kiu kamwe. Je, hiyo inamaanisha nini kuhusu imani? Imani ni nini? Imani katika mafunzo ya Bibilia ya Yohana, ni kumwendea Yesu ili tupate kutoshelezwa nafsi zetu kiwango cha hakuna chochote tena yaweza kututosheleza. Hiyo ni imani. Imani sio kitu kingine kuliko yale nanena kwayo. Nina funua Ukristo msingi kwa lugha yenye hamjauzoea.

d) Kwa kuonyesha dhambi kama wazimu wa kuacha kutafuta furaha yako katika Mungu.

Dhambi ni uovu wa kuacha kufwata wema wako ndani ya Mungu. Hapo kuna nukuu: Yeremia 2:12-13: “Enyi mbingu, staajabuni kwa ajili ya jambo hili, mkaogope sana, na kuw ukiwa sana, asema Bwana. Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; Wameniacha mimi, niliye chemic hemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, Mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji. Nieleze nini ovu? Maelezo ya uovu, ile inayo shangaza ulimwengu, ambayo inafanya malaika wa Mungu kusema, “ La! Haistahili iwe!” . . . . Nini hicho? Inaangalia Mungu, chemichemi ya kutosheleza kwote, maji ya uzima, na kusema “la asante sana,” na kugeukia runinga, kufanya mapenzi, sherehe, pombe, pesa, tohari, nyumba kule kwa wenye mali, starehe, kipindi kipya ya tarakilishi, na kusema “ndio” Hiyo ni wazimu! Na inafanya mbinguyote Ishangazwe, kulingana na Yeremia 2:12.

Kwa njia hiyo nne, kwa kiwango, Bibilia inasema yakuwa John Piper anafunza ukweli asubuhi asemapo weka maisha yako kwa kutafuta mema yako ndani ya Mungu. Kwa hivyo upingaji nambari 1 ulianguka.

2. Ni nini kuhusu kujikana mwenyewe?

Si Yesu alisema katika Mariko 8:35 ”kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza na auchukuwe msalaba wake mwenyewe.” Msalaba ni mahali pa wewe kufa, mahali pa kungamizwa. Sio mama mkwe mwenye kelele, au jirani mbaya, au ugonjwa kwenye mifupa yako. Ni kifo ya ubinafsi. Kwa hivyo Piper, umekosea kwa kutuita kufuata kutosheleka kwa nafsi zetu kama azma kuu ya maisha. Nimehisi hivyo—na kasha nikaendelea kusoma andiko hilo (husaidia pia kusoma kwa kifungu wakati mwingine): kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeingamiza nafsi yake kwa ajili yangu, ataisalimisha.” Maana ni nini hapa? Nini anayomaanisha Yesu katika mistari hiyo?

Anamaanisha hivi:

—“O wafuasi wangu, msiyapoteze maisha yenu. Msiyapoteze maisha yenu! Okoeni maisha yenu. Okoeni maisha yenu!”

—“Vipi?...kwa njia gani Yesu?"

—“Kuipoteza.”

—“Sielewi . . . siyaelewi yesu.”

—“Maanake ni kwamba—wafuasi wangu, wapenzi wangu—yatupeni maisha katika mtazamo kuwa unayatupa yote isipokuwa mimi. ‘Isipokuwa tu punje ya ngano ianguke ardhini na kufa, itabaki pweke. Bali ikifa inazaa matunda mengi.’ Ulifilie ulimwengu, fahari, mali, dhambi ya ngono, udanganyifu ili ufanikiwe, hali ya kutaka kupendeza watu. Ufe, na unipate".

Naamini kujikana mwenyewe. Jinyime mkebi ili upate dhahabu. Jinyime mchanga ili usimame kwenye mwamba. Jinyime maji reja, rejaili upate divai. Hamna hali ya kujikana kwa ujumla kabisa wala Yesu pia hakumaanisha hivyo. Naamini kujikana. Naamini neno hili kuhusu yesu: mathayo 13:44 “ufalme wa mbingu unafananishwa na mtu aliyepata lulu katika shamba na kwa furaha, akaenda na kuuza mali yake yote ili aweze kununua shamba hilo.” Unaita hiyo kujikana? Ndiyo! Aliuza vyote. Alihesabu vitu vyote kama taka ili ampate Kristo.

