Uzazi kwa Imani katika nyakati mbaya

Taabu gani hii niliyo nayo! Nimefanana na Yule akusanyaye matunda ya kiangazi, aokotaye masazo baada ya kuvunwa shamba la mizabibu, hakuna kishada chenye matunda ya kula, hakuna hata ile tin iya mwanzoni ninayoitamani. 2 Wanaomcha Mungu wameondolewa kutoka kkwa nchi,hakuna mtu mnyofu hat mmoja aliyebaki. Watu wote wanavizia kumwaga damu,kila mmoja anamwinda ndugu yake kwa wavu. 3 Mikono yake yote miwili ni hodari katika kufanya ubaya, mtawala anadai zawadi, hakimu anapokea rushwa , wenye nguvu wanaamuru wanachotaka, wote wanafanya shauri baya pamoja. 4 Aliye mwema kupita wote kati yao ni kama mchongoma, anayeonekana mnyofu zaidi miongoni mwao ni mbaya kuliko uzio wa miiba.

Siku ya walinzi wako imewadia, siku atakoyotembela Mungu. Sasa ni wakati wao wa kuchanganyikiwa. 5 Usimtumaini jirani usiweke matumaini kwa rafiki. Hata kwa Yule alalaye kifuani mwako uwe mwangalifu kwa maneno yako. 6 Kwa kuwa mwana humdharau baba yake, binti huinuka dhidi ya mama yake, mkwe kuwa kinyume na mama mkwe wake, adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa.

7 Lakini mimi namtazama BWANA kwa matumaini, namngoja Mungu Mwokozi wangu. Mungu wangu atanisikia mimi. 8 Usifurahie msiba wangu Ee adui yangu! Ingawa nimeanguka nitainuka. Japo ninaketi gizani, BWANA atakuwa nuru yangu. 9 Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake nitabeba ghadhabu ya BWANA, mpaka atakaponitetea shauri langu na kuithibitisha haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaiona haki yake. 10 Kisha adui yangu ataliona naye atafunikwa na aibu, Yule aliyeniambia , “Yu wapi BWANA Mungu wako?” Macho yangu yataona kuanguka kwake, hata sasa atakanyangwa chini ya mguu kama tope barabarani.

11 Siku ya kujenga kuta zako itawadia , siku ya kupanua mipaka yako. 12 Siku hiyo watu watakuja kwako kutoka ashuru na miji ya Misri, hata kutoka Misri hadi Eufrati na kutoka bahari hadi bahari na kutoka mlima hadi mlima. 13 Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake, kwa sababu ya matunda ya matendo yao.

14 Wachunge watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, ambalo linaishi pekee yake msituni, katika nchi yenye malisho ya rutuba. Waache alishe katika Bashani na Gileadi kama ilivyokwa siku za kale.

15 “Kama siku zile mlipotoka Misri, nitawaonyesha maajabu yangu.”16 Mataifa yataona na kuaibika waliondolewa nguvu zao zote. Wataweka mikono yao kwenye vinywa vyao na masikio yao yatakuwa na uziwi. 17 Wataramba mavumbi kama nyoka, kama viumbe vitambaavyo juu ya ardhi. Watatoka nje ya mipango yao wakitetemeka, watamgeukia BWANA Mungu wetu kwa hofu nao watakuogopa.

18 Ni nani Mungu kama wewe, ambaye anaachilia dhambi na kusamehe makosa ya mabaki ya urithi wake? Wewe huwi na hasira milele bali unafurahia kuonyesha rehema. 19 Utatuhurumia tena utazikanyaga dhambi zetu chini ya nyayozako na kutupa maovu yetu yote katika vilindi vya bahari. 20 Utakuwa wa kweli kwa Yakobo, nawe utamwonyesha Abrahamu rehema, kama ulivyowaahidi kwa kiapo baba zetu siku za kale.