Kwa hivyo, ndiyo ni kujikana; na la, sio kujinyima. Kuna mwenyewe ambaye anafaa kusulubishwa: mwenyewe apenaye ulimwengu. Lakini mwenyewe ambaye ni mpya na apendaye kristo juu ya yote, na anaye pata kutosheleka kwake ndani yake—usiangamize ‘mwenyewe’ huyo. Huyo ndiye kiumbe kipya. Jaza mungu katika huyo ‘mwenyewe’

O, naamini kujinyima ambako Yule kijana mtawala na tajiri hakuelewa bali Yesu aliufunza hayo pale pale.

“Enda ukauze vyote ulivyo navyo kijana na uje unifuate, nawe utakuwa na hazina mbinguni.” Naye Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Ni vigumu mno kwa tajiri kuingia katika ufalme wa mbingu. Ni rahisi sana kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kushinda tajiri kuingia katika ufalme wa mbingu.” Kisha wanafunzi wakapigwa na butwaa, na wakasema, “Nani basi ataokoka?” Na Yesu akasema, “Kwa mwanadamu haiwezekani. Hakuna awezaye kuwa na moyo nitafutayo mwenyewe. Lakini na Mungu,” Anasema, “Yote yawezekana.” Kisha Petro akafoka, ”Tumeacha vyote ili tukufuate. Je sisi? Tulijitolea kweli.” Naye Yesu akajibu—Laiti ningelijua sauti aliyotumia—na kusema, “Petro, hakuna aliyeacha nyumba au baba au mama au wandugu na wadada au mashamba na watoto kwa ajili yangu ambaye hata pata mara mia moja ya mama, baba, ndugu, dada, mashamba, na watotokatika haya maisha—pamoja na dhiki—na katika miaka zijazo, uzima wa milele. Hauwezi kutoa chochote ambacho hakitarudishwa kwako mara elfu. Usijihurumie wakati kichwa chako kinapokatwa kwa sababu yangu.” (tazama Marko 10:17-31)

Ndio naamini kujikana mwenyewe. Naamini kujikana kila kitu kitakachosimama kati yangu na kujitosheleza kwangu kikamilifu ndani ya Mungu. Na hivyo ndivyo ninavyoelewa Biblia inamaanisha kwa kusema kujikana mwenyewe. Naamini kuwa Davuid Livingstone na Hudson Taylor—Wanahistoria hawa wakubwa—Walikuwa hakika kikamilifu wakikamilisha maisha yao na baada ya kuwa walipoteza wake wao na afya na kila kitu kingine isipokuwa moja, kuwaambia wanafunzi wa chuo kikuu cha Cambridge na watu wote kote, “Sijawahi kuto chochote.” Ni hakika hio! Nafahamu wanayomaanisha, nawe pia wafahamu. Na ninaamini kuwa Jim Elliot aliyeacha maisha yake kama kijana alikuwa hakika kikamilifu aliposema, “Yesu si mpumbavu anayepeana kile asichoweza kuhifadhi ili kupata kile asiloweza kupoteza.” Ndicho ninachoamini kuhusu kujikana mwenyewe. Kwa hivyo pinzani nambari ya pili ikaanguka.

3. Je si wasababisha mengi kutokana na hisia   

Je si Ukristo ni zaidi uamuzi wa mtu? Kujitoa kwa kupenda? Si hisia ni mambo ya burura tu, uchaguzi, sukari kwenye keki? Jinsi yako ya kunena kuhusu Ukristo, Piper, nadhani, inainua hisia ikafikia hadhi isiyo ya kibibilia.