Tunatamatisha msururu wa mafunzo kuhusu uzazi wa kiroho leo. Dibaji ambalo nimechagua kwa ujumbe huu wa mwisho ni “Uzazi kwa imani katika nyakati mbaya.” Hakuna nyakati rahisi ya kuzaa na kuwalea watoto. Jambo lililoko katika Mwanzo 3, ni kuwa vile tu dhambi iliingia ulimwenguni, kuzaa na kulea watoto umekuwa ngumu sana. Bwana akamwambia Hawa, “Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako, kwa utungu utazaa watoto” (Mwanzo 3:16) Na baada ya yeye pamoja na Adamu walikwisha kuwalea wanaume wawili, mmoja wao akaua mwenzake.

Njia Ya kipekee ya Kuwa Huru

Jambo katika hadithi hiyo ni kwamba sasa dhambi imo ulimwenguni—katika kila mzazi na mtoto. Ni hiki ndicho kitu dhambi itendacho. Inaharibu watu na inaharibu familia. Shida kuu ulimwenguni ni nguvu kukaa katika dhambi. Na ni nguvu. Ni mvuto, ni kiwewe, kizuizi, ufisadi moyoni mwa mwanadamu. Si msururu wa chaguo la bure. Dhambi ni kifungo chenye nguvu uharibiayo uhuru wa binadamu.

Njia ya kipekee ya mwanadamu kuwa huru-kwa mzazi au mtoto kuwa huru-ni kuzaliwa mara ya pili kwa roho ya Mungu; Kumbatia Yesu Kristo kama mwokozi; usamehewe dhambi kupitia muumba wa mbingu na nchi; na upokee Roho mtakatifu kama nguvu ya kipekee ya kushindana na nguvu za dhambi. Hilo ndilo tumaini la pekee kwa ulimwengu na watoto na wazazi. Hili huwa kweli katika kila umri.

Hakuna Nyakati Rahisi katika Uzazi

Hakuna nyakati rahisi ya kuzaa na kuwalea watoto katika unyenyekevu, upendo, haki ubunifu, wenye manufaa, watu wazima wanaotukuza Kristo. Hakuna nyakati rahisi. Lakini nyakati zingine ni ngumu kushinda zingine. Na kuwa kwao vigumu ama rahisi inalingana na hali yako ya kibanfsi ama ya kijamii.

Shauku yangu leo ni kukusaidia wewe mzazi na tumaini katika hali iliyo ngumu zaidi. Na ninamaanisha hali zote mbaya zote kinyumbani na kitamaduni. Na kwa wale ambao sio wazazi, yale yote ninayosema yanawahusu, kwa sababu jinsi ya kuwa na tumaini katika nyakati mbaya ni sawa kwa kila mtu. Tunaihitaji kwa sababu tofauti tofauti.

Nabii Mika

Nabi wa kiyahudi Mika alihubiri wakati wa utawala wa Jothamu, Ahazi na Hezekia, Wafalme wa Yuda. (Mika 1:1). Hiyo ni karibu miaka ya 750 hadi 687 kabla ya kuja kwa Kristo. Neno lililo wazi zaidi ya kuja kwake limepeanwa katika Mika 3:8.

Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu
Nimejazwa Roho ya BWANA, Haki na uweza
Kumtangazia Yakobo kosa lake,
Na Israeli dhambi yake.

Kutangaza Hukumu na Rehema

Mungu aliwatuma manabii kuwaambia watu dhambi zao kwa wazi. Na kupitia dhambi yao manabii walitamka hukumu, na rehema. Hivi ndivyo ilivyo katika Bibilia yote: Hukumu na Rehema. Mungu ni mtukufu na mwenye haki, na analeta hukumu juu ya watu wenye dhambi. Na Mungu ni mwenye rehema na utulivu na mwenye huruma, na anawaokoa wenye dhambi toka kwa hukumu yake. Mika anadhihirisha hii katika Mika 4:10,

Gaa-gaa kwa utungu, Ee Binti Sayuni
Kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa,
Kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji,
Na ukapige kambi uwanjani.
Utakwenda Babeli
Huko utaokolewa.
Huko BWANA atakukomboa
Kutoka mkononi mwa adui zako.

Bwana atawatuma Babeli katika hukumu. Na atawarejesha nchini kwao kwa rehema.

Hukumu Inakuja

Katika fungu la 7, Mika anaongea kuhusu uzazi katika nyakati mbaya-Mbaya sana nyumbani pamoja na kitamaduni. Mstari 1. “Taabu gani hili niliyo nayo! Nimefanana na Yule akusanyaye matunda ya kiangazi, aokotaye masazo baada ya kuvunwa shamba la mzabibu, hakuna kushada chenye matunda ya kula, hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani. Anaweza kuwa anaongea juu ya vile ana tamaa ya chakula. Lakini nahisi anaongea kimafumbo juu ya kukosa marafiki ya kiungu na washirika. Kwa sababu anaendelea kusema, mistari 2-3: “Wanaomcha Mungu wameondolewa kutoka katika nchi, hakuna mtu mnyofu hata mmoja aliyebaki. Watu wote wanavizia kumwaga damu, kila mmoja anamwinda ndugu yake kwa wavu. Mikono yote miwili ni hodari katika kufanya mbaya, mtawala anadai zawadi, hakimu anapokea rushwa, wenye nguvu wanaamuru wanachotaka, wote wanafanya shauri baya pamoja.

Mstari 4: “Aliye mwema kupita wote kati yao ni kama mchongoma, anayeonekana mnyofu zaidi miongoni mwao ni mbaya kuliko uzio wa miiba.” Mika anajaribu kuwakaribia, wanamshikisha. “Siku ya walinzi wako imewadia siku atakayokutembelea Mungu. Sasa ni wakati wao wa kuchanganyikiwa. Basi mlinzi ambaye ameteuliwa kuchungulia adui anapokuja-siku yake imewadia. Hukumu inakuja.

Hata Bibi na Watoto

Sasa Mika nanaileta kutoka kwa tamaduni hadi ujirani na familia. Mstari 5:Usimtumaini jirani, usiweke matumaini kwa rafiki. Hata kwa Yule alalaye kifuani mwako uwe mwangalifu kwa maneno yako. “Kwa maneno mengine, dhambi na ufisadi na uwongo yana athari za kimwili ambapo inastahili uyachunge usije ukasalitiwa na bibi yako—“Yule alalaye kifuani mwako.”

Sasa kwa watoto. Mstari 6: “Kwa kuwa mwana humdharau baba yake, binti huinuka dhidi ya mama yake, mkwe kuwa kinyume na mama mkwe wake, adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa.” Kuna watu watano katika taswira hii. Baba na mama. Mwana wa Kiume na binti na mkwe. Basi mwana ameoa. Mika tayari amesema kuwa mambo si ya hakika kati ya bwana na bibi ( “Kuwa mwangalifu kwa maneno yako hata kwa Yule alalaye kifuani mwako”). Na sasa anasema kwamba mwana anamdharau baba yake, binti huinuka dhidi ya mama yake, mkwe pamoja na binti kuwa kinyume na mama mkwe wake. Mika hata anawaita maadui wa mwanaume. Mwishoni mwa mstari wa 6: “Adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa.” Anamaanisha tu wana wa kiume. Inaonekana kwamba mabinti wanaelekeza hasira zao kwa bibiye. Lakini anaihisi.

Sasa hii yavunja moyo. Wengine wenu wanaishi katika hali kama hii. Hii ndiyo nyakati mbaya zaidi . Utamaduni umejawa ufisadi, na ndoa na familia iko katika hali mbaya. Hiyo ndiyo taswira katika Mika 7. Kwa wengine wenu, hiyo ndiyo taswira ya leo. Na kwa wengine, itakuwa kesho.

Yesu analetaje hii?

Kabla niwatajie tumaini la Mika katika hali hii, nataka muone ile Yesu alifanya na taswira hii ya familia katika mstari wa 6. Fungua Mathayo 10:34-36. Yesu anaongea kuhusu athari za kuja kwake: “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga. [Halafu anatumia Mika 7:6] Kwa kuwa nimekuja kumfanya mwana kumdharau baba yake, binti kuinuka dhidi ya mama yake, mkwe kuwa kinyume na mama mkwe wake. Adui wa watu watakuwa wale wa nyumbani mwake hasa.”