Lakini nisomapo Bibilia—Inasaidia kusoma Bibilia ukiwapo katika mzozo—na nikaona yakuwa:

 • Tumeamuriwa kuhisi furaha Wafilipi 4:4  “Furahia katika Bwana.”
 • Tumeamriwa kuhisi tumaini Zaburi 42:5  “Tumaini Mungu”
 • Tumeamuriwa kuhisi uwoga: Luka 12:5 “Mwogopeni Yule ambaye akisha kumwua mtu ana uwezo wa kumtupa katika Jehanamu.”
 • Tumeamuriwa kuhisi amani: “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu”  Wakolosai 3:15
 • Tumeamriwa kuhisi Bidii: Warumi 12:11  “Kwa Bidii, sio walegevu, mkiwa na juhudi katika roho zenu mkitumikia Bwana.”
 • Tumeamriwa kuhisi huzuni: Warumi 12:15 “Liueni pamoja na waliao.” Hauna chaguo mbadala. Ni lazima ulie, Ni lazima uhisi kulia na wale waliao.
 • Tumeamriwa kuhisi tamaa: 1 Petero 2:2. Yatamani maziwa ya kiroho ya neno.” Upende usipende. Hauwezi kusema. “Siwezi hisi rtamaa ya kutosha, kwa hivyo nitawezaje ku tii hii? HaiweziKuwa Amri.“ Umenoa! Ndio, hauwezi kuwasha na kuzima hisia hizi kwa kupenda kwako. La, yote hayo ni jukumu. Hapo ndani kuna hali ya mshike mshike ambayo tulisikia usiku uliopita.

  Yote ninayo waeleza ambayo mna amuriwa kutenda sasa hivi hamwezi kutenda sasa hivi kwa nguvu zenu wenyewe au uamuzi au kuajibika. Unaweza kuufanya tu kwa miujiza. Je, si unahitaji? Si ni jambo la dharura kuelezwa na mungu mkuu ya kuwa ni lazima utende yale hauwezi tenda? Ikiwa moyo wako ni sawa ungeyatenda. Hatuna utu na tume amriwa kuhisi huruma. “mweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma.” Hauwezi kusema tu yakuwa, msamaha inamaanisha kusema “pole” ni lazima uhisi.
 • Tume amriwa kuhisi shukran: Mfano, mtoto asubuhi moja ya Krismasi anapokea zawadi kutoka kwa nyanyake . . . .na ni soksi nyeusi! Yak! Hakuna mtoto daima atakaye kupata soksi, hata iwe nyeusi, wakati wa Krismasi. Na kisha unasema “ambia nyanya yako asante,” na mtoto anasema “asante kwa soksi.” Hiyo sio yale Bibilia inasema. Mtoto aweza sema hayo kwa kupenda. Lakini hawezi kuhisi shukran kwa sababu ya hayo soksi kwa kupenda. Hata wewe hauwezi hisi shukran kwa Mungu kwa kupenda kwako wenyewe kufuatana na amri katika Waefeso 5:20 “Na kumshukuru Mungu baba siku zote kwa mambo yote.” Basi tumekamilika, kama si Mungu mkuu kufanya kazi.

Pingamizi nambari 3? Si ukubali. Si uamini ya kuwa na inua upendo zaidi kuliko Bibilia ifanyavyo. Nadhani nawarudisha pahali dini ya kimarekani iliyo jawa na  hisia za uamuzi, jitiahada, na nguvu ya binafsi ilipo waangusha kwa sababu hawawezi kudhibitika.

4. Na je, vipi kuhusu maono nzuri ya kumtumikia Mungu?

Je, si ni jukumu kumtumikia Mungu? Haifanai na utumishi jinsi unenavyo kuhusu Ukristo, Piper. Haifanani kamwe kama utumishi . . . kumakinika, kusimama dhidi ya changamoto ya kufanya mapenzi ya Mungu wakti ni mgumu.

Kwa hivyo nimejifunza kujibu sasa, “Basi tuangalie maandiko chache ambayo imejenga kinaya ya utumishi.“ Kinaya zote kuhusu uhusiano wako na Mungu, Iwe kama mtumishi au mwana au Binti au rafiki, Inayo viungo ndani yao ambayo ukiyazingatia sana, yatakuwa uwongo. Yanayo viungo pia ndani yao ambayo ukiyasisitiza huenda yakawa ukweli. Basi ni nini uwongo na ni nini ukweli katika kufanana na kutofautiana katika utumishi?

Maandiko yanayokuusaidia ku tofautisha hayo mawili ili usikufuru unapotumika ni kama Matenjdo ya Mitume 17:25 “Mungu wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu, kana kwamba anahitaji kitu chochote; Kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.” Mungu hatumikiwi, Marafiki. Kuwa makini. Hatumikiwi kana kwamba anakuhitaji au utumishi wako. Ahitaji. Au chukua fungu kama Mariko 10:45 “Mwana wa adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika; na kutoa nafsi yake iwe faida ya wengi.” Hakuja kutumikiwa. Tazama kwa makini! Tazama kwa makini! Ukiwa umeamua kumtumikia kisha upite kusudi lake! Yakushangaza lakini, sivyo. Paulo alijiita mtumishi wa Mungu kwa karibu barua zote. Na hapa katika Matendo ya Mitume 17:25 na Mariko 10:45 Inasema Mungu hatumikiwi na tena mwana wa Adamu alikuja sio kutumikiwa. Ni lazima pawe na aina ya utumishi ambayo ni potovu na aina ya utumishi ambayo ni nzuri. Utumishi nzuri ni upi?

Utumishi nzuri ni 1 Petero 4:11: “Mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu. Ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo.” Mungu hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu chochote. Unapaswa kupata njia ya kuabudu, kuchapisha makaratasi, kuskiza mafundisho, kuendesha gari, kubadilisha nguo ya mtoto mchanga, kuhubiri ujumbe, kwa njia ambayo wewe kila wakati ndie mpokjeaji. Kwa sababu mpeanaji anapata utukufu, na anye pokea apata furaha. Wakati wowote tupitiapo Matendo ya Mitume 17:25 “Mungu wala hatumikiwi kwa mikono ya Binadamu. [Kana kwamba alikuwa ni mpokeaji] kana kwamba anahitaji kitu chochote” . . . ’Tuna fukuru.

Nilipeana mfano jana, kwa viongozi wa kongamano hili, kutoka  Mathayo 6:24 kuhusu utumishi ambayo inasema, “hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; Kwa maana atamchukua huyu, na kumpenda huyu; ama, atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na Mali.” Basi hapa, tunaongea kuhusu utumishi. Utatumikiaje pesa? Hautumikii pesa kwa kutoshelza mahitaji ya pesa. Unatumikia pesa kwa kulinda maisha yako bila kutulia, kwa nguvu zako zote, Mda na juhudi, ili ufahidi kutoka kwa pesa. Akili yako inazunguka huku na huku kwa jinsi ya kuendelza biashara ya magendo, jinsi gani ya kupata makubaliano ya kibishara njzuri, jinsi ya kuwekeza  mahali faida inakuwa polepole hadi wakati itakuwa juu, na unamezwa na jinsi gani ya kupata faida ya pesa, kwa sababu pesa ndio chemichemi yako.

Ikiwa hiyo ni kweli kuhusu unavyo tumikia pesa, basi ni jinsi gani unamtumikia Mungu? Ni hivyo kwa hakika: Unajipanga vizuri, na unaendelea na maisha yako, na unaweka nguvu, juhudi na muda na talanta kujiweka chini ya maji ya Mungu yenyeBaraka, ili abakie kuwa chanzo na ubakie kuwa mpokeaji mtupu. Ubakie anayefaidika, naye abakie anayefaidi: ubakie mwenye njaa, naye abakie mkate, Ubakie mwenye kiu, naye abakie maji. Usifanye kamwe tendo la kukufuru na kubadilisha jukumu la Mungu na lako. Tunapaswa kupata njia ya kutumika kwa njia yenye imo ndani ya nguvu ambayo Mungu anapeana. Mimi nipo mwisho wa kupokea wakati natumika. La sivyo, namweka Mungu kwa sehemu ya kufaidika; na mimi nakuwa mwenye kufaidiisha na basi nakuwa Mungu. Na kunayo dini nyingi kama hayo duniani. Kwa hivyo upingaji ya nne(4) ime anguka.