Hapa ndio wale wale watu watano, ambao wametajwa kama maadui wa nyumba yako, ila tu tofauti mmoja tu. Yesu anasema kuwa aliuleta. Mstari 35: “Nimekuja kufanya mwana kuinuka dhidi ya baba yake . . . .” Haimaanishi, kwa hakika, kuwa anapenda kuvunja familia. Kile anamaanisha ni kwamba mwito wake kuu kwa uanafunzi hauleti uhasama katika uhusiano. Mmoja anaamini, mwingine haamini. Baba anamfuata Yesu, mwana hamfuati. Mwana anamfuata Yesu, baba hamfuati.

Kwa nini Yesu hapa?

Lengo la kuleta Yesu katika taswira hii kwanza ni kuonyesha kwamba uhasama katika familia wakati wa Mika haukuwa hakika ni juu ya ufisadi katika familia. Inaweza kuwa ni kwa sababu ya haki iliiyoko katika familia. Kila kitu kinaweza kuwa kilikuwa kikiendelea vyema mpaka mtu alipochukua Mungu kwa uzito, na agano lake na neno lake. Ndipo lawama ikaanza kuibuka. “Sasa unadhani wewe ni mzuri sana, kwa sababu una dini! Mambo yalikuwa sawa, na sasa unadhani kwamba sisi tuliozalia inafaa turekebishwe.”

Na sababu nyingine ya kutajwa kwa Yesu akitumia andiko hili ni kuonyesha kuwa hakukuwa na jambo lisilokuwa la kawaida katika nyakati za Mika. Ilikuwa kweli katika karne la 8 kabla kuja kwa Kristo. Na ni kweli katika karne ya 21. Kwa mtu fulani, huwa ni nyakati mbaya sana, hata kama si mbaya kwako

Ni nini, basi, Mika anataka kusema kuhusu uzazi kwa tumaini katika nyakati mbaya sana?

Kile Mika anataka kusema: Ujasiri kwa moyo uliovunjika

Anaongea kumhusu-nahisi kama mwakilishi wa baba na wana wa Israeli- Ni msimamo ambao anauchukua ni ile ya ujasiri kwa moyo uliovunjika. Huo ndio mwelekeo ya ule ninataka kukuambia kuhusu ulezi katika nyakati mbaya. Uifanye kwa msimamo wa ujasiri wa moyo uliovunjika. Na ndio nikikishe kuwa mnajua kile mnaimaanisha kwa “moyo uliovunjika” na “ujasiri”, inafaa tuulize: Ni nini imemfanya akavunjika moyo? Na ni kwa msingi gani anastahili kuwa mjasiri? Tutazame mistari 7-9 ndipo tupate jibu la maswali hayo mawili. Ni nini imemfanya akavunjika moyo? Na ni kwa msingi gani anastahili kuwa mjasiri?

Si kwa Haki ya Kibinafsi

Baada tu ya kusema katika mstari 6, “Adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa.” Anasema katika mstari wa 7, “lakini mimi, namtazama BWANA kwa matumaini, namngoja Mungu mwokozi wangu, Mungu wangu atanisikia mimi.” Basi katika nyakati mbaya sana, tunainua macho yetu kwa Bwana. Yawezekana kuwa tumejaribu kuinua macho yetu  kwingine. Hakuna kinachofanyika. Vyote vyaharibika. Tulidhani kuwa labda tungeweza kuleta utangamano katika familia. Labda watoto hawa walikuwa chini ya mamlaka yetu ya kuwatunza kwa njia tuchaguayo. Labda kwa vitabu vizuri vya ndoa, wana hofu itokao kilindini mwa moyo na heshima na kupendeza na upendo ungekuwa kwa nguvu zetu. Na sasa tunainua macho yetu kwa Bwana.

Lakini jihadhari: Je, Mika anainua macho yake kwa Bwana katika haki ya kibinafsi? Jambo kama hilo lawezekana. Je, anasema, “Niliyatenda yote yaliyo haki-yale baba afaa afanye. Kama mambo hayaendi sawa katika familia hii moyo wangu unavunjika, lakini mimi si shida. Wao ndio shida.” Je, ndio msimamo wa huyu mtu? La! Hasha. Na natumaini haitakuwa yako pia.