5. Je, siwajiweka katikati au msingi mwenyewe?

“Wanena kuhusu kutafuta furaha yako na mema yako. Una nena kuhusu jukumu kama jambo linguine tofauti kuliko yale tumeyajua, pia unasema yakuwa tunapaswa ku makinika kuhusu utumishi. Ina nifanania kuwa una chenga na kulazimisha lugha ya Bibilia ili ujiweke katikati.” Hiyo ungekuwa upingaji mkuu zaidi ya yote, Si ungekuwa?

Hii ndio jibu langu: Nimekuwa kwa ndoa kwa miaka 28, kuanzia tarehe 21 Desemba. Nampenda Noeli sana. Tumepitia mengi pamoja, wakati mgumu sana pia wakati nzuri sana. Tumeona watoto wetu vijana wakipitia wakati mgumu wa miaka ya ujana. Nalia kwa urahisi nikiwaza kuhusu watoto wangu wanaume na pia binti yangu mchanga. Tuseme Desemba 21 niende nyumbani na Maua miti 28 yale nyekundu nikiwa nimeuficha mgongoni na niubonyeze kengele ya mlango: Noeli akaja mlangoni, ameshangazwa kwa nini nimebonyeza kengele ya mlango wangu, kisha nitoe maua yale na niseme, “furahia  mwaka wetu wa nbdoa Noeli.” Kisha asema,” Johnny, maua haya ni mazuri! Kwa nini ulizinunua?” na nasema “Ni jukumu langu.”

Jawabu mbovu. Wacha nikarudie.

[Ding Dong]

—“Furahia mwaka wa ndoa Noel!”

—“Johnny, haya ni mazuri! Kwa nini uliyanunua?”

—“Hakuna lolote linalonifanya niwe na furaha kama kukununulia maua. Kwa hakika, mbona  usibadilishe nguo, kwa sababu nime panga ili Yaya aje alinde mtoto na tuende tufanye jambo spesheli usiku wa leo, kwa sababu hakuna jambao ningependa kufanya usiku wa leo kando na kuwa nawe.”

Jibu sahihi.

Kwa nini? Kwa nini angesema,” Wewe ndiye mkristo mchoyo na mpenda rah asana  nimewahi kukutana naye! Yote unayoyafikiria kuhusu ni yale yanayo kufurahisha!” Nini inaendelea hapa? Kwa nini jukumu ndio jibu mbaya na furaha jibu sahihi? Je waelewa?

Ukipata hili basi umeipata, na naweza rejea Minneapolis na nimsifu Mungu. Mke wangu anatukuzwa zaidi ndani yangu wakati nime toshelezwa zaidi ndani yake. Nikijaribu kubadilisha uhusiano wetu iwe uhusiano wa utumishi, uhusiano wa jukumu ambapo sitafuti mema yangu kwake, atadunishwa . . . . Napia Mungu. Ufikapo mbinguni na Baba akutazame na aseme, “Kwa nini uko hapa? Kwa nini ulitupilia maisha yako kwa ajili yangu?” Afadhali useme,” Wapi tena ningependa kwenda? Kwa nani tena ningeenda? Wewe ndiye tamaa ya nafsi yangu!” Na hiyo ndio sababu ya kongamano hii. Kongamano hili ni kuhusu mambo mawili makuu, kuja pamoja katika kizazi cha 268 kutoka katika Isaya 26:8 Ni ari ya Mungu kwa jina lake, sifa na heshima, na Ari ya moyo wangu kutoshelezwa kwa tamaa yangu. Hayo ni vitu viwili ambazo haviwezi kutikiswa ulimwenguni. Na yale na tumainimmeona ni yakuwa yote ni moja, Kwa sababu Mungu na jina lake na sifa na heshima yake wanatukuzwa sana ndani yangu ninapotosheka sana ndani yake.