Tulikosea lakini Tunafahamu Kosa Letu

Sikiza yale anasema katika mistari 8 na 9. Sikiza kwa ujasiri na kwa kuvunjika. Kwa nini amevunjika?

Usifurahie msiba wangu, Ee adui wangu! Ingawa nimeanguka nitainuka. Japo ninaketi gizani, Bwana atakuwa nuru yangu. Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake, nitabeba ghadhabu ya Bwana mpaka atakaponitetea shauri langu na kudhibitisha haki yangu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaiona haki yake.

Usiukose mwanzo wa mstari wa 9, “Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake, nitabeba ghadhabu ya Bwana.” Sababu ya kufanya hili liwe muhimu kwa wachumba na wazazi kuona ni kwa sababu anaisema kwa uambatanisho na kutendewa dhambi kwa hakika. Katika mstari wa 8, anaambia adui yake (labda mwanawe ama mkewe), “Usifurahi msiba wangu, Ee adui yangu.” Usifurahi juu yangu. Na katika mstari wa 9 katikati anasema, Bwana atanitetea shauri langu na kutoa hukumu upande wangu, sio juu yangu. “Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaiona haki yake.”

Kwa maneno mengine anajua kwamba anakosewa. Anajua kuwa baadhi ya madai yao ni ya uongo. Anajua kuwa Mungu yuko upande wake wala sio kinyume naye. Mungu atamleta nje kwenye mwanga; na ataona haki yake. Ni mjasiri kati hali hii na tamshi hili. Mjasiri wa ajabu. Ingawaje, yale anavutia hisia zetu ili kueleza ghadhabu ya Mungu na giza yake mwenyewe ambayo ni dhambi yake. Nitabeba ghadhabu ya Bwana, sababu nimetenda dhambi dhidi yake.”

Kwa nini Kuvunjika Moyo Sana

Basi hapa ni jibu langu la swali: Ni nini imemfanya akavunjika moyo? Si kwamba anatendewa dhambi katika familia, bali kwamba anatenda dhambi. Msimamo wa ulezi kwa imani katika nyakati mbaya ni msimamo wa ujasiri wa kuvunjika moyo. Na kuvunjika kwa moyo kwanza ni kwa ajili ya dhmbi zake, na hatimaye anatendewa dhambi. Hii ndio vita kuu tunaokumbana nayo. Je, kwa neema ya Mungu tutapata aina ya unyenyekevu unaotuwezesha kuona familia zetu na sisi wenyewe kwa njia hiyo?

Ujasiri wa kiasi gani

Swali la pili: anawezaje kuwa mjasiri, kama tayari ametendewa dhambi? Anawezaje kuongea kwa njia hii kama dhambi yake imejaa sana moyoni mwake? Ujasiri wa aina hii unatokea wapi? “Usifurahie msiba wangu, Ee adui yangu! Ingawa nimeanguka, nitainuka . . . Mungu atanitetea shauri langu. Atanileta nje kwenye mwanga, nami nitaiona haki yake.

Jibu lapeanwa mwishoni mwa fungu. Na kwa kuwa inakuja kama kitu cha mwisho kwenye kitabu mzima, na kuwa inakuja na mkazo kama hii, inaonyesha vile ni muhimu sana katika kitabu hiki- Hakika, katika Bibilia yote. Mistari 18-19:

Ni nani Mungu kama wewe, ambaye anaachilia dhambi na kusamehe makosa ya mabaki ya urithi wake? Wewe huwi na hasira milele, bali unafurahia kuonyesha rehema. Utatuhurumia tena, utazikanyaga dhambi zetu kwa nyayo zako na kutupa maovu yetu yote katika vilindi vya bahari.

Sababu Mika ni mjasiri sana katika kuvunjika kwake ni kwa sababu anamjua Mungu. Anajua yale ya ajabu na ya kipekee kuhusu Mungu. “Nani Mungu kama wewe?” Inamaanisha: Hakuna Mungu kama wewe. Njia zako ni kuu kuliko zetu. Njia zako ni kuu kulikoviumbe vikuu duniani. Na nini isiyokuwa kawaida kwako? Unaachilia dhambi na kusamehe makosa ya watu wako. Hivyo basi kutokuwa kawaida kwa Mungu wa Bibilia—Na hakuna Mungu mwingine.

Kuingia ndani kwa Msamaha wa Mungu

Je, basi unaleaje kwa tumaini katika nyakati mbaya sana? Unaeleaje kwa Imani wakati familia yako wanaweza kuwa wamegawanyika watatu kwa wawili ama wawili kwa watatu? Unamtazamia Bwana. Unamlilia Bwana (Mstari 7). Na unamlilia kwa shauku mbili ya kiundani. Kwanza kuwa wewe ni mtenda dhambi na kuwa hustahili chochote kutoka kwake. Hatujakuwa wazazi wakamilifu. Tumetenda dhambi. Sisi ni wapumbavu. Tunajua kuwa pia tumekosewa. Na kila kitu kilicho mwilini mwetu kinataka kukumbuka kuhusu hiyo. Ni Roho mtakatifu tu anayeweza kutufanya kutambua dhambi zetu. Ni Roho mtakatifu tu ndiye anaweza kutufanya tuhisi hatia zetu. Ni shauku moja ya kiundani.

Nyingine ni kwamba, hakuna Mungu mwingine aliye kama Mungu wetu, anayeachilia dhambi na kusamehe kosa na kuondoa ghadhabu, naufurahia katika upendo unaodumu. Tumeshawishika kindani kuhusu hii vile tulivyo kuwa tumewakosea wachumba wetu, watoto wetu, na kwa hayo yote dhidi ya Mungu. Unaona vile yote ni ya muhimu. Vile vinafanya kazi kwa pamoja, kila mmoja ikifanya ndani ya nyingine kuwezekana? Usipohisi dhambi na kosa lako, hutaenda ndani na msamaha wa Mungu. Lakini inafanya kazi kwa njia nyingine, na hii ni muhimu kwa familia: Kama hujui undani wa msamaha wa Mungu, hutaenda ndani pamoja na dhambi zako.

Shauku hizi mbili za kindani zinaleta mtazamo wa ujasiri wa moyo uliovunjika. Na hiyo ndiyo taswira ya ulezi kwa imani katika nyakati mbaya zaidi. Tumevunjika kwa ajili ya dhambi kwa njia ya kukosewa, tu wajasiri kwa sababu, “Ni nani Mungu asamehaye kama wewe!”

Ujasiri wa Moyo uliovunjika—Ulioimarishwa kwa Yesu

Na kwa Wakristo nusu zote za mtazamo huu umekita mizizi na kuimarishwa kwa kujua Yesu Kristo na yale aliyotutendea msalabani. Kwa Mika, Yesu alikuwa tumaini la pekee katika fungu la 5:  “Lakini wewe Bethlehemu Efrata . . . kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli . . . Atasimama na kulichunga kundi lake katika nguvu ya BWANA.” (Mika 5:2-4). Mchungaji huyu mwema aliutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo (Yohana 10:11). Na alipotoa uhai wake, tuliona kwa uwazi kuu kuliko yote ukuu wa dhambi zetu (ambayo ilistahili kiasi ya mateso) na ukuu wa jitihada ya Mungu ya kuusamehe. Na hivyo basi uvunjikaji wa moyo na ujasiri unaimarishwa.

Basi kama unalea katika nyakati mbaya sana, ama unajianda kulea katika nyakati mbaya sana, ama unataka kutarajia nyakati mbaya sana, tazama Mika na Yesu na uuchukuwe msimamo huu. Kuvunjika kwa ajili ya dhambi zako, na ujasiri kwa ajili ya Kristo. Hatimaye kwa nguvu za Roho Mtakatifu, tia moyo wako kuwa mzazi mzuri asiyekamilika vile unavyoweza—Kwa ajili ya Yesu.